Kisa cha Adam 1.
Salamoun Alaykum!
Leo katika muendelezo wetu wa Kisa cha Adam nitaanza na mada ambayo nilisita sana kuiwasilisha jukwaani kwa sababu mbili kuu.
Sababu ya kwanza; ni kua mada hii ni ndefu na inabidi mnivumilie kwani inabidi tuifanyie tafsil kwa kina bila kuacha kitu kikielea (hangig). Tutaitumia sana mbinu ya kiota, kufata na kuonesha maana kusudiwa katika aya zingine au lilipotumika neno kama tunalolifanyia ‘tafsil”.
Sababu ya pili hii mada itakua na mshtuko (shocker) utaotutikisa kidogo uelewawetu, hususan kwa wale wote ambao hawapendi kuisoma Qur’an kama ilivyo na hupenda kuongezea maneno ya watafsiri hata kama hayamo kwenye Qur’an.
Mtikisoko utakua wa ziadsia kua kwa miaka mingi tumefata na kuamini mambo kwa kufata watu ambao wamefanya makosa kataika tafsser zao au wamefata vitabu vingine ambayo visa au mafundisho yake ni ya kibinadam tu, hayana hata chembe na uhusiano na Qur’an.
Nawaasa wote tustahamili kuisoma hii elimu kidogo kidogo, kwani ina mengi ambayo tutayaleta kidogo kidogo ili yatuingie kwa mitindo (methods) ambayo inatokana na Qur’an yenyewe na wala sio ubunifu wa mtu.
Msiniulize mtayoyasoma hapa kwanini wengi wetu hatujayaona kabla na au kwanini “Maulamaa wetu hawajayaona kabla?”. Tustahamili kuuliza hayo kwani naamini kila tutavyoendelea Qur’an yenyewe itatupa majibu,
Tunakusudia kuanza kuifanyia tafsil aya ya 30 na kuendelea, lakini kabla hatujaingia kwenye aya ya 30 itabidi tupitie aya ya 28 na 29.
Ni muhimu sana tujifunze mbinu mbili tofauti za kutusaidia ufahamu wa Qur’an kutokana na Qur’an yenyewe.
Alhamdulillahi, Mwenyezi Mungu ametujaalia kutupa elimu na mwongozo ulio bora kabisa kuliko wowote ule na usio na shaka ndani yake, Qur’an.
Hatuna budi tufanye hima tujikite kwenye Qur’an kama msingi wetu mkuu wa kuielewa Qur’an yenyewe. Maneno ya watu binafsi tuliofundishwa, haijalishi yanatokea kwa mwenye jina kubwa vipi, kama katumia yake binafsi kuongezea ambayo hayamo kwenye Qur’an au kutumia akili yake, ambayo haiwezi kua na ujuzi wa kumpita Allah kwa lolote li;e, tuyapuuze.
Ikiwa kuna Alim au mwanazuoni yeyote yule, kupunguza kitu au kusema kua hiki hakina maana kilizidi tu, kwa sababu yoyote atakayoitoa, huyo au hao tuwatazame mara mbili mbili, kwani naamini hakuna neno au herufi itokayo kwa Muumba wetu isiyo na kazi yake au maana yake kuwepo kwenye Qur’an.
...2
Kisa cha adam. 2
Je, malaika walimuuliza Mwenyezi Mungu?
Katika sehemu hii tunaanza na swali hilo, la kwenye kichwa cha Habari, ambalo In shaa Allah tutalizungumzia kwa kina.
Je, Maklaika waliuliza kweli?
Wakati tunaendelea. kwanza tujikumbushe kitu ambacho tulikiongelea huko nyuma, kwa kiasi na kijuujuu, nacho ni kua, asilimia kubwa sana ya Qur’an, (nadiriki kusema) zaidi ya asilimia 60 ni visa na hadithi mbali mbali zilizomo ndani ya Qur’an. Kwa usisitiza, ikiwa hakuna visa na hadithi ndani ya Qur’an basi hakuna Qur’an.
Tunapata na istilahi nyingine “dhikr” ambayo kama tutavyojionea, mara nyingi inapotajwa “dhikr” inamaanisha kisa, fumbo au hadith ya Qur’an. Hili tutaliongelea kwa kina na kuonesha Ushahidi uliopo ndani ya Qur’an na tutajionea tunavyoweza kujifunza kutokana na dhikr, ambayo kimaana ya Qur'an ni hadith za Qur’an.
Tutaona pia ndimi “lisan” ya Ibrahim (Abrahamic locution) inavyotolewa kwenye dhikr wakati tunaongelea suala hili la Malaika ambao, eti wamemuuliza maswali Muumba wetu, kama tulivyoaminishwa na watafsiri wengi walioitafsiri
aya Q 2:30.
Raha ilioje tunapogundua "bayyinah" mpya na za kipekee ambazo Qur’an yenyewe inatufundisha na kuturekebisha mithili ya “advanced software” ya kompyuta kila tunapoendelea kugundua kuisoma kwa kufata mifumo (methods)yake ya kutuelimisha.
Kwa hakika ni muujiza, wa kushangaza na kustajaabisha. tunapoelewa yote hayo ni kutoka kwenye Qur’an yenyewe. In shaa Allah tutazidi kujionea wenyewe na kuelimika kila tunavyoendelea.
Hii tunaiita moja ya vibainisho “bayyinah” au viashiria vipya tunavyojifundisha kwa pamoja.
In shaa Allah uwe ni ujuzi na elimu yenye manufaa kwetu na kwa wengine wote, pia iwe ni sadaka njema kwetu na kwa Waislam wote, waliopo na waliotutangulia.
Tueleweshane na tuelewe kua, hii ni elimu na sio starehe, raha yake isio na mfano ni pale tunapojitambua kua tunaupata ujuzi wa kina wa kuulewa mwongozo wetu wa Qur’an kwa mbinu za Qur’an yenyewe.
Qur’an ni muujiza ambao huwezi kuufananisha kitabu cha mtu yoyote au chochote au mshairi yoyote duniani. Hakuna mbinu za kujifundishia za mtu yeyote zinayoweza kufanana au hata kuzikaribia mbinu za Qur’an.
...