Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Nina swali ndugu yangu .... Hivi kuongea ongea sana inaathari gani kwenye maswala ya kiroho?!

Maana huwa naona siku mtu ukipiga porojo sana n kama Kuna kitu unapoteza (tofaut na ukiwa kimya zaid
 
Wewe ni Gnostic?
 
Watu wengi sana humu huwa hawamalizi visa vyao humu
Ujuaji wa baadhi ya member, husababisha watu waache kumalizia visa vyao.

Imagine mtu kwa mapenzi yake, kaamua kupoteza mda wake kushare maarifa, ili wengine wajifunze, alafu watu wajinga wajinga wanareply upuuzi as if wanamlipa.

Binafsi, nilitaka kushare baadhi ya vitabu nilivyosoma maktaba za kiroho, kama kupima DNA kwa njia ya namba bt kwa hali hii ni ngumu.

watu wanapaswa itumia mitandao kama platform ya kujifunza & kushare maarifa, na si kutukana na kuleta ujuaji usio na tija.
 
Akijibu Nistue Niachie kuongea hovyo
Hii kitu Thecoder kaiongelea kwenye uzi wake wa hatma. Kuwa kuna watu wana asili ya nguvu hasi kundi hili ndo wale roho mbaya nk

Ukikutana na mtu wa hivi ukaanza kumsimulia simulia mambo yako lazma tu yavurugike.
Hii kitu ina ukweli 100% ukiwa na mipango yako ukaisimulia simulia haifanikiwi aseee ila ukiifanya kimya kimya mambo ni bam bam
 
Mkuu Uko Sahihi Kabisa lakini Ukumbuke Wapo Watu Hadi Dakika hii Wanamkosoa Mungu wameenda mbali Zaidi Hadi kumtukana. Mimi na Wewe ni nani? Mawazo yangu Nafikiri kama mtu anakitu chake Asiache Kushare humu Watu Wapate mwanga!! Kwasababu ya Watu Wachache Wajuaji wa Kila kitu". #Toa Elimu Jamii ijifunze Kupitia wewe kwa ajili Ya Future generation.
 
Huna nia ya kusaidia mkuu, hata Melo angekua na mindset kama yako hii reply yako leo isingekuwepo.

Punguza ego na share unachokifahamu, kama huwezi kupuuza -ve comments za waja basi hivyo vitabu havijakusaidia bado.

Nadhani Arsis ni muda tu anakosa, DR Mambo Jambo nae mambo mengi na sio kua wanakwamishwa na comments za waja.
 
Nimeipenda hii

Huu uzi sometime hauleti status ndio maana hatujui kinachoendelea,yan leo nimeukumbuka tu nikautafuta

Doktori nakupenda kwa ajili ya Allah una tuvituvitu vitamu sana boss
 
Nimeipenda hii

Huu uzi sometime hauleti status ndio maana hatujui kinachoendelea,yan leo nimeukumbuka tu nikautafuta

Doktori nakupenda kwa ajili ya Allah una tuvituvitu vitamu sana boss
Uwe unachungulia chungulia ndugu.
Huu uzi mwenyewe kuna muda sipati notification kabisa
 
Natamani wapinga mungu wa humu jf wajione hapa
 
Boss una point unatakiwa usikilizwe ila tambua kwamba kwenye wengi kuna mengi pia

Kwahiyo usitunyime maarifa sisi ambao tunapenda kujifunza boss wangu

Fanya kitu kimoja,toa maarifa kisha wapotezee wote ambao wanaleta ujinga,na huo ndio ukomavu

Asante
 
Mimi nawausia tu ndugu zangu Waislam, tumche Allah. Tukae mbali na ushirikina na turudi katika Tawheed na tushikamane na Sunnah. Mashaytwaan hawa (wa kijini na kibinadamu) watatupoteza, namuomba Allah afya na salama.

Haifai kuwatumia majini (hata kama watasema ni Waislam) wala kuwafuata eti mkasome kwao. Kuna watu mpaka mnawauliza maswali ya kielimu na wanawapotosha. Watawapotosha na kuwatoa katika njia.

Bakini katika njia ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) na Swahaba zake (Allah awaridhie).

Mashetani wanawadanganya. Huyo Arsis ni katika mashetani tu. Mcheni Allah ndugu zangu.

Maneno mazuri zaidi ni Kitabu cha Allah na Muongozo bora ni Muongozo wa Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake).

Nawanasihi ndugu zangu Waislam, msizingatie haya mambo, yatawatumbukiza katika Ushirikina na kuwaondoa katika Tawheed na kuwaondoa katika muongozo wa Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Allah atuongoze katika njia iliyonyooka na atuthibitishe mioyo yetu katika Dini yake na atuhifadhi na atufishe katika Uislam, atufishe katika Tawheed na Sunnah, Allahumma Aamiin.



Mimi nimefikisha tu.
 
Acha kukurupuka!!!
 
Acha kukurupuka!!!
Wewe ni Muislam? Kama wewe ni Muislam nakuusia kumcha Allah na kutozugwa na kuingia katika haya mambo. Ridhika na Muongozo wa Mtume wako (Swala na Salamu ziwe juu yake), baki katika njia ya Maswahaba (Allah awaridhie).


Achana na mashetani, watakupoteza.

Mtu unamuuliza shetani maswali ya kidini? Yaani seriously unamuuliza shetani!? Unatarajia nini? Adui ambaye hakuonei huruma kabisa!

Unatakiwa umuombe Allah akukinge kutokamana na Shetani, wewe unamfuata shetani kujifunza mambo kwake ikiwemo ya kidini?

Allah atuongoze katika njia iliyonyooka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…