Inatokea post namba 221.
Alfajiri nikaamka kutazama saa ilikua muda wa kusali tayari, nikakoga faster noikasali, Kutoka ukumbini kwa Mzee Ali nikakuta mlango wa nje umeegeshwa tu haukufungwa moja kwa moja, nikatoa salaam. Mzee Ali akanijibu, akanambia njoo nje bwana tunywe kahawa.
Nikatoka nje nikakaa nakunywa nae kahwa, akanambi mimi muda nimeenda msikitini nimerudi, nimeona nisikusumbue. Vipi umelala salama?
Mimi: Nashukuru nimelala salama nimeaka salama nikatia kahawa, yeye alikua kishaanza kunywa, akaniwacha huku nahisi anaitazama.
Mzee Ali: jana nimepigiwa simu usiku na ndugu zake yule binti, wanasema kufika tu kakoga kala vizuri kalala mapema, sio kama kawaida yake, hakusumbua mtu, sema wanasema walikua wanaogopa asiripuke tena. maana yule huwa hali, hakogi na anasema hivyo wakimsemesha, utafikiri mwehu.
Mimi: Mungu amjaalie, kishpona yule, sema kuna kazi kidogo inatakiwa ifanyike kwake, inatakiwa wale vojana waliokua wanamsomea Qur'an wakachimbe mbele ya mlango wao mkubwa wa mbele na mlango wa uanai uliopo pembeni ya nyumba, waanze na wa mbele, watachokikuta wachome moto, kama kuna chupa waivunje vilivyomo ndani wachome moto, wasiwache kitu, wagteketeze kabisa. Na vya uani hivyo hivyo.
Mzee Ali akawa anaitazama kama anataka kuuliza kitu, akshusha pumzi. Akatia kahawa kikombe chake na changu.
Mzee Ali: Sawa nitawafahamisha. lakini ungekuwepo mwenyewe ingekua vizuri sana. Kwanini usibaki bwana?
MImi; Hakuna shaka Mzee Ali hayo ni mazaga zaga yao tru waliweka, tunayaondoa kabisa, isibaki hata alama yao. Lakini hakuna jipya binti kishapona, mtanijulisha hali yake anaendelea vipi siku za mbele.
Mzee Ali; Leo hii utapata simu yangu. hawa vijana walisema wanakuja baada ya alfajiri tuwasubiri kidogo maana kuna chai nzito ya subuhi inawangoja wao tu.
Haijapita muda ikaingia landcruiser prado kuna vijana wawili tu ndani, Wakasalaimia pale.
Mzee Ali: haya twendeni ndani mpate kifungua kinywa, tulikua tunawangoija nyinyi tu, huyu ndio mwenzenu mtakwenda nae.
Tukaingia ndani tukakuta supu ya kuku na mikate ya kuoka nyumbani, maziwa fresha ya moto, tukapiga pale. Tyulipomakiza tukatoka nje.
Mzee Ali: Ngojeni jamani mpakilieni huyu mchelewake kama nilivyowaambia na kitenga chake cha kuku.
Mimi nikwaambia nakuja, ngoja nichukue kibegi changu. Nikaingia ndani nikatoka na kibegi changu chepesi tiu, cha maana ndani yake ni laptop yangu na mawaya ya kuunganisha kwenye magari, na nguo zangu mbili na overoli moja, kwisha.
Nikakuta washapakia vitu tukaagana na Mzee Ali. Safari ikaanza, hatukuchelewa sana tukafka Singida, wale vijana wakanishusha kabla ya kuingia mjini, kuna kituo cha mafita kikubwa tu kizuri, wakashusha mizigo yangu wakanikabidhisha kwa mtu mwenyeji pale, wakamwambia mtafutoe gari haraka iwezekanavyo yoypote atakayopata kwanza ikiwa basi au gari ndogo. AkasemaPoa. Yule aliokua anaendesha akamwabia, usimdai kitu, nauli na posho yako njoo uchukue kwangu. Akasema poa. Wakaondoka.
Sijakaa sana ikaja gari, pickup ya NGO fulani, ndani yumo dereva tu. Akamfata dereva akaongea nae, ile gari ikasogea akaweka mizigo nyuma akanambia huyo na yeye katokea Shy. Anaenda Dar, mpaka nyumbani hiyo. Nikaona kamshikisha poesa pale akatuaga ytukaanz asafari, tukawa tunaongea ingea na dereva, anakwenda spidi huyo mpaka nikawa naogopa. Tukaingia Dodoma mapema tu, akapiga juu kwa juu, hakusimama kabisa Dodoma.
Kutoka toka nje ya Dodoma, akanambia ukitaka kuchimba dawa nambie ndugu yangu.
Mimi' Nikamwabia tusimame Gairo ikiwezekana, kuna mtu nataka kumsalimia kidogo. Akanambia poa. Tulipofika Gairo nikamwelekeza pale kituoni akaweka gari vizuri tukaingia kimgahawa cha ytule dada, tukakuta kiya kumbe alikua kwa ndani anatuona. Akasema Karibuni.
Mimi: Ahsante, habaroi za hapa? Akanikumbuka haraka sana.
Dada: Yule muhuni yuko wapi?
Mimi: Tuliwachana Shy.
dada: Niwape nini, nikamwabia kahawa ipo?
Dada: Ipo ya kopo niwape?
MMimi; Tupe.
Tukanywa kahawa, nikaona dereva kama hana raha anaharaka, tukaaga, nikamwabia mimi sina zawadi nimeona nikusalimie tu.
Dada: Ahsante sana, basi mimi nakupa zawadi ya hio kahawa, juu yangu msiilipie. Akacheka.
Nikamwabia ahsante sana, tukaondoka.
Dereva akachoma kama kwa hasira fulani hivi, tukawa kimya hatuongei. Mbele kidogo kuna sehemu wanauza uza vitu kibao tu, akasema nachukua zawadi za nyumbani kidogo. Nikamwabia poa.
Tukashuka akanunua nyanya na vvitu vitu vingi tua, pembeni kwenye mti nikaona kuna mtu sio wa kawaida, nikasikia sauti ya Arsis, akanambi jini huyo, jifanye kama hukumuona mshenzi tu huyo. Nikasema poa kimoyomoyo, dereva akawa kama anabishana bei na kina mama wale, nikatoa elfu kumi nikawapa, nikawaambia chukueni hii jazilie. Wakapokea, wakasema ahsante. Dereva akaijgia kwenye gari kama kakasirika hivi.
Tukaondoka kimya kimya mpaka tunafika Dar kwenye foleni foleni zile, akanambia nikuwache wapi mimi naishia Sinza, nikamwambia niwache Sinnza tu pale kijiweni ntachukuwa taxi.
Fereva: kwani unaenda wapi?
Mimi: Ilala.
Dereva: sasa badili ya taxi si unipe mimi hiyo pesa nikupeleke mpaka Ilala.
Mimi; Poa, ntakupa.
Dereva: Utanipa elfu ishirini?
Mimi: Poa usijali.
Akanipeleka mpaka Ilala kufika, nikatoa elfu thelathini nikampa, nikamwabia na hiyo nyingine ya kiushikaji bro. Tukasusha mzigo pale akanambia si niongeze japo kumi? Sikufanya hiyana, nikatoa elfu ishirini nikampa. Aknitazama usoni, akanambia ahsante. Nikamwabia karibu, hapa ndio kwangu. Akaondoka zake bila kusema kitu. Nikaoshukuru tumefika salama. Kunamlinzi pale kwetu saa zote akaja, akwaita na vijana wawili wa ndani kwetu, wakamsaidiana wakaingiza mizigo. Sikukuta mtu.
Nilipokwisha ingia ndani nikakoga nikabadili nikampigia mzee, akanambia nimesikia habari zako Shinynga Mzee Ali anakusifu sana, tukaongea kidogo kwenye simu, akanambia hao wote wametoka nyumbani watarudi jioni. Nikamwabia poa tukaagana.
Itaendelea.