Inatokea post namba 197.
Safari yetu ya kuelekea DOM ikawa nzuri sana haina pirika wala vituko Dereva akawa anaendelea kunipiga story tu.
Dareva: Waarabu wa Morogoro wana pesa bwana, ule mzigo wao, Halima kanilipa na wao wamenilipa, tena nimewaambia nimeshapewa nauli ya huu mzigo na Halima, wakanambia hio sio nauli, hizo zako, Kafurahi na wewe. Wakanambia siku wakiambiwa mimi ndio naleta mzigo wanafurahi, madereva wengine wanawakata mirungi yao wanaenda kuuza juu kwa juu hio.
Mimi; Mbona wewe unakula?
Dereva; Mimi yangu ananipa Halima, tena toka Sofi yupo pale, ndio alinizowesha, mimi nilikua sili mirungi mshikaji, Sofi kila nikienda ananipa, sema nashukuru siili hii mpaka nipewe pale, sijawahi kununua wala kuwachomolea mirungi yao Waarabu. Mie nimelelewa kwetu mshikaji. Siijui njaa mimi, kwetu masikini lakini hatukosi riziki, tunakula wali na mboga nne mshikaji wangu.
Nikawa nacheka jinsi anavyoongea.
Dereva: Mshikaji wewe kama mimi, hupendi kula kula njiani, mimi bwana nyama nyama sijui kuku, sijui nani kachinja, sili kabisa, tutalishwa vibudu njiani humu.
Hivi hapa kula yangu mimi Dodoma, kwa Sharifu, uhindini au wimpy, na yeye sharifu vile vile, Kule tena nikimkuta al Habib Jamal pale wimpy, silipi kitu, Mwenyewe ananiita Hheikh wake.
Unajua mwenye wimpy Dodoma?
Mimi; Hapana simui, mimi nimehi kupita tu Dodoma, sijuani na watu.
Dereva: basi leo nitakupeleka ukamjue Al Habib Jamal wa wimpy. Mimi nilijuana nae kuna siku walikua wanagawa sadaka, wakaja chuoni kwetu nyumbani, nikawapiga dua ya kadiria pale. Hajanisahau toka siku hio mwanangu. Ananiita Sheikh wangu. Tena unaweza kuwajua wewe, wanasema alikua na wimpy Dar wakaiuza.
Mimi; Labda mzee wangu atawajua, mimi isiwafahamu.
Dereva; Usijali mshikaji, mradi upo na mimi utawajua watu wa maana njia hii. Wananijua mimi kama shilingi.
Nikawa nacheka tu uongeaji wake, haikupita muda tukafika Gairo, akanambia hapa mshikaji hatuingii mjini huko, tutasimama pembeni hapo kuna kituo cha mafuta na kuna sehemu ya chai nzuri tu, ukitaka kula pia, hakuna wasiwasi.
Mimi; Ntamenya nanasi na machungwa nile, sijisikii kula sasa hivi.
Dereva; Mwili wa tizi huo, kula mshikaji usione haya.
Akapaki vizuri kituo cha mafuta, kuna jamaa pale akamwambia, wewe kila ukija hapa nakwambia paki kule pambeni unajifanya huelewi sio?
Dereva; Nasahau mshikaji wangu, hapa najiona nimefika nyumbani, nipo huru.
Yule jamaa akamwambia, hapo nakwambia kwa usalama, wako watakukwangua, madereva wengine walevi.
Dereva: kweli mwanangu acha niiweke pembeni.
Akaiweka gari pembeni akafungua buti nyuma akanambia lete hayo machungwa, kama kumi hivi watatumenyea hapa, leta na manasi mawaili, moja lako moja langu. Mshikaji usiwe na wasi wasi, tutakula martunda tu leo kama tumbiri. Sem mananasi na machungwa tutakojoa sana njiani.
Mimi; Nimeona msikiti pale, wacha nikapige safar kidogo nakiuja sasa hivi sichelewi.
Dreva' Nenda mshikaji wangu dua kwa wingi tu usiwe na wasiwasi. Dua muhimu sana. Mimi nilishaunganisha zangu, ningekuja na wewe. Utanikuta hapo kwenye kiduka hicho, kuna mrembo humo ndani, balaa. Halafu naambiwa kawachwa na mumewe.
Mimi nikaondoka, nikajua huyu hanyamazi sasa hivi. Nikasali nikarudi nikaingia kwenye kimgahawa, dah kweli, nikamkuta mwanamke mzuri kweli sio mchezo. Mshikaji wangu sikumuona.
Yule mwanamke akaniuliza wewe ndio umekuja na yue dereva wa IT?
Mimi; Ndio sister
Alikua anaonesha ana umri mkubwa kwangu lakini bado ni kijana. mara mshikaji akaja, nimetoka mumenya vitu, pale, hawa wakaguru hapa hawajui kumenya machungwa wala mananasi.
Dada; Kwa kujidai huyu, wewe uje na machungwa yako nani akumenyee? Unaleta ujanja wa mitaani hapa?
Dereva; Usinisemee mbovu, ningepajua kwenu ningeshapeleka posa. mtoto mzuri kama wewe unakaa porini huku? Ningekuweka mjini wewe.
Dada; Nipishe huko, nani alikwambia ana shida ya kuolewa? Una maneno ya kijinga jinga.
Dereva: basi poa, nimekuletea zawadi, ngoja nikupe.
Akatoka akaenda kwenye gari akarudi na nanasi moja kubwa na machungwa kwenye bakuli kubwa tu.
Dada; Nilifikiri utalisahau bakuli langu.
Dereva; Sina akili ya kusahau mimi. Ukila nanasi tu hilo, nimelisomea hilo, ujue hunikatai tena.
Dada; tena ndio nalila kwanza hilo, harufu yake tu linaonesha limewiva. sasa weewe unajidai zawadi kumbe kinanasi kimoja tu?
Dereva; Mwanangu, huyu kanielekea mimi, hakuna mwanamke mwenye shukurani duniani isipokua mama yako mzazi tu. Si unamuona huyu mwanamke, mimi nimemuwazia zawadi, nilikua sina sababu ya kusimama hapa zaidi ya kukuletea wewe zawadi, halafu unaiponda zawadi yangu. Na siku ingine.
Dada: Kwani leo hukusimama kwa ajili ya kusali?
Dereva: Mimi nimeshaunganisha sala ya safari, unajua sala ya safari wewe? Nimesimama kwa ajili yako tu.
Dada; Haya ahsante, Mungu akuzidishie.
Dereva; Hayo ndio maneno, twende zetu mshikaji wangu, anaweza kunizuwia huyu nisiondoke hapa, anajidai tu.
Dada; Nipishe huko, nani akuzuwie wewe. Tena usimfundishe uhuni huyo kijana, mwenyewe anaonesha mpole.
Dereva: Mpole? Simba mwenda kimya huyo. Au nimwache yeye mimi nitangulie?
dda: Huyu mwache ahamie hapahapa, patapendeza, sio wewe. Haya kwaherini.
Akaingia ndani. na sisi tukaondoka zetu.
Dereva: mwanangu lazima ujue nituo vya njiani, sio unajisimamia hovyo tu. Usione tabu mwanangu, umenambia wewe fundi, unaweza kufata migari mibovu huku ujue wapi pa kula, wapi pa kupumzika. Hapa kuna wakaguru, wachawi kama nini.
Tukaendelea na safari mapka nje nje ya Dodoma akanambia mshikaji kuna mawili, au tutafute sehemu tulale hapa Doma au tutembee mpaka Singida, unasemaje?
Mimi; Vyovyote vile niko poa tu.
Dereva; usijali mwanangu, tulale hapa, alfajiri tuondoke haina haja ya kukimbizana na barabara usiku.
Tukaenda moja kwa moja mpaka ki gesti kimoja kipo mjini kabisa, gari inaingia mpaka ndani, aliweka gari akanambia mshikaji, Sasa kama kukoga kutawadha ni kila mtu chumbani kwake. Tukutane hapa nje kama nusu saa hivi twende kwa Sharif Jamal, wimpy, tulkale mapema, halafu tuje kupumzika mapema. In shaa Allah alfajiri sana tukijaaliwa tuondoke. Tutasali kwa Gadafi. Kuna msikiti mkubwa mbele hapo unaitwa kwa Gadafi.
Akaingia chumbani kwake na mimi nikaingia chumbani kwangu, ilikua ndio mara ya kwanza kulala gesti namna ile. Kilikua k9i gesti fukani kidogo lakini ksafi. Nikakoga kuna choo ndani, nikagtoika nje. Baada ya muda akaja, tukaondoka tukaenda wimpy, bahati akamkuta rafiki yake anaitwa Jamali, tukaulizana pale, tukala, Jamali akakataa kabisa kupokea pesa, akasema nyie wageni wangu, Huyu Sheikh wangu. Mtakuepo Dodoma?
Dereva: hapana mjomb Jamal. sisi tuombee dua sharofu, alfajiri ytunachoma.
Jamal: Woi safari hii?
Dereva" Mimi kule kule Burundi, huyu mshikaji anaishia Shinyanga.
Jamal": Kuna kaka yangu pale Shinyanga, chukua namba zake, nhgoja nikuandikie, ukiwa na mwenyeji ni vizuri zzaidi. Jamal alikua namwili wa unene na mtu mzima makamo ya mzee wangu akanipa namba, SAkasema mimi nitamoigia na wewe ukifika usiache kwenda kumuona, au mwenyeji wewe Shinyanga. Nikamwambia hapana, mimi nafata gari tu limeharibika huko.
Jamal; Wrewe fundi au unapeka spea, unaonesha bado kijana mdogo sana?
Mimi: Mimi fundi, tuna gereji kwetu, nimekulia gereji.
Jamal; Basi uone kaka yangu anaitwa Ali, maarufu sana Shinyanga.
Mimi; sawa nitampigia nikifika.
Jamali: Mwambie hata huyu mwezako akupeleke kama hana haraka, anapajua nishampa mizigi ya Ali matra nyingi ampelekee.
Dereva; Nitamuonesha Sharifu, siwezi kukuvunja hata siku moja kijukuu cha mtume.
Tukala pale tiukaondoka, tukatembea mwendo kido mpaka kwa gadafi tukakuta wamesha sali isha, sisi tikasali, tukaunganisha jamaa na wengine waliochelewa kama sisi. Tukarudo hoiteli
Ikawa mimi nimekosa usingizi na sijachoka nikatoka nje, niliona shemu kama garden hivi wakat tunaenda na kurudi msikitini, nikaenda pale, kinyaa hakuna mtu kabisa, nikasema ngoja nimwite Arssis. Nikamwita kimya kimya akaja kweli, nikaanz akusikia sauti.
Asis; Vipi hali yako?
Mimi: Salama, sikutegemea kama utakuja.
Arsis; Hakuna neno, sehemu nzuri hii umechagua sema washenzi wanakojoa kojoa hovyo hapa. nenfda pale ulipfikia nje kuna baraza zuri, tutaonea pale. Najua una maswali. Titaonana baadae kidogo.
Nikaondoka pale, kweli nikaanz akusikia harufu ya mikojo, nikarudi hoteli, nikakaa nje pembeni kibarazani, kumwita tu Arsis akaja.
Arsis; Vipi hali? Unaona hapa pazuri, unasemajje?
Mimi: Arsis; leo nilikua naongea na yule jini mwanamke, mboina yeye anakubali ni jini, wewe unasema sio jini?
Arsis: Mimi nimekwambia naweza kua chochoite kile, naweza kua mtu, naweza kua jini, naweza kua mti. Wewe hilo usijali, amini ninachokwambia.
Mimi; Sijui nianzie wapi?
Arsis: Anza popte tu usiwe na wasiwasi.
Mimi; Yule jini wa kike kasema yeye yuko na mimi ananifundisha, ananifundisha nini? Nani kampa hio kazi ya kunifundusha?
Arsis: Mimi nimempa kazi, kuna mengu sana hayajui. Anayoweza yeye atakujulisha asioweza mimi nitakufundisha.
Mimi; Kwanini mimi?
Arsis: haya mambo yanakua kiukoo, ni viapo vua ukoo kabla ya babu yako kuzliwa sisi tuko kwenye ukoo wenu.
Mimi: Unasema sisi, una maana mko wengi?
Arsis: Hapana, mimi niko peke yangu, yule jini wa kike na mamake, ndio wanafanya kazi kwangu, wapo chini ya himaya yangu. Babu yako sijawahi kufanya nae kazi, zema namfahamu sana nimemsaidia mara nyingi. Yeye ruhani wake aliekurithisha ni yule mwenye ile bakora. Mimi ni mkuwaba wao, eote wapo kwenye himaya yangu, kwa hio hawawezi kupinga na mimi. Mi i nasaidia tu mpaka ulipokabidhiwa wewe kwa yule mwenye bakra nikaona ujuzi ulionao usipotee bure, tulikua tunatafuta binadam siku nyingi wa kumfundisha tunayojua. Wewe ndio nimekuchagua nikufundishe.
Mimi; Mbina unasema "sisi" kama mpo wengi halafu unasema uko peke yako, unanishanganya.
Atrsis: Usichanganyikiwe, wotew wanaofanya kazi chini yangu ina maana ni sisi. Mimi kiukoo nipo peke yangu ni tofauti kabisa na jini wa bakora na hawa majini wa kike, Wao wana ukoo wao mkubwa. Bado wewe pia unakoo mwengine, huo sana upande wa mama yako, ukoo wa simba. Lakini na babu yako yupo ukoo huo, sema yeye hapendi mamboi ya uasherati yeye ameshika dini, alifanya mcheo kidogo akafanya toba yeye sasa akita anaoa tu. Unajua babu yako kishaoa, wake wangapi mpaka sasa?
Mimi: Sijamuuiza lakini zee kanambia wengi tu.
Arsis" Mkionana muulize, wengi kwacha lakini kabaaki na wawili unawaju wewe na mmoja humjui.
Mimi; Kwa hio babu sasa anawake wa tatu?
Arsis: ndio, mullize mwenyewe atakwambia.
Mimi; Hii poete ya nini> N yule mwanamke naona inafanana na hii laikini yeye kiti cha duara.
ARSIS: hiyti pete ni zawadi yako, ni ya kwangu mimi, ipo moja tu dunaiani. Kwa ajili ya mawasiliano tu mimi na wewe. na walw wanawake ni mawasiano tulakini vyao ni vito nadhahabu yawaida tuliwatengeneza alipoana kufanyua kazi na mimi, sio siku nyingi sana, walikiua wanafanya kazi na yiule mwenye bakora, sasa kanipa mimi wanisaidie kwa ajili yako. basi hakuna zaidi.
Mimi: nyinyi ni wachawi?
Arsis: Hapana mimi sio mchwawi kabisa, na wale wanawake yule mama yake zamani alikua mchawi miubwa sana, sasa hana yena uchawi, amefanya toba na sasa nimwema kabisa, akiwa mchawi watamuua wenzake. Na huyu mwanae anaekuja sana kwako, hajawahi kua mchawi, sema anajua mambo mebgi ya kichawim kwa sababu anpiugana sana na wachawi katika kazi zake. Anjua mengi yule, usione anaongea na wewe kiupole nihatari sana ytule kwa wachawi, ana jeshi kunbwa sana wanamuogopa yule. Yule anakufundisha na anakulinda. Mradi wewe unaoete hiyo, wewe ndio boss wake sasa.
Mimi: Sasa wewe nani hasa?
Arsis; Mimi nimwalimu tu ninaekufundusha vile utaweza. Hatuwezi kukufunsisha mabaya wala sina mabaya. Wewe hukukabidhwa kwangu, mimi nimekuja kwako mwenyewe. Baada ya kukuchunguza sana, yule jini wa nakora ndio jini umekabidhiwa, miubwa sana yule, usione vile.
Mimi: Naona kwa leo inatosha, maana inabidi niamke alfajiri sna, tunaondoka.
Arsis: Sawa, sema Inshaallah.
Mimi; In shaa Allah. Haya kwaheti Arsis.
Arsis; Kwaheri, siku nyingine mitakufundisha kitu, leo nenda kapumzike.
Nikaingia zangu kulala.
Itaendelea.