Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Nitafute inbox
 
Inatokea [post namba 672

Vionjo vya Arsis 3 Kumwokoa Msukule 1 C.

Niliporudi nyumbani nikakuta watu wapo macho. Mzee akaanza...
Baba; Vipi simba, kwema baba?
Mama" mwanangu tunaishi nyumba moja kama majirani hatuonani?
Mimi: Niko poa kuna mambo mambo tu yamenishghulisha.
Mama; Usijekua kama babu yako, mie sitaki kujaiwa wateja wa uganga humu ndani. maana babu yako ni hivyo hivyo akijifungia ndani akitoka kuna watu wana matatizo yao.
Baba; Huho karithishwa mikoba na babu yake, huoni bakora yake ile?
Wife: Wasimrithishe mwanangu tu mambi yao, maana kutwa kazi yake kuchewza na hiyoi bakora.
Mama; Nyie mnasema bakora kumbe tunaishi na jini ndani ya nyumba.
Mimi; mama wewe si simba, twambie kweli kama jini lile au sio.
mama: Simba sisi hatuna majini kama ya babu yako huko, majini ya kisimba yanapiga brandy, kazi yao kustarehe tu, hawajui hata kujitibu wenyewe. Hawana kabisa mambo yenu huko.
Wife: Wao watyu wa kujirusha tu.
Mama; Tena wewe hata usiseme, majini ya kwenu huko hawachezi mbali na wewe.
Wigfe' Mie hata sowataki, mie ya upande wako maa, yananitosha kabisa, mimi simba jike.

Naomba ifahamike, mke wangu hata mimi nilikua sijui kama ni mtoto wa shangazi yangu, kalelewa na mama toka mchanga kabisa, ni mtoto wa dada yake baba. Nimekuja kujua kabla ya ndoa. Ni kisa kingine kabisa hakihusiani na Arsis kwa hio kiishia hapo tu.

Baba; Njoo tuongee huku nje simba.

Tukatoka na baba uani, tukaanza kupiga kahawa.
Baba; Simba babu yako kanipigia simu kanambia utakua haupo utakwenda Tanga kwa wiki moja, mbina hujanambia?
Mimi: Ilikua nikwambie, hatujaonana, ndio tunaonana sasa hivi.
Baba: Hakuna tatizo, nilikua nakujulisha tu, wewe nenda tu any time, usijali mambo ya kazi zako, mimi nipo. Maana babu anasema ulimwabia una kazi nyingi.
Mimi; Ndiyo mzee kuna wateja watataka diagnosis ya gari zao.
Baba: Hilo usijali nitamchukua mkeo aje kufamnya diagnosis ikihitajika.
Mimi: Baba wewe unachukulia kila [poa tu, kiwepesi kabisa. Upo kama babu.
baba: Usiwe na wasiwasi simba, kikitushinda kitu tutakupigia simu, ruksa, nenda tu.
Akaondoka, ile naingia ndani nikapata ujumbe niende osisini kwangu kabla sijaingia kulala. Nikaenda.

Nikakamkuta jini mwanamke ananingoja kama kwake. Tukasalimiana akaanzaa...
Jini1: Usistuke simba nimekuja kuweka mambo sawa tu sikucheleweshi. Waambie wageni waende Tanga Jumamosi, wawe pale Jumapili.
Mimi: sawa nitamjulisha mzee Ali kesho.
Jini 1; Mpigie hata sasa hivi ili kesho mapema awaambie wajitayarishe. Na wewe unatakiwa kuanzia kesho uwe Tanga kwa babu yako, huna haja ya kwenda kazini kesho. Mama anakupa salaam. Mpelekee zzawadi Haalima pale Chalinze.

Mimi nikashangaa kidogo.

Jini 1: usishangae mimi hanijui wala simjui lakini si ndio njia yako hio, nakukumbusha tu.
Mimi; Sawa lakini Arsis anasema wewe unajuana na mkewe mzee Ali, sitaki mnifanyiwe mamboya siri zenu za kijini.
Jini1; Mimi namjua Qareen wa mkewe sio mkewe. Arsis kishakueleza kitu. Soisi hatuwezi kua na siri yoyote kuhiusu wewe, tutauliwa. Jambo lingine, hii kazi usimwabie hata mkeo wala mama'ko. ni yako na sisi tu. kwaheri nisikucheleweshe.
Mimi: haya kwaheri.


Nikaenda zangu nikakoga nikalala mpka siku ya pili asubuhi mapema nikaanz kukusanya vitu vyangu vya safari nikamwambia wife nitakua Tanga kwa wiki moja, akanambia ,nikishindwa kukaa peke yangu nakuja hukohuko Tanga, wiki nzima? Kuna nini wewe na babu? Au ushakuwa mwanga kama babu yako? yule mzee anaweza kukuozesha huko mume wangu.

Mimi; Nikacheka, kama mwanga ni wewe na babu yako, mimi simo. Mimi kuna kazi zangu tu zinanipeleka.

Mama alipotoka na yeye nikamuaga, mzee alishakwenda kazini. Nikaondoka, ile nnataka kuondoka nikakumbuka nimesahau bakora yangu nikaifata, nikakumbuka na zawadi ya B Haalima Chalinze, nikamwabia wife kama ana chupa ya perfume haitumii anipe nimpelekee Bi Halimza zawadi. Waife akanitolea chupa mpya ndani ya noz, akanambia hizi ninazo tatu, mtu akijua naipenda hii perfume anailetea zawadi hio hio. akacheka, akasema bora na Halima Msomali anukie kama mimi. Nikajua kijembe cha wanaweke hiko.

nikaanza safari yangu ya Tanga.

Njiani Mzee Ali akanipigia, nikamwabia nipe muda kidogo nitakupigia.

Nilipofika Chalinze kitu cha kwanza nikamueleza kuhusu yule mama na ndgu zake kuja Tanga na lini. Akanambia sasa hivi anaongea nae, yupo kwake pale, Tukakubaliana tuongee juoni kupeana mrajesho. Sikumwambia kama mimi naelekea Tanga.

Nikashuka kwenye gari nikaenda kwa Halima zna zawadi yake. kuniona...

Halima. Mimi nasema boss gani huyu hashuki kwenye gari, kumbe simba mtoto?

Tukasalimiana nikampa zawadi yake, akifungua palepale, akaijaribu akanambia hii perfume mimi naujanja wangu wote siiwezi bei yake, simba umeniroga, umejuaje mimi napenda perfume?
Mimi: Niki[iyta unanukia tu.
Halima: Mie Msomali wewe, wasomali mwanamke kama hanukii huyo feki.
Mimi; Si unukie kwa mumeo tu?
Halima; Harufu ninayomtilia mume wangu wewe huwezi kuielewa wala kuinusa. mwiko kabisa

. Hivi unavyonisikia ni hapa dukani, udi wa kawaida tu huo, sijatia manukato, unataka niwatie wazimu watu?


Nikacheka nikajisemea kimoyomoyo, hivi hawa Watanga mbona hawangoji kusifiwa? Wanajisifu wenyewe.



Itaendelea.
 
Dah! Huyu Arsis 🤣😂 Corazon hana majibu haya
Sio Arsis, hajaja bado. Huyo kijana anatania tu, ni mimi simba. hajaziona chai za za asubuhi kwa kamab huyo.

Hajui kwegtu tanga wanatuikia chai kwa anjari nyeupe ya tangawizi, haitiwi sukari wala viungo qala maji hio.

Anacheza na chai ya Tanga huyo.
 
Chai
 
Tafadhali Arsis ikikupendeza Anza na maoni yako kuhusu ndugu yetu huyu
 
Naam Hoyo wangu alikuwa msomali alikuwa anasema ni matusi kwa mwanamke wa kisomali kunuka wao kununua na nyumba zao nywele wafukiza oud na oud bokhoor ya nyumba sio anayo jifukizia mwilini nywele au kwenye nyumba,asubuhi kisha pika chai ya maziwa somali Xhaa angelo(Angela) maini au nyama (beef sugaar) au sabayad(chapati) nyumba safi yanukia Alkhamis kuamkia ijumaa Mama aliniambia kwao Hergeisa wanawake wanafanya facial na steaming z nywele kwa hinna na qasir (unga wa majani ya mkunazi) sio u Tanga wa Somali wako hivyo ndo maana wanashika waume zao hawafurukuti wana waachia waendeshe mambo wao kula mirungi tu.

Ukienda Tanga niletee anjari haswa nyeupe naipenda harufu yake ya arki rose usisahau kamba wa Maforoni 😄nawapenda sana haswa ukiwa pika prawns curry au prawns biryani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…