Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Ujumbe mwingine wa Arsis nimeupata sasa hivi wakati naanza kuandika. Usijibu mtu "private, this is an educative thread, simba, you are not mganga or mchawi" akaongea Kiswahili, kua yeye Arsis atajibu linaloulizwa hapa, private ni baina yangu na anaeuliza, yeye hahusiki.

Kwa hio mnaokuja private msitegemee kujibiwa na Arsis maswali yenu ya Private, anasema anaeta yeye ili ajibu muulize hapa wazi, watu wengi wapate faida, kwa sababu tatizo la mtu mmoja wanalo watu millioni moja wengine. Anassema wabadilishe jina kama hawataki kujulikana halafu waulizze. Anataka kutoa elimu yake kwa watu wengi.

Du, leo tumemkorofisha nini Arsis?
Naunga mkono hoja,,mwamba hapendi porojo
 
Wana ukumbi, kwanza inabidi nicheke maana Arsis kanipa ujumbe baada ya mimi kuanza kusoma posts. Ninacheka kwa sababu Arsis leo kanipa ujumbe kwa Kingereza, niwaambie wana ukumbi "they've opened the can of worms".

Akanipa maagizo nisijibu mtu leo mpaka baadae, mimi niendelee na kisanilioanza kukiandika jana lakini niwe mwangalifu "dont spill it, spell it".

Wana ukumbi nisaidieni kamaanisha nini, ujumbe wa kwanza wenu wa pili wangu. Leo Arsis anapiga "ngeli" tu.
Wa kwanza: "Wamefungua boksi la matatizo."

Wa pili: "Usimwage, iandike."
 
Wa kwanza: "Wamefungua boksi la matatizo."

Wa pili: "Usimwage, iandike."
Hio tafsiri ya neno kwa neno lakini naona ni misimiati, imebidi nitafute kwenye mtandao anamaanisha nini, nimeanza kuelewa kwa mbali, nitamuuliza baadae nikiongea nae. Hizzo jumbe kazifikisha bila mimi kuongea nae.
 
Nimekuuliza
1.phoenix
2.bohemoth
3.metatron
4.Gregorian Angels
5.Ophanims...

Nataka kujua pia kuhusu...7th Hall....
Mbona kama unakwepa hili swali? Kama Arsis Hajui uniambie tu! Au gumu!
 
Inatokea post namba 221.

Alfajiri nikaamka kutazama saa ilikua muda wa kusali tayari, nikakoga faster noikasali, Kutoka ukumbini kwa Mzee Ali nikakuta mlango wa nje umeegeshwa tu haukufungwa moja kwa moja, nikatoa salaam. Mzee Ali akanijibu, akanambia njoo nje bwana tunywe kahawa.

Nikatoka nje nikakaa nakunywa nae kahwa, akanambi mimi muda nimeenda msikitini nimerudi, nimeona nisikusumbue. Vipi umelala salama?

Mimi: Nashukuru nimelala salama nimeaka salama nikatia kahawa, yeye alikua kishaanza kunywa, akaniwacha huku nahisi anaitazama.

Mzee Ali: jana nimepigiwa simu usiku na ndugu zake yule binti, wanasema kufika tu kakoga kala vizuri kalala mapema, sio kama kawaida yake, hakusumbua mtu, sema wanasema walikua wanaogopa asiripuke tena. maana yule huwa hali, hakogi na anasema hivyo wakimsemesha, utafikiri mwehu.
Mimi: Mungu amjaalie, kishpona yule, sema kuna kazi kidogo inatakiwa ifanyike kwake, inatakiwa wale vojana waliokua wanamsomea Qur'an wakachimbe mbele ya mlango wao mkubwa wa mbele na mlango wa uanai uliopo pembeni ya nyumba, waanze na wa mbele, watachokikuta wachome moto, kama kuna chupa waivunje vilivyomo ndani wachome moto, wasiwache kitu, wagteketeze kabisa. Na vya uani hivyo hivyo.

Mzee Ali akawa anaitazama kama anataka kuuliza kitu, akshusha pumzi. Akatia kahawa kikombe chake na changu.
Mzee Ali: Sawa nitawafahamisha. lakini ungekuwepo mwenyewe ingekua vizuri sana. Kwanini usibaki bwana?
MImi; Hakuna shaka Mzee Ali hayo ni mazaga zaga yao tru waliweka, tunayaondoa kabisa, isibaki hata alama yao. Lakini hakuna jipya binti kishapona, mtanijulisha hali yake anaendelea vipi siku za mbele.
Mzee Ali; Leo hii utapata simu yangu. hawa vijana walisema wanakuja baada ya alfajiri tuwasubiri kidogo maana kuna chai nzito ya subuhi inawangoja wao tu.

Haijapita muda ikaingia landcruiser prado kuna vijana wawili tu ndani, Wakasalaimia pale.

Mzee Ali: haya twendeni ndani mpate kifungua kinywa, tulikua tunawangoija nyinyi tu, huyu ndio mwenzenu mtakwenda nae.

Tukaingia ndani tukakuta supu ya kuku na mikate ya kuoka nyumbani, maziwa fresha ya moto, tukapiga pale. Tyulipomakiza tukatoka nje.

Mzee Ali: Ngojeni jamani mpakilieni huyu mchelewake kama nilivyowaambia na kitenga chake cha kuku.

Mimi nikwaambia nakuja, ngoja nichukue kibegi changu. Nikaingia ndani nikatoka na kibegi changu chepesi tiu, cha maana ndani yake ni laptop yangu na mawaya ya kuunganisha kwenye magari, na nguo zangu mbili na overoli moja, kwisha.

Nikakuta washapakia vitu tukaagana na Mzee Ali. Safari ikaanza, hatukuchelewa sana tukafka Singida, wale vijana wakanishusha kabla ya kuingia mjini, kuna kituo cha mafita kikubwa tu kizuri, wakashusha mizigo yangu wakanikabidhisha kwa mtu mwenyeji pale, wakamwambia mtafutoe gari haraka iwezekanavyo yoypote atakayopata kwanza ikiwa basi au gari ndogo. AkasemaPoa. Yule aliokua anaendesha akamwabia, usimdai kitu, nauli na posho yako njoo uchukue kwangu. Akasema poa. Wakaondoka.

Sijakaa sana ikaja gari, pickup ya NGO fulani, ndani yumo dereva tu. Akamfata dereva akaongea nae, ile gari ikasogea akaweka mizigo nyuma akanambia huyo na yeye katokea Shy. Anaenda Dar, mpaka nyumbani hiyo. Nikaona kamshikisha poesa pale akatuaga ytukaanz asafari, tukawa tunaongea ingea na dereva, anakwenda spidi huyo mpaka nikawa naogopa. Tukaingia Dodoma mapema tu, akapiga juu kwa juu, hakusimama kabisa Dodoma.

Kutoka toka nje ya Dodoma, akanambia ukitaka kuchimba dawa nambie ndugu yangu.
Mimi' Nikamwabia tusimame Gairo ikiwezekana, kuna mtu nataka kumsalimia kidogo. Akanambia poa. Tulipofika Gairo nikamwelekeza pale kituoni akaweka gari vizuri tukaingia kimgahawa cha ytule dada, tukakuta kiya kumbe alikua kwa ndani anatuona. Akasema Karibuni.

Mimi: Ahsante, habaroi za hapa? Akanikumbuka haraka sana.
Dada: Yule muhuni yuko wapi?
Mimi: Tuliwachana Shy.
dada: Niwape nini, nikamwabia kahawa ipo?
Dada: Ipo ya kopo niwape?
MMimi; Tupe.

Tukanywa kahawa, nikaona dereva kama hana raha anaharaka, tukaaga, nikamwabia mimi sina zawadi nimeona nikusalimie tu.
Dada: Ahsante sana, basi mimi nakupa zawadi ya hio kahawa, juu yangu msiilipie. Akacheka.

Nikamwabia ahsante sana, tukaondoka.

Dereva akachoma kama kwa hasira fulani hivi, tukawa kimya hatuongei. Mbele kidogo kuna sehemu wanauza uza vitu kibao tu, akasema nachukua zawadi za nyumbani kidogo. Nikamwabia poa.

Tukashuka akanunua nyanya na vvitu vitu vingi tua, pembeni kwenye mti nikaona kuna mtu sio wa kawaida, nikasikia sauti ya Arsis, akanambi jini huyo, jifanye kama hukumuona mshenzi tu huyo. Nikasema poa kimoyomoyo, dereva akawa kama anabishana bei na kina mama wale, nikatoa elfu kumi nikawapa, nikawaambia chukueni hii jazilie. Wakapokea, wakasema ahsante. Dereva akaijgia kwenye gari kama kakasirika hivi.

Tukaondoka kimya kimya mpaka tunafika Dar kwenye foleni foleni zile, akanambia nikuwache wapi mimi naishia Sinza, nikamwambia niwache Sinnza tu pale kijiweni ntachukuwa taxi.

Fereva: kwani unaenda wapi?
Mimi: Ilala.
Dereva: sasa badili ya taxi si unipe mimi hiyo pesa nikupeleke mpaka Ilala.
Mimi; Poa, ntakupa.
Dereva: Utanipa elfu ishirini?
Mimi: Poa usijali.

Akanipeleka mpaka Ilala kufika, nikatoa elfu thelathini nikampa, nikamwabia na hiyo nyingine ya kiushikaji bro. Tukasusha mzigo pale akanambia si niongeze japo kumi? Sikufanya hiyana, nikatoa elfu ishirini nikampa. Aknitazama usoni, akanambia ahsante. Nikamwabia karibu, hapa ndio kwangu. Akaondoka zake bila kusema kitu. Nikaoshukuru tumefika salama. Kunamlinzi pale kwetu saa zote akaja, akwaita na vijana wawili wa ndani kwetu, wakamsaidiana wakaingiza mizigo. Sikukuta mtu.

Nilipokwisha ingia ndani nikakoga nikabadili nikampigia mzee, akanambia nimesikia habari zako Shinynga Mzee Ali anakusifu sana, tukaongea kidogo kwenye simu, akanambia hao wote wametoka nyumbani watarudi jioni. Nikamwabia poa tukaagana.

Itaendelea.
Una roho nzuri mm huyo dereva nisingempa hata Mia mtu gani hariziki..??
 
Wana ukumbi, kwanza inabidi nicheke maana Arsis kanipa ujumbe baada ya mimi kuanza kusoma posts. Ninacheka kwa sababu Arsis leo kanipa ujumbe kwa Kingereza, niwaambie wana ukumbi "they've opened the can of worms".

Akanipa maagizo nisijibu mtu leo mpaka baadae, mimi niendelee na kisanilioanza kukiandika jana lakini niwe mwangalifu "dont spill it, spell it".

Wana ukumbi nisaidieni kamaanisha nini, ujumbe wa kwanza wenu wa pili wangu. Leo Arsis anapiga "ngeli" tu.
Tumefungua kopo la minyoo/Chambo 😆🤣 maaa yake mwana kulitafuta mwana kulipata.
 
Ujumbe mwingine wa Arsis nimeupata sasa hivi wakati naanza kuandika. Usijibu mtu "private, this is an educative thread, simba, you are not mganga or mchawi" akaongea Kiswahili, kua yeye Arsis atajibu linaloulizwa hapa, private ni baina yangu na anaeuliza, yeye hahusiki.

Kwa hio mnaokuja private msitegemee kujibiwa na Arsis maswali yenu ya Private, anasema anaeta yeye ili ajibu muulize hapa wazi, watu wengi wapate faida, kwa sababu tatizo la mtu mmoja wanalo watu millioni moja wengine. Anassema wabadilishe jina kama hawataki kujulikana halafu waulizze. Anataka kutoa elimu yake kwa watu wengi.

Du, leo tumemkorofisha nini Arsis?

Ujumbe mwingine wa Arsis nimeupata sasa hivi wakati naanza kuandika. Usijibu mtu "private, this is an educative thread, simba, you are not mganga or mchawi" akaongea Kiswahili, kua yeye Arsis atajibu linaloulizwa hapa, private ni baina yangu na anaeuliza, yeye hahusiki.

Kwa hio mnaokuja private msitegemee kujibiwa na Arsis maswali yenu ya Private, anasema anaeta yeye ili ajibu muulize hapa wazi, watu wengi wapate faida, kwa sababu tatizo la mtu mmoja wanalo watu millioni moja wengine. Anassema wabadilishe jina kama hawataki kujulikana halafu waulizze. Anataka kutoa elimu yake kwa watu wengi.

Du, leo tumemkorofisha nini Arsis?
kama Arsis kataka watu waulize hapa basi mm nauliza kwa faida ya wengi swali ni kuhusu janga la Punyeto na kujichua inasemwa wakati unafanya kitendo hiko kuwa hauko peke yake kuna washirika wasionekana je,ni kina nani hao na dhumuni la kuwepo na ww wakati unanyetuka ni nini na kipi hasa kinaendelea kwa uwepo wao hapo? pia ni yapi hasa madhara ya kiroho na kinafsi ya huo mchezo yalio nyuma ya hio nyeto na pia ni namna gani uachane na hio nyeto?
 
Ujumbe mwingine wa Arsis nimeupata sasa hivi wakati naanza kuandika. Usijibu mtu "private, this is an educative thread, simba, you are not mganga or mchawi" akaongea Kiswahili, kua yeye Arsis atajibu linaloulizwa hapa, private ni baina yangu na anaeuliza, yeye hahusiki.

Kwa hio mnaokuja private msitegemee kujibiwa na Arsis maswali yenu ya Private, anasema anaeta yeye ili ajibu muulize hapa wazi, watu wengi wapate faida, kwa sababu tatizo la mtu mmoja wanalo watu millioni moja wengine. Anasema wabadilishe jina kama hawataki kujulikana halafu waulize. Anataka kutoa elimu yake kwa watu wengi.

Du, leo tumemkorofisha nini Arsis?
Sijui nimuulize nini Ila natamani kujua kisa cha Malkia Bilqis na Nabii Suleyman alosema nitakuvutia kiti kabla hujafika hapo kama sijakosea kingine.

Kuhusu Haaruta na Maarut

Kuhusu Allien

Kuhusu Majinn wanao fanya watu wawe gay or lesbians or bisexual najua anaelewa.

Na kingine kwanini majini wanapenda mfanyisha mtu mapenzi kwa hisia au kumfanya apige Bakary Nondo Mwamnyeto.

Kwanini majini wanaingilia mke wa mtu mpaka anazaa mtoto nusu jinn nusu binadamu wasizae na majinn wenzao.

Uchawi wa wapi ndo mkali wa wazungu au wa Misr au wa Kindengereko Kimakonde

Kuhusu Lucifer Freemason

Kuhusu Masih Dajjal
 
kama Arsis kataka watu waulize hapa basi mm nauliza kwa faida ya wengi swali ni kuhusu janga la Punyeto na kujichua inasemwa wakati unafanya kitendo hiko kuwa hauko peke yake kuna washirika wasionekana je,ni kina nani hao na dhumuni la kuwepo na ww wakati unanyetuka ni nini na kipi hasa kinaendelea kwa uwepo wao hapo? pia ni yapi hasa madhara ya kiroho na kinafsi ya huo mchezo yalio nyuma ya hio nyeto na pia ni namna gani uachane na hio nyeto?
I am not Arsis Ila najibu Punyeto ni majini Ashki yakufanyisha 😁kwa kupiga Bakary Nondo Mwamnyetonyeto au kihisia 😁yaani unajikuta unapiga mshindo bila tendo lolote.

Tena mengine unapiga show na mkeo kumbe jinn yupo mwilini kwako hata hujui mnagonga wote mkeo mahari umetoa wewe 😁au mke an akiwa na jinn la kike lamuingia unagonga mke kumbe unagonga na jinn yaani 2 in one 😁na wapo wake wabeba mimba nusu mtoto binadamu nusu jinn😄

Ndo maana Muslim tuna dua una soma kabla ya kuingilia mke kujilimda na majini wanyemelea tendo la ndoa kizazi chako kisichanganyike na majinn.
 
punguza kuangalia movies mkuu.
Kama angejibu halafu ukaniambia hivi ningenyamaza ila kwa kuwa umeingilia basi inabidi pia kunyamaza nafkiri kwa uelewa wangu hapo ndio nimefika mwisho...kwahiyo nilitaka kuongezewa uelewa tu..!
Sa kwa kuwa wewe uliwaona kwenye movie siwezi kukupinga
Ila Mimi nimewasoma kwenye kitabu kinachheshimika sana..Kitabu cha Enoch...sioni mahusiano hapo kati ya hicho kitabu na Movies...!
 
Asante kwa kushare
Pamoja chief..you are welcome.. kuna elim pana sana huku katika ukristo sijui ni kwanin wachungaji wame concerntrate kwenye vitu common common hiv vya kila siku ambavyo pia hawavichimbui kwa ndani, lakin kuna mambo mengi mnoo huku. The doctrine is soo wide about the bible.. the bible explain about earth speherical shape, kuna biblical archeology, huku current days event prophecy ambazo hiz ziko very deeply elaborated katika the study called Eschatology.

Alot of things kwakwel
 
Arsis ni Jinn tena mkubwa mzee maana jinn anavyokuwa mzee ndio anazidi kuwa na nguvu pia anaonekana licha ya nguvu ana elimu na ilmu.
Ila ni muongo kusema yeye anaqeza kuwa chochote kawaida ya making wengi ni waongo hawapendi kusema ukweli kila kitu haswa jina lake asli yake sababu wanaogopa kutumikishwa na mwanandamu, Mwanadamu ana nguvu sana ni khalifa, Ila jinn anamuogopa sana Mwenyeezi Mungu kuliko sie wanadamu na ukiwa Mcha Mungu ndio kabisa wanakuogopa.

Majinn wanapenda sana ubinadamu wanapenda sana kila kitu cha mwanandamu japo wana uwezo Ila hawawezi kitu kuchukua bila idhini ya mwanadamu mfano jinn anataka damu kwanini asikamate mwenyewe akamfyonza jibu ni hawezi mpaka mwanadamu ampe go ahead
mtu wa maana sana huyu
 
Back
Top Bottom