Niliyoyashuhudia Jeshini

Niliyoyashuhudia Jeshini

Nimekumbuka Oljoro JKT tulikuwa tukijongo Ijumaa tunatokea Unga Ltd na kurudi Jumapili na tunaanzia mahabusu.Mara zingine tunatoroka kwa kutumia magari ya mkaa kupitia Olasiti.Nilikaa kambini kwa mujibu wa sheria miezi 6 ya ukuruta na kuhamia Mgambo kumalizia miezi 6.Maisha mazuri hasa.
 
Sio muoga bali haukuwa interested kabisa na Jeshi na sumu walizokuwa wameshakujaza kitaa ukaona ohoo, na uliyoyakuta huko ndio kabisa ukawa unamuwaza mama tu muda gani atakuja kukuchukua. Inaonekana ilibaki kidogo ujikojolee simu zilipokusanywa, ukajua mawasiliano na bi mkubwa ndio bhasi tena 🤣🤣
Hata mimi sikuwa interested kabisaaa ila nilivyoingia kwenye lile geti nikafungua moyo

Sikuwahi kudoji na hata baada ya muda zilipopatikana chance za kutoka, niliwahi toka one time tu. Nilisubiri hadi siku ifike niondoke

Na wajeda baadhi walikuwa wananiheshimu kwa sababu nilikuwa naenda na mfumo na nilikuwa sio lopolopo. Kuna baadhi walinambia kama naweza jifikiria kuingia ila nilijua haiwezekani..

japo nakumbuka ile siku narudi home baba alishtuka na ndugu yangu mmoja alinisahau kabisaa, sikuwahi pata extra care kama ile siku 😁😁😁
 
Interview huanzia kuanzia siku ya kwanza unaripoti hapo getini ripoti wanaandika huyu tumepokea ni selule yaani mtoto wa mama huyu Jeshi hamna kitu wanaweka na marks zinahifadhiwa.Baadaye kwenye Kila eneo la mafunzo unatizamwa na wafunzi tofauti marks zinahiadhiwa Kwa Siri baadaye Kuna lile zoezi la kulenga shabaha unatizamwa unaangaliwa uwezo wako Kuna hizo ajira wengine huondoka nazo siku ya kufunga mafunzo tu anaambiwa Kwa Siri wewe ukitoka hapa karipoti Jeshi Fulani Nenda na barua hii au ukifika pale jitambulishe wewe Fulani usimwambie mambo mengi faili lako litakuwa limemfikia
Sio kuwa tu kuwa umekanyaga JKT ajira ipo.Perfomance ilikuwaje huko ?
Kumbe.
 
Back
Top Bottom