Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Baada ya dhuhur uje muulize bro je majina ya BARHATIYAH ni shirki?
Hili swali nilimuuliza pia Arsis na subira majibu natanguliza shukurani Nourhan
Nimempata Kaka muda huu mjinga kanitaja jina langu 😁🤣 na mie nimemtaja mwanangu anyways I have nothing to afraid of kujulikana kwangu sababu kuna member wanijua na sina shari na mtu majibizano huku mie na elimika naburudika.
 

Attachments

Msemo wa kwanza "they have opened the can of worms" maana yake " wamefungua dumu la matatizo" msemo huu unatumika kumtaarifu mtu kitu unacho kitafuta au kukifuatilia ni kigumu kuliko unavyofikiri na ni bora usiendelee kuchimbachimba.
Msemo wa pili sijajua anacholenga hasa maana don't spill it, Spell it unaweza kumaanisha don't disclose just write or just say
Nimejaribu kwa ninavyofahamu
 
Nimempata Kaka muda huu mjinga kanitaja jina langu 😁🤣 na mie nimemtaja mwanangu anyways I have nothing to afraid of kujulikana kwangu sababu kuna member wanijua na sina shari na mtu majibizano huku mie na elimika naburudika.
Daah! Bro ako yuko vizuri kwakweli nimependa jinsi anavyosisitiza kuwa Sunni wao hawataki kufanya kitu wasicho na uhakika nacho iyo inaonyesha ana elimu juu ya msingi wa Sunni .
Asante sister, Jazakallah khair
 
Chai
 
Bikra anakuaje na Mume jmn...?!
 
Wana ukumbi. Arsis atakuwepo kuanzia saa mbili na nusu usiku anajibu maswali yeye mwenyewe, hapa hapa jukwaa la wazi ili iwe faida kwa wengi.

Amegima kabisa kujibu maswali aua matatizo ya watu private. Anasema yeye anatoa elimu iwe faida kwa wengi, Kama anataka elimu ibaki kwa mtu mmoja tu hana sababu ya kutokujua ampe nani hio elimu. Hana sababu pia ya kujua watu wa kutibu ni kina nani.

Leo Arsis hataki mchezo kabisa. Mtakaokwepo baada ya mbili na nusu usiku mjue anaejibu ni Arsis mwenyewe kupitia kwangu, nitajitahidi nisiogeze langu.
 
Hio aya ndio inaonesha kua Mariam ni bikira?

Nakushauri uwepo saa mbili na nusu usiku, atakuepo Arsis mwenyewe anajibu live. Mimi sio mjuzi wa Qur'an lakini sijaona hapo ubikira wowote kwenye hio aya. Au tunaona vitu tofauti> Isije kiua huyu Arsis badala ya kunifungua macho kanifunga kabisa. Allah aninusuru.
 
Na maswali kama yote nishauliza na muda huo mzuri nisha sali Isha haya tuendelee na msukule.
 
Sawa tunamsubiri
 
Uongo mtupu.
 
Nimekumbuka muulize Arsis mfano Mimi naweza kuota jambo likatokea kweli hii inakuaje. Mfano kuna siku niliota kuna mtaa natembea kuna wazungu wapo mgahawani wanakula ni pizza place nikaona haina maana imepita muda nikasafiri kwenda Nairobi kuna siku nakatisha mtaani nikaona ule ule mtaa mgahawa na wazungu wanakula pizza pia nikaota kuna sehemu nimeenda kuna msikiti mweupe nikapuuza kuna siku nimeenda Yombo ule msikiti nikauona nikashangaa nilishauona kwenye ndoto

Kingine naweza kupita sehemu ikawa kama nimepata kumbukumbu kwamba nilishawahi kuwa hapa, au tukio linatokea naona mbona lilisha tokea kabla kama limejirudia mpaka kaka yangu hunitania labda dada yangu mzimu ulisha ishi zamani umezaliwa upya kama wahindi 😁hii nayo imekaaje naenda kusali Magharini nitarejea kama na maswali zaidi.
 
Chai
 
Swali langu Arsis
Kwanini nashindwa kupata msaada kwa watu kwenye suala langu la jamaa kutumia vyeti vyangu na anapata mshahara mzuri,posho, na marupurupu mengine?
Nimejaribu kufuatilia mpaka baraza la mitihani (NECTA) Kujua jina langu au vyeti vyangu vinatumika ofisi gani au idara gani iii nipate kuchukua hatua za kisheria?
Ukiwa kama unayeona mpaka mambo yasiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu au kwa sisi watu ambao hatuna Mamlaka yoyote kwenye hii nchi. Kinachonisumbua ni kupata upinzani kila mahali, hata watu ambao wana nafasi za kunisaidia lakini bado sifanikishi? Nilienda mpaka NECTA kuhakiki lakini nilikuta upinzani na yule niliyemkuta sehemu ya ukaguzi wa vyeti ikaonesha alijua naenda kufanya nini pale na ananijua. Ninapambana kwa sababu ni haki yangu Chuo ada niliilipa kwa jasho langu mwenyewe hata kuijenga na kuitengeneza CV yangu ni jitihada zangu. Nimeomba msaada kwa ndugu zangu ambao wana nafasi ya kutoa amri mara moja tu lakini nao wanapuuzia. Halafu mtu ambaye hakusoma wala hakupata uzoefu wa kutengeneza wasifu anakula kupitia jina langu. Nikifanya interview kwenye ofisi zingine nafaulu vizuri usaili lakini kuitwa kuanza kazi hakuna. Mpaka nimeamua kufanya mambo yangu binafsi tu na Alhamdulillah nayamudu lakini kwanini nadhurumiwa haki yangu? Na kwanini sipati ushirikiano kutoka kwa Ndugu, marafiki au watu niliosoma nao ? NECTA ni pagumu na UTUMISHI nako ni vikwazo na nimejiapiza sikubali haki yangu ipotee hivi hivi. Ingawa kuna mazingira fulani ya kutishia usalama wangu nayaona au kuhisi hatari ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana. Ushauri wako na mwongozo wako nauomba.
 
chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…