Kisa cha Adam 1.
Salamoun Alaykum!
Leo katika muendelezo wetu wa Kisa cha Adam nitaanza na mada ambayo nilisita sana kuiwasilisha jukwaani kwa sababu mbili kuu.
Sababu ya kwanza; ni kua mada hii ni ndefu na inabidi mnivumilie kwani inabidi tuifanyie tafsil kwa kina bila kuacha kitu kikielea (hangig). Tutaitumia sana mbinu ya kiota, kufata na kuonesha maana kusudiwa katika aya zingine au lilipotumika neno kama tunalolifanyia βtafsilβ.
Sababu ya pili hii mada itakua na mshtuko (shocker) utaotutikisa kidogo uelewawetu, hususan kwa wale wote ambao hawapendi kuisoma Qurβan kama ilivyo na hupenda kuongezea maneno ya watafsiri hata kama hayamo kwenye Qurβan.
Mtikisoko utakua wa ziadsia kua kwa miaka mingi tumefata na kuamini mambo kwa kufata watu ambao wamefanya makosa kataika tafsser zao au wamefata vitabu vingine ambayo visa au mafundisho yake ni ya kibinadam tu, hayana hata chembe na uhusiano na Qurβan.
Nawaasa wote tustahamili kuisoma hii elimu kidogo kidogo, kwani ina mengi ambayo tutayaleta kidogo kidogo ili yatuingie kwa mitindo (methods) ambayo inatokana na Qurβan yenyewe na wala sio ubunifu wa mtu.
Msiniulize mtayoyasoma hapa kwanini wengi wetu hatujayaona kabla na au kwanini βMaulamaa wetu hawajayaona kabla?β. Tustahamili kuuliza hayo kwani naamini kila tutavyoendelea Qurβan yenyewe itatupa majibu,
Tunakusudia kuanza kuifanyia tafsil aya ya 30 na kuendelea, lakini kabla hatujaingia kwenye aya ya 30 itabidi tupitie aya ya 28 na 29.
Ni muhimu sana tujifunze mbinu mbili tofauti za kutusaidia ufahamu wa Qurβan kutokana na Qurβan yenyewe.
Alhamdulillahi, Mwenyezi Mungu ametujaalia kutupa elimu na mwongozo ulio bora kabisa kuliko wowote ule na usio na shaka ndani yake, Qurβan.
Hatuna budi tufanye hima tujikite kwenye Qurβan kama msingi wetu mkuu wa kuielewa Qurβan yenyewe. Maneno ya watu binafsi tuliofundishwa, haijalishi yanatokea kwa mwenye jina kubwa vipi, kama katumia yake binafsi kuongezea ambayo hayamo kwenye Qurβan au kutumia akili yake, ambayo haiwezi kua na ujuzi wa kumpita Allah kwa lolote li;e, tuyapuuze.
Ikiwa kuna Alim au mwanazuoni yeyote yule, kupunguza kitu au kusema kua hiki hakina maana kilizidi tu, kwa sababu yoyote atakayoitoa, huyo au hao tuwatazame mara mbili mbili, kwani naamini hakuna neno au herufi itokayo kwa Muumba wetu isiyo na kazi yake au maana yake kuwepo kwenye Qurβan.
...2
Kisa cha adam. 2
Je, malaika walimuuliza Mwenyezi Mungu?
Katika sehemu hii tunaanza na swali hilo, la kwenye kichwa cha Habari, ambalo In shaa Allah tutalizungumzia kwa kina.
Je, Maklaika waliuliza kweli?
Wakati tunaendelea. kwanza tujikumbushe kitu ambacho tulikiongelea huko nyuma, kwa kiasi na kijuujuu, nacho ni kua, asilimia kubwa sana ya Qurβan, (nadiriki kusema) zaidi ya asilimia 60 ni visa na hadithi mbali mbali zilizomo ndani ya Qurβan. Kwa usisitiza, ikiwa hakuna visa na hadithi ndani ya Qurβan basi hakuna Qurβan.
Tunapata na istilahi nyingine βdhikrβ ambayo kama tutavyojionea, mara nyingi inapotajwa βdhikrβ inamaanisha kisa, fumbo au hadith ya Qurβan. Hili tutaliongelea kwa kina na kuonesha Ushahidi uliopo ndani ya Qurβan na tutajionea tunavyoweza kujifunza kutokana na dhikr, ambayo kimaana ya Qur'an ni hadith za Qurβan.
Tutaona pia ndimi βlisanβ ya Ibrahim (Abrahamic locution) inavyotolewa kwenye dhikr wakati tunaongelea suala hili la Malaika ambao, eti wamemuuliza maswali Muumba wetu, kama tulivyoaminishwa na watafsiri wengi walioitafsiri
aya Q 2:30.
Raha ilioje tunapogundua "bayyinah" mpya na za kipekee ambazo Qurβan yenyewe inatufundisha na kuturekebisha mithili ya βadvanced softwareβ ya kompyuta kila tunapoendelea kugundua kuisoma kwa kufata mifumo (methods)yake ya kutuelimisha.
Kwa hakika ni muujiza, wa kushangaza na kustajaabisha. tunapoelewa yote hayo ni kutoka kwenye Qurβan yenyewe. In shaa Allah tutazidi kujionea wenyewe na kuelimika kila tunavyoendelea.
Hii tunaiita moja ya vibainisho βbayyinahβ au viashiria vipya tunavyojifundisha kwa pamoja.
In shaa Allah uwe ni ujuzi na elimu yenye manufaa kwetu na kwa wengine wote, pia iwe ni sadaka njema kwetu na kwa Waislam wote, waliopo na waliotutangulia.
Tueleweshane na tuelewe kua, hii ni elimu na sio starehe, raha yake isio na mfano ni pale tunapojitambua kua tunaupata ujuzi wa kina wa kuulewa mwongozo wetu wa Qurβan kwa mbinu za Qurβan yenyewe.
Qurβan ni muujiza ambao huwezi kuufananisha kitabu cha mtu yoyote au chochote au mshairi yoyote duniani. Hakuna mbinu za kujifundishia za mtu yeyote zinayoweza kufanana au hata kuzikaribia mbinu za Qurβan.
...