Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Duh... Mambo ya Ounsigaa!
 
hivi inakuwaje watu wanaingiliana na majini wakati sisi na majini tuna asili ya uumbwaji tofauti?

hata kama tunao mwili wa roho inakuwaje majini yanatuingia?

njia za kuepukana nao.
 
Wewe kweli Msomali, mimi nimeishi nao sana Canada. Waislam wazuri sana, wamenipa sana zawadi ya "unsiga" .

Ngoja niwahi swali la kwanza kabisa kwa Arsis.
 
kaka samahani Mzee mabruki unaemuongelea hapa ni huyu mwarabu wa Duga maforoni mwenye magari aliyaandika Bin Nassoro?
 
Arsis ,je kwel jamii ya watu wa misri hapo kwanza walikua watu weusi na mafarao wa kwanza walikua sionwa race hiibya sasa??
Swali lako zuri sana. Kweli na sio kweli. Utawala wa Misri ambao unajulikana na ambao wasomi wa siku hizi wanadanganya una miaka 3000 mpa 5000 au zaidi kidogo, ni utawala wa zamani sana una miaka zaidi ya millioni. Walikuepo watu wa rangi zote na wa mataifa yote. Ni utawala mkubwa sana. Pale Misri, Giza ndio kitovu cha huo utawala lakini ulikua mpaka siku hizi mnaita Amerika, ulikuwepo Mpaka China ulikuwepo mpaka chini ya Afrika Kusini. Kule siku hizi barafu tupu, mnaita Antarctica, ipo miji mikubwa sana chini ya barafu. Mingine ipo chini ya bahari ya Mediterranean. Mengine ipo chini ya bahari yenu hapa Tanzania.

Watu wapo kila rangi ili mafahamiane tu, huyu wa wapi yule wa wapi. Utawala wa zamani wamwisho usioongea kiarabu wa Egypt ni wa rangi mchanganyiko.
 
Hii sio swali yangu. Atajibu simba.
 
Swali langu Arsis
Kwanini nashindwa kupata msaada kwa watu kwenye suala langu la jamaa kutumia vyeti vyangu na anapata mshahara mzuri,posho, na marupurupu mengine?
Nimejaribu kufuatilia mpaka baraza la mitihani (NECTA) Kujua jina langu au vyeti vyangu vinatumika ofisi gani au idara gani iii nipate kuchukua hatua za kisheria?
Ukiwa kama unayeona mpaka mambo yasiyoweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu au kwa sisi watu ambao hatuna Mamlaka yoyote kwenye hii nchi. Kinachonisumbua ni kupata upinzani kila mahali, hata watu ambao wana nafasi za kunisaidia lakini bado sifanikishi? Nilienda mpaka NECTA kuhakiki lakini nilikuta upinzani na yule niliyemkuta sehemu ya ukaguzi wa vyeti ikaonesha alijua naenda kufanya nini pale na ananijua. Ninapambana kwa sababu ni haki yangu Chuo ada niliilipa kwa jasho langu mwenyewe hata kuijenga na kuitengeneza CV yangu ni jitihada zangu. Nimeomba msaada kwa ndugu zangu ambao wana nafasi ya kutoa amri mara moja tu lakini nao wanapuuzia. Halafu mtu ambaye hakusoma wala hakupata uzoefu wa kutengeneza wasifu anakula kupitia jina langu. Nikifanya interview kwenye ofisi zingine nafaulu vizuri usaili lakini kuitwa kuanza kazi hakuna. Mpaka nimeamua kufanya mambo yangu binafsi tu na Alhamdulillah nayamudu lakini kwanini nadhurumiwa haki yangu? Na kwanini sipati ushirikiano kutoka kwa Ndugu, marafiki au watu niliosoma nao ? NECTA ni pagumu na UTUMISHI nako ni vikwazo na nimejiapiza sikubali haki yangu ipotee hivi hivi. Ingawa kuna mazingira fulani ya kutishia usalama wangu nayaona au kuhisi hatari ya kufuatiliwa na watu wasiojulikana. Ushauri wako na mwongozo wako nauomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…