Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

hatari kubwa lakini anasema mbona hata Masheikh wakubwa wanasema hilo, anashangaa kwanini hamsomi? Kwanza anabisha wanaosema Adam ni mtu wa kwanza, anasema hakuna hio kwenye Qur'an, kama ipo leteni aya hapa.
Simba.
Simba au Arsis, tafadhali mmoja wenu aelezee hili. Kuna mambo natamani kuelewa. Hata mimi ninashawishika kabisa kuwa Adam sio mtu wa kwanza. Tuelezee tafadhali.
 
msome Ibn Arabi.

Kaliandika hilo jina wenye sayari, ambayo sasa inajulikana kama Mars. Kipo wazi kabisa.

Jina pekee bila kupewa na Allah mwenyewe hiyo elimu, haitokidhi matakwa yako. Kila mmoja hufunuliwa "pasword" yake. Inawezekana jina hilo alifunuliwa Ibn Arabi tu kama password yake.

Fanya bidii na wewe upewe password yako.
Nimefuatilia kuhusu ibn Arab, Kuna jina limeandikwa kwenye sayari ya Mars ila huenda ikawa iyo ni password yake yeye Ibn Arab kama unavyosema.
 
Sikiliza Lidafo, nilikupa zoezi la kufanya sijui liliishia wapi lakini elimu uitakayo inaitwa "ladoun" imetajwa katika Qur'an, sehemu kadhaa.

Kwa bahati mbaya, sio elimu ambayo unajifundisha moja kwa moja au kuna mtu atakae kufundisha. Ni elimu inayotoka kwa Allah pekee, na yeye kuchagua wa kumpa.

Wewe unachotakiwa kufanya ni kuzidisha kusoma, kila fursa unayoipata, soma kila kitu kutoka kwa kila mtu na omba sana dua ya Allah akuzidishie elimu. Ukikuta boksi lisome, ukikuta pakti ya maziwa isome, ukiona mti usome, ukiona mnyama msome.

Ukitaka niielezee zaidi, nitaielezea mpaka jina lake linavyojulikana kwa maulamaa wengine.
Nimepitia kidogo kuhusu elimu iyo ya ladoun nimeona ikielezwa kama elimu kutoka kwa ALLAH yeye anamruzuku amtakaye.
Neno hili ''Ladoun'' lipo pia katika Quran surat kahf aya ya 10
رَبِّ هَبْ لِى مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً - Mola wetu tupe rehma itokayo kwako
Hapo nimeona matumizi ya neno (لَدُن) - Likimaanisha ''kutoka kwa''
Lakini pia katika surat kahf aya ya 65 Inasema
“وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا'' - Tukamfundisha ilmu itokayo kwetu.
 
Nimepitia kidogo kuhusu elimu iyo ya ladoun nimeona ikielezwa kama elimu kutoka kwa ALLAH yeye anamruzuku amtakaye.
Neno hili ''Ladoun'' lipo pia katika Quran surat kahf aya ya 10
رَبِّ هَبْ لِى مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً - Mola wetu tupe rehma itokayo kwako
Hapo nimeona matumizi ya neno (لَدُن) - Likimaanisha ''kutoka kwa''
Lakini pia katika surat kahf aya ya 65 Inasema
“وَعَلَّمْنَاهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا'' - Tukamfundisha ilmu itokayo kwetu.
Sawa kabisa, ni kama nilivyokueleza juu hapo.

Njia yake ni ucha Mungu tu, nyiradi nyingi na kujiweka pekee kwa muda mrefu mbali na watu, ukifanya tahajud (meditations)tu. Soma sana kuhusu masufi (sufism), ndio wenye ustahamilivu huo.
 
LANGO LA KUZIMU LA DAR ES SALAAM

Lango kuu la kuingilia kuzimu la Upanga Dar es Salaam linajulikana kwa jina la MUSTALLAH. Ndani ya shimo la Mustallah kuna aina kumi na mbili za majini makatili sana yanayoangamiza jamii ya watu wa jiji la Dar es Salaam. Wachawi wa nchi huenda mara kwa mara shimoni kuongeza nguvu za uchawi wao, kabla ya kuingia shimoni ni lazima ufunge kwa siku tatu. Hapa tunajifunza kuwa shetani naye huwa anafunga.

Tuangalie sasa aina za haya majini ya Mustallah na kazi zao.

1. Ratafari ni jini linalosimamia laana zote za ukoo.
Wapo watu wanasema ukoo wetu unasumbuliwa sana na ugonjwa wa pumu, kisukari, presha, kutokuolewa na mambo mengi ambayo utakuta ukoo unakuwa na tatizo moja linalofanana kwa kila mwanaukoo, hili jini ndilo linasimamia laana hizo zimalize ukoo hadi kifo.

2. Muzaphari ni jini linalozuia mafanikio.
Ukitupiwa hili jini, hutaweza kufanya jambo lolote ukafanikiwa. Ukikopa shs 500,000 bank kwa ajili ya kuanza bishara, utafilisika na kuingia kwenye deni, na dhamana yako uliyoweka bank kuuzwa. Ukitaka kujiendeleza kimasomo yatatokea matatizo mengi yatakayosababisha kusimamisha masomo yako.

3. Latifu hili jini linasimamia mambo matatu, ufukara, mateso, na pesa zako kupotea katika mazingara ya ajabu ajabu.

4. Jujan ni jini linalosababisha watu kula udongo.

5. Jahad ni jini la kutorosha mali
Makarani wa bank ndio hasa wanaoadhirika na hili jini, utakuta karani anafanya kazi kwa uangalifu mkubwa, lakini kila siku ana shoti ya pesa. Pia kwenye maduka ya kawaida na hasa supermarket.

6.Hazinan hili jini linalosimamia pombe, uvutaji wa sigara, madawa ya kulevya na mirungi.

7. Jube ni jini linalosimamia utasa, vipimo vya hospitali vitaonyesha kuwa huna tatizo lakini mtoto kamwe hapatikani.

8. Sifafiru hili ni jini linalosimamia ukahaba. Likimwingia mtu yeyote, kwa siku atatembea na watu zaidi ya watano bila hamu ya mapenzi kumalizika.

9. Subian hili ni jini linalosimamia ajali. Chakula cha hili jini ni damu.
Linasababisha wanawake wasipate siku zao, wengine wanapata maumivu makali sana wakiwa katika hedhi, utasikia tumbo linakata kuanzia kushoto kwenda kulia na hali hiyo huendelea kwa muda hadi unanza kusikia maumivu makali ya mgongo.

10. Sumri jini hili linanyonga watoto wakiwa tumboni kabla ya kujifungua, pia linajihusisha na kuchukua watoto hospitali kichawi.

11. Munsar hili ni jini linalosimamia ndoa ya jinsia moja.
mwanamke kwa mwanamke au mwanamume kwa mwanamume.

12. Waidadat hili jini linasababisha vijana wa kiume kuvaa hereni, kusuka nywele na rasta.

(MOJA YA HAYO MAJINI NDIO ARSIS)
 
mkuu Arsis mimi naona kisa cha adam ni bora ungeuanzishia uzi wake tu ujitegemee sababu kisa cha adamu kina mambo mengi complex yanachanganya na jinsi ulivyoanza mbali sijui mambo ya tafsili mara lisan na tafsiri za mashkhe haya yanafaa ukiwa umesoma japo vitabu vya dini ndio utaunga doti..ushauri wangu yafungulie uzi mpya uite"UKweli Kuhusu Adam-je, ni binadamu wa kwanza kuumbwa?" maana tulianza vizuri sana kuhusu ww kufunguliwa macho tukaja visa na vionjo vya Arsis ilikuwa moto sana ila hili darasa la lisan na tafsiri na maandiko ya mashekhe inachosha tena inaboa maana inahitaji uwe na akili pana na kisomi ya kuchanganua vitu hiyo wanayo wachache humu hadi lengo la uzi mama wa visa na vionjo vya arisis linapotea fanya kusitisha hili darasa la adam lipe uzi wake linaonekana refu sana kisha turudi tuendelee kwenye Visa na vionjo vya Arsis..
Kumbuka lengo ni kutoa elimu basi ni bora uwe na nyuzi nyingi tofauti zinazojitegemea zenye elimu tofauti kwa ajili ya marejeo kuliko hii ya kutumia nyuzi moja kurundika mambo kibao yenye maudhui tofauti yasiyohusiana na yaliyotangulia haileti maana zaidi ya kuchoshana.
Naunga mkono hoja..Mimi hii sehemu ya Adam siielewi kabisa hivyo nasoma Kwa ku scan tu
 
Back
Top Bottom