- Thread starter
- #301
Inatokea post namba 299.
Baada ya kuhadithiwa hayo na Arsis nikawa na hamu kubwa sana ya kumsikia babu yangu atanieleza nini kuhusu tukio hilo lililowakutanisha na Arsis. Nikaweka nia ya kufunga safari kwenda Duga kwa babu.
Ikapita muda, ikawa kuna msimu mdogo wa Kamba, nikamwambia wife kuhusu kwenda kwa babu, akanambia kule nenda tu mume wangu, mzee si anakwenda, fatana nae. Nikamwambia ndio nilikua namtaimu niende nae. Mke wangu akaniuliza umeshamwambia, si unamjua mzee? Anaweza kuondoka akapiga simu yuko Tanga. Nikaona ni kweli, nikampigia simu mzee muda huo huo.
Mzee akanambia msimu haukai, nilikua nafikiria leo niende. Nikamwambia mzee muda sasa hivi umekwenda, na mimi nataka kwenda twende wote Alfajiri, akanambia itakua vizuri nimepata kampani.
Mke wangu akanambia, si umeona usingemwambia asubuhi ungemsikia kwenye bomba tu, msimu akae hapa, kwani ana wazimu?
Nikamuuliza mke wangu, kwanini wewe na mama hampendi kwenda msimu wa kamba na kuna pesa za nje nje? Mke wangu akanambia tatizo kutwa nyie mnavuna kamba, watu wote wanavuna kamba, tunakua pekeetu nyumbani, mpaka jioni, saa zingine mpaka usiku. Nikamwambia twende tutakua tunakwenda kuvuna wote kamba. Akagoma kabisa. Akasema, wewe kawalete tu mimi nitakupikia, kwenda kuchomwa chomwa na ile miba yao, sikuwezi kabisa.
Tukaondoka na mzee, kama kawaoida kituo chake cha kwanza Chalinze, tukamkuta Halima, mimi kishanizowea sana lakini hajawahi kuniona na mzee pamoja. Alivyoniona nae siku hio, akaanza.
Halima; Nilijua tu utakuja nae, ingawa jana hukunambia kwenye simu, ulijifanya kama unapita peke yako. kahawa nishakuwekea kwenye chupa, hii kunyweni hapa. Handsome na wewe kopo lako la visheti lipo tayari;
Mzee; na mimi visheti vyangu vipo tayri, unakumbuka nilikuagiza jana?
Halima; Vipo, nikusahau wewe tena?
Mzee tuna haraka leo, toa tuondoke.
Halima; handsome usinisahau kamba, wale sijui bibi yako anawakausha vipi, si ulinambia unakaushiwa na bibi yako? maana mimi nilikua najua uduvi tu wa kukausha kumbe hata wale wakubwa bibi yako anawakausha. baba yako kupita kote hapa huwa ananipa kamba wabichi tu.
Mimi: Wale huwa sio mzigo wake ule, wale bibi anawapack anpelekewa mama nyumbani. Mimi nilimwabia aniwekee pembeni wangu, tofauti na wa nyumbani, ndio maana safari iliopita ukawapata.
Halima akatoa visheti vyetu akatupa, tukaondoka zetu.
Tanga hatukukaa, mzee akapita kwa bibi yangu mzaa mama, tukawasalimia alikua na mizogo yao, mimi nikampa noti mbili tatu, akafurahi, dua nyingi, tukaondoka zetu.
Tukafika Duga mapema tu. Tukamkuta babu yupo bize na wateja wake, anawauzia kamba kwa mizani, walikua wanapima kamba kwake. Wengi wengi tu. baada ya kusalimiana, mzee akasema mimi nashuka nakwenda kuvuna huko, akachukua vina pale, anakingia stoo akachukua nyavu zake za mkono, akashuka chini huko. Mimisafari yangu ilikua kwa babu na bibi tu, sikua kabisa kwenye mpango wa kuuza kamba.
Mimi; Babu huu, mguu wako huu, sio wa kamba.
Babu; Sema bwana mkubwa.
Mimi; Sio saa hizi tukisha sali usiku, nataka kuongea na wewe peke yako.
Babu; aknambia sawa bwna mkuba, tutaongea usiwe na shaka.
a
Nikamtafuta bibi nikampata yupo bize kweli kweli na kamba, Baada ya kusalimiana akanambia...
Bibi; Mie toka asubuhi nipo mavunoni huko, tunahofia bamvua, likija linaondoka nao wote.
Mimi; mnalitegemea mapema safari hii?
Bibi; ndio wakati wake huu, maji yashaanza kupanda b, , aharini, lakini tumewahi kuvuna wengi tu, si unajua huu msimu mdogo.
Bibi huyo akachomoka huku ananambia, chakula chenu kipo nenda ukale, babu yako kishakula, babako yuko chini huko, usimngoje kula, anavuna.
Basi ikawa mambo ndio hayo ya shamba. Nikaingia kula mimi, kama kawaida, bibi chakula chake kitamu, anajua kupika.
Usiku baada ya kusali, babu akanitazama akanambi twebda hapo nje babu, kahawa tutainywea nje. Tukatoka, akanambia babu maongezi maerefu au mafupi? maana kama maregfu kidogo twende pale kilingeni, haji mtu, hapa sasa hivi watajazana. Nikamwabia tushule pale babu. Tukashuka kilingeni kwake.
Babu; kwanza nipe habari za mjini.
Mimi; Kwema babu, mjini wewe unayajua mambo yake kuliko mimi, labda unipe wewe mambo ya mjini.
Babu akacheka, unaendeleaje na kazi zako?
Mimi: Babu siku hizi nazimudu sana, hata mzee akiondoka sina wasi wasi kazini, nafanya mwenyewe kazi zote.
Babu: Vizuri sana, haya nambie babu.
Mimi: babu mimi sina mengi sana, mimi nina maswali mawili matatu, kuhusu wewe na rafiki yako Arsis.
babu akacheka sana.
Babu; Kakwambia uniulize mimi? Yule kuna swali linamshinda kujibu?
Mimi: Sio hivyo babu, mimi nilimuuliza mlivyofahamiana, akanielezea kwa upande wake, sasa nataka kujua kwa upoande wako.
Babu: Sawa bwana mkibwa ulia unachotaka kujua maana kisa ni kirefu sana.
Mimi: babu, nataka unieleze ulipoivunja chupa pngoni uliona nini?
Babu: mambo makubwa sana bwana mkubwa, kwani Ramsis hajakwambia?
Mimi; Kanambia yake mimi nataka kusikia yako.
Uzuri wa babu alikua ana namna fulani ya kuongea amabyo hutaki awache kuongea, hajui kukasirishwa na swali.
Babu; Siku ile Bwana mkubwa, niliona mabo ambayo nao,mba nisiyaone tena na namshukuru Menyezi Mungu kunitoa uoga, maana nikiyakumbuka huwa naogopa mpaka leo. Babu nilipewwa kisu kikali halafu kigumu hicho, niliambiwa hicho hara chuma naweza kukatia kwa kukigonga na hakiweki meno. Kipo hicho kisu mpaka leo, sina pa kukitumia, kili[potea siku ile lakini huyu Ramsis kupitia Jini Bakra wakajulisha kiko wapi, Jini Bakora akaniletea.
Babu; Hicho kisu nilipewa kazi yake ilikua moja tu, kukata seal ya chupa, ilikua inaonesha ni ngumu kweli lakini kile kisu kiliikata mpaka mimi nikawa naona raha. babu mambo yalilkua kabla sijaikata hio lakiri, babu kma umewahi kuwaona ma dragon wale wanatoa moto kinywani, basi walikua watatu mmoja wa kijani kulia ya chupa mkubwa ajabu, kafungua mdomo unatia moto, moto sauiti yake inatisha unafika mpaka karibu ya chupa, kulia ya chupa kuna mnyama mbwa si mbwa mkubwa kuliko simba, ana miguu sita na yeye anatoa moto mdomoni. Juu ya chupaa kuna joka lina vichwa vitatu, joka kubwa kweli linaning'ginia saw nachupa, kidogo nikimbie, ikanijia sauti huku nasoma Qur'an inanambia wahi fanya kilichokuleta hawana ujanja mbele ya Qur'an, basi babu nikaibeba, nikafanya kama naichinja ile chupa, ikakatika lakini na mfuniko wake, sikuona kilixhotaka, wale wanyama sasa wananikaribia mimi kila upande, kuna mawe nilipewa ndio ya kuivunjia ile chupa, nikaivunja nikaitupia kwenye moto, babu kulikua na moto mpaka mimi ulikuwa unaniwivisha naona ule moto ndio salama yangu pia ile midudu ilikua hainifikii, maana kila ikinisogelea ule moto kama unapanda kuwachoma, moto wao hakufua dafu, walikua wakubwa sana babu. Baada kuitupa ile chupa na kisu kikawa kimeniponyoka na chenyewe kikaingia kwenye moto. Nikarushwa huko babu sijui na nini, bahati sijapigizwa kwenye pango, nimeangukia chini kama futi kumi kutoka ule moto, kuna kichanga pale, si unalijua lile pango kichanga chake, nikafikia hapo.
Muda wote huo sikuacha kusoma Qur'an. Kuna Jini moja tulikua nalo pale, limejigeuza kama Mzee mmoja alikua Sheikh Wakigunya, alikuwa maarufu sana huyo mzee kwa elimu, Mwenyemungu amrehemu, hajakaa sana baada ya ile kazi, akatangulia mbele ya haki, wanawe wapo Tanga, wengine wametawanyika. Tunajuana sana, lakini hicho kisa sidhani kama wanakijua maana babu hii ilikua siri kubwa, wewe ingekua Ranses hajakuhadithia mimi nisingekuelezea, ulivyonambia, kakuhadithia nikapata na meseji, ndio nafunguka babu. Hakuna ajuae hicho kisa mpaka leo hii, ni mimi, wewe sasa Bwana mkubwa, jini bakora na Ramses. kama wengine wanajua anajua Mwenyezi Mungu babu.
Babu yangu alikua anamwita Ramses, kuna siku nilimuuliza, mbona mimi najua anaitwa Arsis, kwanini Babu unamwita Ramses? Babu akanambia, ndio hao hao babu. Haina shida.
Mimi; babu ikawaje baada ya hapo?
Babu; twende tukale kwanza babu, tutaongea tukisha kula, babako na watu pengine wanatungoja sisi kula.
Itaendelea.