Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Unapaswa kujifunza kwanza kabla ya kuwa mbishi.Ushahidi upo wa aina nyingi, ikijumuisha ushaidi wa kuona na hata kusikia. Hivyo ni mawazo potofu kudhania ushahidi ni lazima uwe ni nyaraka, picha, video etc. Mtu kuelezea kile alichokiona ni ushahidi tosha.
Kwahiyo niamini chochote kwasababu nimesikia kutoka kwako? Lazima mtu uwe na akili ya kuchuja mambo si kila nilimwalo ni kweli. Nashangaa ambavyo unataka niamini ya kwako au ya mtu mwingine lakini ya kwangu hutaki kuyaamini. Mimi silazimoshi uamini ya kwangu na si lazima niamini ya kwako. Tubaki hivyo
 
Alishindwa Lowasa sembuse huyo shoga. Ninyi ni wa kuburuzwa tu na hamna la kufanya. Kila kitu kinabuma, laani ya Dr. Slaa inawatafuna.
Kwani Magufuli amepata hata kura Miloni 3, thubutu!!!!!
 
Kwahiyo niamini chochote kwasababu nimesikia kutoka kwako? Lazima mtu uwe na akili ya kuchuja mambo si kila nilimwalo ni kweli. Nashangaa ambavyo unataka niamini ya kwako au ya mtu mwingine lakini ya kwangu hutaki kuyaamini. Mimi silazimoshi uamini ya kwangu na si lazima niamini ya kwako. Tubaki hivyo
Mimi sijatoa hoja yoyote ambayo nataka uiamini, nilikuwa nakujibu uliposema alete ushahidi, nikasema ushahidi unajumuisha yale mtu alioyaona na hata kuyasikia. Hivyo kumwambia alete ushahidi kuna mawili, ni hujui maana ya ushahidi au kuna aina flan ya ushahidi unaoutaka
 
Kwenye social psychology kuna somo kuwa watu wanaotangulia kuwaambia wengine kwamba ni wapumbavu (kama trump alivyokuwa akiwasema marais waliotangulia) au hawajui kutumia akili zao; huwa ni watu wenye majeraha makubwa sana bongoni mwao na hutaka kila wakati wajionyeshe kuwa wako timamu hata kama hakuna haja ya kufanya hivyo. Matajiri wengi wenye majeraha ubongoni huwa ni watambaji sana hata kama kila mtu anatamabua utajiri wake. Maandiko yako ni ya aina ya watu hao; ama walitelekezwa na wazazi wao wangali wadogo, au wazazi wao walikuwa wanadharau sana wangali watoto, na mambo ya namna hiyo.
Mental constipation coupled with mouth diarrhea.
 
Nimekuwa msaidizi katika moja ya kituo cha kupigia kura katika moja ya wilaya mkoani Mara.

Niliyoyaona ki ukweli yanatisha juu wizi wa kura. Kituo nilichosimamia kilikuwa mwambao wa ziwa Victoria, Tundu Antipas Lissu aliongoza kura katika kituo changu kwa kuapata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyotangazwa Magufuli 37O, Tundu Antipas Lissu kura 6 hii ilitoka na msimamizi msaidizi ngazi ya wilaya kutaka tutoe matokeo yake.

Hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
CDM mnashida sana badala mfufue chama chenu kinachokufa mmenga'ang'ana tu Lisu Lisu

Inamaana basi katika hicho kitongoji chunu mmepsta diwani wa CDM na kama alitangazwa wa CCM basi mmepe huo ushahidi wako huyo mgombea wenu udiwani aende mahakamani

Maana cha kushangaza katika hicho kituo chako haujatutajia matokeo ya udiwani na mmbunge wenu wa CDM umekimbilia kwa Lisu ndio maana mmefeli
 
Nakuunga mkono ilikuwa ni balaa kuna sehemu Magufuli alishinda ndio kwa mfano amepata kula 100 hapo inaongezwa sifuri afisa elimu msaidizi wilaya ya Kaliua unajua ulichokifanya Mungu anawaona kwa kweli
Ingependeza kupata ushuhuda wa aina hii toka sehemu mbalimbali nchini. Kazi ya kukusanya ushahidi kama huu ndipo CHADEMA na ACT - Wazalendo ilipowashinda kazi. Ilijulikana kungali mapema kabisa kuwa huu usingekuwa uchaguzi wa haki na huru, lakini bado hawakujiandaa kukusanya ushahidi usiopingika.
Unao ushahidi?
Tukikutaka utoe ushirikiano upo tayari?
Hapa unamtisha?

Kuna ushahidi zaidi ya kuwaondoa watu wao kwenye vituo vya kupigia kura?
Wewe unataka ushahidi wa namna gani?
 
Nakuunga mkono ilikuwa ni balaa kuna sehemu Magufuli alishinda ndio kwa mfano amepata kula 100 hapo inaongezwa sifuri afisa elimu msaidizi wilaya ya Kaliua unajua ulichokifanya Mungu anawaona kwa kweli
Mkuu 'hito', nikuulize swali:
Hivi kuna sababu zozote zilizowafanya CHADEMA na ACT-Wazalendo kuamini kwamba uchaguzi huu ungekuwa wa HAKI na HURU, hadi wakajiona kwamba hawakuwa na sababu ya kujiandaa kwa kunasa ushahidi wa madudu yote yaliyokuwa wazi kabisa kufanywa ili wasipate ushindi?

Kwa nini, licha ya mizengwe yote waliyokuwa wanafanyiwa, hata kabla ya uchaguzi wwasingeweka mitego ya kujihami na kuzuia haya yasiendelee, na hata kuzuia matokeo huko huko kwenye vituo?

Mbinu alizofanya ni zile zile alizokuwa akizitumia tokea huko nyuma kwenye chaguzi ndogo..., hebu niambie, kuna chaguzi ndogo hata moja waliyowahi kushinda wapinzani kwenye ngwe ya kwanza?
Katumia njia hizo hizo kuwafyekelea mbali wapinzani nchi nzima.

Mtu anajulikana tabia yake, na amekwishakuonyesha wazi kwa vitendo asivyokuwa muungwana, utaanzia wapi kuamini kwamba sasa atakuwa amebadilika wakati wa uchaguzi mkuu?

CHADEMA na ACT-Wazalendo wanastahiri lawama kwa kutochukua tahadhari mapema.
 
Ndiyo; yanaweza kuhojiwa kabla tume haijamtangaza. Siyo sheria nzuri lakini ndivyo ilivyo. Sheria inakataza kuwa akishatangazwa na tume basi hakuna mahakama inayoweza kuyatengua, ila mahakama bado ina mamlaka ya kutengua matokeo hayo kabla tuume haijayatangaza. Ndiyo maana wasimamizi wa uchaguzi huko majimboni walikuwa wanatangaza matokeo ya rais na ya wabunge, kama mtu hakukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Rais kama yalivyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi, basi anaruhusiwa kuyapinga mara moja mahakamani kabla tume haijayathibitisha. na kwa kawaida kukisha nkuwa na shauri mahakani basi tume haiwezi kuoverule na kutangaza matokeo ya rais. Mwanasheria bingwa Lissu alitakiwa ajue hilo; angeweza kuweka pingamizi wa matokeo ya jimbo moja tu na hivyo kuzuia matokeo yote ya uchaguzi wa rais yasitangazwe na tume hadi shauri hilo liamuriwe na mahakama. Ulalamishi ndio mweingi kwenye jamii yetu hii.
Hayo yanawezekana Marekani, na ndiyo kinachoendelea hivi sasa, Kwetu hakuna jaji wa kuthubutu
 
Siamini kuwa kweli alikuwa msimamizi bali namuona kama conspiracist fulani anayejaribu kupose kama mtu aliyekuwa msimamizi! Hajatoa proof yoyote ya kunifanya niamini kama kweli alikuwa msimamizi hasa kwa vile anarudia yale yale ya conspiracy theories zilizoko mitaani leo. Hajui electroral politics na anadhani kuwa uchaguzi ni kupiga kelele majukwaani kuomba kura bila kuelewa kuwa huwa kuna grasroot activtities zinazoendelea baada ya mgombea kusimama jukwaani ili kumobilize wapiga kura.

Ni ndoto ya kipuuzi sana kuamini kuwa CHADEMA isiyokuwa na matawi ingeweza kuendesha grasroot electoral politics hadi wapate kura nyingi kiasi cha kushinda urais. Mnyika na Mbowe ndio walioiua CHADEMA ingawa ni vigumu kukubali ukweli huo; wana akili ndogo sana ya kudhani kuwa politics ni maandamanao na mikutano ya hadhara tu. Leo hii Biden kashinda uchaguzi bila kufanya mikutano ya hadhara ingawa Trump alikuwa anaitisha mikutano ya aina hiyo sita au saba kwa siku. Dr Slaa alipokosa urais mwaka 2010 alianza kujenga grasroots za CHADEMA ambazo zilisaidia sana CHADEMA kupata kura nyingi sana mwaka 2015 lakini leo hii hakuna kitu kilichobaki.

Mkosaji yeyote hupenda kupata faraja kwa kutafuta sababu za kukosa
Kama hakuna grassroots wagombea wote wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji nchi nzima walitoka wapi?
 
Anaweza kusaidia kupatikana kwa ushahidi.
Mkuu hukuona video zinazoonesha mabegi ya kura za rais, wabunge na madiwani?? Ushahidi upi zaidi ya huo? kuzima internet ili watu wasione haya majizi pia. Naamini Mungu yupo kazini anaandaa Radi itakayo tusaidia kuondoa watesi wetu.
 
Ata huku Nansio ni ayo ayo
Nimekuwa msaidizi katika moja ya kituo cha kupigia kura katika moja ya wilaya mkoani Mara.

Niliyoyaona ki ukweli yanatisha juu wizi wa kura. Kituo nilichosimamia kilikuwa mwambao wa ziwa Victoria, Tundu Antipas Lissu aliongoza kura katika kituo changu kwa kuapata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyotangazwa Magufuli 37O, Tundu Antipas Lissu kura 6 hii ilitoka na msimamizi msaidizi ngazi ya wilaya kutaka tutoe matokeo yake.

Hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
Nenda mahakamani ww n mnafiki mkubwa ,,kama ulishuhudia na una ushahidi kwann usiende mahakamani ?sasa hapa Jamii forum ndo kuna mahakama ?
 
Kwa upande wangu nimemshukuru Allah TAL amesalimika,

uko ataieleza dunia ukweli nasi tutayajua mengi ambayo katu hapa hasingeyasema na zaidi maisha yake yangekuwa hatarini mda wote.
Kuna watu hamjui kusoma nyakati! Anguko la Magufuli kupitia uchaguzi huu liko wazi sana! Mungu amemfunua wazi kabisa uwovu wake, hila na dhuruma! Sasa unataka Afanye nini tena cha ziada?

Ujinga, woga, umaskini (fikra, Mawazo) ndo kitanzi chetu, sasa walio tuongoza ktk mapambano wanaikimbia nchi!

Na ukitaka tusubiri Mungu ashuke kwa style yako bila jitihada za Watanzania kuiponya nchi, tutajikuta level ya Zimbabwe ama mbali zaidi!
 
Uchaguzi umeisha wewe hujasikia? Leo ukitueleza upuuzi wako huu unadhani sisi ni UN? Nenda Mahakamani
Huo sio upuuzi, jaribu na jifunze kuheshimu hoja za watu wengine hata kama huwapendi, mataga na ccm mmeiba, kila kona wanasema.
 
Back
Top Bottom