Uchaguzi 2020 Niliyoyaona kwenye Uchaguzi huu yanatisha

Kwahiyo niamini chochote kwasababu nimesikia kutoka kwako? Lazima mtu uwe na akili ya kuchuja mambo si kila nilimwalo ni kweli. Nashangaa ambavyo unataka niamini ya kwako au ya mtu mwingine lakini ya kwangu hutaki kuyaamini. Mimi silazimoshi uamini ya kwangu na si lazima niamini ya kwako. Tubaki hivyo
 
Alishindwa Lowasa sembuse huyo shoga. Ninyi ni wa kuburuzwa tu na hamna la kufanya. Kila kitu kinabuma, laani ya Dr. Slaa inawatafuna.
Kwani Magufuli amepata hata kura Miloni 3, thubutu!!!!!
 
Mimi sijatoa hoja yoyote ambayo nataka uiamini, nilikuwa nakujibu uliposema alete ushahidi, nikasema ushahidi unajumuisha yale mtu alioyaona na hata kuyasikia. Hivyo kumwambia alete ushahidi kuna mawili, ni hujui maana ya ushahidi au kuna aina flan ya ushahidi unaoutaka
 
Mental constipation coupled with mouth diarrhea.
 
CDM mnashida sana badala mfufue chama chenu kinachokufa mmenga'ang'ana tu Lisu Lisu

Inamaana basi katika hicho kitongoji chunu mmepsta diwani wa CDM na kama alitangazwa wa CCM basi mmepe huo ushahidi wako huyo mgombea wenu udiwani aende mahakamani

Maana cha kushangaza katika hicho kituo chako haujatutajia matokeo ya udiwani na mmbunge wenu wa CDM umekimbilia kwa Lisu ndio maana mmefeli
 
Nakuunga mkono ilikuwa ni balaa kuna sehemu Magufuli alishinda ndio kwa mfano amepata kula 100 hapo inaongezwa sifuri afisa elimu msaidizi wilaya ya Kaliua unajua ulichokifanya Mungu anawaona kwa kweli
Ingependeza kupata ushuhuda wa aina hii toka sehemu mbalimbali nchini. Kazi ya kukusanya ushahidi kama huu ndipo CHADEMA na ACT - Wazalendo ilipowashinda kazi. Ilijulikana kungali mapema kabisa kuwa huu usingekuwa uchaguzi wa haki na huru, lakini bado hawakujiandaa kukusanya ushahidi usiopingika.
Unao ushahidi?
Tukikutaka utoe ushirikiano upo tayari?
Hapa unamtisha?

Kuna ushahidi zaidi ya kuwaondoa watu wao kwenye vituo vya kupigia kura?
Wewe unataka ushahidi wa namna gani?
 
Nakuunga mkono ilikuwa ni balaa kuna sehemu Magufuli alishinda ndio kwa mfano amepata kula 100 hapo inaongezwa sifuri afisa elimu msaidizi wilaya ya Kaliua unajua ulichokifanya Mungu anawaona kwa kweli
Mkuu 'hito', nikuulize swali:
Hivi kuna sababu zozote zilizowafanya CHADEMA na ACT-Wazalendo kuamini kwamba uchaguzi huu ungekuwa wa HAKI na HURU, hadi wakajiona kwamba hawakuwa na sababu ya kujiandaa kwa kunasa ushahidi wa madudu yote yaliyokuwa wazi kabisa kufanywa ili wasipate ushindi?

Kwa nini, licha ya mizengwe yote waliyokuwa wanafanyiwa, hata kabla ya uchaguzi wwasingeweka mitego ya kujihami na kuzuia haya yasiendelee, na hata kuzuia matokeo huko huko kwenye vituo?

Mbinu alizofanya ni zile zile alizokuwa akizitumia tokea huko nyuma kwenye chaguzi ndogo..., hebu niambie, kuna chaguzi ndogo hata moja waliyowahi kushinda wapinzani kwenye ngwe ya kwanza?
Katumia njia hizo hizo kuwafyekelea mbali wapinzani nchi nzima.

Mtu anajulikana tabia yake, na amekwishakuonyesha wazi kwa vitendo asivyokuwa muungwana, utaanzia wapi kuamini kwamba sasa atakuwa amebadilika wakati wa uchaguzi mkuu?

CHADEMA na ACT-Wazalendo wanastahiri lawama kwa kutochukua tahadhari mapema.
 
Hayo yanawezekana Marekani, na ndiyo kinachoendelea hivi sasa, Kwetu hakuna jaji wa kuthubutu
 
Kama hakuna grassroots wagombea wote wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji nchi nzima walitoka wapi?
 
Anaweza kusaidia kupatikana kwa ushahidi.
Mkuu hukuona video zinazoonesha mabegi ya kura za rais, wabunge na madiwani?? Ushahidi upi zaidi ya huo? kuzima internet ili watu wasione haya majizi pia. Naamini Mungu yupo kazini anaandaa Radi itakayo tusaidia kuondoa watesi wetu.
 
Ata huku Nansio ni ayo ayo
Nenda mahakamani ww n mnafiki mkubwa ,,kama ulishuhudia na una ushahidi kwann usiende mahakamani ?sasa hapa Jamii forum ndo kuna mahakama ?
 
Kwa upande wangu nimemshukuru Allah TAL amesalimika,

uko ataieleza dunia ukweli nasi tutayajua mengi ambayo katu hapa hasingeyasema na zaidi maisha yake yangekuwa hatarini mda wote.
 
Uchaguzi umeisha wewe hujasikia? Leo ukitueleza upuuzi wako huu unadhani sisi ni UN? Nenda Mahakamani
Huo sio upuuzi, jaribu na jifunze kuheshimu hoja za watu wengine hata kama huwapendi, mataga na ccm mmeiba, kila kona wanasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…