Unapokuja kwenye jukwaa hili hakikisha una elimu kuhusu majini,watu, na mashetani,mfano ukisoma Surat jin Allah ananukuu kuwa kundi mojawapo la majini lilisikia Qurani ya ajabu inaongoza kwenye uongofu ,je unataka kuniambia Hawa ni mashetani hawapaswi kuaminiwa?
Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) ndio kawazungumzia, kawanukuu. Na Allah ni Mkweli na Yeye ana habari zote, Yeye Allah ni Mjuzi wa kila kitu. Wale majini waliamini walipoisikia Qur'an na Allah akamfunulia hilo Mtume wake katika Qur'an na kumpa habari hiyo na Allah akatuambia waliyoyasema. Ni Allah ndio ametupa habari ile.
Tunaifuata Qur'an na Sunnah iliyothibiti kwa ufahamu wa wema waliotangulia (Maswahaba na walioifuata njia yao katika vizazi vitatu bora vya kwanza).
Hatufuati manenomaneno ya majini hata kama watadai kuwa ni Waislam.
Sisi tumeshatoshelezwa, tunayo Qur'an, aliletwa Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) aliyeteremshiwa hiyo Qur'an akaifikisha na kuifundisha hiyo Qur'an na akatufikishia Dini ya Allah kama alivyofunuliwa na Mola wake.
Mtume akatuamrisha yale yote yatakayotuweka karibu na Pepo na kutuweka mbali na Moto, na akatukataza kila litakalotuweka karibu na Moto na kutuweka mbali na Pepo.
Na walikuwepo Maswahaba zake (Allah awaridhie wote) ambao walizichukua Qur'an na Sunnah, wakafundishwa na Mtume na wakazifahamu na Maswahaba wote wanajulikana. Na tukatakiwa kufuata njia yao na ufahamu wao. Na wao ndio wakazifundisha Qur'an na Sunnah kama walivyomsikia Mtume na kumuona Mtume. Walikuwa kama hawakuelewa jambo wanamfuata Mtume kumuuliza na Mtume anawafafanulia na haya yamepokelewa na kuhifadhiwa.
Ametuacha Mtume Muhammad (Swala na Salamu ziwe juu yake) katika njia nyeupe kabisa.
Wala hatuwafuati majini kuchukua Elimu kwao. Huwezi ukasema naenda kusoma Dini kwa jini. Na wala haifai kuwatumia majini.
Hivi unajua kuwa haipokelewi riwaya ya jini (mapokezi kutoka kwa jini)? Hakuna hadith ya Mtume iliyopokelewa kutoka kwa jini.
Kuna misingi ya kupokea habari tumepewa. Waislam tuna misingi ya kupokea khabari na riwaya.
Na jini haichukuliwi riwaya kutoka kwake. Kwanza utamchunguzaje jini ili ujue hali yake? Utajuaje kama ni thiqah ama la? Ni mkweli ama muongo? (na wengi ni waongo waki take advantage ya maumbile yao).
Sikuambii anayesema uongo wa wazi wazi kama huyu anayejiita Arsis. Mtu anakuambia kabisa eti kaambiwa na shaytwaan wake kuwa Bibi Maryam hakuwa bikra kabla ya kumzaa Nabii Issa (Amani iwe juu yake) na kwamba Nabii Issa (Amani iwe juu yake) sio mtoto wake wa kwanza, haya ni maneno yaliokuwa kinyume kabisa na wahyi (Qur'an na Sunnah).
Ndio maana kuna watu wanakuja na mambo ya ajabu ajabu unajiuliza wanayatoa wapi haya mambo ambayo yako mbali kabisa na Uislam! Kumbe wanadanganywa na mashetani wa kijini. Wengine wanaoteshwa na mashetani halafu wanakuja na mambo ya uzushi anakuambia kaota ndotoni.
Tubaki katika Qur'an na Sunnah iliyothibiti juu ya ufahamu wa Salafu Swaalih.
Tumche Allah ndugu zangu.
Mimi nimefikisha. Naondoka humu.