Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Sasa kama wewe wasema hivyo wakristo waseme nn?maana sijaona dini iliyosifiwa na jamaa kama uislam na Quran.Nyie ndio wale wafia dini na wagumu kujifunza,tulitakiwa tuchemke ni sisi wakristo ambapo Kuna sehemu kasema hata sio dini ya kweli.
Huyo jamaa anajificha nyuma ya uislam, mafundisho yetu sio ya kuabudia majini kama anavyo sema yeye. Ila anafanya shirki.
 
Ukiisoma moja katika sura ndogo za Qur'an iitwayo An-Nas (Q 114:4) kwenye aya ya 4 inawataja hao kua ni "Al khannasi" مِن شَرِّ ٱلْوَسْوَاسِ ٱلْخَنَّاسِ ٤ Isome aya yote hio ni kinga kubwa ya wasiwasi, aya zake ni fupi tu, naamini hakuna Muislam aliesoma madrasa ambae hajaihifadshi. Ina aya 6 fupi fupi. Link hii hapa; An Nas
Simba.
Sawa Kwa mkristo???

Cc Smart911
 
Sawa Kwa mkristo???

Cc Smart911
Qur'an haipo kwa ajili ya Waislam tu, ni kwa watu wote. Soma yenyewe inasema nini;

Q 45:20. Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu wanao yakinisha. 20

Naamini Mwenyezi Mungu hawezi kuleta kitabu kwa ajili ya watu fulani tu. Atakua mbaguzi, ubaguzi ni mapungufu ya kibinadam sio ya Mwenyezi Mungu.
Simba.
 
Huyo jamaa anajificha nyuma ya uislam, mafundisho yetu sio ya kuabudia majini kama anavyo sema yeye. Ila anafanya shirki.
Ma Shaa Allah, kujificha "nyuma ya Uislam" ni sifa njema kabisa hio, ulitaka nisijifiche nyuma ya Uislam? Mbona hunitakii mema ndugu yangu?

Hivi "shirki" uisemayo ndio kushirikisha? Maana nimeona aya hii kwenye Qur'an...

4_48.gif

Q 4:48. Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa 48
Simba.
 
Wongofu maana yake nin? Je anayekizngatia hicho kitabu maana yake amepata wongofu right?
Swali lako zuri sana, Raha ya Qur'an hua inajibu yenyewe, tafadhali jisomee;

Q 2:1. Alif Lam Mim. 1
2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, 2
3. Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa.3
4. Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo. 4
5. Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa. 5

Unaweza kuendelea kujisomea; Al Baqara
Simba.
 
Kwenye kupata PESA na mafanikio umewahi kujaribu kuwatumia hao viumbe ?
Sijawahi.

Uislam unanifundisha kua mali ni moja ya furaha za duniani nayo pia ni moja ya fitina za duniani.

Pia Uislam unanifundisha kua mwenye ubora kati yetu ni mcha Mungu. Kwa hio kwangu mimi, mafanikio ya msingi ni ucha Mungu, mengine yoite ni sekondari.

Halafu kwa ujuzi kidogo nilionao, una dua za kuomba mafanikio bila kutumia majini, kwani binadamu tuna uwezo wa hali ya juu sana zaidi ya majini.

Ukifanya mchezo unaweza kudondokea kwenye uchawi, nakuomba fata fahirisi usome visa vya misukule.
Simba.
 
Swali lako zuri sana, Raha ya Qur'an hua inajibu yenyewe, tafadhali jisomee;

Q 2:1. Alif Lam Mim. 1
2. Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu, 2
3. Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa.3
4. Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo. 4
5. Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa. 5

Unaweza kuendelea kujisomea; Al Baqara
Simba.
Ahsante..nini maana ya wongofu according to quran
 
Back
Top Bottom