Nimeambiwa mahari Millioni 18. Sina Pesa hiyo na nataka kuoa, nifanyeje?

Ni vile mie ni team kataa ndoa ingekua sio hivyo ilikua Musahaf chapuuu
 
Kubali oa waambie sawa ngoja nikatafute mahari huwa hailipwi mara moja mimi mzee wangu alimalizia kupeleka ndama na mbuzi akiwa ndani ya 60's.
Wakukuokoa hapo ni wazee na sio wewe,tafuta wazee wakasemelee jambo lako
 
Inavyoonekana huyu jamaa hakuwa na mpango wa kumwoa huyo dada, kampa mimba kazaa halafu jamaa baada ya kulipa faini kakaa kimya. Hii barua aliyoletewa ni kama kumkumbusha kuwa kakaa kimya bila kuanza mchakato wa posa na mambo mengine. Jambo la msingi hapo jamaa qtume mshenga kwenda kwa wazazi wa binti wakajadili mambo ya mahari, mbona jambo hili linazungumzika?
 
18M?? Pengine wamekuona unajimudu!!

Mimi hata nguvu za ku- bargain zitaniishia,sirudi tena nam-block na Baba mkwe!!😁
 
Peleka hio hio huo ni mtihani tu wamekupa Mahari hailipwi yote lazima u-bargain kiume ndicho wanachokitaka kutoka kwako sio hizo million 18.5 wanataka maelezo yako ndani ya hio Million 2 ni yapi ambayo yatawashawishi wao wakupe binti yao?
Nimewaza hivi pia mkuu, asante .
 
Huko nimeelewa kabisa, aliponiacha ni kuletewa barua ya posa yenye kichwa cha barua "POSA YA BINTI MSOMI"😀😀.
Mkuu, huyu binti nilikuwa na mahusiano naye ya siri hatujawahi kwwnda kwao wanitambue rasmi na baada ya kupata ujauzito tena sikwenda na ndipo baada ya ujauzito kuonekana wazazi wake ndio wakanitafuta na siku tuliyoenda kukutana wao walikuja moja kwa moja na karatasi yenye vitu vinavyoorodhesha mahari ambapo kwa siku ile kwa hesabu za haraka haraka ilifika kama millioni 6.

Wakati wanaendelea kutaja jamaa mmoja akawakatisha kuwauliza swali kuwa, Je mnataja hivyo vitu vya mahari mna uhakika kuwa jamaa anaoa? Basi wale wajomba zake binti nddipo wakaniuliza kama naoa au la!
Baada ya kuwajibu ikabidi suala la mahari likazitishwa kwanza ndipo nikapigwa hiyo faini ya laki 7.

Siku zilisonga na binti akaja kujifungua na hatimae juzi wakanilitea hiyo karatasi ya posa au mahari ya millioni 18.

Nachojiuliza hapa ni kuwa mimi ndio muoaji na ndiye ninayepanga mipango yote ya kuoa na kutoa mahari kiujumla. Kwa nini wao ndio walete hiyo barua na wasisubiri mimi muoaji nipeleke?
 
Eti faini ya laki 7.. FAINI YA NINI?? binti kupanua mapaja??

Bila shaka hii ni chai
 
Mkuu fanya hivi:
Kwenye hiyo M2 tenga Laki 2 ( tu) ya mahari. Waambie hiyo Laki2 ndio utatoa kwa ajili ya chai kwenye vikao vya ndoa na siku ya ndoa pia. Wakisema haitoshi, waambie viungo vya chai unaweza kuwachukulia kutoka same ukawaletea ( kwa mfano tangawizi mbichi)

Wakikataa funga mlango bahari wa Hormuz kisha kaa kimya. Utakuja kunishukuru.
 
Asante kwa ufafanuzi zaidi mkuu. Nikuulize mpaka sasa wewe unajisikiaje kuhusu hiyo familia unayotaka kuoa na mkeo anasemaje kuhusu haya yote.
NB: Don't ignore red flags.
Watu wengi baada ya divorce huwa wanasema haya niliyaona kabla ya ndoa ila nilidhani mambo yatabadilka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…