Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ngoja nifanye urafiki na Arsis na Jini la bakora mtanikoma humu JF.

Simba Corazon Espinado niazime bakora yako, wewe umeiweka show tu huitumii.
Ile mpaka ukabidhwe na wenyewe mimi hata nikikuazima hauishiki, inakuponyoka kimaajabu.

Mke wangu kila siku ana mchezo kujaribu kuivua vua pete yangu, anashindwa kuitoa kidoleni, anambia hii imekubana sana itakuumiza kidole haitoki, basi anamimina mpaka mafuta yao kidopo iteleze, haitoki. Kuna siku kajaribu wee kashindwa, mimi nikaivua ikatoka free kabisa nikampa aivae, haikuingia kidole chake hata kidogo, kila akiingza ikipita kwenye kucha tu haiingii kabisa. Mpaka siku hizi kachoka, na anaiogopa haigusi tena.

Ile pete ina kisa kirefu sana kwa masonara wa Dar. Ngoja nikilete kama kionjo cha Arsis.
 
Hicho kitabu Arsis alishakiongelea kwangu sana tu. Nikumbushe nilete katika safu mpya zinazokuja za "vionjo vya Arsis".

Ngoja nitafute mkanda waInao
Inaonekana anajua vitu vingi sana.
Usisahau kuteta habari zake nitakuwa nakukumbusha pia.
Kwa ninavyofahamu mimi kitabu hiki kiliandikwa na Ahmad Al Buni alipokuwa anaishi Algeria na kilipigwa chapa yake huko Beirut mamlaka ya saudia Arabia ilikifungia kitabu hiki kisifundishwe kwani kinafundisha mambo ya uchawi na jinsi ya ku summon majini kitu ambacho ni kufru katika uislamu.
Ila natamani kujua Arsis ana mtazamo gani katika kitabu hiki
 
Sorry, Uislamu wote kwangu sio dini sahihi, ni ushirikina mtupu, mmejiunganisha sana na majini kwenye mambo yenu mpaka nashindwa kuiona nguvu ya Mungu na uwezo wake kwenye kutatua shida zenu.

Matatizo yenu mengi mnatatuliwa na majini, huku jina la Mungu mkilitaja juu juu tu ili ionekane mnamuamini, nashangaa nikimsoma huyu mleta story kuna mahali mpaka inaonekana Quran inashindwa kuondoa majini kwa wagonjwa, ila jini la mgonjwa linaondolewa na jini lingine {refer. mwanamke aliyetolewa jini na jini la mleta story Shinyanga}, sasa nyie msaada wenu mnaupata kwa Mungu au majini?!

Hii story nawaambia ukweli, imekuja kuivua nguo kabisa dini yenu, na kitabu chenu, na ndio maana nikimsoma faiza foxy kwenye hii story anaonekana kuipotezea, kama kukipuuza kile mleta mada anachoandika, ni kwasababu ameshaona dini yake anayoipigania humu kila siku, ina muunganiko wa moja kwa moja na majini, anaona aibu anajaribu kuificha, lakini haifichiki!.

Pesa za jamii ya waarabu wengi ni kwa msaada wa majini, sio Mungu, kufanikiwa kwenye mambo mengine kama safarini ni kwa ulinzi wa majini, sio Mungu, wengine wenu mnayaafuga majini ndani, mimi nitashangaa sana kama siku ikifika nikamuona muislamu yeyote wa hii dunia ameurithi ufalme wa Mungu, unless muwe na hiyo pepo yenu wenyewe ya mabikra 72!, lakini sio yule Mungu wa rohoni ninae mwabudu mimi na kumtumikia, kwa jina la Yesu Kristu wa Nazareth.


Uislam uko mbali na ushirikina na unaupiga vita kweli kweli.

Shirki ndio dhambi kubwa kuliko zote katika Uislam

‘‘Verily Shirk is a great injustice.’’
[Sūrah Luqmān 31:13]
"Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa. "


Na ndio dhambi ambayo mtu akifa bila kutubia hatosamehewa.

‘‘Verily Allāh does not forgive that Shirk be made with Him, but He forgives whatever is below that to whomever He wishes.’’
[Sūrah-Nisāʾ 4:48]
"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. "

Shirki inasababisha mfanyaji aharamishiwe pepo

‘‘Verily whosoever associates partners with Allāh, then indeed Allāh has made Paradise unlawful for him, and his station is the Fire. And the transgressors will not have any helpers.’’
[Sūrah al-Māʾidah 5:72]
"Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru"

Shirki inaharibu amali zote njema anazozifanya mtu, zinabomoka. Swala, funga, hijja na ibada nyengine za mtu na amali zake njema zinaharibika na kuporomoka kwa sababu ya shirki

‘‘And if they associate others with Allāh, whatever they have done is nullified.’’
[Sūrah-Anʿām 6:88]
"Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda."

‘‘And it was already revealed to you and to those before you, that if you should associate anything with Allāh, your work would surely become worthless, and you would surely be amongst the losers.’’
[Sūrah al-Zumar 39:65]
"Na kwa yakini yamefunuliwa kwako na kwa walio kuwa kabla yako: Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri"

Na aya nyengine nyingi pamoja na dalili kutoka katika Sunnah. Itoshe tu kumshirikisha Allah kuwa ni dhambi kubwa kuliko zote na inayomtoa mtu katika Uislam.

Haya mambo ya ushirikina na kuwatumia majini ni mambo mbali na Uislam. Ushirikina unamtoa mtu katika Uislam. Ni dhambi inayomtoa mtu katika Uislam. Ni kichenguzi kikuu cha Uislam.
 
Mtoa mada hayo ni maarifa ya Dunia nyingine kabisa.
Ambayo binadamu hatukupewa.
Nadhani kwa sababu maalum.
Ndio maana naifuatilia.
We endelea tu kushusha Nondo.
Kwa uhalisia hayo maarifa sio yetu sisi wanadamu.
Ni Siri za ufalme mwingine.
Kuna siku Arsis tulikua tunaongea kuhusu viumbe wenye nguvu na maarifa zaidi katika viumbe avijuavyo. Akanijibu Binadam anawashinda wote kasoro kuna viumbe wanaishi dunia ya nne tano, wanaitwa Ramadiyin. anesema hao pekee ndio wana nguvu, wana uwezo na wana akili aidi ya binbdam, Anasema hao wako 12 tu ndio idadi yao.

Mmoja wao tu anaweza kutuangamiza sisi wote, wakiwa wawili wanaweza kuangamiza kila cha duniani ikabaki tupu kama imevuliwa nguo.
 
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِىٍّ عَدُوًّا شَيَٰطِينَ ٱلْإِنسِ وَٱلْجِنِّ يُوحِى بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ ٱلْقَوْلِ غُرُورًا وَلَوْ شَآءَ رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ

And thus We have made for every prophet an enemy - devils from mankind and jinn, inspiring to one another decorative speech in delusion. But if your Lord had willed, they would not have done it, so leave them and that which they invent.
"Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet'ani wa kiwatu, na kijini, wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli penda Mola wako Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na wanayo yazua."

(Suurat An'aam: 112)
 
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا يَٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ قَدِ ٱسْتَكْثَرْتُم مِّنَ ٱلْإِنسِ وَقَالَ أَوْلِيَآؤُهُم مِّنَ ٱلْإِنسِ رَبَّنَا ٱسْتَمْتَعَ بَعْضُنَا بِبَعْضٍ وَبَلَغْنَآ أَجَلَنَا ٱلَّذِىٓ أَجَّلْتَ لَنَا قَالَ ٱلنَّارُ مَثْوَىٰكُمْ خَٰلِدِينَ فِيهَآ إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ

"And on the Day when He will gather them (all) together (and say): "O you assembly of jinns! Many did you mislead of men," and their Auliya' (friends and helpers, etc.) amongst men will say: "Our Lord! We benefited one from the other, but now we have reached our appointed term which You did appoint for us." He will say: "The Fire be your dwelling-place, you will dwell therein forever, except as Allah may will. Certainly your Lord is All-Wise, All-Knowing."

"Na ile Siku atapo wakusanya wote awaambie: Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu. Na marafiki zao katika wanaadamu waseme: Mola Mlezi wetu! Tulinufaishana sisi na wao. Na tumefikia ukomo wetu ulio tuwekea. Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndio makaazi yenu, mtadumu humo, ila apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hikima, na Mwenye kujua."

(Suurat An'aam: 128)
 
Kama tuna anza kulinganisha haya maelezo ya mtoa mada na dini flani sioni kama mada itakuwa na mantiki.

Hebu tuache Imani zetu pembeni na tusikilize maarifa mapya ya mtoa mada.

La sivyo kuna mahali tutaanza kumshambilia mtoa mada.

Habari za dini tayari tunazo kwenye vitabu vyetu.
Na hazijaongelea kinachoelezwa na mtoa mada.

Wengine tunataka kusikiliza kile tu kinachoelezwa na mtoa mada.
 
Tuombe tusome hiki kisa kama jinsi mtoa mada anavyokileta na si vinginevyo,kitendo cha kuhusisha uislamu kwa baadhi ya watu humu si sahihi kabisa kwakuwa hamjui lolote juu ya uislamu.

Mfano hakuna jini mzuri anayekaa au kumuingia mwanadamu,na hii hata kwa baadhi ya waislamu hawajui,utasikia mm nina jini mzuri,huyo siyo mzuri ana maslahi yake

Allah anasma sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu,sasa kama hivyo ndivyo je iweje jini au ruhani aje kuishi kichwani au mwilini kwa mtu?

Majini wema wanafanya ibada zao.kwa Allah na wana maisha yao huko.

Pili,wasio waislamu huwa wanaona majini ni vitu vya ajabu sana,ishu ni kwamba hamna elimu yao,yaan kuwakataa majini ni sawa na kukataa kuwa wanyama sio viumbe wa Mungu,kama hamkatai wanyama sio viumbe wa Mungu kwanini mnakataa majini na kuwaona ni wa ajabu sana.

Hao ni viumbe wa Mungu,wameumbwa kwa moto,wana maisha yao huko,wanauwezo wa kujibadilisha kwa namna watakavyo na mambo kadha wa kadha

Wapo waislamu na wakristo pia,wapo wema na wabaya pia,wana majeshi,waimbaji kifupi kama binadamu walivyo,walevi nakadhalika.

Kwahiyo kama una imani yako.mbovu juu ya uislamu na majini,ebu jifunze zaidi kuna mengu huyajui

Mwisho kuna mengi arsis amesema sio sawa kwa maana yana utata sana na vitabu vyetu vya dini,yeye ni kiumbe pia wa Mungu tusimchukulie anajua kweli yote,tumsome lakini akili kichwani kwako
 
Tuombe tusome hiki kisa kama jinsi mtoa mada anavyokileta na si vinginevyo,kitendo cha kuhusisha uislamu kwa baadhi ya watu humu si sahihi kabisa kwakuwa hamjui lolote juu ya uislamu.

Mfano hakuna jini mzuri anayekaa au kumuingia mwanadamu,na hii hata kwa baadhi ya waislamu hawajui,utasikia mm nina jini mzuri,huyo siyo mzuri ana maslahi yake

Allah anasma sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu,sasa kama hivyo ndivyo je iweje jini au ruhani aje kuishi kichwani au mwilini kwa mtu?

Majini wema wanafanya ibada zao.kwa Allah na wana maisha yao huko.

Pili,wasio waislamu huwa wanaona majini ni vitu vya ajabu sana,ishu ni kwamba hamna elimu yao,yaan kuwakataa majini ni sawa na kukataa kuwa wanyama sio viumbe wa Mungu,kama hamkatai wanyama sio viumbe wa Mungu kwanini mnakataa majini na kuwaona ni wa ajabu sana.

Hao ni viumbe wa Mungu,wameumbwa kwa moto,wana maisha yao huko,wanauwezo wa kujibadilisha kwa namna watakavyo na mambo kadha wa kadha

Wapo waislamu na wakristo pia,wapo wema na wabaya pia,wana majeshi,waimbaji kifupi kama binadamu walivyo,walevi nakadhalika.

Kwahiyo kama una imani yako.mbovu juu ya uislamu na majini,ebu jifunze zaidi kuna mengu huyajui

Mwisho kuna mengi arsis amesema sio sawa kwa maana yana utata sana na vitabu vyetu vya dini,yeye ni kiumbe pia wa Mungu tusimchukulie anajua kweli yote,tumsome lakini akili kichwani kwako
Kidogo imeongea vizuri.
Ila unapotosha unaposema Kuna Majini Wakristo.

Tuache tu Majini wawe Waislamu na inatosha.

La sivyo nitakuomba uweke Aya inayoeleza Ukristo wa Majini.
Ni wapi Majini walibatizwa na kuwa Wakristo?

Tusianze kumchangamya mtoa mada kwa mambo ya Imani zetu.
 
Kidogo imeongea vizuri.
Ila unapotosha unaposema Kuna Majini Wakristo.

Tuache tu Majini wawe Waislamu na inatosha.

La sivyo nitakuomba uweke Aya inayoeleza Ukristo wa Majini.
Ni wapi Majini walibatizwa na kuwa Wakristo?

Tusianze kumchangamya mtoa mada kwa mambo ya Imani zetu.
Ndo hayo ninayo sema kwakuwa huna elimu ya kitu haimaanishi kuwa jambo hilo halipo

Sipo hapa kukuaminisha hilo

Tuendelee kusoma mada

Asante
 
Tuombe tusome hiki kisa kama jinsi mtoa mada anavyokileta na si vinginevyo,kitendo cha kuhusisha uislamu kwa baadhi ya watu humu si sahihi kabisa kwakuwa hamjui lolote juu ya uislamu.

Mfano hakuna jini mzuri anayekaa au kumuingia mwanadamu,na hii hata kwa baadhi ya waislamu hawajui,utasikia mm nina jini mzuri,huyo siyo mzuri ana maslahi yake

Allah anasma sikuumba majini na watu isipokuwa waniabudu,sasa kama hivyo ndivyo je iweje jini au ruhani aje kuishi kichwani au mwilini kwa mtu?

Majini wema wanafanya ibada zao.kwa Allah na wana maisha yao huko.

Pili,wasio waislamu huwa wanaona majini ni vitu vya ajabu sana,ishu ni kwamba hamna elimu yao,yaan kuwakataa majini ni sawa na kukataa kuwa wanyama sio viumbe wa Mungu,kama hamkatai wanyama sio viumbe wa Mungu kwanini mnakataa majini na kuwaona ni wa ajabu sana.

Hao ni viumbe wa Mungu,wameumbwa kwa moto,wana maisha yao huko,wanauwezo wa kujibadilisha kwa namna watakavyo na mambo kadha wa kadha

Wapo waislamu na wakristo pia,wapo wema na wabaya pia,wana majeshi,waimbaji kifupi kama binadamu walivyo,walevi nakadhalika.

Kwahiyo kama una imani yako.mbovu juu ya uislamu na majini,ebu jifunze zaidi kuna mengu huyajui

Mwisho kuna mengi arsis amesema sio sawa kwa maana yana utata sana na vitabu vyetu vya dini,yeye ni kiumbe pia wa Mungu tusimchukulie anajua kweli yote,tumsome lakini akili kichwani kwako
Aseielewa hapa hawezi elewa tena itoshe kusema kuwa watu wengi hawana uelewa na majini hata waislamu wengi hawajui ukweli kuhusu majini nikuombe bwana Corazon Espinado endelea na story wengine tunataka kujifunza wanaoleta mambo ya kuhusanisha huu uzi na dini ya uislamu wapoteze wewe shusha episode Simba.
 
Kuna siku Arsis tulikua tunaongea kuhusu viumbe wenye nguvu na maarifa zaidi katika viumbe avijuavyo. Akanijibu Binadam anawashinda wote kasoro kuna viumbe wanaishi dunia ya nne tano, wanaitwa Ramadiyin. anesema hao pekee ndio wana nguvu, wana uwezo na wana akili aidi ya binbdam, Anasema hao wako 12 tu ndio idadi yao.

Mmoja wao tu anaweza kutuamngamiza sisi wote, wakiwa wawili wanaweza kuangamiza kila cha duniani ikabaki gtupu kama imevuliwa nguo.
Hawa viumbe ndio nasikia leo Ramadiyin.
Nita research kidogo about them.
Endelea kushusha episode simba
 
Vionjo vya Arsis 1 - Pete yake.

Kuna siku nilimuuliza Arsis thamani ya hii pete alionipa. Arsis akacheka sana akanambia haijui thamani yake.

Mimi; Arsis, babu yangu alinambia hii pete ulionipa ni yako binafsi, ile uliompa yeye ni kopi ya hii kwa kutumia vitu vya hapa dunia yetu, nifahamishe zaidi kuhusu hilo.

Arsis; Kweli, zipo pete zangu tano mpaka sasa. Hio yako ilikua yangu binafsi, ni ya kipekee, imetenezwa kiustadi mkubwa sana, nilitengezewa na rafiki zangu wa dunia ya tano Ramadiyin, lakini walikataa kabisa kunambia hicho kito chake kinaitwa nini au wamekitoa wapi. Nikawuliza na na hiy pete yenyewe ni ya dhahabu au ya material ipi.? Walinambia wewe chukua hii na wakanielekeza namna ya kutengeza pete nyingine na kuzipa nguvu ya mawasiliano kwa kutumia hii yako. Nimetengeza moja nyingine kama hio lakini ya kito sio cha hapa kwenye dunia hii na nimechanganya chuma aina nyingi, ina mawasiano ya moja kwa moja na hio pete yako na zingine tatu ndio maana naweza kujua wewe unafanya nini wakati wowote, ukiivaa au usiivae, mradi ipo kwako nafahamu.

Mimi; Na zingine?

Arsis: Moja ile ya babu yako, siku hizi anavaa dada yake. Mbili za wale wasaidizi wangu alionipa Jini Bakora. Ndio hizo tu.

Mimi; Thamani yake si lazima ijulikane, hakuna kitu kisichokua na thamani.
Arsis; Sikiliza Smba, hapa kwenu wapo masonara na watu wa madini, wapelekee wakakupe thamani yake, hata mimi natamani kujua hilo.

Mimi; Ile ya babu?

Arsis: ile hata wewe unaweza kujua thamni yake, ile na ile ya wale majini wawili wanawake, ni vito vya ruby, na dhahabu imechanganywa na fedha kidogo na shaba. Huwezi kutengeza dhabu tuu ikawa ngumu.

Mimi; Ile ya babu lakini ni rangi ya silver ila kito cha damu ya mzee, zile za wanawake wa kijini kito kinafanana na cha babu lakini yake mraba kama yangu a)za wanawake wa kijini za duara. Na pete zao rangi ya dhahabu.

Arsis; Ya babu yako ni dhahabu nyeupe za wanawake ni dhahabu ya njano. Sikiliza simba, kesho nenda na wale wanawake wa kijini duka la sonara ujue thamani yake hio pete, na mimi nitakua na nyinyi. Leo atakuja yule jini mwanamke kukufundisha kitu kuhusu hio pete yako, mimi nitamfundisha atakuelekeza kuivua na kuivisha kito chake, hakuna anaeweza hata jini, bila kupata ruksa yangu au yako.

basi kweli, muda kidogo yule jini wa kike akaja akanambia ivue hio pete yako nikuoneshe namna ya kulivua hilo jiwe lake na kulirudishia. Nikaiuvua akanionesha. Ile pete yangu ilikua jiwe la mraba lakini kwa juu limetuna kiaina. kwa hini ni jiwe lenyewe lakini limefata mzunguko kwa mbali kama wa pete. Akanambia tazama nikatazama, akaiminya juu lile jiwe, kuelekea chini kwa mkono wa kulia kwa kidole gumba huku kaizuwia na mkono wa kushoto, niasikia kup, jiwe likatoka, akanambia kuirudishia ni hivi, akaliweka jiwe lini kwa ndani, akaliminya mkwa mkono wa kuliai kutokea kwa ndani kwenda nje, ikalia tena kup, akanambia tayari. Fanya wewe sasa.

Nikaiminya mara mojambili, ya tatu ikakubali, nikairudishia. Ikawa sawa.
jini1; Kama hukuusikia huo mlio ujue jiwe halijatoka kwenye pete na ukilirudishia kama hukusikia mlio ujue jiwe halijaingia.
Haya, tutaonana kesho twende kwa sonara, tumeagizwa na Arsis. nikamwambia poa. Akasema saa nne asubuhi tuwe tumeshafika kwa sonara, unapajua?
Mimi; Napajua, maduka yamejipanga mtaa wa Mkunguni pale.
Jini1; basi tukutane pale saa nne kamili, usinisahau tu nitavaa abaya.
Mimi; Poa.


Siku iliofata nikaenda nikawakuta wawili yeye na mamake, tiukasalimiana wakanambia haya sonara yoyote unaependa wewe. Tukaingia moja ya duka kubwa kubwa hivi pale Mkunguni, mlinzi akatufungulia, kuingia ndani wale wanawake mmoja akaanza, tuna pete zetu tunataka uzithaminishe, kama bei nzuri tujue. Jamaa wa dukani akawatazama mkononi, wakamwabia hizi hapa, wakamtolea pete kama nne hivi za dhahabu na moja ya kito, sio zile zao lakini moja ina kito cha Rubi, sonara akazipima zile tatu. Ile ya nne akaitazama na kidude kimoja cha machoni akawaambia hii mpaka niitoe hili jiwe kwenye pete. ruksa?
Jini 1 itoe tu.

Yule jamaa, alikua muhindi, akaichukua kifaa chake akakitoa kile kito akakitazama tena akasema hii ruby nzuri imechongwa kitaalam kabisa. Akaichungulia kama mara mbili tatu akaiweka pembeni, aksema hii pete peke yake bila jiwe, laki moja na elfu 60, hizi zingine pete ni nzito zaidi, hii moja laki tatu nahii nyingine laki mbili sitini. Hii Ruby peke yake million moja laki mbili kwa ajili yenu. mtaziuza?
Jini1; Bado hatujamaliza, mpe na hio, wakanambia mimi.

Nikaivua nikampa. Hapo ndio kasheshe likaanza, akaanza kuitazama, akasema hii inaonesha dhahabu imechanganywa kizamani sana hii. Hii ruby pia lakini sina uhakika, huku anaitazama sana ianaigeuza, akasema na hii inabidi niitoe, nikamwabia sawa.akahangaika kulitoa jiwe kwenye pete, aakatia vifaa vyake akashindwa, nikamwambia nipe nikusaidie. Akanipa nikaitoa nikampa akaipokea akaitazama pete kwanza, akaitazama mara mbili mbili, akatia kama zile koleo (pliers) zenye pua ndefu, ikawa kama anaisugua hivi, nikaona anashangaa inateleza, haisuguliki. akatoa kipande cha msasa wa chuma, akasema kidogo naisugua, haiharibiki,, nkamwabia poa, msasa ukawa

Akamwita mwenzake akamwambia hii dhahabu imechanganywa na nini? Yule aakishika akaitazama akasema sina uhakika lakini nzito sana, hii sijui wamechanganywa na chuma gani, hii bwana mpaka itiwe kwenye moto na sisi hatuna fundi hapa, tukiipima hivihivi tuanweza kula hasara, Hii lakini inaonesha ya zamani sana, hakuna mchongo huu siku hizi, sijui sonara gani huyu, umenunua wapi hii? Nikamwabia hio nimerithi.

Akaongea na mwenzake kihindi , yule akaanza kulitazama jiwe, akalitazama akasema hii ruby lakini na yenyewe ya zamani sana, hii cutting yake sijawahi kuiona na sijui inashikaje kwenye pete haitoki. Hili jiwe bwana siwezi kulithaminisha mimi ntakupa bei kama ya riby kwa uzito wake, nikamwabia sawa, akaiweka kwenye mzani wake wa vito, akalitoa akarudia mara ya pili, akamwita mwenzake, akaliweka na yeye kwenye mizani wakaongea tena kihindi.

Muhindi: Sikilizeniu jamani, hii inabidi itiwe moto au acid ili kujua dhahabu peke yake ni kiasi gani tuithaminishe. Na hili jiwe zito sana kuliko ruby ya size hiyo mara tatu, hii itakua sio ruby, sijui jiwe gani, Nawashauri nendeni Zanzibar Jewellers kule India street pale wana moto, wana acid watawapimia na hili jiwe. Akawa analiingiza jiwe haliingi, akacheka, sasa hii pete imekua ndogo au jiwe limekua kubwa? mbona haipiti kabisa? Nikamwambia nipe. aliponipa nikaweka kama nilivyofundishwa likaingia. Akanambia jamani hii pelekeni kule, haya vipi tumalizane dada?
Jini 1 akamwambia tunataka tujue thamani ya zote kwa pamoja, uli tujue tugnagawana vipi.
Muhindi: Nendeni basi kule mkijua thamani yake mnaweza kurudi hapa tutanunua.
Mimi; Poa, twendeni.

Tukaondoka mpaka Zanzibar Jewellers, mambo yakawa yale yale. wakasema hii tuipige moto, mnatupa tuksa? halafu tunaitia kwenye acid, hili jiwe ngoja niwashauri kitu. Nitawaelekeza mahali, hapa hapa karibu mwende pale wale wana mshine na kazi yao ni mawe tu, watasema thamani yake, mnaweza kuwauzia wao, lakini msiitie moto hii kabla hamjajua thamani ya hili jiwe, maana mnaweza kuiyayusha dhahabu ikawa mpaka mtengezee pete nyingine.

Tukaamua twende kwa watu wa mwawe kwa kua wapo karibu, ni pale mbele ya jamatini clock tower Dar.

Kuingia ndani bahati nikamkuta mtu wa mawe namjua siku nyingi, anaitwa Husseni Baniani,nikalitoa kabisa lile jiwe nikampa jiwe na pete, yeye alikua interested na jiwe tu, akachukua vitu vyake kama kuna kipimo kinatumia maji hivi, akanambia hiki kipimo ahakidanganyi, kinapima specific gravity, kitu kama hivo. Akaanza kupima akanipa chart moja ina uzani kwa kila aina ya germ stone na poicha picha za kila jiwe. Chart inaonesha kila jiwe na maelezo yake.


Akahangaika mwisho akanambia hii sio ruby, akasema hii labda red diamond. Akacheki, akalisugua na tupa inateleza, akanambia hili jiwe umepata wapi? hapa umelamba dume, lakini sijui jiwe gani. Hili bwana tuwachie tulipime taratibu, mie nikacheka. Akamleta sonara mmoja akampa ile pete, sonara akasema njooni muone tunachofanya, si mmeamua kuuza hili? mMaaana hii itayeyuka tutaibakisha dhahabu tu. Yule Jini akasema sawa hakuna shida, sonara akawasha gas akaiweka pete kwenye bakuli fulani la kigae akawa inaipiga moto, piga moto kweli kweli, ipo vile vile, akasema haiwezakanai, akaongeza moto, akamwita jamaa mwingine akamwita na yule Husseni, wakaipiga moto mambo yako vile vile. Yule sonara akasema tuitie kwenye acid, nikasema swa, wakafungua acid akaitia, ipo vile vile, haina hata kutoa moshi wala nini, wakamwita mzee mmoja wa kihindi, anaonesha boss wao, wakamweleza.

Akalitazama jiwe, pete ikatolewa walipokua wanajaribu kuichoma kwa acid, wakaitia kwenye maji, akawaambia pengine acid imekufa? Wakatoa kibati fulani wakakiingiza kwenye acid, haijachukua hata dakika kikayeyuka chite.Sonara akasema, hii acid mpya kabisa ndio nimeimimina sasa hivi. Wakatazamana wakaongeaongea pale. Boss wao akaelezwa kuhusu jiwe, akalitazama akamuuliza Huseni umepima weight yake. Akamwambia nimepima mpaka nahisi mizani yangu mbovu, haiwezekani jiwe hili liwe gram zaidi ya 250, muhindi akasema wewe umepima vibaya labda 2.50 sio 250. Husseni akacheka, akamwabia twende ukaone, tukaenda wote, wakapima, mhindi akasema hii mizani inataka ifanyiw calibration, ngoja nileta yangu, kaingia ofisini kwake akatoka na mizani yake ya digital, mambo yale yale, haamini macho yake. Akasema hii pelekeni kwenye mashine kubwa kule TGC, akatuelekeza, nikasema poa. akasema na hio pete wapeni waitest, pale mtapata jibu kitaalam lakini watawa charge gharazama za kupima kwa sababu biashra yao ni vipimo tu.


Husseni akasema sikiliza, mimi nachukua risk, hilo jiwe lamba million mbili mimi nikafe nalo, hio pete baki nayo mwenyewe utaweka jiwe lingine. Nikamwambia hapana, zinaenda pamoja, Nikalirudishia jiwe lamngu tukaondoka. Kutoka nje tukaagana na majini wale wa kike, wakaondoka zao, nafika nyumbani, kalba sija paki vizuri gari nikamsikia Arsis, umeona mambo? Utahangaika dunia nzima, una kitu ambacho hakina thamani yaani "priceless".


Hicho ndio kisa cha pete ya Arsis kwa uchache.

Itaendelea kwa kionjo kingine cha Arsis.
 
Back
Top Bottom