Inatokea post namba 146.
Leo nitawaletea kisa cha nilivyooneshwa shemu ya kumita Arsis na kuongea nae kwa kina nikimuhoitaji.
Siku moja usiku nimevizia watu wote wamelala nyumbani, nikaiweka bakora yangu mbele yangu, nikaanza kumuita mwenye bakora kwa jina lake alilonipa, siliweki hapa. Haijapita muda nikaona ka ma kivuli, ghafla nikasikia salam nikaona mtu kakaa kwenye kiti chumani kwangu. Nikamkubuka ndio niliuonana nae mapngoni huko Duga. Tukaulizana hali, ni mtu wa kawaida tu, tena kaja kavaa kimjini kabisa, shatoi na suruali na alikua kama wa umri wa miaka 50 hivi. Akanambia unasemaje bwana mkubwa, umeniita. Nikamwabia mwenye pete yangu hii alinambia yeye hawezi kuja hapa, nikitaka wa kuja nikuite wewe. Ndio nimekuita.
Jini; Sawa, nimekuelewa, unasemaje?
Mimi: nilikua nataka kuuliza?
Jini: Mimi niulize mambo yanayohusiana na na mambo ya mitishamba na tiba zingine kwa uchache, Kuhusu mambo ya kieleimu zingine yoite muulize mwenye hiyo pete.
Mimi: Sina swali kuhusu miti shamba kwa leo.
Jini: Nilikuwekea dawa kwenye mkoba wako kule pangoni, uliiona?
Mimi: Nikamwabia niliona vipande vya vijiti vikavu vimefungwa pamoja na kamba za miti, ndio hizo?
Jini: Ndio hizo, mbona huulizi za kazi gani?
Mimi: Haikunijia kabisa kuuliza, wacha niulize sasa hivi, vijiti vya nini vile?
Jini: Vile vijiti vya zamani sana, kwanza ulle mzizi hauliwi na mdudu yoyote duniani, vile vina miaka mingi sana. Vile sio vijiti tu, ile ni dawa ina kazi kubwa sana. Kwanza wewe inatakiwa ukate kipande kidogo sana kama kucha ya kidole chako utie kwenye chai au maji ya moto, wacha mpaka chai au maji yapoe kabisa, halafu yanwe uyamalize. Hiyo itakutoa uchovu na sumu sumu zote mwilini. Fanya hivyo ukipata nafasi.
Mimi: Sawa, lakini nilisikia inatoa harufu nzuri ya manukato.
Jini: Sawa kabisa, yale sio manukato, ni harufu yake, na haiishi ile harufu hata vijiti vile vikae daima, harufu itabaki vile vile. Shani yake Mungu hio. Vijiti hivyo vile vile vinatoa uchawi wpowote mtu akilishwa na pia vinatibu matatizo ya tumbo ya kina mama, Vile vile vilivyom kama kuna mwanamke anapoteza siku zake bila mpango, zinazidi au zinapungua, au anatokwa damu kwa wingi kuliko kawaida, au anaharivu haribu uja uzito. Ukimpa kama nilivyokuelekeza Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu anakua sawa kabisa. Imewasaidia wengi sana.
Kwa ufupi, wewe unatakiwa unywe, nyinyi mnakula kula hoivyo kwa hawa kina mama wanauza vyakula, wanaweka mamboi memngi kwenye vyakula, kila kama kuna chochote hakitabaki.
Matumizi yake mengine, ni kama nilivukueleza, lakini hauinywi, unaitia kwenye jagi hivi la maji ya moto, halagfu unaiacha ikae humo wiki moja, unakogea yale maji kwa kujipaka mwili mzima mpaka yaishe, usiyamwage chini, hayo maji yanathamni kubwa sana. Hiyo itakua ni kinga yako kwa muda mrefu sana, kwa uchache unaweza kufanya hivyo kila mika mitano, basi hakuna mchawi mchawi atakae kuona kwenye mitego yake.
Mimi; Mitego yake tena?
Jini; Ndio kijana, wachawi kabla ya kukuchawi, wanakutafuta kwa njia zao, wakisha kupata wakuwekea mtego wa kichawi, huwa wanachukua kivuli chako, wanakifanyia mambo yao halafu wanakurudishia unakua kwenye mtego wao wamekunasa, wanakufanyia wanachotaka. Lakini ukijipaka hii, hawakuoni kabisa na watakuogopa wakianza kukutafuta. Ingawa nafahamu wewe vabu yako alikukinga nayo hii kuanzia utotoni lakini si vibaya na wewe ukaijua. Na itunze sana hiyto miti, haipatikani isipokua kwangu tu.
Mimi; Sawa. Sasa mimi niliongea na mwenye pete akanambia nikitaka kuongea nae atanionesha wapi pa kukutana nae, hapo unanisaidia vipi?
Jini: hapo mpaka uongee na yeye mwenyewe, mimi siwezi kuingilia maongezi yenu kabisa, itakua namvunjia heshima, ni mkubwa wangu sana mwenye hio pete. Yeye anaweza kuongelea yangu yote na wewe. Ukitaka mimi niulize ya wale mabinti wawili, watumishi wako wa hio pete, naweza kukuitia, yule mmoja mdogo wakati wowote lakini ni vizuri nalo ukaongea yeye, wale hawatakiwi kuja bila kazi, na wapo sana na wewe huwaoni tu. Mimi sipo sana na wewe mpaka uniite au itakikane dawa, mimi ulinzi wangu kwako ni hiyo bakora na dawa ninazokupa tu. Hivi nimekuja kwa kua una bakora yangu na nimekabidhiwa kwako, lakini sio kaida yangu kuja kwa maswali yasiohusiana na mitishamba.
Mimi: Ahsante kwa kuja, kwaheri.
Jini: Usione tabu lakini kuniita, wewe ni bwana mkubwa wangu, mimi niko chini ya amri zako. Nawea kuondoka?
Mimi: sawa nenda tu, kwaheri.
Basi alipoondoka nikamuita Arsis kimoyoomoyo hajachukua hata dakika moja akaniuliza kichwani, unasemaje simba?
Mimi" Arsis wewe si ulinambia unajua nataka kukuuliza nini hata kama sijakuuliza?
Arsis: Ndio, haya kama upo tayari sasa hivi, twende nikakuoneshe. Usijali uo na mimi hakuna ataekuona. Haya twende.
Mimi; Kama mbali si nichukue gari?
Jini: Haya chukua ywende, mimi utanikuta ndani ya gari. Nikwamwambia poa ngoja niombe gari. Nikampigia simu mama, nikamwambia mama natoka gari lako.
Mama; Usiku huu mwanangu?
Mimi: mama usiwe na wasiwasi kuna kazi babu alinipa nikija niifanye, ndiuo nakwenda kuimalizia.
Mama: haya baba, huyu babu yako nae kazi za usiku, mnakwenda kuwanga?
Mimi: Huku nacheka, ndio baba mkwe wako, anaifundisha kuwanga.
Mama: Yatawashinda. Usichelewe kurudi.
Mimi; poa, nikatoka, mlinzi akanifungulia hti. Ile naingia tu ndani ya gari nilipokuwa natoka getini, Sautri ya Arsis ikanijia, Akanambia tqebde viwanja vya bunge lenu kule mjini kabisa. Nikamuuliza kule njia ya Ikulu. Akasema ndio, wewe twende, ukifika gtakwambia gari uwache wapi.
Nikaenda mpaka barabara ya bunge, sauti ikanambia usisimame twende mpaka hospita ile ya wajerumani, nyie siku hizi mnaita oshen rodi. Ingiza gari kwenye parking ushuke takuelekeza unaelekea wapi. Hakuna ataekuuliza wala kukuzuwia.
Nikaenda mpoaka oshen road kuna parking kubwa tum palikua kiya kabisa mpaka panaytisha, sijakuta hata mlinzi nikawa nasukia sauti za mawimbi tu baharini. Sauti ikaja ikanambia haya fanya kama unakwenda hiyo nyumba mbele yako lakini kabla hujafika utaona njia ndogo inaenda kulia, ifate hio mpaka utakuta mbeke huko mawe mawe ndio hapo utakua umefika, Ukifika niite tu usiogope hakuna atakae kuona wewe wala mimi. Kweli nikaenda kama alivyonielekeza nikajiona kama naenda Ikulu kwa nyuma lakini kabla sijafika nyavu za ikulum, naziona kwa mbali nikaona kuna kama mawe mawe na kiwanja kizuri, pako kimya kabisa lakini taa za mjini, naziona taa za hispita naziona kwa mabali, kama mita 200 hivi. Nikaita palem kama dakika moja tu, Arsis akaingia, simuoni kama kawaida.
aRSIS; Naam, vipi hali yako?
Mimi: Salama,huku umepajuaje?
Arsis: Hapo mbele kidogo kuna mlango wa kuendea dunia nyingine, wewe huwezi kuuona, hakuna mtu anaeuona hata akiwa mchawi vipi.
Mimi; Dunia nyingine?
Arsis: Ndio, kuna dunia saba, hii tuliopo sasa hivi ni ya kwanza, zingine zinakaa viumbe wengine, si niliwahi kukwambia?
Mimi; Kweli ulinambia lakini sikuzingatia.
Arsis: Unakumbuka nilikwambia ukiniita kuongea na mimi uchukue hizi simu uwe unarekodi kila kitu, ili ukisahau ujikumbushe?
Mimi: Nakumbuka:.
Arsis; Haya: Fanya hivyo, usiogope mimi siwezi kuonekana, itasikika sauti yangu tu, na hakuna hapa anaetusikia wala kutuona nimeweka pazia.
Nikatayarisha simu yangu nikaiweka ikawa ina rikodi na kupiga picha nikaiengesha vizuri kwenyue jiwe moja nikanza kuongea nae.
Mimi; Kila nikiongea na wewe maswali yanazidi sana, sijui nianzie wapi. Wewe si ulisema unajua mimi nataka kuuliza nini? Anza kunijibuninachotaka kuuliza.
Arsis akacheka, akasema utakomaa tu, hakuna neno. Wakati naongea na simu nikaona kama vizuli halafu simu yangu ikaanguka kwa pale pale juu ya jiwe.
Arsis; Iweke sawa tu usiogope watotowa kijini hao wanachea cheza.
Mimi; Watotto wa kijini? mbina siwaoni na mimi nimefunguliwa macho?
Arsis akacheka, akanambia hawa huwezi kuwaona upoo na mimi. Usijali tuendelee. Wewe simba unataka kuuliza kuhusu dunia saba. Nikueeleze kwa uchache?
Mimi; nieleze.
Arsis; Ondoa fikra nyingi kwa sasa hivi, usiwe na haraka ya kujua mengi kwa wakati mmoja. Dunia zipo saba, ya kwanza ni hii yetu, ya pili wanaishi juju wa majuju (Gog Magog), ya tatu wanaishi majini. Ya nne wanaishi wanyama wakubwa sana ambao hapa duniani waliondoshwa wote. Ya tano wanaishi Ramadiyin. Umewahi kuwasikia Ramadiyin?
Mimi; Hapana, nadhani niliwasikia kwako mara moja tu.
Arsis: Inawezekana, lakini mimi naamini umeshawasikia lakini hujatia maanani. Hilo la siku nyingine. Kuhusu dunia ya tano. Dunia ya sita na ya saba, sina "authoirity" ya kuziongelea, kwa hiyo usiulie chochote kuhusu hizo.
Mimi : Ya nne umesem kuna wanyama?
Arsis: ndiyo kuna wanyama, wale mnaowasoma kuwa wametoweka duniani kama kina Godzila na Mammoth na wengine kama hao. Huko ni dunia ya vitu vikubwa vikubwa tu.
Arsis; hahahahaa, uliza tu usiogope, unauliza mimi ninajuaje na vipi uamini kama ni ukweli? au sivyo ulivyotaka kuuliza?
Mimi; Ndivyo nilivyotaka kuuliza. Sasa mimi naona hakuna sababu ya kujliza, wewe unajuwa fikra zangu, sifahamu vipi?
Arsis; Ni elimu tu, utaielewa kidogo kidogo. Mimi kwa sasa nina miaka inazidi elfu tano. Si ulitaka kuuliza hivyo?
Mimi: Ndiyo, unanifanya nisiulize kitu.
Arsis; Raha ya maongezi uulize, nilikua nataka uelewe kua naelewa ninachokwambi na sina sababu kukudanganya.
Mimi: Wewe ni jini au binadam au ni kiumbe wa aina gani?
Arsis: Mimi kwa sasa hivi ni mtu, lakini chukulia vyovyote upendavyo kwa kua mimi naweza kua vyovyote vile.
Mimi: Huo uwezo wa kua chochote unautoa wapi?
Arsis: Ni elimu anayotujaalia Muumba wetu. alieniumba mimi ndiye aliyeumba kila kiumbe na kila kitu ulimwenguni.
Mimi: Dunia ipi kubwa katika ulizonitajia?
Itaendelea.