Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 1,628
- 2,720
Namsalimia arsis mwambie nafurahia na kufatilia darasa lake ! Ila naomba kuuliza hivi ni kweli mtume Muhammad ,alimuoa Bi Aisha akiwa na miaka sita? Kama ni kweli naomba ufafanuzi wa kimazingira kipindi hicho,kidini,kisayansi, lingine hii ndoa naona Kama inanipotezea muda nataka kuacha mke je? Una lipi la kunishauri?
Wewe ni Muislam? Kama wewe ni Muislam nakuusia kumcha Allah na kutozugwa na kuingia katika haya mambo. Ridhika na Muongozo wa Mtume wako (Swala na Salamu ziwe juu yake), baki katika njia ya Maswahaba (Allah awaridhie).
Achana na mashetani, watakupoteza.
Mtu unamuuliza shetani maswali ya kidini? Yaani seriously unamuuliza shetani!? Unatarajia nini? Adui ambaye hakuonei huruma kabisa!
Unatakiwa umuombe Allah akukinge kutokamana na Shetani, wewe unamfuata shetani kujifunza mambo kwake ikiwemo ya kidini?
Allah atuongoze katika njia iliyonyooka.
Unapokuja kwenye jukwaa hili hakikisha una elimu kuhusu majini,watu, na mashetani,mfano ukisoma Surat jin Allah ananukuu kuwa kundi mojawapo la majini lilisikia Qurani ya ajabu inaongoza kwenye uongofu ,je unataka kuniambia Hawa ni mashetani hawapaswi kuaminiwa?SubhaanaAllah!
Allah awaongoze ndugu zangu, aniongoze mimi na nyinyi katika njia iliyonyoka, Aamiin.
Unapokuja kwenye jukwaa hili hakikisha una elimu kuhusu majini,watu, na mashetani,mfano ukisoma Surat jin Allah ananukuu kuwa kundi mojawapo la majini lilisikia Qurani ya ajabu inaongoza kwenye uongofu ,je unataka kuniambia Hawa ni mashetani hawapaswi kuaminiwa?
Mkuu DR Mambo Jambo umetuacha na kiu kwenye zile stage za ukuaji wa kiroho fanya jambo mkuuNaimalizia maana Niko Interrupted sana ila nitaimaliza
Mkuu Upo Sahihi Kabisa Ila,, Nafkiri Unge "quote" alipokosea Arsis Kwa mujibu wa dini Then ukatufumbua!! Kwa kutoa Ufafanunuzi Mzuri Unge saidia Wengi Hapa Tupo Kupeana Elimu Na sio Kumezeshana Matango Pori.NawasilishaAllah (Subhaanahu Wa Ta'ala) ndio kawazungumzia, kawanukuu. Na Allah ni Mkweli na Yeye ana habari zote, Yeye Allah ni Mjuzi wa kila kitu. Wale majini waliamini walipoisikia Qur'an na Allah akamfunulia hilo Mtume wake katika Qur'an na kumpa habari hiyo na Allah akatuambia waliyoyasema. Ni Allah ndio ametupa habari ile.
Tunaifuata Qur'an na Sunnah iliyothibiti kwa ufahamu wa wema waliotangulia (Maswahaba na walioifuata njia yao katika vizazi vitatu bora vya kwanza).
Hatufuati manenomaneno ya majini hata kama watadai kuwa ni Waislam.
Sisi tumeshatoshelezwa, tunayo Qur'an, aliletwa Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) aliyeteremshiwa hiyo Qur'an akaifikisha na kuifundisha hiyo Qur'an na akatufikishia Dini ya Allah kama alivyofunuliwa na Mola wake.
Mtume akatuamrisha yale yote yatakayotuweka karibu na Pepo na kutuweka mbali na Moto, na akatukataza kila litakalotuweka karibu na Moto na kutuweka mbali na Pepo.
Na walikuwepo Maswahaba zake (Allah awaridhie wote) ambao walizichukua Qur'an na Sunnah, wakafundishwa na Mtume na wakazifahamu na Maswahaba wote wanajulikana. Na tukatakiwa kufuata njia yao na ufahamu wao. Na wao ndio wakazifundisha Qur'an na Sunnah kama walivyomsikia Mtume na kumuona Mtume. Walikuwa kama hawakuelewa jambo wanamfuata Mtume kumuuliza na Mtume anawafafanulia na haya yamepokelewa na kuhifadhiwa.
Ametuacha Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) katika njia nyeupe kabisa.
Wala hatuwafuati majini kuchukua Elimu kwao. Huwezi ukasema naenda kusoma Dini kwa jini. Na wala haifai kuwatumia majini.
Hivi unajua kuwa haipokelewi riwaya ya jini (mapokezi kutoka kwa jini)? Hakuna hadith ya Mtume iliyopokelewa kutoka kwa jini.
Kuna misingi ya kupokea habari tumepewa. Waislam tuna misingi ya kupokea khabari na riwaya.
Na jini haichukuliwi riwaya kutoka kwake. Kwanza utamchunguzaje jini ili ujue hali yake? Utajuaje kama ni thiqah ama la? Ni mkweli ama muongo? (na wengi ni waongo waki take advantage ya maumbile yao).
Sikuambii anayesema uongo wa wazi wazi kama huyu anayejiita Arsis. Mtu anakuambia kabisa eti kaambiwa na shaytwaan wake kuwa Bibi Maryam hakuwa bikra kabla ya kumzaa Nabii Issa (Amani iwe juu yake) na kwamba Nabii Issa (Amani iwe juu yake) sio mtoto wake wa kwanza, haya ni maneno yaliokuwa kinyume kabisa na wahyi (Qur'an na Sunnah).
Ndio maana kuna watu wanakuja na mambo ya ajabu ajabu unajiuliza wanayatoa wapi haya mambo ambayo yako mbali kabisa na Uislam! Kumbe wanadanganywa na mashetani wa kijini. Wengine wanaoteshwa na mashetani halafu wanakuja na mambo ya uzushi anakuambia kaota ndotoni.
Tubaki katika Qur'an na Sunnah iliyothibiti juu ya ufahamu wa Salafu Swaalih.
Tumche Allah ndugu zangu.
Mimi nimefikisha. Naondoka humu.
Mungu ajaliapo KakaMkuu DR Mambo Jambo umetuacha na kiu kwenye zile stage za ukuaji wa kiroho fanya jambo mkuu
AmeenMungu ajaliapo Kaka
"Hatufuati maneno ya majini hata Kama wanadai kuwa waislamu" haya ni maneno yako naomba nikuulize swali wewe una mamlaka gani katika dini hii ya uislamu kufikia hatua ya kusema hayo? Ikiwa Allah amekubali kuwa majini kuwa waislamu Mimi Nani nipinge? Alafu si kila jini ni shetani hata binadamu anaweza kuwa shetani (ushetani ni matendo maovu yanayomchukiza Allah). Allah anasema sikuumba majini na wanaadamu Ila waniabudu, je majini wanamuabudu Allah kwa Imani ipi? Kitabu kipi? Wanafuata mtume yupi kwa uma huu? Qurani hiyo ambayo wewe unasisitiza tuifuate ndio imetupa habari na hadithi za majini mfano kisa cha Nabii Suleimani,majini wapo na walitumiwa na Suleimani. Si kila jini ni muongo au shetani,Qurani ndio kila kitu hata majini waislamu wanafuata Qurani na Sunnah za mtume au umesahau kuwa Mtume ni rehema kwa viumbe vyote?Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) ndio kawazungumzia, kawanukuu. Na Allah ni Mkweli na Yeye ana habari zote, Yeye Allah ni Mjuzi wa kila kitu. Wale majini waliamini walipoisikia Qur'an na Allah akamfunulia hilo Mtume wake katika Qur'an na kumpa habari hiyo na Allah akatuambia waliyoyasema. Ni Allah ndio ametupa habari ile.
Tunaifuata Qur'an na Sunnah iliyothibiti kwa ufahamu wa wema waliotangulia (Maswahaba na walioifuata njia yao katika vizazi vitatu bora vya kwanza).
Hatufuati manenomaneno ya majini hata kama watadai kuwa ni Waislam.
Sisi tumeshatoshelezwa, tunayo Qur'an, aliletwa Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) aliyeteremshiwa hiyo Qur'an akaifikisha na kuifundisha hiyo Qur'an na akatufikishia Dini ya Allah kama alivyofunuliwa na Mola wake.
Mtume akatuamrisha yale yote yatakayotuweka karibu na Pepo na kutuweka mbali na Moto, na akatukataza kila litakalotuweka karibu na Moto na kutuweka mbali na Pepo.
Na walikuwepo Maswahaba zake (Allah awaridhie wote) ambao walizichukua Qur'an na Sunnah, wakafundishwa na Mtume na wakazifahamu na Maswahaba wote wanajulikana. Na tukatakiwa kufuata njia yao na ufahamu wao. Na wao ndio wakazifundisha Qur'an na Sunnah kama walivyomsikia Mtume na kumuona Mtume. Walikuwa kama hawakuelewa jambo wanamfuata Mtume kumuuliza na Mtume anawafafanulia na haya yamepokelewa na kuhifadhiwa.
Ametuacha Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) katika njia nyeupe kabisa.
Wala hatuwafuati majini kuchukua Elimu kwao. Huwezi ukasema naenda kusoma Dini kwa jini. Na wala haifai kuwatumia majini.
Hivi unajua kuwa haipokelewi riwaya ya jini (mapokezi kutoka kwa jini)? Hakuna hadith ya Mtume iliyopokelewa kutoka kwa jini.
Kuna misingi ya kupokea habari tumepewa. Waislam tuna misingi ya kupokea khabari na riwaya.
Na jini haichukuliwi riwaya kutoka kwake. Kwanza utamchunguzaje jini ili ujue hali yake? Utajuaje kama ni thiqah ama la? Ni mkweli ama muongo? (na wengi ni waongo waki take advantage ya maumbile yao).
Sikuambii anayesema uongo wa wazi wazi kama huyu anayejiita Arsis. Mtu anakuambia kabisa eti kaambiwa na shaytwaan wake kuwa Bibi Maryam hakuwa bikra kabla ya kumzaa Nabii Issa (Amani iwe juu yake) na kwamba Nabii Issa (Amani iwe juu yake) sio mtoto wake wa kwanza, haya ni maneno yaliokuwa kinyume kabisa na wahyi (Qur'an na Sunnah).
Ndio maana kuna watu wanakuja na mambo ya ajabu ajabu unajiuliza wanayatoa wapi haya mambo ambayo yako mbali kabisa na Uislam! Kumbe wanadanganywa na mashetani wa kijini. Wengine wanaoteshwa na mashetani halafu wanakuja na mambo ya uzushi anakuambia kaota ndotoni.
Tubaki katika Qur'an na Sunnah iliyothibiti juu ya ufahamu wa Salafu Swaalih.
Tumche Allah ndugu zangu.
Mimi nimefikisha. Naondoka humu.
Bado tunasubiriMungu ajaliapo Kaka
Habari yako mkuu DR Mambo JamboMungu ajaliapo Kaka
Hebu nitag huo UziHabari yako mkuu DR Mambo Jambo
Kimya sana, Ule mwendelezo wa hatua za ukuaji kiroho vipi... Tuliishia kanisa la kwanza.
Ndio huu huuHebu nitag huo Uzi
Ooh sawa ngoja nisome maana niliishia katNdio huu huu
Fuatilia comments za mwishoni mwishoni ndio aliandika hiyo madaHebu nitag huo Uzi
Sawa shukraniFuatilia comments za mwishoni mwishoni ndio aliandika hiyo mada