Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Pole sana ndugu. Unaacha ubwabwa wa nazi na njegere.oooh ama kweli dunia mapito
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it is..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk

Powerful!, kudos mkuu you don't let down.
We need this kind to make the World a little better place to live, and as an encouragement for those who're weak.
 
Naamini baada ya miez 4 utakuja hapa na kuandika chochote....mipango ya Mungu sio ya wanadam
Keep faith muombe mungu roho yako iwe na amani...furaha
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Pia soma > Atakayenisaidia hili nitampa Tsh milioni moja taslimu

Bye bye Mother earth.
Imeandikwa: WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA: Wengi wanapenda miujiza ya papo kwa papo baada ya maombezi wanaendelea na maisha yao ya dhambi lakini hawataki kumpokea Yesu katika maisha yao, Hakuna linaloshindikana mbele za Mungu, Kifo hakijawahi kuwa suluhisho LA mtu kuishi vizuri kama utakufa kama hujaokoka huko uendako ni mateso makubwa kuliko ya duniani...
 
Kwa muda baada ya kuusoma ujumbe wako moyo ulikufa ganzi,na matukio yakapita haraka sana kwenye ubongo wangu.Nilijukuta nashindwa nikupe pole ama nifanyeje.Namshukuru Mungu leo kanipa ujasiri wa kusoma tena na kutafakari kwa kina.Kwako Folk,kifo kwako ni ushindi baada ya mapambano magumu na mazuri.Ni magumu kwa vile unapitia kipindi kigumu chenye fadhaa nyingi na maumivu lakini jipe moyo ni ya kitambo tu.Ni mazuri kwa vile ulikuwa na nyakati nzuri maishani.Nyakati za furaha na vicheko pamoja na ndugu na marafiki hata sasa daima tunakukumbuka na kukuombea mema,neema na rehema.Nafurahi baada ya mapambano hayo ni ushindi.Ndio ni ushindi kwakuwa tunaamini kifo si mwisho wa maisha yetu bali ni mwanzo wa maisha bora zaidi yasiyo maumivu na bila mwisho.Je tujiue ili tupate ushindi?La!ni lazima tupambane ili kuufikia mwisho mwema.Kujiua ni woga na kutaka ushindi rahisi ni ushindi wa kinyonge bali majasiri hupambana mpaka mwisho.Ugua pole Folk nawe hutakufa bali kwa pumzi yako utasimulia makuu ya Mungu aliyotenda kwako
 
Powerful!, kudos mkuu you don't let down.
We need this kind to make the World a little better place to live, and as an encouragement for those who're weak.
I'm humbled and impressed to hear from you the smartest woman I know hapa JF Nalendwa appreciating my writings.. What an honour?

Thank you!
 
kuna harufu ya utapeli au matayarisho yake..Kuna watu watapigwa soon
 
Kwanza nikupe pole ndugu,lakini jambo la pili nikwambie lililoshindikana kwa binadamu kwa Mungu linawezekana ni wewe ku take strong faith,na mwisho nikwambie biblia inasema heri tangu sasa wafao katika Kristo,hivyo basi tengeneza na Mungu rafiki mpokew Kristo awe Bwana na mwokozi wako ili uepukane na adhabu na ukapate pumziko la milele,hii ndio zawadi ninayokupa mimi.
 
Death is a surprise. Hakuna daktari anayeweza kujua kuwa utakufa lini. Mungu alivyo mkubwa, huyo aliyekwambia kuhusu miezi ya kufa kwako anaweza akafa kabla yako ( ukaenda kumzika ). Jipe moyo ndugu yangu. If death comes, take it with courage and confidence. Tambua tu kwamba "ikiwa Yesu hajarudi, wote tulala kaburini tukiisubiria asubuhi ya ufufuo". KIFO NI USINGIZI MTAMU USIOSUMBULIWA HATA NA NDOTO.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom