Hii audio ni very informative kwajinsi ninavyofahamu mimi naweza sema zaidi ya asilimia 95 amesema kweli.
Ndio maana tumefundishwa unapotaka kula anza kwa jina la Mungu kwa maana usipofanya hivyo utakula na mashayatwin sasa binadamu situnakula vitu tofauti basi hata majini wanakula vitu tofauti na hao ndio masubiani
Kwa upande wa maruhani kujifananisha na malaika pia ni kweli. Ngoja namimi nitoe elimu kidogo
Mwanadamu yeyote anapofanya jambo baya mfano wizi, Kula riba, uzinzi ,ushirikina ,hasadi, chuki, kiburi, kukata undugu n.k moyoni mwake kunakuwa na doa jeusi doa hili litakuwa linakuwa kadri unavyofanya maasi, hivyo basi jini akitaka kukuingia au mchawi akitaka kukuloga anawatumia majini waovu kuangalia je moyo wako una doa jeusi nalina ukubwa gani wakikuta moyo wako ni mweusi sana ni rahisi kulogeka kinyume chake mtu mchamungu hana doa katika moyo wake hivyo ni ngumu kulogeka.
Sasa kwa upande wa majini wao kadri jini anavyo mtumikia iblis na kunywa damu za kafara na kuharibu maisha ya watu jini huyo anabadilika kutoka umbo lake la asili anakuwa na umbo baya la kutisha mfano anaanza kuota mapembe, mikia na anakuwa anatisha na huyu sasa ataitwa shetani wa kijini kinyume chake ni kuwa kadri jini anavyo muabudu mola wake akajiweka mbali na maaswi basi anakuwa anang'aa kama malaika yaani anaanza kufanana na malaika ndio maana iblis kabla ya kuasi alikuwa kama malaika na aliishi nao. Sasa majini wanaokuwa hivi wengi ndio hao maruhan wanapenda kujifananisha na malaika.
Pamoja na hayo mwanadamu na jini wote wanaweza kutubu kwa mola wao kabla ya umati na lile doa jeusi linaondoka kwa mwanadamu na umbo la kishetani likaondoka kwa jini
Nimefunguka tu kidogo jamani Ila natamani bwana
Arsis aje na muendelezo