Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Baada ya dhuhur uje muulize bro je majina ya BARHATIYAH ni shirki?
Hili swali nilimuuliza pia Arsis na subira majibu natanguliza shukurani Nourhan
Nimempata Kaka muda huu mjinga kanitaja jina langu 😁🤣 na mie nimemtaja mwanangu anyways I have nothing to afraid of kujulikana kwangu sababu kuna member wanijua na sina shari na mtu majibizano huku mie na elimika naburudika.
 
Attachments

Wana ukumbi, kwanza inabidi nicheke maana Arsis kanipa ujumbe baada ya mimi kuanza kusoma posts. Ninacheka kwa sababu Arsis leo kanipa ujumbe kwa Kingereza, niwaambie wana ukumbi "they've opened the can of worms".

Akanipa maagizo nisijibu mtu leo mpaka baadae, mimi niendelee na kisanilioanza kukiandika jana lakini niwe mwangalifu "dont spill it, spell it".

Wana ukumbi nisaidieni kamaanisha nini, ujumbe wa kwanza wenu wa pili wangu. Leo Arsis anapiga "ngeli" tu.
Msemo wa kwanza "they have opened the can of worms" maana yake " wamefungua dumu la matatizo" msemo huu unatumika kumtaarifu mtu kitu unacho kitafuta au kukifuatilia ni kigumu kuliko unavyofikiri na ni bora usiendelee kuchimbachimba.
Msemo wa pili sijajua anacholenga hasa maana don't spill it, Spell it unaweza kumaanisha don't disclose just write or just say
Nimejaribu kwa ninavyofahamu
 
Nimempata Kaka muda huu mjinga kanitaja jina langu 😁🤣 na mie nimemtaja mwanangu anyways I have nothing to afraid of kujulikana kwangu sababu kuna member wanijua na sina shari na mtu majibizano huku mie na elimika naburudika.
Daah! Bro ako yuko vizuri kwakweli nimependa jinsi anavyosisitiza kuwa Sunni wao hawataki kufanya kitu wasicho na uhakika nacho iyo inaonyesha ana elimu juu ya msingi wa Sunni .
Asante sister, Jazakallah khair
 
Kuna watu wamenitumia pm kuniuliza kama hiki kisa cha kweli. Napenda kuwafahamisha kua hiki kisa ni cha kweli kwa asilimia 98, labda kuna vionjo vya hapa na pale katika kuandika na fahamu zetu haziwezi kua na kumbukumbu ya mia kwa mia wakati wote, pia kiuhadithia moia kwa mia ni kazi ngumu sa, Kwa hio maelezo ya muhimu yoe ni ya kweli. Kuonana na vumbe visivyoonekana ki kawaida ni kweli, kua babu yangu yuko huko ninapohadithia ni kweli.

Nawahakikishia hakuna ninachozidisha wala kupunguyza isipokua vionjo vichache sana. Pia ieleweke mimi sio mwndishi wa hadithi na jaribu kukifanya hiki kisa kama cha kaiwada lakini naamini si kawaida kwa wengi wenu.

Pia naamini kuna wengine wana visa vya ukweli vingi na vya kusisimua sana lakini hawawezi kuvieleza kwa sababu moja au nyingine. Hata mimi kuyaeleza haya na mengine ya maisha yangu ninafanya juhudi kubwa sana.

Sio wepesi kama nilivyodhani na kuna nguvu kubwa sana inanizuwia, sema nipo namtaalamu, Arsis, siuna shaka wala wasi wasi kabisa.

Kwanza sikuelewa kama Arsis anaongia kunisoma JF, akanambia chochote ninachokifanya yeye anaelewa, kwa sababu yupo kariubu sana na mimi kuliko ninavyofikiria, akanitahadharisha, kama hataki niandike nisingeweza kuandika habari zake.

Sema Arsis, ni muelewa sana, amenikumbusha kua maandiko yangu yawe kwa njia ya kusaidia wengine kuelewa asioyaelewa. Wakiwa wana maswali wajibu kwa kadiri ujuavyo kwa faida yao, sio yako.

Wana JF mnaonisoma hayo ni kwa uchache sana, mengine, nakariisha sana maswali wakati wowote, nipo kwa ajili ya jamii.

Haya ninayoyaandika hapa hayahusiani kabisa na ushirikina. Mimi ni "braza men kwedli kweli" tena yule wa kujirisha sana, Tanzania na duniani, sema majukumu mengine yamenipiga breki kali sana. Na utu uzima umenijia naona niyaeleze niyajuayo labda itakua faiada japo kwa mooja wetu mwengine.

Karibuni muulize mnapokua na swali au maswali, lolote lile, linalohusiana na hiki kisa au lisilohusiana.
Chai
 
Bikra anakuaje na Mume jmn...?!
Kusema mariam sio bikira tu ushaikataa Quran na huenda ukawa miongoni mwa waliokufuru
Maisha ya dunia ni mafupi haya ogopa sana usije kuingia kwenye aya hii
14:22
Na Shet'ani atasema itapo katwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli. Nami nalikuahidini; lakini sikukutimizieni. Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipo kuwa nilikuiteni, nanyi mkaniitikia. Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe. Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu, wala nyinyi hamwezi kuwa watetezi wangu. Hakika mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha na Mwenyezi Mungu. Hakika madhaalimu watakuwa na adhabu chungu.
 
Wana ukumbi. Arsis atakuwepo kuanzia saa mbili na nusu usiku anajibu maswali yeye mwenyewe, hapa hapa jukwaa la wazi ili iwe faida kwa wengi.

Amegima kabisa kujibu maswali aua matatizo ya watu private. Anasema yeye anatoa elimu iwe faida kwa wengi, Kama anataka elimu ibaki kwa mtu mmoja tu hana sababu ya kutokujua ampe nani hio elimu. Hana sababu pia ya kujua watu wa kutibu ni kina nani.

Leo Arsis hataki mchezo kabisa. Mtakaokwepo baada ya mbili na nusu usiku mjue anaejibu ni Arsis mwenyewe kupitia kwangu, nitajitahidi nisiogeze langu.
 
Hio aya ndio inaonesha kua Mariam ni bikira?

Nakushauri uwepo saa mbili na nusu usiku, atakuepo Arsis mwenyewe anajibu live. Mimi sio mjuzi wa Qur'an lakini sijaona hapo ubikira wowote kwenye hio aya. Au tunaona vitu tofauti> Isije kiua huyu Arsis badala ya kunifungua macho kanifunga kabisa. Allah aninusuru.
 
Na maswali kama yote nishauliza na muda huo mzuri nisha sali Isha haya tuendelee na msukule.
Wana ukumbi. Arsis atakuwepo kuanzia saa mbili na nusu usiku anajibu maswali yeye mwenyewe, hapa hapa jukwaa la wazi ili iwe faida kwa wengi.

Amegima kabisa kujibu maswali aua matatizo ya watu private. Anasema yeye anatoa elimu iwe faida kwa wengi, Kama anataka elimu ibaki kwa mtu mmoja tu hana sababu ya kutokujua ampe nani hio elimu. Hana sababu pia ya kujua watu wa kutibu ni kina nani.

Leo Arsis hataki mchezo kabisa. Mtakaokwepo baada ya mbili na nusu usiku mjue anaejibu ni Arsis mwenyewe kupitia kwangu, nitajitahidi nisiogeze langu.
 
Wana ukumbi. Arsis atakuwepo kuanzia saa mbili na nusu usiku anajibu maswali yeye mwenyewe, hapa hapa jukwaa la wazi ili iwe faida kwa wengi.

Amegima kabisa kujibu maswali aua matatizo ya watu private. Anasema yeye anatoa elimu iwe faida kwa wengi, Kama anataka elimu ibaki kwa mtu mmoja tu hana sababu ya kutokujua ampe nani hio elimu. Hana sababu pia ya kujua watu wa kutibu ni kina nani.

Leo Arsis hataki mchezo kabisa. Mtakaokwepo baada ya mbili na nusu usiku mjue anaejibu ni Arsis mwenyewe kupitia kwangu, nitajitahidi nisiogeze langu.
Sawa tunamsubiri
 
Uongo mtupu.
 
Nimekumbuka muulize Arsis mfano Mimi naweza kuota jambo likatokea kweli hii inakuaje. Mfano kuna siku niliota kuna mtaa natembea kuna wazungu wapo mgahawani wanakula ni pizza place nikaona haina maana imepita muda nikasafiri kwenda Nairobi kuna siku nakatisha mtaani nikaona ule ule mtaa mgahawa na wazungu wanakula pizza pia nikaota kuna sehemu nimeenda kuna msikiti mweupe nikapuuza kuna siku nimeenda Yombo ule msikiti nikauona nikashangaa nilishauona kwenye ndoto

Kingine naweza kupita sehemu ikawa kama nimepata kumbukumbu kwamba nilishawahi kuwa hapa, au tukio linatokea naona mbona lilisha tokea kabla kama limejirudia mpaka kaka yangu hunitania labda dada yangu mzimu ulisha ishi zamani umezaliwa upya kama wahindi 😁hii nayo imekaaje naenda kusali Magharini nitarejea kama na maswali zaidi.
 
Mleta mada kaeleza mambo mengi makubwa ila juu juu (siwezi sema kakosea maana target yake ni kufikisha ujumbe kuhusu alichokiona baada ya kufunguka macho, na alhamdulillah ujumbe umefika,,,, japo utata umebaki mwingi kwenye vichwa vya watu)

Ngoja nisawazishe eneo dogo hapa kwajinsi ninavyoelewa!!
Mada kubwa mezani ni SPIRITUAL AWAKENING

Viumbe wa kiroho... Ni viumbe wote ambao hawaonekani kwa macho ya kawaida (malaika, majin n.k kila mtu anawafaham kwa mujibu wa imani yake) viumbe Hawa huwa na connection kwa watu maalum pekee

Watu maalum ni hawa 👉 Manabii na mitume, wachamungu sana, waganga wa kichawi na watu waliopendelewa

Ili uwe kwenye special group lazima uwe connected na source of power yoyote kati ya hizi
A. Mungu
B. Ibiris

Sasa viumbe wa kiroho wao pia wapo makundi mawili tu.... Kutokana na uanachama wao kweny hizo source of power (hapo either awe upande wa Mungu au Shetani🤝

Sasa hao special group pia wananamna yao ya kuwasiliana na hao viumbe.....
Baadhi ni hisia, ndoto, telepathy na kuona

(Hii njia ya kuona ndio njia ya juu zaidi tuseme ndio maqam ya mwisho.... Sasa huwa unaanza kwa kupanda daraja
Utaanza njia ya hisia, ndoto, telepathy mwisho utaona🤝

Mleta mada yupo kwenye special group upande wa watu waliopendelewa... Maana hajafata process wala hajaandaliwa ila karushwa daraja moja kwa moja

(Kwa imani ya kiislam huwa Kuna watu wanazaliwa wakiwa n mawalii wa Mwenyezi Mungu,,,,, kitu ambacho n nadra sana mtu kukipata

Au mfano mtu ufanye ibada mpk uwe nabii😁😁😁🏃
Ngum sana, nabii huzaliwa akiwa tayar ni nabii

(Dah mambo ya kiroho huwa yanamaelezo mengi sana...... Ila ukiweza kuwasiliana na viumbe wa kiroho hii Dunia umeiweza🤝
Njaa kwako sahau, kuonewa kwako sahau, kukataliwa kwako sahau,,, hii ni Siri ambayo wazungu wanaitumia sana

Ushuhuda:
Baba yangu alikuwa na uwezo wa kwenda kwenye mlima wowote au mto mkubwa, akifika anawaita watawala wa huo mto au mlima wanakuja live anawaeleza anataka nn kutoka kweny himaya yao halafu wakielewana kazi kwisha
(Anaenda kweny kaburi la mtu aliyekufa anamuamsha anaongea nae akimaliza anarudi kulala..... (Najua hapa ntaonekana muongo)
Anazama kweny maji anatoka mkavu bila kuloana
Anaweza kuchukua ile sarafu ya zaman inayotafutwa kila kona
SIMBA MBILI au Rupia (akafanya yake akamtoa yule Simba na king George wakakaa na kuanza mazungumzo

Alikuwa na uwezo wa ajabu sana.....

Note: source yake ya Power haikuwa GOD
(Kwenye hii Dunia ukitaka kuwa mtu hatari we chagua njia moja upite hiyo kikamilifu utaona balaa lake.... Kama n Mungu swali sana acha dhambi kwa ukamilifu wake utaona utavyokuwa hatari

Kama n upande wa shetwani... Roga sana, usisite kutoa mtu kafara Yani kuwa nyambisi haswaa utaona ibiris atavyokupenda😂

Fanya juu chini upate mapenzi either ya Mungu au Ibiris.... Usikubali kukaa katikati maana utakuwa mtumwa
Chai
 
Swali langu Arsis
Kwanini nashindwa kupata msaada kwa watu kwenye suala langu la jamaa kutumia vyeti vyangu na anapata mshahara mzuri,posho, na marupurupu mengine?
Nimejaribu kufuatilia mpaka baraza la mitihani (NECTA) Kujua jina langu au vyeti vyangu vinatumika ofisi gani au idara gani iii nipate kuchukua hatua za kisheria?
Ukiwa kama unayeona mpaka mambo yasiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu au kwa sisi watu ambao hatuna Mamlaka yoyote kwenye hii nchi. Kinachonisumbua ni kupata upinzani kila mahali, hata watu ambao wana nafasi za kunisaidia lakini bado sifanikishi? Nilienda mpaka NECTA kuhakiki lakini nilikuta upinzani na yule niliyemkuta sehemu ya ukaguzi wa vyeti ikaonesha alijua naenda kufanya nini pale na ananijua. Ninapambana kwa sababu ni haki yangu Chuo ada niliilipa kwa jasho langu mwenyewe hata kuijenga na kuitengeneza CV yangu ni jitihada zangu. Nimeomba msaada kwa ndugu zangu ambao wana nafasi ya kutoa amri mara moja tu lakini nao wanapuuzia. Halafu mtu ambaye hakusoma wala hakupata uzoefu wa kutengeneza wasifu anakula kupitia jina langu. Nikifanya interview kwenye ofisi zingine nafaulu vizuri usaili lakini kuitwa kuanza kazi hakuna. Mpaka nimeamua kufanya mambo yangu binafsi tu na Alhamdulillah nayamudu lakini kwanini nadhurumiwa haki yangu? Na kwanini sipati ushirikiano kutoka kwa Ndugu, marafiki au watu niliosoma nao ? NECTA ni pagumu na UTUMISHI nako ni vikwazo na nimejiapiza sikubali haki yangu ipotee hivi hivi. Ingawa kuna mazingira fulani ya kutishia usalama wangu nayaona au kuhisi hatari ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana. Ushauri wako na mwongozo wako nauomba.
 
Nimekumbuka muulize Arsis mfano Mimi naweza kuota jambo likatokea kweli hii inakuaje. Mfano kuna siku niliota kuna mtaa natembea kuna wazungu wapo mgahawani wanakula ni pizza place nikaona haina maana imepita muda nikasafiri kwenda Nairobi kuna siku nakatisha mtaani nikaona ule ule mtaa mgahawa na wazungu wanakula pizza pia nikaota kuna sehemu nimeenda kuna msikiti mweupe nikapuuza kuna siku nimeenda Yombo ule msikiti nikauona nikashangaa nilishauona kwenye ndoto

Kingine naweza kupita sehemu ikawa kama nimepata kumbukumbu kwamba nilishawahi kuwa hapa kabla mpaka kaka yangu hunitania labda dada yangu mzimu ulisha ishi zamani umezaliwa upya kama wahindi 😁hii nayo imekaaje naenda kusali Magharini nitarejea kama na maswali zaidi.
chai
 
Back
Top Bottom