- Thread starter
- #321
Ahsante, tuko pamoja.Stori Nzuri.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ahsante, tuko pamoja.Stori Nzuri.
Anamfahamu sana, nimemuuliza siku nyingi, kisa chake alichonipa kitakuja, tufanye subira. Ndio kwanzza tumeanza.Muulize Arsis kama anamfahamu YESU KRISTO? Ikiwezekana atupe maelezo kumhusu
Waziri gani ameshafika kwa Babu? Tuanzie hapoInaendelea kutokea post namba 1.
Babu akatupokea pale, tukakumbatiana kwa futraha, mara na bibi nae akaja aliposikia nimefika, akanambia "aah, sasa mume wangu ndio kaingia, sio hiki kizee, sina habari nacho tena". na yeye bibi akanikumbatia akanipiga mabusu ya ngubu ya shavuni, akanambia twende ndni mume wangu, nimekutayarishia chumba chako.
Nyumba ya babu yangu ilikua ni kubwa sana kwa maisha ya kijijini, inavyumba self contain vitatu, umeme utafikiri upo mjini. maana umeme umepita hapo hapo kijijini kwao, wenyewe wanasema huu unakwenda Kenya, unagtikea Hale. Kwa ufupi hauhisi kabisa kama upo kijijini mpaka utoke nje ya bma lake. babu alikua na nyumba hiyo yake kubwa na nyingine ndogo ndogo z vyumba viwili auj kimoja zimetapakaa pote kumzunguka. Nyingi zilikua za kufikia wageni wanaokuja kwa matatizo yao kwa babu yangu, babu alikua mganga wa jadi, tena anaesifika kweli. Kwake hapakosi wageni, mpaka mawaziri utawakuta huko. Kila mmoja na shida yake.
Babu toka nimefika alikua haniwachi peke yangu, ana nyumba moja ipo karibu na kwake hiyo mwenyewe ndio ofisi yake, ina chumba kizuri tu, cha kufanyia shughuli za ke na wageni wake, na kama ina baraza kubwa ndipo wanapoisubiri wageni wanaokuja kumuona, na ina vumba viwili vidogo ndani, mwenyewe anavoiita "operation rooms". Babu alikua anaongea na kuandika Kingereza na Kijerumani kwa ufasaha kabisa. Kabla ya kaumua kurudi kuishi kijijini alikua ni fundi mekanika, tena fireman, wa idara ya vifaa na magari ya serikali hapo tanga. Alikua ni mtua anaejulikana sana Tanga na anaheshimika sana. Ni mcheshi sana, kutwa anatabasamu, akikasirika humjui kabisa, wewe kutwa kucha unamuona ni mtu wa furaha tu.
Itaendelea.
Siwezi kwa sasa, kuna siku ataniruhusu lakini bado kwanza.Weka hata audio fupi, tusikie sauti ya Arsis, jini
Kielimu inawezekana lakini hairuhusiwi. Wanaofanya hayo ni washirikina. Utakiona kisa chake kikifikia.Mkuu inawezekana kumfanya mtu akusahau asikumbuke lolote kuhusu wewe na wala kamwe asiweze kukutana nawe? Inakuwaje hiyo?
Hivi malaika wao huwa hawajihusishi kabisa na mambo yetu wanaadam?Kielimu inawezekana lakini hairuhusiwi. Wanaofanya hayo ni washirikina. Utakiona kisa chake kikifikia.
Naomba kujua tiba ya nguvu za kiumeMimi ninachoweza kufanya ni kukuelekeza tiba ninazozifahamu tu. sina kilinge kama marehemu babu yangu.
Kwa ufupi, mimi sio mganga isipokua kuna tiba nazifahamu na mwenye kutibu ni Muumba wetu.
Bwana mkubwaInatokea post namba 304.
Tulipomaliza tukatoka nje na babu, akanambia haina haja ya kwenda kilingeni, saa hizi hakuna atakaekuja hapa, watu wamechoka wanakwenda kulala. Wewe bwana mkubwa huendi kulala? Kisa kirefu.
mimi; bbu nikikukosa leo naweza nisikupate mpaka msimu mwingine, mwanao anaweza kutimua kurudi Dar wakati wowote, gereji siku hizi akiwa yeye yupo mimi naweza kusafiri, nikiwa mimi nipo yeye anasafiri, Hivi imebidi jana njiani ampigoie msomi aende pale mpka yeye au mimi nirudi, nasikia wanabishana siku ya kurudi.
Babu; haondoki kesho huyo kwa sababu kesho kutwa kuna gari inakuja kuchukua nazi, shambani kwake.
Mimi: hajanambia.
Babu; Atakwambia kesho akisha kua na uhakika, lakini mimi niliongea na wale watu, kesho hawawezi kuja, wanakuja keshoi kutwa. labda akuwache wewe uwapakilie nazi.
Mimi; kama kina pesa haondoki, namjua mwanao mimi, anapenda pesa kama Mpemba.
Babu: Hio kachukua kwa bibi yako, mimi sina hio. Vipi wewe?
Mimi: Mimi nakurithi wewe babu, nakumbiuka simo ulinambia kama mali inakuja jhakuna wakuizuia na kama haiji hakuna wakuileta.
Babu; Hio ni kweli kabisa babu. Tulifikia wapi bwana mkubwa?
Mimi: Plae unasema umetupwa chini pangoni.
Babu; babu nadhani nilizimia, maana nakumbuka kurushwa na kuanguka na kingine nakumbuka nimesimama pale nilipoangukia na Jini la Mzee Mgunya limenisimamia, mimi mpaka hapo nilikua najua ni Mzee Mgunya mwenyewe, kumbe ni jini wake, alikuja kunambia baadae.
Babu; Ikawa kama nimepagawa kidogo, nasikia joto, ule moto unawaka kweli kweli tuliouwasha sisi, kulikua kuna magogo yapo pale akanambia yote tuyaweke kwenye ule moto, tukayaweka na manyasi yote tukayaweka, akanambia haya twende nje, kutoka nje akanambia wewe pumzika hapo mchangani, mimi nakwenda zangu tutaonana mjini ukija. Nikakaa mbali kidogo na ule mlango wa kuingilia pangoni, pale ambapo siku hizi tunachoma choma samaki na kamba wakija wageni.
Babu; Basi bwana mkubwa nikakaa nikapiwa pigwa na upepo nikaanza kupata fahamu vizuri , muda wote nimekaa nasoma QAAur'an tu. Nikaanza kuwaza huyu mzee mgunya usiku wa manane huu peke yake saa hizi akatize hili pori, siku hizo babu hili pori ni kubwa kweli kweli, miti mikubwa manyasi mengi, wanyama na wadudu wengi sana. Kumbe ilikua muda wa alfajiri sio mbali. Kidogo akatoka Jini Bakora.
Tukauliza hali zetu, akanambia wewe soma Qur'an hapa mpaka ukisha sali alafjiri uende Tanga lakini usiende nyumbani kwako nenda moja kwa moja kwa Mgunya, mimi mtaniita baadae. Kazi imefanikiwa. Nilikua nataka kumuuliza lakini nikahisi hataki kuongelea lolote kuhusu kazi iliotuleta pale, basi baada kusali alfajiri nikatwang mpaka barabarani, zikukaa sana nikapata gari ya kwenda Tanga, nimeingia Tanga jioni, zamani barabara mbaya sio kama sasa.
Babu; Kufika Tnaga moja kwa moja kwa mgunya, muda wote babu nasoma Qur'an kimoyo moyo. Kufik pale nikapumzika baadaya ishaa akaitwa Jini Bakora akaja, pale ndio nikajua kua yule alikuwa jini niliekua nae pangoni hakua Mgunya, tulishinda nae toka mchana tunavita magogo na walewagiriama wa bindeni kule niwachukua asubuhi wanisaidie kujaza manyasi na magogoya kuni, Tulifanya kazi nzuri sana babu.
Ndio pale sasa jini Bakora akatueleza kua yule mtu tumwfanikiwa kumtoa kifungoni ndio huytu Ramses, alikua kifungoni mda nrefu, utamuuliza mwenyewe atakwambia. Siku ile babu sikuruhusiwa kwenda nyumbani, mkewe Mzee Mgunya akamfata mke wangu mimi nikakaa pale mpaka ule moto tuliouwasha kule ukachima magogo yote pakwa jivu tupu, lile jivu babu tulilipakia kwenye ngarawa tukaenda kulimwaga baharini mpaka pakawa hakuna hata jivu kabisa pakabaki mchanga mgtupu kama palivyokua mwanza, hayo ndio tuliyafanya baadae lakini.
Nikakaa pale kama nipo saba ya harusi ikawa kazi yetu kula kulala siku tatu ya nne nikaondoka na mke wangu nikasindikiwa na Sheikh Mgunya mpaka nyumnai tukafanya dua. Sheikh Mgunya akasema siku ya saba atafanya sadaka ya chakula pale kwake, tukale pale watu wa nyumba nima, basi ikawa hivyo babiu.
Siku tuliomaliza takrima ya Sheikh Mgunya, kurudi nyumnani usiku akaja Jini Bakora, kaja kafurahi kweli kweli nikajua mambo mazuri. Akanambia nimekuletwa mgeni wako, utaongea nae mwenyewe lakini hutiweza kumuona isipokua mtaongea kama kawaida. Kwa hio chumba kile chako tunachokutana nikiondoka mimi ukisikia unasemesha usistuke mgeni wako alietoka kifungoni, Mtaingea wenyewe mimi sitaki kuingilia maongezi yenu. Jini Bakora akaondoka.
Itaendelea.
Ombi zuri sana.
Kwa sisi wa koo za simba, hilo ni jqmbo dogo sana na dawa zake zipo, tena tunakulekeza uzifanya mwenyewe.
Tiba ya nguvu za kiume ina mlolongo wa kufatiliwa kwa watu wa kisasa.
Kwanza ulijuaje hauna nguvu za kiume?
Una mke?
Kwa muda gani sasa?
Una watoto?
Wa ngapi?
Una umri gani?
Unajichua (punyeto)?
Unatembea na wanawake zaidi ya mkeo au ya wale aliokuruhusu mkeo?
Una lawiti au kulawitiwa (ushoga). -?
Unatumia sigara?
Unatumia bangi? Elezea unaitumia vbipi na kwanini?
Mkeo ndiye mwenye kulalamika kua huna nguvu za kiume?
Au ni wewe mwenyewe yeye hajawahi kulalamika?
hayo ni baadhi wa maswali ya awali, unaweza kuyajibu kwa faida ya wengi au unaweza kuja PM kama hutopenda kuwa muwazi.
nilijua tu utakua shombe.hao wakina wimpy si warabu wa dodoma hao na kina marehem mzee makuber.ndio wazee wa dodoma hao sasa mpaka akukaribishe nikajua tu ipo namna.hapo pia kwa zahoro .na kahawa za asubuh nikajua tu huyu maaarabu.sisi wagen nyumban wakija ni kutoa vikombe na chupa la kahawa.hakuna mambo ya soda nimetokea kunywa kahawa toka nnanmiaka 6 mpaka leoMimi nishombe wa Kiarabu na kidigo tokea babu yangu wa kabla ya babu yangu ndio nadhani hawajachanganya damu.
Wengi sana. Hatuna haja ya kutaja majina.Waziri gani ameshafika kwa Babu? Tuanzie hapo
Sana tena sana, maswali hayo nayarudia mara nyingi kwa kua na watu wanayauliza, mpaka ananambia majibu yote unayo.Hiki kisa ni balaa.
Umeshawah kumuuliza kuhusu mpinga kristo, israel na kuhusu mwisho dunia na kiyama??
Pia kuhusu uumbaji, adam na eva, edeni, sodoma na gomora, gharika ya enzi za Nuhu??
Wote uliowataja sijawataja sehemu na siwafahamu. Ninae mjua na niliemtaja anaitwa Jamal na nilijulishwa kua ni mwenye Wimpy.nilijua tu utakua shombe.hao wakina wimpy si warabu wa dodoma hao na kina marehem mzee makuber.ndio wazee wa dodoma hao sasa mpaka akukaribishe nikajua tu ipo namna.hapo pia kwa zahoro .na kahawa za asubuh nikajua tu huyu maaarabu.sisi wagen nyumban wakija ni kutoa vikombe na chupa la kahawa.hakuna mambo ya soda nimetokea kunywa kahawa toka nnanmiaka 6 mpaka leo
Una haraka za kukimbilia wapiStori yako ni nzuri mkuu ila kama unaweza hzo story za kamba zipunguze sana
Imefanya nini tena?Punyeto
Bwana mkubwa
Nataka kujua kwanini irsis alifungwa????
Simba yupi ambae hana u "foxy"?Nafahamu kuwa wewe ni simba, kwanini simba unajiita foxy?
Mimi daima simba mwenzio.