Ndoa ni utapeli, ndoa ni biashara! Nimekuwa nikikutana na hizi kampeni za kataa ndoa humu jukwaani nikawa nazichukulia kama ni porojo tu, sikuwa nazichukulia kwa uzito hadi leo yamenikuta.
Back to the topic,
Wakuu, naomba nishirikishe hali yangu na kupata ushauri wenu.
Nina binti niliingia naye kwenye mahusiano mwaka 2022. Mwaka 2023 alianza chuo kikuu hadi 2025, na tulikuwa kwenye mahusiano ya siri. Hajawahi kunitambulisha kwao, ingawa mimi na Baba yake tumejuana kwa muda. Mwaka 2024 mwishoni, Baba yake aliniuliza kuhusu uhusiano wetu. Nikamjibu kwa uwazi kwa namna ya heshima, lakini sikusema kila kitu.
Mwaka 2025 binti akapata ujauzito na baada ya kumaliza chuo akarudi nyumbani. Nikaitwa na familia yake, tukakubaliana na faini ya Tsh laki 7. Baada ya hapo, niliendelea kutunza ujauzito hadi mtoto alipozaliwa Desemba 2025.
Sasa hivi, nimepewa barua ya mahari ya jumla ya Tsh milioni 18.5 (ng’ombe milioni 9, mbuzi milioni 7, mablanketi laki 2 na mengine). Awali, waliorodhesha mahari kiasi cha milioni 6. Waliuliza kama mimi ni mume wa dhati, kisha wakakubaliana tu na kulipa faini ya laki 7.
Nina nia ya dhati ya kumuoa binti huyu, lakini siwezi kulipa kiasi walichotaka (nina milioni 2 tu).
Swali: Je, mahari kama hii ni halali kwa taratibu za Kichaga?
Kwenye barua ya Posa imeandikwa "POSA KWA MCHAGGA MSOMI" hili la Mchagga msomi limenikera sana. Ndoa na usomi vinahusiana nini?
Ni mbinu gani za busara ninaweza kutumia kushughulikia hili bila kuvunja heshima za familia na desturi? Hivi Millioni 18 nanunua nini aisee? Wamenipa hasira sana nimepanga kuwajibu kwa barua kuwaambia sioi tena! Ni sahihi kuwajibu kwa barua?
Nimefupisha tu stori wakuu, naombeni ushauri wenu.
Intelligent businessman
Natafuta Ajira
Liverpool VPN
min -me
Xi Jinping