Sasa Nachotaka Ufute mawazo yote uliyowahi Kuambiwa na Dini Kuhusu Haya makanisa..
Kila Siku huwa Namwambia hata Mchungaji wa Jf Rabboni Kuwa biblia Imesukwa na Kuandikwa Kwa Codes nyingi sana..
Nitaanza Kanisa Moja Moja Mpaka Mwisho..
Tuanze na Kanisa La Efeso UFUNUO 2:1:-
Cha Kwanza Kabisa Ujumbe Huu wengi wanaamini kabisa Uliandikwa Kwa Malaika Wa makanisa fulani kama Efeso na Mengineyo..
Lakini hebu Tuangalie Maana Ya maneno Yaliyotumika..
Kwakuwa Mwandishi wa Ufunuo Kiasili aliandika kwa Lugha ya Kiyunani(kigiriki) tutaanza kwa Kucheza Humo Ili Tulainishe maana Kabla ya Kuanza Kuichambua Vizuri..
Ufunuo 2:1..
Τῷ ἀγγέλῳ τῆς ἐκκλησίας ἐν Ἐφέσῳ γράψον· Τάδε λέγει ὁ κρατῶν τοὺς ἑπτὰ ἀστέρας ἐν τῇ δεξιᾷ αὐτοῦ, ὁ περιπατῶν ἐν μέσῳ τῶν ἑπτὰ λυχνιῶν τῶν χρυσῶν·
WAnaitamka Hivi...
Tō angélōs tēs ekklēsí en Ephesō grápson: Tade légei ho kratōn tous heptá astéras en tē dexiá autou, ho peripatōn en mésō tōn heptá lychniōn tōn chrysōn.
Tafsiri yake kwa Lugha ya Malkia (lugha ya mayai):
"To the angel of the church in Ephesus write: 'These are the words of Him who holds the seven stars in His right hand and walks among the seven golden lampstands
Neno ἀγγέλῳ (Angelos) kwa Kigiriki lilitafasiriwa Kama Mjumbe Mpaka ilipofika karne ya 4 Baada ya Kuenea Kwa Ukristo walipoamua Kuwa Litafasiriwe kama malaika kwa sababu nao ni Wajumbe wa Mungu..
Ila Neno Hilo Asili yake ni Mjumbe So Badilisha Hiyo neno Malaika Weka Neno Mjumbe au Mpeleka Taarifa..
Neno ἐκκλησίας (ekklēsías) ambalo limetafasiriwa kama Kanisa ni neno la Kigiriki ambalo Linamaanisha Mkusanyo au Mkusanyiko au Mjumuisho au Kutaniko.. na Wala si lazima Liwe katika Muktadha wa Dini...
(Unaweza Ukayahakiki maneno kwa Sehemu Yoyote Ukitaka.)
Sasa Tufanye Mabadilko Kwenye Neno Kanisa Tuweke Mjumuiko au Mkutano au Kutaniko na kwenye Malaika tuweke Mjumbe..
Ufunuo wa Yohana 2:1
"Kwa mjumbe (Mtoa taarifa) wa Kutaniko (Jumuiko) la Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu."
Na hiyo Ndiyo Ilipaswa Kusomeka Hivyo kwa Kiswahili..
Kufika Hapo Nadhani Umenielewa Sasa Twende kwe ye Nyota saba na Vinara saba..
Unafahamu Chochote Kuhusu Menorah?
Iliyokuwa Inakaa Kwenye Hekalu la Mungu Yerusalem na Kwenye Tabernacle ?
Ilikuwaje?
Hii Hapa Chini..
View attachment 3169285
Sasa Biblia inapozungumzia Vinara vya dhahabu inamaanisha Menorah nadhani umeshawahi kuiona Sana hii..
Chimbuko Lake..
Kutoka 25:37-38
"Nawe zifanye taa zake saba; nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.
Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi."
Kwenye Quran Pia Unaweza Ukasoma Kwenye
Surah An-Naba aya 12
وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًۭا شِدَادًۭا
وَجَعَلْنَا سِرَاجًۭا وَهَّاجًۭا
Inatamkwa Hivi..
Wabanayna fawqakum sabAAan shidadan
WajaAAalna sirajan wahhajan
Maana Yake..
Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
Na tukajalia kati yake Mianga
Umeona hata kwenye Quran?
Kwahyo Kumbe Kwenye Hivyo vinara Vilivyojengwa Kuna Mianga 7...
Sasa Lets see What is These 7 lamp au Menorah?
Unafahamu Chochote Kuhusu Chakrah 7 za Mwili wa Binadamu kiroho?
Ziko Chakra 7 Ambazo ndo Muongozo wa Ukuaji Kiroho kuanzia Chakra ya Chini kabisa Root chakra mpaka Chakra ya Juu Crown chakra..
Crown chakra Au Chakra ya Taji ni chakra ambayo humuunganisha Moja kwa Moja Muhusika na Nguvu ya Juu sana ya Kiroho unaweza Ukaita Mungu au Vyovyote utakavyoita..
Hujawahi Kusikia Watu wakiimba..
🎶
Tukimaliza Kazi tutavalishwa Taji🎵
Wengi Huwa wanaimba wakifikiri kuna Siku watakuja Kuvalishwa Taji kama Ya Kifalme..
Hiyo inamaanisha Ukivumilia Katika Kiroho mpaka Mwisho utafika Kwenye Crown Chakra..
Sasa twendelee..
View attachment 3169340
Sasa Upi Uhusiano Huu na Fungu la Ufunuo 2 mpaka 3..
Au Makanisa hayo..
Tuanze na Tabia za Mtu aliyefungua Chakra ya kwanza au root chakra..
Tuanze na maana Yake kama Ilivyoandikwa Hapo "I AM"
Moja..
Sasa Mara Nyingi Mtu anapofungua ama Kuanza kupata Uelewa Kuhusu Mambo ya Kiroho na akaanza Kupractise..
Hufungua kwanza Root chakra (mlango wa Elimu na Maarifa)..
Na baadhi Huishia Kwenye Imbalance Power of The Chakrah..
Wanajikuta Chakra haijabalance..
Na Imbalance Root chakra husababisha..
Insecurity feelings, anxiety, fear, lack of trust. Trouble concentrating and deciding, being isolated from one's self as well as others..
sasa Hii ndo sababu Ikaja Maelezo ya Kuhusu Makutano au Majumuiko yote ya Watu wa Root chakra Yaani mtoa taatifa kuwaeleza Kitakachowakuta na maelezo yao..
turejee Maana Yetu sasa ya Kutoka kwenye Ufunuo tulivyoiweka Vizuri..
Ufunuo wa Yohana 2:1
"Kwa mjumbe (Mtoa taarifa) wa Kutaniko (Jumuiko) la Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu."
sasa Naona baada ya Kukuelezea Hapo Umeweza Kuona utofauti wa fungu Hilo kabla ya Kueleza Na baada ya Kueleza..
View attachment 3169358
Sasa Twende Ndani..
Mpaka Ufike Kufungua Root chakra huwa Ni strugle na uvumilivu wa Kutosha na Ukiifungua Utapata elimu na Maarifa na Unaweza Kupewa Gift ya Utambuzi..
Na ndo maana Ya verse ya Pili na kama Umeona Hiyo ndo Imbalance ya Toot chakra kama Nilivyokuelezea Kabla..
Sasa onyo umeliona?
"
Umeuacha Upendo wako wa Kwanza"
Unajua maana Yake ni Kila mtu anayefungua Root chakra Ugundua kuwa Mafundisho ya Kidini yanafundishwa Tofauti na jinsi anavyoyachambua Yeye na Hugundua Uongo mwingi wa Wachungaji na hao wanaojiita Watu wa Mungu.
Shida Inakuja wanaofungua Wao Kujiona ni bora Kuliko wote na ndo maana Ya rootchakra Umeona Imeandikwa "I AM"..
Kwahyo Baada ya Kujua Ukweli na Kuingia Ulimwengu wa Kiroho Hujiona Ni bora na Huanza Kuwasema Vbaya wale wasioweza Kuwa ndani ya Ukweli alionao..
Na Huanza kujenga Chuki Kwa watu ambao Zamani aliwaheshimu na Kuwajali kama wachungaji na Masheikh Na hata wafia Dini wengine..
Na ndo maana Ukienda Fungu la Tano la Sura hiyo hiyo Anaamrishwa Kurudia matendo ya kwanza..
Ufunuo wa Yohana 2:5..
"
Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye matendo ya kwanza. Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu."
maana Yake Yale matendo yake anayofanya Hayafai anatakuwa abalance Kuujua Ukweli sio chanzo cha kuwaona wasio Jua hawana maana..Na ndo maana Anasema naja kwako na Nitakiondoa Kinara chako..
Na watu wasiotii kurudi kwenye Upendo wa Awali kuwaona walio Katika Imani zingine hawako sawa na wao na Kuendeleza Umimi Au ego!
Hunyang'anywa Uwezo w Kiroho na Maarifa hivyo huelekea Katika Kutokuwa na Imani kabisa..
Na hao ndo Huwa Wanakuwa wapinga Mungu (Atheists)
Kwa sababu ya Kungolewa Vinara vyao...
Sasa sijui kama Umenielewa?
Kama Una swali Kuhusu Kanisa La.kwanza Uliza