Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Angalia video hiyo niliyoweka mpaka mwisho; yaani lawma ni zile zile kama nilizosikia kutokana na uchaguzi Tanzaniauna video yoyote kura huko Marekani zipo kwenye vikapu na mabegi binafsi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Angalia video hiyo niliyoweka mpaka mwisho; yaani lawma ni zile zile kama nilizosikia kutokana na uchaguzi Tanzaniauna video yoyote kura huko Marekani zipo kwenye vikapu na mabegi binafsi?
Haki ipo kwa Muumba, hapa duniani kilichobakia ni uvumilivu.Haki ya mtu haiwezi kupotea bure
Kituo nilichopigia kura hapa kibaha Lissu alikuwa na 278 Magu 43 matokeo yalobandikwa Lissu 8 magu 377Nimekuwa msaidizi katika moja ya kituo cha kupigia kura katika moja ya wilaya mkoani Mara.
Niliyoyaona ki ukweli yanatisha juu wizi wa kura. Kituo nilichosimamia kilikuwa mwambao wa ziwa Victoria, Tundu Antipas Lissu aliongoza kura katika kituo changu kwa kuapata kura 79 na Magufuli kura 31 lakini matokeo yaliyotangazwa Magufuli 37O, Tundu Antipas Lissu kura 6 hii ilitoka na msimamizi msaidizi ngazi ya wilaya kutaka tutoe matokeo yake.
Hapakuwa na uchaguzi ilikuwa ni ujinga tu.
Aibu Kubwa Sana, alafu wanashangilia ushindi.Kituo nilichopigia kura hapa kibaha Lissu alikuwa na 278 Magu 43 matokeo yalobandikwa Lissu 8 magu 377
Wizi wa kura ulikuwa katika njia NNE nitazielezea zote, haukuwa uchaguzi ilikuwa ni dhuluma tu.Kwa nilivyousoma mchezo walioengineer mchezo mzima from the grassroots ni ARO kata (Afisa utumishi kata) na Mtendaji wa Kata walitakiwa kutoa ahadi kwa mkurugenzi wa halmashauri kuwa watakipa ushindi chama kwa asilimia kadhaa.
So hapo ni yeye sasa achague kutumia polisi, mabalozi, makada wabebe kura za wizi au wasimamizi au vyote kwa pamoja.
Anyway kwa njaa niliyokuwa nayo 355,000 jumla ya malipo imenisaidia ila roho inauma
Hawa wala usiwalaumu, kilichotokea ilikuwa ni agizo kuna baadhi walikataa ila waliibiwa hata wao bila kujua, karatasi za matokeo zilibadilushwa kwa matokeo kutumwa yasio sahihi .Ushahidi kuupata ni simple tu wawaulize walimu wote ndo waliokuwa wasimamizi. Hii kada ya ualimu ina laana kabisa
DuhJinsi wizi wa kura ulivyofanyika.
1.kwa kuingiza karatasi zilizopigwa kura tayari, njia hii ilifanyika sehemu za mijini, kura zilitangulizwa mapema hasubuhi, walioshiriki huu ujinga ni wasimamizi, asikari, na wasimamizi wasaidizi wa ngazi ya kata. Mawakala waliondolewa kwa kigezo kuwa msimamizi anaongea na wasimamizi wa vituo.
2.kwa wasimamizi ngazi za vituo kugeuka kuwa mawakala wa CCM, baada ya kupiga kura vitabu vilivyobaki waliagizwa kupiga kura za CCM na kuingiza ndani ya sanduku, wakala wa upinzani aliletewa zengwe kisha kuondolewa na wizi kufanyika.
3. Kubadili karatasi za matokeo, njia hii ilitumika hasa palipo na mawakala makini , wao walipewa nakala halisi za matokeo kisha matokeo yaliyopelekwa yalikuwa ni tofauti na Yale yalitoka vituoni.
Njia ni nyingi nitaendelea kuzileta hapa jukwaani ili wana jf waelewe dhuluma iliyofanyika.
Ukiwa kama nani? Na hata ukipewa huo ushahidi utaufanyia nini?Unao ushahidi?
Tukikutaka utoe ushirikiano upo tayari?
Usiwape watu matumaini ya uongo, raisi alishatangazwa na kuapishwa, hata mikithibitisha ni kweli aliiba kura hamuwezi kumfanya chochote, matokeo ya uraisi yakishatangazwa hayahojiwi popote kwenye mahakama zetu.Sawa siku nikikuhitaji tafadhali usituangushe.
We tulia, haukufi!!
Na hii ni kwa wale wote wanaodhani wanaweza kuthibitisha, tafadhali muwe tayari.
Jifunze kutumia akili, Trump anatoa madai tu wakati wala hakwepo eneo la tukio, hapa wanazungumza ni hao hao waliokuwa wanasimamia uchaguzi.Ni tabia ya walioshindwa kujenga conspiracy theories; hata Trump ameshindwa uchaguzi wakati akiwa rais, naye anatoa theories kama hizi. Ni jambo la kawaida sana kwa walioshindwa kudai wameibiwa kura. Kama uliyaona kwa nini usipeleke uashahidi mahakamani? Angalu Trump amekuwa anakwenda mahakani ambako anakutana na vigingi, tena wakati mwingine kutoka kwa majaji aliowateua yeye mwenyewe.
Kuiba kura siyo kosa la jinai, na uchaguzi wa rais hauhojiwi mahakamani. Ndio utuambie unaandaa mashtaka gani na dhidi ya nani?Mkuu, kuna mashtaka nayaandaa kuhusu huo wizi wa kura unaolalamikiwa. Je uko tayari kusimama kuzimbani kusaidia kutoa ushahidi?
majina hayanisumbui kabisa; kama yanakusumbua wewe chagua jina zuri. Kichuguu lenyewe siyo jina zuri lakini nimedumu nalio miaka 14 sasa hapa JF, kwa hiyo ukiniita Mpumbavu bado nitaishi nalo tu, kwani jina siyo reflection ya intellect ya mtu.
Unapaswa kujifunza kwanza kabla ya kuwa mbishi.Ushahidi upo wa aina nyingi, ikijumuisha ushaidi wa kuona na hata kusikia. Hivyo ni mawazo potofu kudhania ushahidi ni lazima uwe ni nyaraka, picha, video etc. Mtu kuelezea kile alichokiona ni ushahidi tosha.Basi msilazimishe watu waamini kila lisemwalo, mtu akihoji anavurumishiwa matusi..si kila ushahidi unaowekwa mtandaoni ni ukweli, mtu yoyote anaweza kuzusha chochote.
Kumbe ndio maana Magu na wana CCM wenzie hawana furaha. Watu walifunga kuombea Uchaguzi. Hii kitu haitapita bure, kwa huyu MUNGU tunayemlilia kila siku. Haki ya mtu haipotei, inacheleweshwa tu.
Sasa ulikuwa unakataa nini kwamba hamkuiba kura? Kumbe nchi ilikuwa inaenda kwa 'wahuni' mwaka huu ndio maana mkaamua kuiba kura? Sasa nimekuelewa mkuu[emoji122][emoji1666]. Unadhani huo wizi wenu utaleta manufaa kwa taifa zaidi ya kuchochea chuki na hatimaye kuiingiza nchi kwenye mauaji ya kimbari? Kumbuka hata Rwanda ilianza taratibu kama hivi na hatimaye ikaingia kwenye matatizo makubwa ya kihistoria.
Kwenye social psychology kuna somo kuwa watu wanaotangulia kuwaambia wengine kwamba ni wapumbavu (kama trump alivyokuwa akiwasema marais waliotangulia) au hawajui kutumia akili zao; huwa ni watu wenye majeraha makubwa sana bongoni mwao na hutaka kila wakati wajionyeshe kuwa wako timamu hata kama hakuna haja ya kufanya hivyo. Matajiri wengi wenye majeraha ubongoni huwa ni watambaji sana hata kama kila mtu anatamabua utajiri wake. Maandiko yako ni ya aina ya watu hao; ama walitelekezwa na wazazi wao wangali wadogo, au wazazi wao walikuwa wanadharau sana wangali watoto, na mambo ya namna hiyo.Jifunze kutumia akili, Trump anatoa madai tu wakati wala hakwepo eneo la tukio, hapa wanazungumza ni hao hao waliokuwa wanasimamia uchaguzi.
Usijaribu kudanganya watu kwa mambo ya uongo uongo. Kufungua shauri mahakamani siyo sababu ya matokeo kutokutangazwa.Ndiyo; yanaweza kuhojiwa kabla tume haijamtangaza. Siyo sheria nzuri lakini ndivyo ilivyo. Sheria inakataza kuwa akishatangazwa na tume basi hakuna mahakama inayoweza kuyatengua, ila mahakama bado ina mamlaka ya kutengua matokeo hayo kabla tuume haijayatangaza. Ndiyo maana wasimamizi wa uchaguzi huko majimboni walikuwa wanatangaza matokeo ya rais na ya wabunge, kama mtu hakukubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Rais kama yalivyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi, basi anaruhusiwa kuyapinga mara moja mahakamani kabla tume haijayathibitisha. na kwa kawaida kukisha nkuwa na shauri mahakani basi tume haiwezi kuoverule na kutangaza matokeo ya rais. Mwanasheria bingwa Lissu alitakiwa ajue hilo; angeweza kuweka pingamizi wa matokeo ya jimbo moja tu na hivyo kuzuia matokeo yote ya uchaguzi wa rais yasitangazwe na tume hadi shauri hilo liamuriwe na mahakama. Ulalamishi ndio mweingi kwenye jamii yetu hii.