Inatokewa post namba 97.
Sikukaa sana, kabla kiza hakijaingia vijana wa babu wakarudi na kama nyavu za mkono zile zile zina fimbo ndefu kushikia. Wakanambia twende tukavune kamba wa kuchoma. Tukaenda mtoni, tukapita lile dimbwi la kamba, kulikua na kamaba wengi sana, tukalipita tukaenda mbele kidogo, kama kuna kichaka hivi, kukipta, kati kati ya kichaka tukakuta dimbwi lingine kubwa, limezfichwa kabisa na kichaka, kama haujui kama ipo pale hulioni. Mmoja akasema "chimboi la babu hili" yeye ndio katuonesha, haingii mtu huku kama hajaoneshwa na babu. Nikamuuliza, mbona mimi hajanionesha? Akajibu si ndio tunakuonesha hivi kwa idhini yake mwenyewe. Mmoja alikua kaja na kapu kubwa, tukaanza kuvuna kamba pale, haikuchukua hata dakika kumi, kapu limejaa. Kamba wakubwa wakubwa , yaani ukiwala wawili au watatu umeshashiba. Tukaondoka pale tukarudi karibu na angoni mmoja akasema kalete lile bakuli kubwa, akawajaza wengine kwenye bakuli, wengine akashuka nao kwenye bwawa lile la kamba wadogo, akafinga kikapu chake, akakiingiza kwenye bwawa, akasema mula watabaki wazima nahawaribiki hata mwezi, hawatoki kabisa. Nikajisemea moyoni, kweli kila mtu na ujuzi wake.
Tyuliporudi angoni mmoja akaingia kichakani kuleta kuni za kuchomea kamba, mmoja nikaja nae akatoa kwenye kapu walilokuja nalo, kama bakuli hivi lina rojo nene la viungo vilivyopikwa, vinnukia. Akasema wale tunaowachoma wote tuwatie humu wakae nusuu saaa, maamgizo ya bibi ndio tuwachome, tusiwachome kaba ya nusu saa. Na wengine kasema tuwachome bila viungo, bali tutachoivyea wkati wa kula, kuna vitu vingine hapa bibi kapika, Lakini kasema hii ina pilipili mbichi, hii ya kupiki ina pilipili manga. Haya jamni kwa raha zetu.
Alieenda kuchukua kuni akarudi na rundo la kuni na rundo la majani fulani hivi mabiuchi, mengi tu. yapo kwenye matawi yake. Akasema haya majani, ya babu akipika nyama choma au samaki choma lazima ayaweke haya kabla nyama hazijawiva zijae moshi wake. Nikayakumbuka, hata tukifanya nyama choma nyumbani mjini, baba huwa anayaleta kwa wingi, Nyajua, yanafanya nyama inakua na harufu nzurin na mwenyewe anasema ukiyapondea kwenye nyama haya, dakika kumi tu, hata uwe na mshipa mgumu vipi utalainika. Nikauliza jina la yale majani, wakanitajia jina la kizigua, wakanambia haya tutakuchumia ukiondoka, pale karibu ya babu yapo mengi sana, babu aliyapanda. Haiwei miti mikiubwa kama mibaazi ya kusimama, ukikuwa sana ni futi sita au sabam haizidi hapo.
Basi tukatayarisha kamba wetu huku moto unawaka halafu wakauzima ukabaki mkaa tu unawaka kama mkaa, wakatia majani yale ya kunukia juu, yakawa yanatoa moshi kwa wingi, walikuwa wamechonga na vijiti virefu vingi tu, uanwaingiza watatu wanne, mnachoma mnakula hapo hapo, wengine tunaweka kwenye sahani, Mpaka babu akaja, na yeye tukawa tunachoima nae, aknambia bibi yako kanipa haya mandazi yakuoka ya kulia kamba. Basi mambo yakawa mazuri pale, ikawa nikamba maongezi kidogo, mandazi makavu kwa kamba, yaani wale kamba na zile pilipili za kupika za bibi ilikuwa kiboko, Haijapita muda, babu akasema nitilieni kamba wa bibi yenu, nimepelekee, babu mimi ntarudi baadae. Babu akachukua kamba kwa wingi tu tukampa, akasema wanatisha hawa, kama hawatishi watachoma wa nyumbani, kuna wageni watatu na kazi nao, nikimaliza narudi huku, akondoka na kijana wake mmoja, nikabaki na yule partner wangu wa kila siku. Nikakaa kidogo nikaona imekaribia saa tatu, nikamwambia narudi sasa hivi, nikaelekewa mtoni nikanawa, nikaenda kwenye uwanja wa kumuita jini. Kufika nikaanza kuita kama mara mbili tatu, nikakaa kimya nikaita tena nikatoa na salaam, mara nikassikia, aah bwana mkiubea vipi hali yako? Nikaitikia salama, aknambia kaa chini. Nikakaa, akanambia haya umeniita unasemaje? Nikamwambia si ulinambi nije saa tatu, akasema ndio, nataka uniulize maswali yako uliyonayo.
Nikamuuliza, mbona hutaki nikuone, kwanini sauti tu? Akanambia mimi hiuwezi kuniona kwa sasa lakini umeshwahi kuniona sana sema hunijui tu mimi ni nani/ Nikamuuliza wewe jinni? Akasema mimi ni mtu kama wewe lakini naweza kua chochote kile nipendacho, nikamuulizakama nimtu, mbona huonekani? Akanambia hiyo ni elimu tu, na wewe leo si umepewa mizizi ukiila utakua huonekani? Nikamwabia ndio alivyonambia, umejuaje? Akasema si nimekwambia mimi najua mambo yako yotem huweizi kunificha kitu. Nikamwabia sasa nitakula ile mizizi usinione, aknambia ile kwa yeye hata nikiila atanipona tu, haimuwii yeye kuniona. Akanambia yeye kutokuonekana hatumii mizizi, antumia tekbolojia nyingine kavbisa, akanambia kuna siku za usoni utaijua. Nikamuuliza nitaijuaje, Akasema mimi nipo hapa kukufundisha mengi usioyajua. Ni lazima nikupe elimu usiyoijua wewed na wasioijua binadasam wengine. Nikamwabia watu wanajua mambo mengi utasemaje kuna elimu haijui? Akacheka akasema kweli binadam wana elimu togfauti tofauti nyingi sana., lakini kuna ambazo hakuna mwenye nzo dunia nzima, sio binadam sio jini, mimi nnazo. Utaziona tu. Kidogo kidogo, unaswali lolote?Sikumjibu. Akasema mimi najua unataka kuuliza nini lakini unaona haya kuuliza. Nikamwabia huwezi kujua nilikua nataka kukuuliza nini, aknambia nikwambie? Nikamwabia nambie. Akanambia unataka kujua kama naweza kukufundisha kusafiri kwa haraka sana. Nikamwambia umejuaje, akaema hiyo haikuhusu, kwa sasa, sema ni kweli uita kuuliza hivyo? Nikamwabia hilo lilikua moja tu, akasema nafahamu, sasa wewe kaa kimya mimi nakujibu maswali yako bila kuuliza.
Akaanza, ndio, mimi naweza kusafiri kwend popote duniani kwa muda mfuoi sana, na sio mimi naweza kukuafrisha na wewe na mizigo yako, Hata kama una gari, mimi naweza kukusafirisha wewe na gari lako nikakupeleka popote Tanzania ndani ya dakika tatu au chini kabisa ya hapo. Hapana huo sio uchwi, hio ni elimu tu. Utaijua kidogo kidogo. Halfu dunia haipo duara bwana mkubwa, dunia ni kama zulia lililotandikwa. Mnadanganywa na wasomi wenu, wanafahamu hilo, lakinihawataki kua wa kweli. Kuna mengi sana wanayafucha kwa faida zao, na menhgine ukiyajua watakuua. Ndio zipo dunia saba. Na zote zina viumbe wake.
Nikawa nashangaa, hayo yote nilikua nikitaka kumuuliza yeye anajibu kabla sijamuuliza, Nikamwabia unanitisha. Akasema kwanini, nikamwambia unajuaje ninachotaka kukuuliza, Aksema hio ni elimu ya "telepathy", hivohivyo akitaka kwa Kinegreza. Aakasema ni mawasiliano tu ya hali ya juu, utayajua tu, akasema hizi simu zenu za siku hizi, miaka 100 mnyma ungemwabia mtu zinavyofanya kazi angekuona mchawi, mtu yupo London mnaonana na mnaongea wakati huohuo. Sasa teknolojia ime[pungua, zamani ilikua kubwa sana, mimi naifahamu, nimebahatika kuwepo zamani na sasa hivi. Kw ahio ninayo teknolojia iliofuchwa, wakujua na wewe unaijua wankuua, hawakuachi. Maadui ni wengi sana, hawataki uwazidi kitu. Mimi hawawezi kuniua, najua mbinu zao zote, wamejaribu sana wameshindwa, sasa wananiogopa sana.
Nikawa nashangaa shangaaakanambia nadhani umeelewa machavhe kila tukikutana uwe unauliza uyatakayo, chukulia hii kama mwanzo tu. Nikamuuliza naweza kuja kukurikodi na simu yangu. Akasema unaweza kuja nayi na utaweza kurikodi sauti, picha yangu huwzi kuipata labda nitake mwenyewe. Mikamwabia natamani sana nikuone, unaonesha una hikma nyingi, Akasema kawaida tu, nikija siku nyingine nitakufundusha kuhusu dunia saba zizlizopo, lakini niyawea kukufundisha kuhus nne tu, ya tanoi sita na saba, siwezi. Nikawa nawaza tu. Tukaagana kabla hajaondoka nikamwabia sasa ndio yamenijia maswali mengi sana, akasema anajua lakini vizuriniwe na maswali yasioidi matatu ili anifahamishe kwa kina na niwe na rikodi. Tukaagana akaondoka.
Nikarudi pangoni, nikamkuta kijana wa babu bado anachoma kamba pale karibia na lango la pangoni. akanambia nimekula kamba mpaka mdomo unawasha, nimeona niwamaliziwe kuwachoma hawa kwenye bakuli, tutawala tukisikia njj usiku au tukiamka kusali alfajiri. Nikamwambia poa, niakchukua kamba nikaanza kuwala, nikala watatu nikajisikia nipo full kabisa. Nikamwa bia babu alisema atkuja lakini mimi nasikia usingizi wa shibe, akanambia hata mimi naosha vyombo halagu nalala, nikamsaidia tukaosha vyombo tukaufukia moto na michangam akasema huu hauzimiki, tutaukutamoaka asubuhi unawaka ndani ya m9changa, akachomeka vijiti vya kuni kuuzunguka alipoyufukia moto, akasema vibwengi baharini vinapenda kufanya utundu, hiviu nimezuwia visiuchezee moto. Nikacheka, nikamwambi ahawa vibwangi nasikia tu sijawaona, akasema wapo wengi hukul lalini haya mapango hawayasogelei, babu anasema kuna viumbe vikali sana humu mapangoni. Bibwengo watauliwa wakifanya mchezo, nikacheka. Nikasema babu ana mikwara ya kizamni. Kijana wake akacheka, aksema babu yako mtaalam yule, Usimcheee, Tanga nzima hii na Mombasa yake wakishindwa mgonjwa wanamletea yeye. anamtibu. Anajua sana tiba. Nikacheka nikamwambia mimi nalala akija ataniamsha. Akasema babu yako,m hana tabia ya kumwamsha mtu akilala. Anaweza kukuacha ulale ahata siku mbili hakuamshi. ukimuuliza kwanini hupendi kumuamsha mtu anasema mwache anakua dunia nyingine pale. Utamkatia raha za ndoto zake.
Itaendelea.