Nimeambiwa mahari Millioni 18. Sina Pesa hiyo na nataka kuoa, nifanyeje?

Mkuu, mke wangu hana tatizo kabisa na nimejaribu kuongea nae akasema yeye anachounga mkono ni mahari tu, kuhusu gharama zisizo na umuhimu kwenye ndoa yeye haungi mkono.
Mfano, sijui mambo ya mbege, kreti za bia n.k...

Hata ishu za gharama za sherehe za harusi sio muhimu sana kwake ni bora hizo pesa za hizo sherehe na vinywaji tufanyie mambo mengine ya maana.
Just ni kutoa mahari tu then tunaendelea na maisha mengine, mambo ya send off sijui sio muhimu kwake.

Kuhusu hiyo familia sioni shida kabisa kwa mzee hadi Mama mkwe wananikubali mkuu.

Lakini hivi vikao vyote tulivyowahi kukaa wazungumzaji ni wajomba wa binti, Baba mkwe hajawahi hata kuhudhuria kikao.
Na kwa mujibu wa Binti ni kwamba, kuna mjomba wake kati ya hao nae ni kam hamkubali kabisa.

Anadai kuwa kuna mabinti wa huyo mjomba wake wapo ndoa zimeharibika kisa huyo mjomba wake! Yaani huyo mjomba anataka binti zake waolewe na mtu anayemkubali yeye.

Binti wa kwanza aliolewa na jamaa akatoa mahari nusu, na muoaji akaahidi kipindi ambacho atakuja kumalizia mahari. Muda huo ulipofika jamaa akawa hajapata pesa yote, sasa huyo mjomba wake akakasirika akaenda kumrudisha binti yake nyumbani.

Binti wa pili nae alikuja kumpata jamaa akampenda wakaanza kuwa na mahusiano kimya kimya, then huyu mjomba wa mke wangu alipokuja kugundua akamfukuza binti yake akaishi na jamaa.


Kiufupi mkuu, naona wajomba tu ndio wanaweza kuleta shida ila familia kwanzia Baba, Mama na Kaka wa Binti hawana shida kabisa na mimi.
Na hata kwenye kikao cha mwisho Kaka wa Binti alikuwepo lakini hajawahi hata kuchangia neno yeye anasema hana pingamizi lolote.
 
Mkuu, bahati mbaya mzee hajawahi kuhudhuria kikao chochote, kiufupi wajomba ndio wananipelekesha.
 
Naomba hyo m1niwekeke mkeka nitafute odds 200 kesho nakurudishia m 10
 

Mimi sina ushauri maana mimi nilioa binti bikra na nilifunga ndoa kanisani bila kulipa mahari. Nilikuja kulipa mahari baada ya miezi 6. na nililipa kama laki 2 na nusu hivi.
 
Mkuu una uhakika mtoto ni wako? Maana umeshafukuzwa kiaina.
 
wanajua tayari una mtoto hivyo wanataka kujua upo tayari kuoa na kutunza familia na kufanya maendeleo mengine au unataka kuoa ukatunzwe?
Angalia kama unamkakati wa kuweza kuilipa hiyo mahari ndani ya miaka 2 hivi uende na huo mkakati kuonesha kuwa unakipato cha kuweza kutunza familia ya watu angau watatu na sio kipato cha bahati nasibu....
kwa kuwa mtoto wao anamtoto, wanaogopa asije kwenda kuteseka......
Kama huna mkakati wowote....jua tu hapo imeshakuwa ngumu........
 
Still kama wazazi wa binti wanashindwa kutoa msimamo wao juu ya binti yao pia ni tatizo. Mjomba hawezi kuwa na authority juu ya binti wakati baba na mama yake wapo hai. Kuna shida kwenye hiyo familia
 
Kama hela ipo au una uhakika utaipata kwa miaka hata 3 mbeleni, lipa. au la, ongea nao ili ulipe kidogo kidogo kwa hizo miaka 3. 18M ni ndogo kulinganisha na thamani na upendo wa mwanamke huyo kwako wewe. Just pay for that woman. 18M is nothing as compared to true love.
 
We true love umeipima vipi mkuu?
 
Mpe mimba nyingine kama unamtaka kweli,watakuita wenyewe na mahali utapanga wewe,kama ukiona wamekukela mwache ila mtunze mtoto.
 
Huoi, unauziwa binadamu! Kataa mdau...
 
Waulize kama ulimkuta bikra. Hiyo heka kafanyie mengine, yaani 18M ulipie **** ambayo kuna msenge anapewa bure
Daaah me ndio mana huwa hawa viumbe siwapagi muda wangu kivilee, they are unpredictable, leo wako poa , kesho chengachenga.....
 
Kuwaza kuowa ni kukomaa kihisia na kimhemko ila sio kukomaa kiakili ,
 
Mkuu kama mambo hayaeleweki basi December njoo Mbeya nikupe dada yangu kwa mahari ya laki 3 tu na mbuzi wawili.

ANGALIZO: Wahi mapema mana wateja wamekuwa wengi
 
wajibu kwa kumpa mimba ya pili binti yao kisha umkatae........na mtoto akizaliwa aitwe M18. au hata M23
 
Kumshauri mtu anayekaribia kutapeliwa ni ngumu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…