Nimeachwa na nimekubali, ingawa naumia moyoni

Una hela za kuchezea wewe kuna wanawake kibao wanatamani kukaa na mtu bila ndoa. Achana na kununua mtu. Mungu kakuepusha na mwizi wa kura huyo.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Na pia nadhani ulijitoa sana kwake kwa kila kitu. Going forward be careful unapodeal na mwanadamu; na angalau uwe tayari kwa lo lote maana mwanadamu anaweza kubadilika wakati wo wote. Jitoe kwa upendo huku ukijua kuwa ni sadaka tu unatoa lakini siyo kwa kutegemea cho chote maana kusema kweli loyalty ya mtu huwezi kuinunua ama kwa material things wala upendo wako wa kweli. Mwanadamu anaweza kuwa kiumbe katili sana akiamua!

Lakini pia kama malengo yako yalikuwa safi kwa huyu binti (if your intentions were pure) basi ondoka na dhamira safi huku ukijua kuwa hukumpotezea muda wake...and the Universe will reward you handsomely. Mwache aende na mtakie mema ila usije ukashangaa huko mbele ya safari kama atataka kurudi tena.

Kwa sasa hakuna njia ya mkato. Kuumia ni lazima utaumia lakini utavuka. Kwa kadri muda unavyokwenda maumivu nayo polepole yatapungua; na nati hizo zinazokaza kwenye moyo zitaanza kuachia na furaha yako itarudi.

Na ni lazima uchukue tahadhari. Usije ukaishia kuchukia wanawake wote. Huyu hakuwa wako na imeonyesha hivyo. Hata kama ungelazimisha basi huko mbele ya safari ungeumia zaidi ya unavyoumia sasa. Angalia tu usije ukaenda huko ukilalama na kuita kila mwanamke ni laghai, mbwa na malaya. Hutakuwa sahihi. Na siku moja utakuja kumpata aliye wako ambaye atakuonyesha mwanamke mwema na waifu matirio yukoje. Endelea kumtafuta mwanamke huyo kwa roho njema, moyo safi na dhamira isiyo na mawaa na siku moja utampata tu.

Sasa umekua! 👏🏼👏🏼👏🏼💪💪
Nimeishia hapa.
Umetoa uponyaji mkuu.
Ushauri sahii kabisa.
Huu ushauri umebeba experience za mapenzi.
Binafsi nimeuchukuwa.
 
Kumbe tupo wengi, japo mimi ni tofauti kidogo.
Nina maumivu nimezaa na binti mmoja, mtoto bado ana umri wa miezi 5 juzi ananiambia nikamchukue anataka kuolewa. Kumbuka nina mke ndani hajui chochote na akijua ndoa inayumba. Maumivu x2, kwanza nampenda binti mpaka nikamzalisha. Pili hilo la mtoto sielewi cha kufanya, na anadai nisipoenda kumchukua atamleta mwenyewe kwangu
 
Pole sana mkuu..
 
Anajua mimi ni wakili, tajiri na najielewa.

Sasa Kwa uelewa na exposure walizonazo unazani ukisema wewe ni Wakili watakuelewa?!

Lakini akiambiwa na Mwanaume anafanya kazi bank utaona faster analazimisha ndoa hata ya bomani bila ndugu kujua [emoji1787][emoji1787]

Yaani hawajali huko bank ni Teller wa kawaida au hata mfagizi ilimradi unafanya kazi bank [emoji3][emoji28]
 
Maisha ni lazima yaendelee.

Nakiri kwamba nilikuwa malaya sana zamani lakini nikaamua kubadilika baada ya kugundua kwamba mahusiano mengi kwa wakati mmoja yanapoteza muda, rasilimali fedha, yanadhoofisha mwili, akili n.k.

Nimekuwa kwenye mahusiano serious kwa takribani mwaka na nusu na Mwl mmoja wa Shule ya msingi. Mpole, msikivu, mcha Mungu, mnyenyekevu, sio mbinafsi, mshauri mzuri na zaidi ya yote amekuwa mfano bora wa mama wa familia. Nikaamua kumpenda kwa dhati. Nikawaambia hadi ma-x wangu. Nikawa najiachia nae, nikamtambulisha kwa baadhi ya wana.

Nikakaa kitako na Baba nipeleke barua ya posa, binti akaridhia. Barua ikaandikwa, mwanangu mmoja ambaye ameshaoa akakubali kuwa mshenga. Barua ilikuwa ipelekwe tangu j5 ya wiki iliyopita ila nikapata dharura tukaahirisha. Ilikuwa baada ya kupeleka posa ndio nikamtambulishe home.

J'mosi ya juzi akaanza kubadilika kuanzia kwenye mawasiliano na kila kitu. Jana nampigia simu aniambie barua tupeleke lini, akashtuka kama hajui kinachoendelea! Akajibu nisubiri kwanza, mara anaomba tupeane muda kuna mambo ajiridhishe!

Nikajiongeza, nikamwambia muda siwezi kumpa kwasababu tulishalizungumza hili. Aseme tu kama anadhani hatuwezi kuwa pamoja tena nitamuelewa. Akasisitiza nimpe muda! Nikamjaribu kwa kumwambia tuachane ili tusipotezeane muda (kumbuka hapa nilikuwa namjaribu); ili nione anawaza nini.

Lahaulaa, akasema 'SAWA'. Nikaishiwa nguvu. Nilikuwa barabarani nikasimama kwanza kwasababu nilipatwa na wenge nikahisi naweza kusababisha ajali.

Ina maana ile kupenana muda ilikuwa ni gia tu, alishaamua tuachane. Sikumtafuta tena tangu jana na yeye kakaa kimya mpaka muda huu!

Huyu ni msichana aliyeniaminisha kwamba hawezi kuniacha. Kwamba hata nikijaribu kumuacha atafanya jambo baya (ni kama alikuwa anatishia kujiua).

LAWAMA ZANGU ZOTE NAZIELEKEZA KWA RAFIKI YAKE MWENYE JINA LINALOANZA NA HERUFI 'J', ANAYEISHI MKOA UNAOANZA NA HERUFI 'M'. Mpenzi wangu alikuwa anamsikiliza sana, na mara nyingi wamekuwa wakiniongelea, nina kila sababu ya kuamini kwamba ushauri wake umechangia kumfanya mwanamke wangu afikie uamuzi huu. Huyu dada yeye kaolewa, leo kaamua kumfanyia figisu rafiki yake! We dada wewee....

Biblia imesema tushukuru kwa kila jambo. Pengine kuna jambo Mungu ameniepusha nalo. Naumia ila najikaza.
Pole sana mkuu ila kiufupi ulikuwa unaishi na jini kwenye chupa😀! Hapo ni kama amechoropoka.
 
Kumbe tupo wengi, japo mimi ni tofauti kidogo.
Nina maumivu nimezaa na binti mmoja, mtoto bado ana umri wa miezi 5 juzi ananiambia nikamchukue anataka kuolewa. Kumbuka nina mke ndani hajui chochote na akijua ndoa inayumba. Maumivu x2, kwanza nampenda binti mpaka nikamzalisha. Pili hilo la mtoto sielewi cha kufanya, na anadai nisipoenda kumchukua atamleta mwenyewe kwangu
Daaaah pole aisee
 
Yaani jumamosi hadi leo jumanne unasema umeachwa. Kwa taarifa yako kuachana sio rahisi kama unavyodhani. Kuachana na demu ni mchakato unaweza kuchukua zaidi ya mwaka au zaidi. Wewe umepumzishwa tu kuachana sijapaona bado. Kwanza hakuna sababu yoyote ya kuachana hapo sema tu unagongewa ambayo sio issue ya kusababisha usipeleke barua. Unagongewa na unaoa hivyo hivyo mambo yatajirekebisha mbele kwa mbele
 
Maisha ni lazima yaendelee.

Nakiri kwamba nilikuwa malaya sana zamani lakini nikaamua kubadilika baada ya kugundua kwamba mahusiano mengi kwa wakati mmoja yanapoteza muda, rasilimali fedha, yanadhoofisha mwili, akili n.k.

Nimekuwa kwenye mahusiano serious kwa takribani mwaka na nusu na Mwl mmoja wa Shule ya msingi. Mpole, msikivu, mcha Mungu, mnyenyekevu, sio mbinafsi, mshauri mzuri na zaidi ya yote amekuwa mfano bora wa mama wa familia. Nikaamua kumpenda kwa dhati. Nikawaambia hadi ma-x wangu. Nikawa najiachia nae, nikamtambulisha kwa baadhi ya wana.

Nikakaa kitako na Baba nipeleke barua ya posa, binti akaridhia. Barua ikaandikwa, mwanangu mmoja ambaye ameshaoa akakubali kuwa mshenga. Barua ilikuwa ipelekwe tangu j5 ya wiki iliyopita ila nikapata dharura tukaahirisha. Ilikuwa baada ya kupeleka posa ndio nikamtambulishe home.

J'mosi ya juzi akaanza kubadilika kuanzia kwenye mawasiliano na kila kitu. Jana nampigia simu aniambie barua tupeleke lini, akashtuka kama hajui kinachoendelea! Akajibu nisubiri kwanza, mara anaomba tupeane muda kuna mambo ajiridhishe!

Nikajiongeza, nikamwambia muda siwezi kumpa kwasababu tulishalizungumza hili. Aseme tu kama anadhani hatuwezi kuwa pamoja tena nitamuelewa. Akasisitiza nimpe muda! Nikamjaribu kwa kumwambia tuachane ili tusipotezeane muda (kumbuka hapa nilikuwa namjaribu); ili nione anawaza nini.

Lahaulaa, akasema 'SAWA'. Nikaishiwa nguvu. Nilikuwa barabarani nikasimama kwanza kwasababu nilipatwa na wenge nikahisi naweza kusababisha ajali.

Ina maana ile kupenana muda ilikuwa ni gia tu, alishaamua tuachane. Sikumtafuta tena tangu jana na yeye kakaa kimya mpaka muda huu!

Huyu ni msichana aliyeniaminisha kwamba hawezi kuniacha. Kwamba hata nikijaribu kumuacha atafanya jambo baya (ni kama alikuwa anatishia kujiua).

LAWAMA ZANGU ZOTE NAZIELEKEZA KWA RAFIKI YAKE MWENYE JINA LINALOANZA NA HERUFI 'J', ANAYEISHI MKOA UNAOANZA NA HERUFI 'M'. Mpenzi wangu alikuwa anamsikiliza sana, na mara nyingi wamekuwa wakiniongelea, nina kila sababu ya kuamini kwamba ushauri wake umechangia kumfanya mwanamke wangu afikie uamuzi huu. Huyu dada yeye kaolewa, leo kaamua kumfanyia figisu rafiki yake! We dada wewee....

Biblia imesema tushukuru kwa kila jambo. Pengine kuna jambo Mungu ameniepusha nalo. Naumia ila najikaza.
Hivi kuna wanaume malaya ama malaya ni wanawake?
 
Back
Top Bottom