Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

hatari kubwa lakini anasema mbona hata Masheikh wakubwa wanasema hilo, anashangaa kwanini hamsomi? Kwanza anabisha wanaosema Adam ni mtu wa kwanza, anasema hakuna hio kwenye Qur'an, kama ipo leteni aya hapa.
Simba.
Simba au Arsis, tafadhali mmoja wenu aelezee hili. Kuna mambo natamani kuelewa. Hata mimi ninashawishika kabisa kuwa Adam sio mtu wa kwanza. Tuelezee tafadhali.
 
Nimefuatilia kuhusu ibn Arab, Kuna jina limeandikwa kwenye sayari ya Mars ila huenda ikawa iyo ni password yake yeye Ibn Arab kama unavyosema.
 
Nimepitia kidogo kuhusu elimu iyo ya ladoun nimeona ikielezwa kama elimu kutoka kwa ALLAH yeye anamruzuku amtakaye.
Neno hili ''Ladoun'' lipo pia katika Quran surat kahf aya ya 10
رَبِّ هَبْ لِى مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً - Mola wetu tupe rehma itokayo kwako
Hapo nimeona matumizi ya neno (لَدُن) - Likimaanisha ''kutoka kwa''
Lakini pia katika surat kahf aya ya 65 Inasema
“وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا'' - Tukamfundisha ilmu itokayo kwetu.
 
Sawa kabisa, ni kama nilivyokueleza juu hapo.

Njia yake ni ucha Mungu tu, nyiradi nyingi na kujiweka pekee kwa muda mrefu mbali na watu, ukifanya tahajud (meditations)tu. Soma sana kuhusu masufi (sufism), ndio wenye ustahamilivu huo.
 
LANGO LA KUZIMU LA DAR ES SALAAM

Lango kuu la kuingilia kuzimu la Upanga Dar es Salaam linajulikana kwa jina la MUSTALLAH. Ndani ya shimo la Mustallah kuna aina kumi na mbili za majini makatili sana yanayoangamiza jamii ya watu wa jiji la Dar es Salaam. Wachawi wa nchi huenda mara kwa mara shimoni kuongeza nguvu za uchawi wao, kabla ya kuingia shimoni ni lazima ufunge kwa siku tatu. Hapa tunajifunza kuwa shetani naye huwa anafunga.

Tuangalie sasa aina za haya majini ya Mustallah na kazi zao.

1. Ratafari ni jini linalosimamia laana zote za ukoo.
Wapo watu wanasema ukoo wetu unasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, kisukari, presha, kutokuolewa na mambo mengi ambayo utakuta ukoo unakuwa na tatizo moja linalofanana kwa kila mwanaukoo, hili jini ndilo linasimamia laana hizo zimalize ukoo hadi kifo.

2. Muzaphari ni jini linalozuia mafanikio.
Ukitupiwa hili jini, hutaweza kufanya jambo lolote ukafanikiwa. Ukikopa shs 500,000 bank kwa ajili ya kuanza bishara, utafilisika na kuingia kwenye deni, na dhamana yako uliyoweka bank kuuzwa. Ukitaka kujiendeleza kimasomo yatatokea matatizo mengi yatakayosababisha kusimamisha masomo yako.

3. Latifu hili jini linasimamia mambo matatu, ufukara, mateso, na pesa zako kupotea katika mazingara ya ajabu ajabu.

4. Jujan ni jini linalosababisha watu kula udongo.

5. Jahad ni jini la kutorosha mali
Makarani wa bank ndio hasa wanaoadhirika na hili jini, utakuta karani anafanya kazi kwa uangalifu mkubwa, lakini kila siku ana shoti ya pesa. Pia kwenye maduka ya kawaida na hasa supermarket.

6.Hazinan hili jini linalosimamia pombe, uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya na mirungi.

7. Jube ni jini linalosimamia utasa, vipimo vya hospitali vitaonyesha kuwa huna tatizo lakini mtoto kamwe hapatikani.

8. Sifafiru hili ni jini linalosimamia ukahaba. Likimwingia mtu yeyote, kwa siku atatembea na watu zaidi ya watano bila hamu ya mapenzi kumalizika.

9. Subian hili ni jini linalosimamia ajali. Chakula cha hili jini ni damu.
Linasababisha wanawake wasipate siku zao, wengine wanapata maumivu makali sana wakiwa katika hedhi, utasikia tumbo linakata kuanzia kushoto kwenda kulia na hali hiyo huendelea kwa muda hadi unanza kusikia maumivu makali ya mgongo.

10. Sumri jini hili linanyonga watoto wakiwa tumboni kabla ya kujifungua, pia linajihusisha na kuchukua watoto hospitali kichawi.

11. Munsar hili ni jini linalosimamia ndoa ya jinsia moja.
mwanamke kwa mwanamke au mwanamume kwa mwanamume.

12. Waidadat hili jini linasababisha vijana wa kiume kuvaa hereni, kusuka nywele na rasta.

(MOJA YA HAYO MAJINI NDIO ARSIS)
 
Naunga mkono hoja..Mimi hii sehemu ya Adam siielewi kabisa hivyo nasoma Kwa ku scan tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…