Vionjo vya Arsis 1 - Pete yake.
Kuna siku nilimuuliza Arsis thamani ya hii pete alionipa. Arsis akacheka sana akanambia haijui thamani yake.
Mimi; Arsis, babu yangu alinambia hii pete ulionipa ni yako binafsi, ile uliompa yeye ni kopi ya hii kwa kutumia vitu vya hapa dunia yetu, nifahamishe zaidi kuhusu hilo.
Arsis; Kweli, zipo pete zangu tano mpaka sasa. Hio yako ilikua yangu binafsi, ni ya kipekee, imetenezwa kiustadi mkubwa sana, nilitengezewa na rafiki zangu wa dunia ya tano Ramadiyin, lakini walikataa kabisa kunambia hicho kito chake kinaitwa nini au wamekitoa wapi. Nikawuliza na na hiy pete yenyewe ni ya dhahabu au ya material ipi.? Walinambia wewe chukua hii na wakanielekeza namna ya kutengeza pete nyingine na kuzipa nguvu ya mawasiliano kwa kutumia hii yako. Nimetengeza moja nyingine kama hio lakini ya kito sio cha hapa kwenye dunia hii na nimechanganya chuma aina nyingi, ina mawasiano ya moja kwa moja na hio pete yako na zingine tatu ndio maana naweza kujua wewe unafanya nini wakati wowote, ukiivaa au usiivae, mradi ipo kwako nafahamu.
Mimi; Na zingine?
Arsis: Moja ile ya babu yako, siku hizi anavaa dada yake. Mbili za wale wasaidizi wangu alionipa Jini Bakora. Ndio hizo tu.
Mimi; Thamani yake si lazima ijulikane, hakuna kitu kisichokua na thamani.
Arsis; Sikiliza Smba, hapa kwenu wapo masonara na watu wa madini, wapelekee wakakupe thamani yake, hata mimi natamani kujua hilo.
Mimi; Ile ya babu?
Arsis: ile hata wewe unaweza kujua thamni yake, ile na ile ya wale majini wawili wanawake, ni vito vya ruby, na dhahabu imechanganywa na fedha kidogo na shaba. Huwezi kutengeza dhabu tuu ikawa ngumu.
Mimi; Ile ya babu lakini ni rangi ya silver ila kito cha damu ya mzee, zile za wanawake wa kijini kito kinafanana na cha babu lakini yake mraba kama yangu a)za wanawake wa kijini za duara. Na pete zao rangi ya dhahabu.
Arsis; Ya babu yako ni dhahabu nyeupe za wanawake ni dhahabu ya njano. Sikiliza simba, kesho nenda na wale wanawake wa kijini duka la sonara ujue thamani yake hio pete, na mimi nitakua na nyinyi. Leo atakuja yule jini mwanamke kukufundisha kitu kuhusu hio pete yako, mimi nitamfundisha atakuelekeza kuivua na kuivisha kito chake, hakuna anaeweza hata jini, bila kupata ruksa yangu au yako.
basi kweli, muda kidogo yule jini wa kike akaja akanambia ivue hio pete yako nikuoneshe namna ya kulivua hilo jiwe lake na kulirudishia. Nikaiuvua akanionesha. Ile pete yangu ilikua jiwe la mraba lakini kwa juu limetuna kiaina. kwa hini ni jiwe lenyewe lakini limefata mzunguko kwa mbali kama wa pete. Akanambia tazama nikatazama, akaiminya juu lile jiwe, kuelekea chini kwa mkono wa kulia kwa kidole gumba huku kaizuwia na mkono wa kushoto, niasikia kup, jiwe likatoka, akanambia kuirudishia ni hivi, akaliweka jiwe lini kwa ndani, akaliminya mkwa mkono wa kuliai kutokea kwa ndani kwenda nje, ikalia tena kup, akanambia tayari. Fanya wewe sasa.
Nikaiminya mara mojambili, ya tatu ikakubali, nikairudishia. Ikawa sawa.
jini1; Kama hukuusikia huo mlio ujue jiwe halijatoka kwenye pete na ukilirudishia kama hukusikia mlio ujue jiwe halijaingia.
Haya, tutaonana kesho twende kwa sonara, tumeagizwa na Arsis. nikamwambia poa. Akasema saa nne asubuhi tuwe tumeshafika kwa sonara, unapajua?
Mimi; Napajua, maduka yamejipanga mtaa wa Mkunguni pale.
Jini1; basi tukutane pale saa nne kamili, usinisahau tu nitavaa abaya.
Mimi; Poa.
Siku iliofata nikaenda nikawakuta wawili yeye na mamake, tiukasalimiana wakanambia haya sonara yoyote unaependa wewe. Tukaingia moja ya duka kubwa kubwa hivi pale Mkunguni, mlinzi akatufungulia, kuingia ndani wale wanawake mmoja akaanza, tuna pete zetu tunataka uzithaminishe, kama bei nzuri tujue. Jamaa wa dukani akawatazama mkononi, wakamwabia hizi hapa, wakamtolea pete kama nne hivi za dhahabu na moja ya kito, sio zile zao lakini moja ina kito cha Rubi, sonara akazipima zile tatu. Ile ya nne akaitazama na kidude kimoja cha machoni akawaambia hii mpaka niitoe hili jiwe kwenye pete. ruksa?
Jini 1 itoe tu.
Yule jamaa, alikua muhindi, akaichukua kifaa chake akakitoa kile kito akakitazama tena akasema hii ruby nzuri imechongwa kitaalam kabisa. Akaichungulia kama mara mbili tatu akaiweka pembeni, aksema hii pete peke yake bila jiwe, laki moja na elfu 60, hizi zingine pete ni nzito zaidi, hii moja laki tatu nahii nyingine laki mbili sitini. Hii Ruby peke yake million moja laki mbili kwa ajili yenu. mtaziuza?
Jini1; Bado hatujamaliza, mpe na hio, wakanambia mimi.
Nikaivua nikampa. Hapo ndio kasheshe likaanza, akaanza kuitazama, akasema hii inaonesha dhahabu imechanganywa kizamani sana hii. Hii ruby pia lakini sina uhakika, huku anaitazama sana ianaigeuza, akasema na hii inabidi niitoe, nikamwabia sawa.akahangaika kulitoa jiwe kwenye pete, aakatia vifaa vyake akashindwa, nikamwambia nipe nikusaidie. Akanipa nikaitoa nikampa akaipokea akaitazama pete kwanza, akaitazama mara mbili mbili, akatia kama zile koleo (pliers) zenye pua ndefu, ikawa kama anaisugua hivi, nikaona anashangaa inateleza, haisuguliki. akatoa kipande cha msasa wa chuma, akasema kidogo naisugua, haiharibiki,, nkamwabia poa, msasa ukawa
Akamwita mwenzake akamwambia hii dhahabu imechanganywa na nini? Yule aakishika akaitazama akasema sina uhakika lakini nzito sana, hii sijui wamechanganywa na chuma gani, hii bwana mpaka itiwe kwenye moto na sisi hatuna fundi hapa, tukiipima hivihivi tuanweza kula hasara, Hii lakini inaonesha ya zamani sana, hakuna mchongo huu siku hizi, sijui sonara gani huyu, umenunua wapi hii? Nikamwabia hio nimerithi.
Akaongea na mwenzake kihindi , yule akaanza kulitazama jiwe, akalitazama akasema hii ruby lakini na yenyewe ya zamani sana, hii cutting yake sijawahi kuiona na sijui inashikaje kwenye pete haitoki. Hili jiwe bwana siwezi kulithaminisha mimi ntakupa bei kama ya riby kwa uzito wake, nikamwabia sawa, akaiweka kwenye mzani wake wa vito, akalitoa akarudia mara ya pili, akamwita mwenzake, akaliweka na yeye kwenye mizani wakaongea tena kihindi.
Muhindi: Sikilizeniu jamani, hii inabidi itiwe moto au acid ili kujua dhahabu peke yake ni kiasi gani tuithaminishe. Na hili jiwe zito sana kuliko ruby ya size hiyo mara tatu, hii itakua sio ruby, sijui jiwe gani, Nawashauri nendeni Zanzibar Jewellers kule India street pale wana moto, wana acid watawapimia na hili jiwe. Akawa analiingiza jiwe haliingi, akacheka, sasa hii pete imekua ndogo au jiwe limekua kubwa? mbona haipiti kabisa? Nikamwambia nipe. aliponipa nikaweka kama nilivyofundishwa likaingia. Akanambia jamani hii pelekeni kule, haya vipi tumalizane dada?
Jini 1 akamwambia tunataka tujue thamani ya zote kwa pamoja, uli tujue tugnagawana vipi.
Muhindi: Nendeni basi kule mkijua thamani yake mnaweza kurudi hapa tutanunua.
Mimi; Poa, twendeni.
Tukaondoka mpaka Zanzibar Jewellers, mambo yakawa yale yale. wakasema hii tuipige moto, mnatupa tuksa? halafu tunaitia kwenye acid, hili jiwe ngoja niwashauri kitu. Nitawaelekeza mahali, hapa hapa karibu mwende pale wale wana mshine na kazi yao ni mawe tu, watasema thamani yake, mnaweza kuwauzia wao, lakini msiitie moto hii kabla hamjajua thamani ya hili jiwe, maana mnaweza kuiyayusha dhahabu ikawa mpaka mtengezee pete nyingine.
Tukaamua twende kwa watu wa mwawe kwa kua wapo karibu, ni pale mbele ya jamatini clock tower Dar.
Kuingia ndani bahati nikamkuta mtu wa mawe namjua siku nyingi, anaitwa Husseni Baniani,nikalitoa kabisa lile jiwe nikampa jiwe na pete, yeye alikua interested na jiwe tu, akachukua vitu vyake kama kuna kipimo kinatumia maji hivi, akanambia hiki kipimo ahakidanganyi, kinapima specific gravity, kitu kama hivo. Akaanza kupima akanipa chart moja ina uzani kwa kila aina ya germ stone na poicha picha za kila jiwe. Chart inaonesha kila jiwe na maelezo yake.
Akahangaika mwisho akanambia hii sio ruby, akasema hii labda red diamond. Akacheki, akalisugua na tupa inateleza, akanambia hili jiwe umepata wapi? hapa umelamba dume, lakini sijui jiwe gani. Hili bwana tuwachie tulipime taratibu, mie nikacheka. Akamleta sonara mmoja akampa ile pete, sonara akasema njooni muone tunachofanya, si mmeamua kuuza hili? mMaaana hii itayeyuka tutaibakisha dhahabu tu. Yule Jini akasema sawa hakuna shida, sonara akawasha gas akaiweka pete kwenye bakuli fulani la kigae akawa inaipiga moto, piga moto kweli kweli, ipo vile vile, akasema haiwezakanai, akaongeza moto, akamwita jamaa mwingine akamwita na yule Husseni, wakaipiga moto mambo yako vile vile. Yule sonara akasema tuitie kwenye acid, nikasema swa, wakafungua acid akaitia, ipo vile vile, haina hata kutoa moshi wala nini, wakamwita mzee mmoja wa kihindi, anaonesha boss wao, wakamweleza.
Akalitazama jiwe, pete ikatolewa walipokua wanajaribu kuichoma kwa acid, wakaitia kwenye maji, akawaambia pengine acid imekufa? Wakatoa kibati fulani wakakiingiza kwenye acid, haijachukua hata dakika kikayeyuka chite.Sonara akasema, hii acid mpya kabisa ndio nimeimimina sasa hivi. Wakatazamana wakaongeaongea pale. Boss wao akaelezwa kuhusu jiwe, akalitazama akamuuliza Huseni umepima weight yake. Akamwambia nimepima mpaka nahisi mizani yangu mbovu, haiwezekani jiwe hili liwe gram zaidi ya 250, muhindi akasema wewe umepima vibaya labda 2.50 sio 250. Husseni akacheka, akamwabia twende ukaone, tukaenda wote, wakapima, mhindi akasema hii mizani inataka ifanyiw calibration, ngoja nileta yangu, kaingia ofisini kwake akatoka na mizani yake ya digital, mambo yale yale, haamini macho yake. Akasema hii pelekeni kwenye mashine kubwa kule TGC, akatuelekeza, nikasema poa. akasema na hio pete wapeni waitest, pale mtapata jibu kitaalam lakini watawa charge gharazama za kupima kwa sababu biashra yao ni vipimo tu.
Husseni akasema sikiliza, mimi nachukua risk, hilo jiwe lamba million mbili mimi nikafe nalo, hio pete baki nayo mwenyewe utaweka jiwe lingine. Nikamwambia hapana, zinaenda pamoja, Nikalirudishia jiwe lamngu tukaondoka. Kutoka nje tukaagana na majini wale wa kike, wakaondoka zao, nafika nyumbani, kalba sija paki vizuri gari nikamsikia Arsis, umeona mambo? Utahangaika dunia nzima, una kitu ambacho hakina thamani yaani "priceless".
Hicho ndio kisa cha pete ya Arsis kwa uchache.
Itaendelea kwa kionjo kingine cha Arsis.