1. Mahojiano na Arsis
Yafuatayo ni mahojianao yangu (nitajiita simba kuanzia sasa) ambayo sio ya kwanza kati yangu na Arsis, lakini nimwyaweka namba 1 kwa kua nahisi yataleta mpangilio mzuri wa mahojiano yatakayofatia.
Mimi; Arsis, Arsis, Arsis, upooo?
Baada ya kumwita ikapita kama nusu dakika hivi.
Arsis; Nipo Simba, vipi hali yako?
Mimi; Mimi mzima kabisa na wewe?
Arsis; Mimi nipo salama namshukuru Muumba wetu.
Mimi; Arsis, leo nina swali moja tu, nataka nikuulize utakaponijibu ndio naweza kua na maswali mengine.
Arsis; Uliza Simba.
Mimi; Arsis kuna siku nilikuuliza wewe umejuana vipi na Babu yangu, nikahisi kama kuna vitu umenificha hukunieleza vyote. Ulinielezq umefahamu kupitia Jini wa bakora, nikahisi umenip9ga [piga chenga. Leo nieleze bila chenga, tumeshakua marafiki muda sasa.
Kabla ya kujibu Arsis akacheka kma mtu aliyefurahi. Naomba kusisitiza hapa, Arsis ni kiumbe mmoja ambae ukiongea nae utaona raha sana, hacheki kwa majivuno au kwa kebehi, unamhisi anacheka kwa kua anacheka kweli.
Arsis; Sikiliza, leo umenifutrahisha sana, nilikua nanhgoja siku uwe serious kama leo ili unielewe vizuri. Nilikiua nakuhisi kama ninayokwambia yanakuingia na kutoka. Nisikilize kwa makini.
Simba, mimi nilikua kifungoni kwa miaka zaidi ya 900, mndio ni 925 alaiejitahidi mpaka nikafunguliwa kifungojni ni babu yako kupitia jini wa bakora. Simba nataka uelewe, jini wa bakora ni jini mwenye heshima sana katika majini. Nafahamu kua ukoo wake walikua na uhusiano na ukoo wa babu yako, yaani ukoo wako kwa baba yako kwa muda mrefu sana., karne nyingi sana, vizazi na vizazi, lakini ni wachache sana katika ukoo wenu siku za nyuma wakaweza kukabidhiwa bakora kama uliopewa wewe. Wote wengine waliopewa bakora au wanapewa bakora za ukoo tu, lakini babu yako alipewa bakora kutoka kwa mwenyewe jini bakora, lakini liitengeza, sio ya kurithi. Bakora ya jini bakora ya kurithi kwa wazeewake ni ile uliopewa wewe tu. Ile bakora kuwepo tu kwako ni kinga kubwa na heshima kubwa sana kutoka kwa majini wote watakao kuona nayo. Nakushangaa wewe umeifungia chumbani.
Miimi; Nimeiweka Arsis, siwezi kutoka na kutembea nayo kila mahali.
Arsis; Nafahamu hilo na Jini bakora anafahamu hilo, dunia ya siku hizi hambebi bakora kama zamani, ni watu na makabila machache sana yenye kujua thamni ya mwanamme kubeba bakora. Mimi nakwambia jizoeshe kua nayo katribu zaidi ile bakora. Usiwe na wasi wasi, Jini bakora hasikii haya maongezi yetu wala hawezi kusogea hapa kusikiliza tunachoongea, tunaheshimiana sana.
Mimi; Arsis; Unaanza kunipiga chenga tena? Hujajibu swali langu.
Arsis; Tafadhali tumia lugha nzuri ukiongea na mimi, kqnza mimi ni mtu mazima sana kwako kwa kiwango chochote kile, halafu mimi ni Mwalimu wako. Acha lugha hizo mitaani. Sikupigi chenga, nipo katika kukujibu swali lako lakini nataka uelewe kwa undani zaisi, fanya dsubira.
Mimi; Samahani, unajua lugha zetu za siku hizi, Nitakua mwangalifu.
Arsis; Usijali Simba. Nisikilize kwa makini. Babu yako alikutana na watu kutoka Pemba wakati anaishi Tanga, hao watu walikuja kutafuta mali za Mjetrumani, miaka mingi sana nyuma.
Mimi: Hujui mwaka gani?
Arsis; Najua ilikuwa mwaka gani, ni mwaka wa 1072 kwa miaka ya dunia ya kwanza, hii dunia tuliopo. Hawa watu, alikua ni kijana mmoja ambae alihadithiwa na babu yake kabla hajafa, kua Tanga, nje kidogo ya mji kuna mali ya Wajerumani imefukiwa. Babu yake alimwabia na yeye kahadithiwa na rafiki yake ambae ameshfariki, lakini ameandika jina ya hio sehemu na alama zilizowekwa. Aliambiwa kua asijaribu kwenda boila kutafuta mwenye nguvu za majini na mwenyeji wa Tanga. Bila hivyo itakua ni hatari sana. Ataekwenda tu bila ulinzi wa nguvu za majini anaweza kufa.
Huyo kijana ndio akaanza kutafuta mtu mwenye nguvu hizo kwao Pemba, wapemba kila akiwaambia au wengine wanadhatrau hio habari au wengine wanaogopa. Ukapata mtu mmoja akamwabia kuna mama wa Kipenda yupo Darisalam, anajua kua huyo mama ana majini wakubwa anawatumia kwa kuondoa matatizo ya watu. Ndio kafunga safari akaja Mjini Dar. Akafanikiwa kumuona huyo mama, huyo mama kweli alikua na majini wakubwa sana na anapandisha kichwanikwake. Walipokuja wale majini wakasema sisi hatujui kuhusu hizo mali lakini kuna mganga mmoja yupo Tanga, huyo mganga ni mtu wa Lamu, Mgunya lakini anaishi Tanga, yeye ana majini wakubwa wa kutokea Tanga wanaweza kujua Yule jini wa mama akawapa anuani mpaka mtaa watakapompata huyo mganga wa kigunya, alikua barabara ya tisa, karibusana na sokoni pale Tanga.
Yule mama wa Kipemba hafanyi ile kazi yake peke yake, yeye anapandisha jini lakini mtu anaetafsiri na lazima anakua karibu yake ni mume wake. Yule mume akasikia kisa chote kile akawa na yeye kapata tamaa ya mali.
Mimi; Arsis kumbe ni mtu wa mikasa mingi wewe.
Arsis; Leo umesikia mali ndio unasikiliza kwa makini? Subiri nimalize, usije kusema nakupiga chenga, nyamaza usikilize mpaka nimalize, usitie neno lako.
Mimi; sawa Arsis, mbona leo unakua mkali hivi?
Arsis; Umeuliza kitu ambacho inabidi nikueleze kwa yundani, vipi nimejuana na babu yako, au hutaki tena kujua?Nyamaza. usijibu.
Nikanyamaza kimya.
Arsis; Leo huondoki hapa mpaka nimalize kukufahamisha.
Basi yule mume na ytule kijana wakahangaika kufanya safari ya kuja Tanga kwa mganaga wa Kigunya, alikua hodari sana wa kusoma vitabu huyo mganga, mtu mzima sana, lakini alikua anajulikana sana kwa kutibu watu na alikua anaweza kuita majini wakubw wakubwa sana. Alikua na maarifa mingi sana.
Baada ya muda, wakafanikiwa kuja Tanga, wakakutana na yule Mzee wa Kigunya wakamueleza ile habari. Yule mzee akawasikiliza kawaambia basi nyinyi kaeni hapa kwangu wakati mimi nafanya uchunguzi wa hiyo habari. Watu wengi wanakuja kuuliza habari za mali za Wajerumani, na wanakwenda kuhangaika san, hakuna alierudi kwangu akanambia kama kafanikiwa au hajafanikiwa, lakini inasemekana zipo, wapi mimi sijui, Kwa sababu mmenipa jina ya hio sehemu, wacheni mimi ntauliza nipeni siku mbili tatu, nikipata jibu lolote nitawajulisha.
Basi wale mabwana wakakaa pale siku ya tatu akwaita. Akawaambia nisikilieni kwa umakini sana.
Hapa Tanga Wajerumani wamekaa sana na njia hio mlionambia kuna mtu hapa anfanya kazi serikalini, ni fundi mkubwa sana, huyu amerithi majini wakubwa sana wa ukoo wake, bipi nimejua hii habari msiniulize. Lakini mimi simjui huyo mtu. Nyie tafdoiteni wenyeji wakepelekeni ile sehemu ya serikali wanapotengeza mashine na magari yao, Muulize fundi mkubwa wa pale, mkimpata njooni nae hapa tuongee nae.
Wale wageni hawakupata tabu kuna baraza ya kahwa na hakua pale jirani waklikua wameshizoea na watu wanacheza bao. Wakauliza pale. Kuna mtu akawaambia kuna fundi pale nyumba ile wa hukohuko karakana, ngija tumtume mtoto akamuite kama yupo.
Basi akatumwa mtoto akaenda, kuuliza akaambiwa hajarudi lakini akirudi watampa salaa kua kuna wageni wao kwenye kahawa atakuja, basi akija kama hampo hapa tutawafata hapo kwa Sheikh.
Basi kufika jioni wanarudi kusali alasiri hawjakaa sana wakaja kuitwa wakedna kibaraza cha kahawa, wakampata yule mtu wakamuita pembeni wakamwabia wao wageni kuna mtu wanamtafuta lakinihamwajui jina isipokua ndio fundi mkubwa wa serikali. Yule mtu akawauliza mzungu huyo au mtu wa hapa tanga? maana pale mimi ndipo ninapofanya kazi, kuna Mzungu ndio Worksjop manager. Na kuna funid wetu mkubwa, mtu wa hapa hapa Tanga maarufu sana anaitwa Mabruki. Wakasema itakua huyo wa Tanga. Maana ingekua mzungu wangetuambiwa mzungu. Akawaambia kama ni huyto basi mmeshampata turudi tukanywe kahawa niwape mtoto awapeleke nyumnai kwake, hayupo mali yupo hapo usagrfam barabara ya saba mwisho kule.
Wakarudi kwenye kahawa, akwaambia wale waliokwenda kumwita , hawa wanamtafuta Mabruk sio mimi jamani. Watu wakasheka, walikua hawamjui jina wanaemtafuta, mbona wangeshafika zamani kwa Mabruki.
Wakapewa mtoto akawapeleka kwa babu yako. Wal wakamwabia unaitwa na Sheikh Mgunya katutuma tuje kukita. Huyu Sheikh Mgunya wa barabara ya tisa? Wakamwabia ndio yeye anakuhitaji kwa ajili yetu. Akawaabia haya, tangulieni nikisha sali magharibi nakiuja huko. Mwambieni ikisha magaharib tu mguu wake huu.
Wakaondoka, kweli baada ya kusali magharibi babu yako akaenda, w)alipofika Mzee wa Kigunya kawaambia haya muhadithieni na mwenyeji wa hapa. Mbruki akmwambia mzee Mgunya, wewe ushaoa wake wanne Tanga mimi nakuona wewe kuaniz mdogo hata huko ugunyani kwenu sijui kama unapajua tena, unasema mi mi mwenyeji. Wewre mwenyeji zaidi yangu bwana.
Mzee wa kigunya kawaambia wale wageni wampoishe kidogo aongee faragha na babu yako wakanywe kahawa akiwa tauayari wataenda kuitwa. Mzee Mgunya akamwabia kwanini alimwita yeye, alimwabia mimi nimeongea na majini wakubwa sana, wao wakanmbia wewe una jini mkubwa mwenye hiyo bakora ulioibeba, yeye mwenyeji wa mitaa hiyo walioitaja, si umeisikia bwana wametaja Amboni lkini sio mapangomi upande unaotazama mapango kwa bharini. Nikaambiwa wewe una wenyeji wa huko watatoa mwangza ndio kisa cha kukuita bwana Mabruki.
Babu yako aksema usemayo kweli lakini hio mali sijawahi kusikia, ningeisikia si ningeshakwenda kuichukua? Mzee mgunya akmwabia akmwabia kweli huijui, hata mimi siijui lakini uradi uliopo hapa, ni uwaulize hao wakubwa huko, tutapata fununiu. Babu yako akasema swa atawaita kwa muda wao wampe siku mbili tatu ataleta majibu.
Wakakubalina hivyo. Wakaitwa wlae mbawna waendelee kusubiri, ikwa yule bwana Mihamed hawei kusuniri tena, akrudimDar, yule kijana akasema miminitasubiri. Mzee Mgunya kamwabia wewe subiri na usiwe na shka ni mgeniwa y. Tuombe iwe heri tu. Tumsubiri Mabruki atupe jibi lake na yeye.
Itaendelea.