Babu yangu alijaaliwa maarifa siku nyingi sana. Alijichagulia hiyo sehemu ambayo watu wote walikua wanaiogoppa. ikawa kajichagulia katikati ya matawi mawili ya mto ambayo yote,a yanatoa kamba kwa wingi wakati wa msimu, lile tawi kubwala mashariki na lile lenye mapango ya kiajabu, yote yapo kwenye eneo la shamba lake. Ule mto wa Mashariki ndio kwa upande wa pili jamii wanapata kuvuna msimu wa kamba, mto ule ndio mpaka wa shambani kwetu, huu mto wa Magharibi ni tawi dogo tu lisilokauka, linapita katikati ya shamba letu, mapango mawili makubwa moja ni kama ukumbi tu mkubwa, hayakutani kwa ndani, yote yapo ndani ya shamba letu.
Mji wa babu bado wanakaa wana familia au wanafunzi wanaokuja hapo mpaka leo hii.
Ukifika kuanzia mpakani horohoro mpaka unafika Duga maforoni ukiuliza Mzee mabruki kwake wapi, unaletwa hata na mtoto mdogo. Babu wengi wanafikiri Mbaruki ni jina lake, lakini ukweli ni kua kuanzia anafanya kazi Tanga 'Mabruki" ulikua ni msemo wake mkubwa, akimaanisha kupongeza kila zuri utaloilfanya,anakupongeza kwa kusema "mabruk" basi ikashika ndio likawa jina lake "Mzee Mabruki". Ukija Duga Maforoni tuna kwetu, vizazi vya Mzee Mabruki mpaka kesho. Lakini kwa Mzee Mabruki alipo ni kule shamba, baharini kwenye kamba wa kufa mtu. Qengi wanajua anakaa Duga mjini, hawajui pale ni kwake anakuja kwa shughuli zake tu, lakini makazi yake hasa ni kule shamba.
Kamba wa kufuga ilishindikana kabisa kule. Walikua na kazi kubwa sana, babu akasema sina hamu nao, hawa wa msimu wanatutosha na pesa zake hatuzimalizi. Ndio miradi ya kuvuna kamba kwa mwaka mzima ikaishia kwa kauli hiyo ya babu. Sasa kuna misimu miwili tu, msimu mkubwa na mdogo, na kila msimu una aina tofauti ya kamba. Miuiiza ya Muumba wetu hio.
Mpaka kesho, misimu yote ya kamba, nakua shmbani kwetu, navuna kamba tu.