Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Death is a surprise. Hakuna daktari anayeweza kujua kuwa utakufa lini. Mungu alivyo mkubwa, huyo aliyekwambia kuhusu miezi ya kufa kwako anaweza akafa kabla yako ( ukaenda kumzika ). Jipe moyo ndugu yangu. If death comes, take it with courage and confidence. Tambua tu kwamba "ikiwa Yesu hajarudi, wote tulala kaburini tukiisubiria asubuhi ya ufufuo". KIFO NI USINGIZI MTAMU USIOSUMBULIWA HATA NA NDOTO.
Kuna suprise death ila sio kansa. Mimi mama yangu alikufa kwa hii kansa. Zilivyobaki wiki nne ikabidi watuandae kisaikolojia ikiwa ni pamoja na mgonjwa kwamba after four weeks atakufa. And zilipobakia siku saba alikata kauli exactly siku ya saba akafa. Huwa wana vipimo vyao ambavyo vinawapa majibu hayo. Japo huwa ni round figure inaweza kuzidi ama kupungua ila ni +-7
 
Pole sana folk. Kwa maelezo yako inaonyesha kama umeikubali hali. You are strong. Kwa hisani ya Google hizi ni dalili za pancreatic cancer. Kwa maelezo yao ni ngumu mno huu ugonjwa kuujua mapema.
-kutokuwa na hamu ya kula au kujisikia umeshiba haya kama ulikula kidogo kwa sababu chakula hakijisagi ipatavyo inakufanya upungue uzito.
-macho na Ngozi kuwa njano ( jaundice )
- maumivu ya tumbo na mgongo au baada ya kula unasikia maumivu ya tumbo.
-kujisikia ovyo na kutapika
-tabu kumeza chakula unahisi kama chakula kimekaba kooni.
- mabadiliko yako ya choo, ukienda haja kubwa mavi yanakuwa na harufu mbaya mno au yanakuwa na mchanganyiko kama mafuta mafuta, au choo kinabadilika kinaweza kigumu au siku nyengine unaharisha. Digestive system inakuwa haiko sawa .
Check up inayotakiwa ni CT scan, endoscopic ultra sound (EUS) na biopsy
 
Ni sababu tu uwapendao utawaachaje? Lakini kufa mapema ni vizuri maana baada ya karne moja unazaliwa tena. Sasa by the time unaweza kuja duniani tena ukakuta taifa la wastaarabu; siyo lile la kutekana tekana au kuuana bila sababu za msingi.

Tangulia tunakuja huko nasi... sonner is better.....
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it is..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk
SOMA: HUTAKUFA UKIFUATA HAYA SOMA KITABU CHA THE POWER OF SUBCONSCIOUS MIND (DOWNLOAD SOMA). KWA KUANZIA IKATAE KANSA KWA MANENO SUBUHI MCHANA JIONI KILA SIKU UONE KAMA KANSA ITAKUWA NA WEWE TENA UNAPONA. PIA TAFUTA HABATI SODA CHANGANGANYA NA ASALI KULA KIDOGO KIDOGO KILA SIKU MAISHA YAKO YOTE HUTAKUFA KIRAHISI HIVYO. KATAA KANSA KWA MANENO HALI UKITUMIA HIVYO VITU...UKIAAMINI UTAKFA KWA KANSA KWELI UTAKUFA AMINI HUTAKUFA NA UIKATAAE KANSA KILA SIKU. USIPUUZE HAYA!
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Pia soma > Atakayenisaidia hili nitampa Tsh milioni moja taslimu

Bye bye Mother earth.

Kuwa imara kamanda. Hauko mwenyewe ktk hili, na wewe sio wa kwanza kupata habari kama hizi, na hata ikitokea ukafa pia hutakuwa wa kwanza...watu tunakufa kila siku.

Kwa sasa inaonekana ulishakubali hiyo hali, but still lipo tumaini kwake yeye aaminiye. ILA ulipaswa pale ulipopewa majibu kama hayo ungeyakataa na kusema huna tatizo, na unahisi ni ya mtu mwingine au mashine imekosea. HII inaitwa imani, na inaaply zaidi ikiwa una imani nzuri juu ya nguvu zake Mola. Kuna shuhuda kibao za namna hii, watu walipewa majibu kama hayo na kuyakataa, na walipopima mara ya pili ilionekana hawana tatizo. This is how God works in mysterious ways.

Bwana Yesu akupe tumaini lililetalo uzima na toba ya kweli. Kwa kupigwa kwake sisi sote tumepona, na tu mauhuru kweli kweli.

Zaburi 103:3 - "Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote".
 
SOMA: HUTAKUFA UKIFUATA HAYA SOMA KITABU CHA THE POWER OF SUBCONSCIOUS MIND (DOWNLOAD SOMA). KWA KUANZIA IKATAE KANSA KWA MANENO SUBUHI MCHANA JIONI KILA SIKU UONE KAMA KANSA ITAKUWA NA WEWE TENA UNAPONA. PIA TAFUTA HABATI SODA CHANGANGANYA NA ASALI KULA KIDOGO KIDOGO KILA SIKU MAISHA YAKO YOTE HUTAKUFA KIRAHISI HIVYO. KATAA KANSA KWA MANENO HALI UKITUMIA HIVYO VITU...UKIAAMINI UTAKFA KWA KANSA KWELI UTAKUFA AMINI HUTAKUFA NA UIKATAAE KANSA KILA SIKU. USIPUUZE HAYA!

Hichi kitabu ni kizuri sana mkuu. Mtu akiweza kukiweka kwenye matendo na kujituma kuchapa kazi basi maisha yatakuwa safi sana.
 
Aisee. Nimejikuta napatwa na huzuni kubwa, pole ndugu. Jiweke tayari kwa maombi juu ya kujitakasa na Mwenyezi Mungu akupokee.
 
Kuna jamaa yangu naye aliwahi kuambiwa hivyo, sasa karibu miaka 10 jamaa yupo, sipati picha kama angeamini hayo maneno akafuja vimali vyake. Kaza roho na kusali mkuu.
 
Majibu ya Daktari yasikupe hofu
Yupo Daktari wa Madaktari ambaye anaitwa Yesu


Ukimuita anaitika
Mwambie sintakufa Bali Bali nitaishi
Niyasimlie matendo makuu ya Mungu

Hakika Mungu Mungu hawezi kukuacha
Amini tu uzima uko kinywani mwako.
 
Uyo dokta hakufaa kukwambia ivyo sijapenda hajui miiko......kila mtu atakufa najua ivyo ila ni siri kati ya mungu na wewe .....sasa iyo miezi4 ikifika kama hujafa.
Hajui miiko ya kazi sijapenda ila usife moyo mungu ndie ajuae kesho yako
Daktari hajakosea yy huwa anaaangalia probability ya ukuaji wa hiyo cancer mpaka muda gani itakuwa ni critical na amemuambia miezi 4 si kwamba ana uhakika kuwa atakufa ndani ya miezi minne bali ameangalia ukuaji wa cance r hiyo.
Pia miiko haijavunjwa kwa kuwa ameongea na mgonjwa direct na hajavujisha siri kwa watu wa nnje pia amemuambia ili kama jamaa ana uwezo awahi kuitibu .
Kingine ambacho haujafikiria ndugu ni kuwa hivi itakuwaje ukaenda kupima ukimwi halafu daktari asikuambie kuwa umeathirika akakuficha je atakuwa amefanya jambo jema?
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Pia soma > Atakayenisaidia hili nitampa Tsh milioni moja taslimu

Bye bye Mother earth.
naumia sana, pole sana ndugu yangu, pili nakuomba usizungumzie kifo just pray Mungu ni muweza wa yote, nmeanhalia thread uliyotuma link yaonyesha ni 2013, status yako ilikuaje mwaka huo, na mwaka huu ipoje, tazama wangapi wametangulia tangu ulipoisi wewe ndie unaefata, Pole sana, na Mungu akupe nguvu.
 
Daktari hajakosea yy huwa anaaangalia probability ya ukuaji wa hiyo cancer mpaka muda gani itakuwa ni critical na amemuambia miezi 4 si kwamba ana uhakika kuwa atakufa ndani ya miezi minne bali ameangalia ukuaji wa cance r hiyo.
Pia miiko haijavunjwa kwa kuwa ameongea na mgonjwa direct na hajavujisha siri kwa watu wa nnje pia amemuambia ili kama jamaa ana uwezo awahi kuitibu .
Kingine ambacho haujafikiria ndugu ni kuwa hivi itakuwaje ukaenda kupima ukimwi halafu daktari asikuambie kuwa umeathirika akakuficha je atakuwa amefanya jambo jema?
Soma post yake vizuri

Sent from my VFD 1100 using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom