Nimeacha CHADEMA vijana wengi imara, vyama sita vimeniomba nijiunge nao

Dr Slaa siku ya leo jioni akiwa Club house amesema yeye ataendelea kutetea sera nzuri za chama cha CDM kwa kuwa ana uzoefu nao na amekijenga kutoka zero mpaka hapa kinapewa heshima.

Kwa upande mwingine amesema yeye sio tena mwanachama hai wa chadema na hata hivyo vyama sita vimemuomba ajiunge nao na amekataa.

Hongera sana Dr Slaa kwa kazi nzuri uliyofanya wakati wako.

Naona sasa uko mtari wa mbele kutetea maridhiano na ujio wa Katiba Mpya.

Mungu akubariki.
Uzuri wenu mataga ni propaganda na kuwahadaa watanzania, ila mkumbuke wapo weledi na wamekaa pale wanaona mnavyojifanya wehu. Dr. Slaa hata kama alifanya kazi nzuri lakini alishafuta kwa mdomo na mikono yake mwenyewe, aliondoka na kusaliti wakati akitakiwa sana leo hii akisifia chama ambacho aliowaacha wamekaa magerezani, aliyekuwa anamshobokea wengine amewaua, hao vijana wamemiminiwa mijegejo na bado alikuwa pamoja na hao kuwamaliza hata leo hii akirudi anawakuta wako hoi na sio wale aliowaacha.

Ajipimie mwenyewe na ajichukulie hatua ambayo yeye ataona inafaa, mie ningemshauri aachane na jamaa amechangia kuwaumiza, wengine wanamaswali mengi mno kuliko majibu. Labda kama ataanza kusema waliompiga risasi Lissu na walioua akina Ben. Mwenyekiti amemkuta mzee kwa kukaa magerezani bila sababu yeye alikuwa ubarozini akisifu juhudi za walioshika hatamu kwa hila. Leo nyie mnalipwa buku 5000 kujaza thread za propaganda JF.
 
Mkuu niombe msamaha kwa kuniita mataga. Vinginevyo uko sahihi.
 
Back
Top Bottom