Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Labda wameona utaogopa. Mimi sijawahi kuona upepo wakija. Au kipupwe tu hicho?
 
Mm nililetewa mwanamke wa kijini ndotoni na babu zangu waliokufa miaka mingi,Mwanamke alijitambulisha kwa jina la Aisha bint Afrit.Alinipa na pete kabisa nikawa naivaa ila baadaye niliitupa nikaachana naye.Ila ajabu sasa siku moja alikuja ndotoni akaniambia kwamba nilimzalisha nikamtelekeza,aliniletea mtoto aje kunisalimia,alikuwa mtoto wa kike mwenye miaka kama sita hivi mzuri kweli.
 
Naona kataa ndoa kaingia😂😂😂.... Kwahyo huyo jinn sahivi ni single mother 🏃🏃🏃

(Natania...
 
Naona kataa ndoa kaingia😂😂😂.... Kwahyo huyo jinn sahivi ni single mother 🏃🏃🏃

(Natania...
Hapana kiongozi mm haya mambo siyajui kiundani.Maana walikuja babu zangu wanne ila wameshakufa kitambo,na ndani ya hao mababu niliyemtambua ni mmoja tu ambaye ni wajina wangu yaani aliyenirithisha jina,wakiwa wameshika mwanamke mrembo kama mwarabu hivi,wakanikabidhi wao wakasepa,baada ya hapo ndo tukaanza kufahamiana.Yeye alikuwa anakuja ndotoni tunasex sana tu ila kilichokuja kuniudhi ni yeye kutotimiza ahadi yake ya kunikabidhi hazina ya almasi na dhahabu kama alivyoniambia yy ni sex tu,so nikaamua kuitupa na pete aliyonipa ila akaendelea kunifuatilia ila mm nikampotezea tu
 
Hongera sana.

Hao wachawi wanacheza na akili yako.

Nakuahidi, hakuna mwanamke wa kijini mwema atakaefanya hivyo hata siku moja. Usiwajaribu.
 
Itakuwa kweli ni kipupwe 😂😂😂😂😂😂😂

Labda ndo huo uoga....maana pale hata angekatiza panya ningesema ni jinn
(Dah haya mambo yanahitaji roho sana
Endelea kuusoma uzi, utaelewa namna ya kuwaita ili waje kama wapo na kama hawapo watakuja wengine wakueleze ukweli. Ukiwaita hawana sababu ya kujificha.
 
Inatokea post namba 228.

Arsis; Siku ilipofika wakakutana tena, babu yako, Jini bakora na Mzee Mgunya. Baada ya kusalimiana.

Mabruki; Kuna yepi mapya jamani?
Jini Bakora: Mimi nina mapya mengi mazuri tu.

Mzee Mgunya: Anza tu, mimi pia kuna nilioyapata lakini naona ni katika hayohayo yako.
Jini Bakora: Ndio, tulikua tunawasiliana sana na kupanga na majini wako na majini wengine wa Mbruki. Kilichokuwepo sasa ni hiki, kapatikana jini wakuweza kupata chupa aliofungiwa huyo mtu, ni kama tulivyosema sema mwanzo, ipo hapa duniani, inalindwa sana, lakini haimshindi huyo jini kuchukua, kinachomshinda ni kufika tu ilipo, lakini jini wa Mgunya kasema Mzee atatusaidia kwa hilo. Sheikh Mgunya nadhani ni hayo yaliopo kwa sasa.
Mgunya; Na wewe Mabruki sema.
Mabruki; Mimi nimepata habari na mimi katika maongezi ya majini yangu wamesema walikua na nyinyi na kazi yangu itakua ni kuichukua hiyo chupa huku nasoma Qur'an mfululizo, nikisha ichukua niipasue kwa utarartibu wako ili uhai ulio[o ndani usife, kisha vilivyobaki nivivunje na hio chupa na niichome moto. Hakuna jini ataeweza kufanya hivyuo isipokua mimi kama binafdam, kwa kua majini walioiwekea ulinzi na mitego hio chupa hawakulenga binadam walilenga majini wengine wasiwweze kuibeba ilipo.

Jini bakora; Sawa kabisa mabruki, ndio namna hio.
Mgunya; Mimi nimefahamishwa yote na nitakchokifanya nitaivuta ardhi iliopo hio chupa itasogea mpaka tunapopataka, ikionekana tu chupa, iwahiwe haraka sana ndani ya chini ya dakika moja iwe imeshafunguliwa na imeshateketezwa. Lakini jamani, kama kuna binadamu wanahusika watakaputika maana majini waliopewa ulinzi watauliwa wote na majini wenzao na wakubwa hawatakubali, sote tupo mashakani kwa vita kali na majini wa kishetani.
Jini bakora; Hilo nimeongea na wakubwa wengi wa kijini, wamesema watatoa ulinzi kwa kiwangi fulani kwa heshima yetu, lakini kwa bahati nzuri kabisa, kuna jini mmoja mkubwa sana anaejua kisa cha kugfungwa huyo mtu, ni kua akitoka kifungoni ana uwezo wa kuzuia vita na machafuko. Nilipomuuliza kivipi? Akasema atasema mwenye akifunguliwa, mimi siwezi kumsemea, kwa sababu anaweza kua hana tena hizo nguvu.
Jini bakora: umesikia Mabruki, kunamawili tumfungue atoke bila kufahamu uwezo wake aliokua nao kabla ya kufungiwa kama anao tena, na kuomba Mwenyezi Mungu kua atakua sio msaliti. Sababu zake za kufungwa ni wema wake sio usaliti wake. Najua unataka kuuliza kwanini alifungwa, mimi sifahamu, kama hatodhurika ataeleza yeye mwenyewe.

Kwa upande wangu naona kazi ifanyike mapangoni kwetu, mabruki unajua vizuri, lakini wewe Mabruki ukachukue ile sehemu inyozunguka mapango haraka sana ili mapango yawe kwenye himaya yako. Pale hakuna mwenyewe ila kuna wenyeji wawili watatu kwa mbali kidogo, wamehamia tu, sio watu wa asili ya pale, watu wa asili ya pale. pale hakai mtu sisi hatuhusu, binadam wanafanya fujo sana.

Mabruki; Hilo halina tabvu, tena ile sehemu niliipenda, kila navyokuja mapangoni naitamani sana.

Jini: haya fanya hivyo, ukija niiute tukaweke mipaka, halafu fanya karatasi za shamba ziwe zako na wale wote hamisha pale ndani ya mipaka yako, wake nje. Hakuna tabu, wale hawapo pale muda mrefu, hawana makaburi pale, sisi tiuytakuonesha mipaka.
Mgunya: Mikiwa tayari mimi nipo tayari wakati wowote.

mabruki; Mimi nitakuja Jumapili ijayo niangalie mipaka, nigtakuja na mwanangu.
Jini bakora: usije na mtu yoyote, hii vita kubwa, usihatarishe maisha ya mtu mwingine. Ile ile mwenyeji itakusaidia wewe. Chukua chokaa mingi, ile taweka alama, halafu sisi takufahamisha ufunge vipi mipaka.
Mgunya: hta mimi nitakupa ujuzi wa kugfiunhga mipaka niujuao.
Jini bakora: haya, takua na ulinzi aina ya mipaka. fanya bidii sana.


Arsis; basi ikawa kama walivyppanga, Babu yako akaemnda akaweka mipaka, akaambiwa awe anakwenda kupanda migti ya kudumu kwenye mpaka, akapewa na migti mingine anaayoijua Jini Bakora. Yyule ni mataalamu sana wa miti na tiba zake zote ni za miti, majani, mizizi n vitu kama hivyo.


Wakati SArsis anaendelea kuongea tukasikia adhana ya alfajiri kwa mabli, nikamwabia kumbe tumekaa sana.

Arsis; Washa gari yako nenda kasali ukimaliza rudi hapa, leo mpaka tumalize hii habari, maana unasema mimi napiga chenga.

Mimi: Arsis, wacha niende tukutane tena usiku, mimi leo nalala tu, sijategemea kama tutafika mpaka saaa hizi.
Arsis: Siku nyingine usiseme mimi nakupiga chenga. Haya kwa heri usiku ikiniita mimi nitakuja.

Tukaagana nikaondoka zangu.


Itaendelea.
 
Ngoja niweke kituo.
 
Inatokea post namba 294.


usiku kama nilivyoahidi kama saa 4 hivi nikaenda viwanja vya kukutana na Arsis, nilipomwita hajachelew akaja.

Arsis; Vipi hali yako Simba?
Mimi; salama, Arsis.
Arsis; Tuendelee. Simab ndio baba yakao akaenda pale mapoangoni akamwita Jini Balra, wakatoka wakaenda kuweka alama ya shamba, wamemaliza siku nzima ya kwanza hawakumaliza, wakafanya ile kazi wiki mzima. Ilikua pori kubwa sana, wanyama wengi, nyoka wengi, tena wewe unapenda pale kwenye mto ule mdogo, pale kuna chatu wakubwa sana, bahati mzuri Jini Bakora ameweka jini inakimbiza ile kila akija. Majani yale ya nyasi ya kule kwenu, manyoezekea yalikua mengi sana, Bahati mzuri walichukua wale wenyeji wanakaa pale karibu karibu wakawasaidia sana, na kundi kubwa ya majini ya Jini Bakora yamesaidia sana kusafisha njia.

Alipomaliza baba yako akaenda kumueleza Mzee Mgunya, wakapanga siku wakaja baba yako na mzee Mgunya mpaka kwenye mapango yale uliolala wewe, wakafanya mkutano wao iakapangwa siku waje pale ndani kugfanya kazi.

Siku ilipofika Mzee Mgunya akasoma vitabu vyake, babu yako amesshapewa njia zote za kufanya, amepewa na kisu cha kukatia lakiri ya ile chupa akaelekezwa akiiona imefika mbele yake, asiogope kitu chochote atachokiona, achukue chupoa akate lakiri, kitu chochote kitakachotoka kwenye chupa asiogope wala asikisemeshe, kikitoka tu ye avunje chupa aikate lakiri na kisu, aifungue akisha ifungua, kuna mawe ya kuvunjia chupa alipewa, alipewa na miti minne aigongelee chini kama mita kila mti kwa pembe nne, kabla ya kuwasha moto. Pale ndani ya miti ndio awashe moto, akiipata chupa akisha ifungua aivunjie chupa pale ndani na atupie pale kwenye moto. Zikaletwa kwanza nyasi nyingi sanaz ikawekwa pembeni zikaletwa kuni nyingi zikawashwa kwanza kuni, ukikolea moto, ndio Mgunya aanze kazi ya kuivuta ardhi kwa elimu yake.

Basi walipowasha moto wa kuni, haikuchukua muda Mgunya akaanza kazi yake, chupa ikaonekana, babu yako akaiona, ilikua imezungukwa na vitu vitu vya kutisha lakini shjaaa yule hakuogopa kabisa na Qur'an aliokua anasoma vile vitu havikuweza kumsogelea, hakupoteza muda akafanya kama alivyoelekezwa huku anaendelea kusoma, akifungua chupa, akaivunjia mule ndani ya moto akaongeza nyasi na juu ya nyasi akaweka magogo ya kuni akjaza nyasi juu yake, Mgunya akamwabia sasa mimi nakwenda zangu, kazi imekwisha. Wewe ondoka hapa, moshi mwingi, kaa nje pale mchangani usiwe na wasi wasi endelea kusoma Qur'an baadae atakuja jini Bakora atakupa maelkezo. Babu akauliza mbona sikuona kitu kilichotoka? Mgunya akacheka akatoka nje. babu yako kutoka nje hamuoni Mgunya, kisha ondoka haonekani hata njia aliopitia. Basi babu yako akakaa pale nje akawa ansoma Qur'an, akasoma pale kama masaa mawili au zaidi kidogo ndio Jini Bakora akaja.


Itaendelea.
 
Inatokea namba 298.


Arsis: Jini bakora akmsalimia babu yako, wakaanza kungea.
Jini Bakora; Mbaruki, wewe mzima heikh?
Mabruki; Mimi mzima sana, mbona hajamtoka mtu?
Jini Bakora: Akacheka akamwambia tumedfanikiwa lakini hayafai kuongelwa sasa hivi. wewe irabidi uendelee kusoma hapa, alfajiri ikiingia ukisha sali uondoke zako, Tutakutana mjini, ukifika salama huko, uniite. Nenda moja kwa moja kwa Mgunya.

Jini Bakora akaondoka bila kuaga, Mabruki akakaa pale hakuwea kulala, hauku[ita ikaingia alfajiri, akasali, akaondoka. Akafika salama mjini Jioni kabisa, zamani gari sio nyingo kam sasa lakini alipta gari.

Arsis: Babu yako akafika kwa Mgunya akamkuta, alipomuona akacheka sana, nbasikia kulikua na hatari huko?
Mabruki: S; tulikua pamoja unaondoka, umefika salama usiku ule?
Mgunya; Mabruki hukua na mimi kule, binadam ulikua peke yako, yule alikua jini kachukua umbo langu, jini mubwa sana yule, kazi yake ilipoishia na kuona kuna usalama akaondoka zake. Lakini habari zote ninazo, nihadithie na wewe kwa muono wako.
Mabruki: Mimi zina ziaidi nilifanya kama nilivyotakiwa kufanya, sikuona mtu akitoka kwenye chupa , lakini nimeivunja vunja nikatia kwenye moto, moto na magogo yale nadhani unawaka mpaka saa hizi.

Mgunya; Ule utawka siku tatu, maana kwanza 8utakua mkaa, mkaa utaungua taratibu mpaka litabaki jivu tu. akwanza ngoja tufuturu, mie nimefunga leo, tukimaliza baada ya Ishaa tutamwita Bakora aje. Wewe mabruki kurudi kwako nyumbani itakua sio leo, mpaka moto uishe kule pangoni. Tutapata habari kwa hio utakua mgani wangu hapa, usiwe na wasi wasi.
Mabruki; Hakuna tabu.


Wakamaliza mambo yao baada ya Ishaa wakamwita Jini bakot)ra akaja.

Mgunya; hanbari zahuko Sheikh?
Jini Bakora; Njema sana, kazi yetu imefanikiwa, tuliemtarajia tunae huko, tumemwekea ulinzi mkali ingawa hauhitaji ni mtu wa elimu kubwa sana, lakini mwenyewe kaamua awe kule anafanya mambo yake kwa muda fulani. Kwa hio nawapa homnngera sna.
Mgunya: Haya; cha mdsingi umemuuliza kuhusu hicho kitabu? maana ndio msingi wa hatari yote hii.
Jini Bakora; Tena ni hatari kweli, bado tupo kwenye harari sote, lakini tuwe na amani mambo yamedhibitiwa vizuri, Mbaruki hapa ndio asoiwache kusoma Qur'an mpaka hili wimbi la hatari liondoke ake. Majini wamekasirika sana, sema tuna bahati kubwa sana.
Mgunya: Ipi hio?
Jini Bakora: Yule bwana kumbe alikua ni mlinza wa lango la kuendea dunia zingine kwa upoande wa huku kwetu duniani, kwa hio kalifunga lango wa kule yupo kule wa huku yupo huku, hakuna jini atakuja kutoka dunia yao akaingia huku bila yule bwana kufungua lango lake. na yeye kasema mpaka aingie nao mkataba ndio atafungua. Lakini hio itachukua muda kutokea, vikao vitafanywa na jaumu nyingoine kavbisa, sio ya kijini wala ya lkkibinadam.
Mgunya: nani tena hao? malaika?
JiniBakota; Tuishie hapo, nimeshayasema memngi ambayo nimeapishwa nisiyaseme, yasinikute mengine tena. Atayasema mwenyewe yule bwana akiwa tayari.
Mgunya; Sawa, nimeelewa.
Mbaruki: kwanini mimi sikumuona?
Jini Bakora; Alifanya vie kwa usalama wake lakini ataongea na wewe, anakushukuru sana tena sana, bila wewe hili zoezi lisingefanyika, hakuna kitu kigumu na cha hatari kama kuifungua ile lakiri ya chupa. Pale ndipo penye kazi kubwa kuliko zote. Kwa hio Mbaruki hgoimgera sana, una rafiki pya na anatoa shukran zake na kasem yeye atakutembelea ataongea na wewee kwa nia mbili lakini hautomuona kwa sasa, mpaka mambo atakapoona yanfaa sasa ajitokeze. hata majini hatumuoni yuke mtu, mimi nimeongea nae tukafanyiana vipimi vua kuhakikisha yupo kweli, yupo kweli na akitaka kuonekana ataonekana, lakini kwa sas tumpe muda ajiweke sawa. Kuhusu vitabu vipo, kasema tusiwe na wasi wasi atamueleza Mbaruki cha kufanya. Anajua jinsi ya kumpta Mbruki, jna usiku kamuona, asiwe na wasi wasi, salaam zake kwa Mabruki ni kua sasa ana rafiki mpya na salaam zako Mzee Mgunya anasema yupo tayari kwa kazi yoyote utakoyitaka kwake lakini hawezi kua na mba)waba waeili, kwa hio utampta kupitia kwa Mbaruki aliekata lakiri.
Mgunya; Nimemuelewa sana, Mabruki akishatulizana na kurudi kwake tutakua na mengi ya kujadilki mimi na yeye.

Bakora; Niliona nije kuwapa huo ujumbe, moto uke tutauacha siku tatu, yaani leo ni moja, kesho ni bili, kesho kutwa tatu, baada yahapo mabruki unawea kurudi kwako nakufanya mabo yako upendavyo. Usifanye ubishi, ni katika kulinda usalama tu.

Mabruki; Sawa, itabidi Mgunya unipe chumba nimuagize mke wangu aje, sijazoea kulala peke yangu.
Mgunya; Tena sasa hivi tumtume mke wangu waende arudi nae. Nilitaka kusema hili, vipi utakaa peke yako siku tatu kwenye mji wako?

Arsis: Wakafanya hivyo na ndio kisa changu cha kuanza kujuana na babu yako. nafahamu una maswali mengi sana ya kuniuliza, utaniuliza taratibu taratibu hautoyamaliza, kila nikukujibu moja liytazaq mengine kumi na moja. Umenielewa Simba?

Mimi; Nimekuelewa Arsis, kweli nina maswali mengi ya jukuuliza lakini yarasubiri, hayana hatraka.


Natumai wasomaji wangu mmeelewa vipi Arsis alionana na babu yangu. Mnaweza kuuliza chochote kinachohusiana na huu mkasa, kwa sababu baada ya hapo nikawa nauliza kidogokidgo kwa Arsis kwa muda mrefu sana, nimengi sana.

Hayo ni kwa mujibu wa Arsis lakini niliongea na babu yangu baada ya kuyajua hayo kwa Arsis, nae alikua na yake alionieleza, nayo nitayaleta kama nilivyoongea na babu yangu.

Itaendelea.
 
Stori Nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…