Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Kila jambo binadamu analopitia lina maana yake kiroho, yawe magonjwa, karaha, furaha, mafanikio au mateso yote huja kwa sababu. Rohoni hakuna jambo linalokuja bure yote yana sababu na hata ramani ya kupita yanayo. Nothing comes for free, kila tukio juu ya maisha ya mtu linasababucha msingi tu kujua ni nani kalileta na unaweza kukataa rufaa kwa nani. Kizuri ajuaye sababu ya kila jambo ni MUNGU peeke yake na bahati nzuri huwa anaongea na anazungumza aulizwapo.
Na raha kuliko yote Kuishi au kufa kwa mtu ni kazi ya ulimi wa mtu, ukiamua kufaa unakufaa na ukiamua kuishi unaishi. kama ungesema nikushauri ningekwambia, isikilize roho yako sana ukiwa kwenye utulivu na kuomba MUNGU kama unaona imo nguvu ndani yako Tafuta kuishi na ondoa hofu ya mauti, kwa sabau kifo si chochote kwa MUNGU ni siraha ya shetani kuwatisha wanadamu., kwa maana anajua hofu ya mwisho ya mtu ni mauti.
Ongeza uhusiano wako na Mungu, usisikilize mawazo na sauti za watu, isikilize roho yako inasea nini, hiyo ndiyo inaufahamu uhalisia wako na sababu ya tatizo. NAKUHAKIKISHIA HALI ULIYONAYO INAWEZA KUBADILIKA NA UZIMA UKAWEPO, kumbuka mifupa mikavu inaweza kuishi.
angalia yafuatayo.
1. Jenga kwanza mahusiano yako na MUNGU mpaka usikie amani moyoni, na hofu ya kifo itaondoka kabisaa. kwanini itaondoka kwa sababu kufa kwake MUNGU sio mzigo, ila kwa shetani ni mzigo. Naukiona unaogopa kufa ujue unahitaji kujenga uhusiano na MUNGU.(kifupi OKOKA)
2.Ukisha pata amani moyoni, anzaa kumuuliza MUNGU rehema na akuongezee Miaka ya kuishi, hapa kama kuna watumishi unawaamini unaweza kuwaita wakuongezee ufahmamu na kukuombe. Usijipe haki hata kidogo kwenye lolote kwa sababu wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na uukufu wa MUNGU, wewe omba toba na rehema.
3.Kiri kwa kinywa chako kwamba sitakufaa nitaishi, futa maneno yote uliyokiri kufaa. futa kila neno ulilosema vibaya juu ya maisha yako. ukiwa na mahusiano mazuri rohoni na MUNGU atakuonyesha na kukumbusha ya kukiri na kufuata, kile roho inachokuambia kufanya ,kufanya maana hilo ndilo la kweli. kwa sasa punguza sana kuwasikiliza watu bila jambo la Msingi, kwa sababu kwa sasa hawezi kukusaidia.
4. Amini kuishi tena kwa afya kunawezekana na awezaye haya yafanikiwe ni MUNGU tuu. Hivyo mahusiano yake naye ni muhimu kuliko chochote kwa sasa.
Nenda you tube angalia baadhi ya magonjwa na shuhuda ambazo wengine waliokuwa kwenye hali mbaya sana lkn MUNGU aliwaponya, angali TB joshua itainua roho yako na kukufikirisha upya na kuongeza hamu yako ya kuishi tena.
5. Commitment yako kwa MUNGU iwe akikupa tena nafsi kuishi utamtumikia na kuisha kwa kumpendeza yaye.