Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Sisi tutakusaidia hapa JF. Usisahau.

Major Government officials are reading you now. Some, not all. Usishitaki mtu sababu anaweza kupata aibu yeye au watu waliomsaidia. hapa tutakupa njia, hakuna mchawi au anasema Sheikh atakusaidia.

Hapa JF utapata msaada, lakini sio kwa njia wewe unafanya. Njoo hii uzi, utapata njia.
Nipo hapa Mkuu Arsis kupata muongozo sahihi maana hao watu siwawezi kwa lolote ila Mimi haki yangu naitaka. Najua nafuatiliwa sana mpaka mtaani. Roho inaniuma kwanini wale jasho la Mnyonge kama Mimi wakati wao wana kila kitu wanachokitaka?
 
Swali zuri sana hilo.

Usfungue biashara kwa faida yako, fungua biashara kwa faida ya wengi. Utapata faida kubwa sana. Sawa?
naomba utufafanulie hapo kufungua biashara kwa faida yako ndio iko vp hiyo maana wengi kufungua biashara kwa kuwauzia watu ili kupata mapato vp wewe useme fanya biashara kwa faida ya wengi na biashara hiyo ipo kwa ajili ya watu..embu fanya kutuwekea kwa mifano iyo kauli yako.
 
Fanya ibada, sali sala za usiku, usikae na mwili mchafu. Kuna aya na sura ndogo ndogo sana kwenye Qur'an zina nguvu sana kuliko chochote.

Qur'an ni shifa. Unajua maana yake? Ni hopital.
Hizo sura zinaweza kuwa Surat ikhilasw, falaq na mass ndio sura ndogondogo zinazohusiana na mambo ya uchawi na ukubwa wa Allah. Nimejaribu au kuna nyingine ndogo tofauti na hizo bwana Arsis tupe elimu
 
Kuna watu wanasoma kama story halafu kunawengine tupo darasani🤝

Kwahyo ukiwa unaeleza kwenye mafunzo elezea kwa kina, maana kuna watu tunajifunza na kuingiza kwenye utendaji


Mfano juzi.... Baada ya kusoma uzi hapa, na mm nikaenda kuwaita hawa marohani niliorith kwa mzee wangu (nikapanda juu kwenye uwazi sehem ilotulia kwa mbaramwezi, si nikawaita bhana........... Maana nishawazoea kila siku lazima waje karibu muda wote nikiwa pekeangu wanapenda kuja

Sasa juzi nikawaita huku nawapiga beat,,,,, leo staki mje kimyakimya nataka mje muongee hapa au niwaone live😁😁😁😁

Bwama weeeh si upepo ukaanza kuvuma pale,,,,,, nikaanza kuwaza kimoyomoyo "Leo yule jamaa wa Jf kaniponza😂😂😂😂"


Ila walikuja lakini sikuwaona wala hawakusema chochote.... Nikashuka zangu huyooooooo safari🚶🚶🚶
chai
 
Nimejikuta nakucheka wajifanya wajua kumbe hujui.

Na humjui pia,na nisingependa kumuongelea hata yeye tu kujiongelea kujimwambafai kamwe huwezi kuta anaongelea, halafu mbona hata yeye amesema jinn huwa hasemi ukweli asli yake jina Ila kuna hesabu unapata umeishi nao miaka 20 mwenzio kazaliwa kalelewa nao nini yeye kuongea nao mie tu wanijia ndani kwangu naona nao japo wanakuja kwa umbo lake haswa mida ya mchana unakuta kama nalewa usingizi anyways niishie hapa sipo hapa kuongelea habari za mtu nipo kujifunza.weka elimu yako wewe tujifunze kuhusu majinn
Huyu hana elim ya majini..... Elim ya majini utaipata kwa majini wenyewe,

Pia hawapendi kuitoa elim kuhusu wao
huyu shekh wetu ni kama anaongea vitu alivyosikia 🤝
(Unawazungumziaje majinn ikiwa hujawah hata kuwaona wala huna uwezo kwa kufanya nao communication

Bora mleta mada mara 💯 kuliko huyu ostadh🚶🚶

(Mimi miaka zaid ya 20 mpk nishawazoea wamekuwa kama ndugu sasa..... Ila nawafaham juu juu tu🤝
Jinn kusema asili yake sio kitu kidogo (akwambie koo yake na jina lake la asili hiyo story nyingine
Hasa hao maruhan ndo hatari kabisa, mara 💯 hao wengine wapo kawaida kiasi
 
mkuu mimi swali langu ni huko masokoni hivi wale wanaofanya biashara wakiwa uchi lakini kwa macho yetu ya kawaida tunaona wamevaa nguo kuna siri gani wao kuuza wakiwa uchi na je,madhara yoyote kwa wateja wanaonunua na kula hivyo wanavyo viuza maana vyaweza kuwa vichafu pia na ipi njia ya kuwaepuka? na vitu wanavyouza ni halisi au kiini macho?
 
Fanya ibada, sali sala za usiku, usikae na mwili mchafu. Kuna aya na sura ndogo ndogo sana kwenye Qur'an zina nguvu sana kuliko chochote.

Qur'an ni shifa. Unajua maana yake? Ni hopital.
Sura hizo ni ikhilasw, falaq na nass au kuna sura nyingine ndogo zinahusiana na ushirikina na uwezo wa ALLAH tupe elimu Arsis
 
Back
Top Bottom