Nimeacha kazi: Nianzie wapi kwenye biashara?

Nimeacha kazi: Nianzie wapi kwenye biashara?

deni

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Posts
255
Reaction score
191
Habari zenu wana jamvi,

Nimeacha ajira kwa hasira. Nimefanya maamuzi ya kipuuzi? sijui! Ngoja nianzie mbali kidogo kuwasimulia:

Nilihitimu Shahada yangu ya Uhandisi mwaka jana na baada ya kukaa mtaani kwa miezi mitatu tu nilifanikiwa kupata ajira. Nilipata ajira kama fundi mchundo (Technician) na sio Muhandisi kama nilivyotegemea. Kwa kweli nilivunjika moyo kwa hilo kwa kuwa wakati huo naingia kazini niliingia na jamaa mmoja naye akaajiriwa kama Technician ila yeye amesoma Veta Level 2.

Kilichoniuma mimi ni kwamba nina Stashahada Ya Uhandisi Pamoja na Shahada ya Uhandisi alafu bado nalipwa sawa sawa na mtu mwenye cheti cha Veta, tena kiuhalisia yeye analipwa kiasi kikubwa kwa kuwa yeye hana makato ya Bodi ya Mkopo ila mimi bodi wananinyoosha.

Wakati naanza kazi nilimuuliza bosi wangu kwa nini naajiriwa kama Technician na sio Engineer, akanijibu kwamba nitaweza kupandishwa huko mbeleni kulingana na utendaji. Basi mimi nikaanza kazi.

Kwa kweli kazi ilikuwa na changamoto kwa sababu nilikuwa na majukumu mengi. Nikiwa ofisini nilikuwa nikihusika katika usanifu na kuandaa mpango kazi na nikiienda site nilikuwa napigika zaidi maana nilikuwa nahusika kwenye kusimamia kazi, ununuzi wa materials, na pia nilikuwa nikihusika katika kazi za kufanya kwa mikono.

Yaani kwa ufupi nilikuwa nikifanya kazi za fundi mpaka za muhandisi mimi mwenyewe. Katika mradi wangu wa kwanza nikagundua hata dereva analipwa pesa nyingi kuliko mimi, nikazidi kuumia.

Sasa bwana mwezi uliopita, mwisho wa mkataba wangu ukafika, bosi akaniita akanikabidhi mkataba mpya, lakini baada ya kuupitia nikagundua mshahara ni ule ule na cheo ni kile kile. Basi mimi nikamuomba bosi anipe siku moja nikafikirie alafu nitakuja kusaini au la. Baada ya siku moja nilirudi na nikaamua kuweka dau la mshahara ninaloona mimi ni sahihi. Kwa kifupi bosi alikataa na mimi nilikataa na mimi nikaishia hapo kufanya kazi.

Sasa turudi kwenye kichwa cha uzi huu. Naomba mnishauri niazie wapi maisha ya biashara maana kazi nimeshaacha (na sijui kama lilikuwa wazo la busara), hapa nina 2 million ambayo nilifanikiwa kuikusanya kwa mwaka huo mmoja niliokuwa nikifanya kazi.

Sijawaambia wazazi wangu wala watu wangu wa karibu kwamba nimeacha kazi na ninafikiria kwenda mkoa ambao nitakuwa mbali nao nikaaendelee kujifunza maisha huko.

Nipo tayari kufanya biashara ya hali yoyote, nakaribisha ushauri.

Asanteni.
 
Umefanya uamuzi wa busara sana ila biashara siyo rahisi kama mtu anavyofikiri au vitabu vya CBE, TIA vinavyofundisha.

Ulimwengu wa sasa hivi umehamia kwenye skills economy na sio professional economy. Kabla ya kuingia kwenye biashara ningekushauri tafuta kwanza skills moja halafu tushauriane mambo ya kufanya.
 
Well, wewe ni fundi wa nini? Kama fundi wa ujenzi, tumia akaunti zako za mtandaoni kujitangaza kwamba unajenga kwa ubora, uaminifu na bei nafuu.

Ukipewa kazi ya kujenga kuwa muaminifu kweli na fanya kazi nzuri. Utapata kazi hadi zitakushinda. Tatizo kubwa tulilonalo Tanzania ni mafundi wasio waaminifu. Ukiwa mwaminifu utakuwa tajiri ndani ya miaka mitano.

Huyo million 2 iweke vizuri, ili ukishafanikiwa utanipa kama malipo ya ushauri huu.
 
Brother kwanza nakupongeza sana kwa kufanya maamuzi magumu. Wengi wetu wanaburuzwa tu kwenye ajira bila kuwa na kipato kinachomsogeza kwenye maisha.

Ushauri wangu huo mtaji mkubwa sana ubane bank kisha taratibu fanya uchunguzi kwa ndugu jamaa na marafiki wafanyabiashara upate somo la kutosha na usiingie kichwa kichwa kwenye biashara yoyote ile.

Karibu sana
 
Umefanya uamuzi wa busara sana ila biashara siyo rahisi kama mtu anavyo fikiri au vitabu vya CBE, TIA vinavyofundisha
Ulimwengu wa sasa hivi umehamia kwenye skills economy na siyo professional economy. Kabla ya kuingia kwenye biashara ningekushauri tafuta kwanza skills moja halafu tushauriane mambo ya kufanya.
Skill Gani hiyo ndugu?
 
Brother Kwanza nakupongeza Sana kwa kufanya maamuzi magumu. Wengi wetu wanaburuzwa tu kwenye ajira bila kuwa na kipato kinachomsogeza kwenye maisha. Ushauri wangu huo mtaji mkubwa sana ubane bank Kisha taratibu fanya uchunguzi kwa ndugu jamaa na marafiki wafanya biashara upate somo la kutosha na usiingie kichwa kichwa kwenye biashara yoyote ile. Karibu sana
asante kwa ushauri
 
Hali ya uchumi kwenye sekta binafsi imekuwa ngumu sana, sekta nyingi binafsi zinayumba ndiyo maana mwajiri wako alikataa kukuongeza, naamini wewe bado ni kijana mdogo unazo nguvu nyingi na unazo fursa nyingi za kufanya maishani huku ukiendelea kujifunza maisha.

Ushauri wangu ni huu, Fanya Kazi kwa bidii lakini usije ukavutwa na akili ya kutaka mafanikio ya haraka, maisha hayapo hivyo kama vijana wengi tunavyofikiria. Pia jitahidi usiwe na tabia ya kujilinganisha na mwingine itakukatisha tamaa
 
Asingejipanga maana yake hata hiyo milioni mbili asingekuwa nayo. Anachoomba hapa ni wazo la biashara kwa mtaji wa milion mbili.
bado taarifa zimepinda. unafanya kazi, unapata million mbili huyo! unatimka na kuanza kuplan uifanyike kazi gani!! nilihani inaacha kazi una mikllion mbili tayari umepata fursa sasa unaona million mbili kwa mradi wako ukizifanyia zitakuwa a faia kuliko kazi hiyo.
hapo hajafunguka! unless hakuwa na kazi sasa kakwapua pahala anajikuta ana million mbili na hajui azifanyire nini!! Lakini wafabnya kazi , unalipwa unapata million mbili unaamua kupumzika kazi halafu unaleta jamvini hapo kwanza tuambie wewe una mawazo gani tuanzie hapo
 
Mshahara wake sio kwamba ni million mbili hiyo amekusanya mwaka mzima
 
bado taarifa zimepinda. unafanya kazi, unapata million mbili huyo! unatimka na kuanza kuplan uifanyike kazi gani!! nilihani inaacha kazi una mikllion mbili tayari umepata fursa sasa unaona million mbili kwa mradi wako ukizifanyia zitakuwa a faia kuliko kazi hiyo.
hapo hajafunguka! unless hakuwa na kazi sasa kakwapua pahala anajikuta ana million mbili na hajui azifanyire nini!! Lakini wafabnya kazi , unalipwa unapata million mbili unaamua kupumzika kazi halafu unaleta jamvini hapo kwanza tuambie wewe una mawazo gani tuanzie hapo
milioni mbili hiyo nimeikusanya kwa mwaka mzima sio kwamba nimeipata kwa mara moja. Ni kweli nimeacha kazi nikiwa bado sina detailed plan ya nini cha kufanya. ila ndo nimeshaacha na nnaamini nitasavaiv, hapa nimekuja kuomba ushauri kwa watu wenye uzoefu. Kama wewe unahisi nimeleta habari ya uongo ni siwezi kukuaminisha tofauti ila kama unaweza kunisaidia kwa mwongozo, nitakushukuru sana.
 
Unaishi wapi kwa sasa?
 
Back
Top Bottom