Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Unaniumiza moyo jamaniii. Pole sana sina lingine la kusema. kuona kifo mbele nadhani ni jambo linaloumiza sana
 
Huu uzi umeniumiza roho sana .....mkuu kabidhi maisha yako kwa Mungu yeye ndie aijuae kesho yako.
 
Bila kujali kama wewe ni dhehebu gani,kama kama kuna watu ambao wanaweza kukusaidia ukapata USD 3000 KWA HARAKA,Nenda LAGOS Kwa Prophet T.B.JOSHUA.Ninao uhakika more than 100% kwamba T.B.JOSHUA Akikugusa na mkono wake wa kulia mara moja tuu! utapona kabisa na wewe mwenyewe utakuwa a Living testmony.Nipigie kwa no.0784 269805 kwa ushauri zaidi.

Asante kwa kumshauri. Hata mimi nimempa ushauri huo huo. Ila gharama ulizomtajia ni kubwa sana. Sidhani kama zimefika huko. Mara ya mwisho mwaka jana (July 2017) nilikwenda mwenyewe kuulizia kwa wakala pale opposite na Mbezi Beach secondary niliambiwa shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki sita (2,600,000/=). Sasa hiyo rate uliyompa wewe ukibadilisha kwa shilingi ya Tanzania inakaribia shs 6,500,000/=. Namshauri aende pale Mbezi Beach Secondary, aonane na yule mama kiongozi wa kituo. Ni mama mwaminifu sana na hata TB Joshua anamkubali na kumtumia pia kusambaza annointing water, vitabu n.k. Pale atapata na maombi na gharama zote ikiwa atahitaji kwenda kwa TB Joshua.
 
Mwenye mamlaka ya kutangaza mwisho wa maisha ya mtu ni MUNGU pekee. Hayo ya umebakiza miezi, siku ni mawazo (yenye ukomo wa kufikiria wa mwanadamu). MUNGU atakupa maisha marefu mpaka ushangae. Barikiwa ndugu yangu. Hutakufa bali utaishi ... na kuyasimulia matendo makuu ya Bwana Zaburi 118:17

Tukutane kwenye Birthday party yako ya mwaka 2019 ndugu yangu... unikaribishe kabisa niandae na zawadi. See you Pal.
 
Asante kwa kumshauri. Hata mimi nimempa ushauri huo huo. Ila gharama ulizomtajia ni kubwa sana. Sidhani kama zimefika huko. Mara ya mwisho mwaka jana (July 2017) nilikwenda mwenyewe kuulizia kwa wakala pale opposite na Mbezi Beach secondary niliambiwa shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki sita (2,600,000/=). Sasa hiyo rate uliyompa wewe ukibadilisha kwa shilingi ya Tanzania inakaribia shs 6,500,000/=. Namshauri aende pale Mbezi Beach Secondary, aonane na yule mama kiongozi wa kituo. Ni mama mwaminifu sana na hata TB Joshua anamkubali na kumtumia pia kusambaza annointing water, vitabu n.k. Pale atapata na maombi na gharama zote ikiwa atahitaji kwenda kwa TB Joshua.
Distance is NOT a Barrier... If you have faith.
 
Nimeuona uzi huu ghafla nikajikuta naingiwa ubaridi moyoni. Ndugu hata kama umedhoofika vipi, nuru ninaamini ipo na haiko mbali nawe ingawa giza unaliona linazidi kutapakaa kote unakoangalia. Kuwa na imani ya kupona ingawa sio rahisi kuwa na imani hiyo kikawaida. Bado nafasi unayo ndugu.
 
Tutafute kuona Mungu anatukuzwa iwe katika kuishi kwetu au kufa kwetu. Hii itawezekana tukiishi maisha masafi ya kumpendeza Mungu tukiwa mbali na dhambi. Tutafakari ujumbe huu kwa pamoja ili tuweze kuandaa mioyo yetu , maana hata sisi tunaojiona ni wazima sasa tunaweza tukaondoka tukamuacha huyu ndugu akiendelea na maisha.



JEHANUM YA MOTO



zachary-kakobe.jpg
Neno la Uzima kutoka kwa Askofu Zachary Kakobe

Tovuti : www.bishopzacharykakobe.org

Facebook : www.facebook.com/bishopkakobeministries

Youtube : www.youtube.com/user/bishopkakobe

SOMO LA 6: JEHANUM YA MOTO

Yesu Kristo anatufundisha waziwazi kuhusu Jehanum ya moto, akituonya kumwogopa Mungu mwenye uwezo wa kututupa Jehanum. Anaendelea kutuonya kwamba, ni heri kukubali lolote lile litupate kuliko kwenda kwenye mateso makali ya Jehanum (LUKA 12:5, MATHAYO 5:22, 29-30). Maandiko pia yanaendelea kusisitiza kwa msisitizo mkubwa kwamba, ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai na kutupwa katika Jehanum ya moto (WAEBRANIA 10:26-27, 31). Jehanum hii ya moto inaitwa pia kuzimu (ZABURI 9:17) na tena inaitwa Tofeni (ISAYA 30:33). Hatupaswi kulipuuza jambo hili na kulifanya juu juu tu. Kwa sababu hii, leo, tutajifunza kwa undani kuhusu Jehanum ya moto, na tutaligawa somo letu katika vipengele vinne:-

(1) HUKUMU BAADA TU YA KUFA

(2) JEHANUM YA MOTO IKO WAP?

(3) HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO

(4) JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO

( 1 ). HUKUMU BAADA YA KUFA

Biblia inaeleza waziwazi kwamba mtu anapokufa, sekunde ileile ya kufa kwake anakabiliwa na hukumu (WAEBRANIA 9:27). Watu wanaofundisha kinyume na kweli ya neno, hufundisha kwamba mtu anapokufa analala tu na hakuna lolote la hukumu ya mara moja. Wanatumia maandiko yanayozungumzia kulala kwa kuyatafsiri isivyo (MATHAYO 27:52; 1 WAKORINTHO 15:20; YOHANA 11:11-14 n.k ) na pia wanasema wafu hawajui lolote kwa kutumia maandiko kama MHUBIRI 9:5. Ilivyo ni kwamba kinachobaki kaburini ni mwili tu. Nafsi na roho ya mtu huondoka kwa kuvalishwa mwili mwingine ( 1WAKORINTHO 15:40 ). Mwili unaobaki kaburini ndiyo ambao umelala haujui lolote na hauna kumbukumbu, lakini pasipo mwili huo mtu atamwona Mungu ikiwa ameishi katika mapenzi yake (AYUBU 19:26). Mwili hubaki kaburini, lakini roho ya mtu huondoka (MHUBIRI 12:7). Ikiwa mtu ameishi katika mapenzi ya Mungu mara tu ya kufa huchukuliwa mbinguni na malaika kwa kutumia magari maalum ya mbinguni (LUKA 23:43; 16:22; 2WAFALME 2:11-12; ZABURI 68:17; WAEBRANIA 1:7, 14). Ikiwa ameishi katika dhambi hukumu yake huwa kutupwa katika Jehanum ya moto mara tu baada ya kufa (MITHALI 9:13-18; ISAYA 5:11-15; MITHALI 17:24-27).

( 2 ). JEHANUM YA MMOTO IKO WAPI?

Mtu anapokufa tu, huwa kwenye njia panda. Kila mmoja hupenda kwenda mbinguni, hata hivo ikiwa jina lake haliko katika kitabu cha uzima cha mbinguni, hulazimika kwenda Jehanum ya moto. Mtu anayetakiwa kwenda motoni huchachamaa na kukataa kwenda kwenye njia mbaya inayotisha ya motoni na hulazimika kukamatwa na kutupwa Jehanum (UFUNUO 19:20; 20:10). Mbinguni ni juu (mbingu ya tatu) lakini kuzimu au Jehanum ya moto ni chini (pande za chini za nchi) 2WAKORINTHO 12:1-4; ITHALI 15:24; ZABURI 63:9; EZEKIELI 31:14.

( 3 ). HALI HALISI YA JEHANUM NA WALE WALIOKO HUKO

Jehanum ya moto ni kuzimu au shimo kubwa na refu sana lililojaa moto. Moto huu huwashwa mfululizo kwa pumzi ya Bwana (ISAYA 14:15; 30:33). Moto ni mkali kuliko moto wowote tunaoufahamu duniani, uwe gesi, umeme, makaa yam awe au lolote jingine (WAEBRANIA 10:27). Moto huu ni mweusi unaosababisha giza na kufanya mtu awaone wenzake wachache tu wa karibu naye (MATHAYO 11-12; 22:13; 25:30 YUDA 1:6).Moto huu una uwezo wa kula na kutafuna, kwa hiyo huwatafuna au kuwala wale walioko motoni (KUMBUKUMBU LA TORATI 32:22; WAEBRANIA 10:36-27). Hata hivyo, kama jinsi ambavyo chumvi inavyozuia nyama kuharibika, moto humtafuna mtu lakini hamaliziki (MARKO 9:43-49). Ni moto wa milele (MATAYO 25:41). Mafundisho potofu ysnswafariji watu na kusema eti mtu ataunguzwa na moto na kutoweshwa au kupotea na kuangamia kabisa na ndiyo mwisho wake. Wanatumia maandiko kama MATHAYO 10:28 ( kuangamizwa ) na YOHANA 3:16 ( kupotea ). Kuangamia hakumaanishi kualizika kabisa (ESTA 4:16). Kondoo akipotea haimaanishi hayupo kabisa ila ametengwa na mchungaji (angalia ISAYA 57:1-3). Vilevile neno “kuharibu” linapotumika kuhusiana na adhabu ya milele halina maana ya kufanya kitu kisiwepo, bali ni la kuzdhibu vikali ( 1WAKORINTHO 3:16-17 ). Waalimu hawa wa uongo hufundisha pia kwamba ati watu watatoweshwa kama moshi baada kwa kuunguzwa kwa kutumia ZABURI 37:20. Kutoweshwa hapa ni kutenganishwa mbali na Mungu. Moto wa milele, huambatana na madini yanayoitwa kiberiti (lugha ya kitaalam, “sulphur”). Madini haya yakiwaka huwa kama mpira na hutoa harufu kama ya mayai yaliyooza. Harufu ya namna hii inafunika kuzimu yote. Siyo hayo tu, katika moto huu wamo funza maalum ambao huwatafuna watu na kufanya matundu mengi katika miili yao wakiingia na kutoka. Hii hufanya sura zao kuwa mbaya mno kama madude tu! (ISAYA 14:11; MARKO 9:43-49; ISAYA 66:24).Jehanum ya moto, huitwa pia mauti ya pili (UFUNUO 21:8). Uchungu wa mauti unaompata mtu anapokufa, huwa juu ya mtu motoni, milele na milele (UFUNUO 20:10). Watu walioko motoni hujawa wakati wote na vilio na tena husaga meno yao kama mtu anayeona baridi kali MATHAYO 8:12). Kuzimu, urikalo ni pigo lif urikalo ambalo huwachukua wenye dhambi asubuhi, mchana na usiku (ISAYA 28:15, 18-19). Walioko motoni wanajifahamu, na kuwakumbuka wenzao waliowaacha duniani na tena hutoa ndimi zao nje wakitamani maji kidogo kupoza ulimi (LUKA 16:19-24). Juu ya yote hayo, katika vilio vyao, humwomba Mungu awahurumie na kuwasamehe lakini Yeye amekwishasema, “Nami jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma” (EZEKIELI9:10;8:18).

USEMI NA FIKRA ZA WALE WALIOKO MOTONI

Watu walioko motoni hutamani mtu mmoja kati yao aje awashuhudie ndugu zao ili wayoache dhambi na kukwepa mateso yao (LUKA 16:27-31). Wale walioko huko wajiopata mafundisho haya kabla, husema, “Jinsi nilivyochukia maonyo, na na moyo wangu ukadharau kukemewa; wala sikuisikia sauti ya waalimu wangu, wala sikuwategea sikio langu walionifundisha (MITHALI 5:11-13)” Wakimwona yeyote anayejiunga nao, humwambia, “Jew ewe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe ummekuwa kama sisi!” ( ISAYA 14:9-10).

WALIO MBINGUNI HUPEWA NAFASI YA KUWACHUNGULIA

Walioko mbinguni watatoka kidogo kuwaangalia (ISAYA 66:24) ila hawatakuwa na machozi yoyote juu yao.

TOFAUTI KATI YA JEHANUM YA MOTO NA ZIWA LA MOTO

Jehanum ya moto ni tofauti na ziwa la moto linalotajwa katika UFUNUO 20:14-15; 21:8 kwa jinsi ileile mbingu ya sasa ilivyo tofauti na mbingu mpya inayotajwa katika UFUNUO 21:1. Ziwa la moto kwa sasa halina mkazi ndani yake. Watakaokuwa wa kwanza kuingia humo watakuwa mnyama (Mpinga Kristo) na nabii wa uongo (UFUNUO 19:20). Kisha atafuata ibilisi ambaye atatupwa humo baada ya vita ya Gogu na Magogu (UFUNUO 20:7-10). Baada ya hapo kutafuata hukumu ya jiti cha enzi, kikubwa cheupe. Hukumu hii itatolewa baada ya ufufuo wa pili au ufufuo wa hukumu ambao utawafufua walioko Jehanum ya moto.Baada ya hawa kuelezwa kwa nini wamehukumiwa adhabu ya matesoya milele, ndipo watakapotupwa katika ziwa la moto. Mateso yaliyoko ziwa la moto ni zaidi sana kuliko mateso ya Jehanum ya moto. Ni kama Jehanum walikuwa mahabusu na sasa wanapelekwa gerezani. Kama mbingu mpya itakavyokuwa nzuri zaidi kuliko mbingu ya sasa, vivyo ziwa la moto litakuwa na mateso yaliyokithiri kuliko Jehanum ya moto.

( 4 ). JINSI YA KUIKWEPA JEHANUM YA MOTO

1 .Kuungama dhambi na kuziacha (MITHALI 28:13).

2. Kulishika Neno la Mungu kwa kufanya maagizo yote ya Mungu na kuwakata wafariji wenye kutaabisha wanaosema kufanya hili na lile siyo lazima ( YOHANA 8:51; ZABURI 119:6; AYUBU 16:1-2 ).

3. Kutohesabu sheria kuwa kutu kigeni. Kukubali kuongozwa na sheria ya Kristo. Hakuna mwanafunzi asiyeishi kwa sheria ( HOSEA 8:12; WAGALATIA 6:2; ISAYA 8:16 ).

4. Kuwa mtakatifu na kutoifuatisha namna ya dunia hii katika mavazi, usemi, matendo n.k. ( WAEBRANIA 12:14; WARUMI 12:2; YAKOBO 4:4; 1YOHANA 2:15-17 )

JE! WEWE NAWE UMEKUWA DHAIFU KAMA SISI!

ISAYA 14:9-10


Mpendwa msomaji, baada ya kusikia yote haya , usifanye moyo wako kuwa mgumu. Hii ni nafasi ya kipekee ya juisalimisha na hatari ya kutupwa katika jehanam ya moto . Je, unajuaje kama utaamka kitandani baada ya kulala usiku wa leo? Wakati uliokubalika wa wokovu ni sasa (2 WAKORINTHO 6:2). Labda utaniuliza, ili uokoke, ufanyeje? Jibu ni rahisi, kwa imani ukitubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, na kumwambia Yesu Kristo akusamehe, utasamehewa sasa hivi, na msamaha wa dhambi, huambatana na wokovu (LUKA 1:77). Je, uko tayari kuokoka sasa hivi? Najua uko tayari. Basi fuatisha sala hii kwa dhati toka moyoni, “Mungu baba asante kwa kuniletea ujumbe huu.Natubu dhambi zangu zote, kwa kumaanisha kuziacha. Yesu Kristo nakuomba unisamehe dhambi zangu na kunipa uwezo wa kushinda dhambi na kuniokoa kutoka katika mateso ya moto wa milele. Asante, kwa kuniokoa katika Jina la Yesu. Amen”. Tayari sasa umeokoka, na kwa hakika unakwenda mbinguni sasa, hata ukifa leo. Ili uzidi kuukulia wokovu, hakikisha unahudhuria mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!

Masomo ya matukio ya mwisho wa Dunia. Unaweza kuingia kwenye link ya kila somo.
1. KUNYAKULIWA KWA KANISA
KUNYAKULIWA KWA KANISA
2. DHIKI KUBWA
DHIKI KUBWA
3. TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO
TAJI KWA WATAKATIFU NA HARUSI YA MWANAKONDOO– ya-mwanakondoo/
4. KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA VYA HAR-MAGEDONI
KUJA KWA YESU KRISTO MARA YA PILI DUNIANI NA VITA YA HAR-MAGEDONI
5. MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
MIAKA 1,000 YA UTAWALA WA YESU KRISTO DUNIANI NA VITA VYA GOGU NA MAGOGU
6. UFUFUO WA WAFU
UFUFUO WA WAFU
7. JEHANUM YA MOTO
JEHANUM YA MOTO
8. KITI CHA ENZI KIKUBWA CHEUPE CHA HUKUMU
https://davidcarol719.wordpress.com/229-2/
9. MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA
 
Asante kwa kumshauri. Hata mimi nimempa ushauri huo huo. Ila gharama ulizomtajia ni kubwa sana. Sidhani kama zimefika huko. Mara ya mwisho mwaka jana (July 2017) nilikwenda mwenyewe kuulizia kwa wakala pale opposite na Mbezi Beach secondary niliambiwa shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki sita (2,600,000/=). Sasa hiyo rate uliyompa wewe ukibadilisha kwa shilingi ya Tanzania inakaribia shs 6,500,000/=. Namshauri aende pale Mbezi Beach Secondary, aonane na yule mama kiongozi wa kituo. Ni mama mwaminifu sana na hata TB Joshua anamkubali na kumtumia pia kusambaza annointing water, vitabu n.k. Pale atapata na maombi na gharama zote ikiwa atahitaji kwenda kwa TB Joshua.

Acheni kumdanganya!!! Pancreatic cancer stage 4 has no treatment. Only he supposed to palliative care including psychosocial support.
Duniani wote tunapita!!! Tangulia kamanda na sisi tutakufuata, tuandalie makazi yetu huko.
Inauma sana hii!!! Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu.
Wakati mwingine huwa nawaza ni nani alianzisha maradhi yote haya makali.
 
Acheni kumdanganya!!! Pancreatic cancer stage 4 has no treatment. Only he supposed to palliative care including psychosocial support.
Duniani wote tunapita!!! Tangulia kamanda na sisi tutakufuata, tuandalie makazi yetu huko.
Inauma sana hii!!! Mungu akupe nguvu katika wakati huu mgumu.
Wakati mwingine huwa nawaza ni nani alianzisha maradhi yote haya makali.

Kwako wewe usiyemwamini Mungu hakuna treatment. Kumbuka kuwa Daktari Mkuu kabisa ni Mungu. Yeye ndiye aliyemuumba na yeye ana uwezo na afya yake. Tumeshuhudia waliokuwa na hali mbaya kuliko Folk, lakini kwa uwezo wa Mungu wamepona na wako hai. Acha kumfanya mwenzio akate tamaa. Mwache apambane na Mungu wake.
 
Siamini kama kuna mtu mwenye uwezo wa kutabiri muda wa kifo cha mtu. Hilo sitoliamini kamwe. Kama Allah amekupa mtihani wa maradhi rudi kwake yeye ndie anaeweza kukuponesha ukaona maajabu.wala usikate tamaa ni dhambi kufanya ivo

Unaweza kuishi hadi ahadi yako itakapofika hayo ni majaribu tu.
 
Nimedhoofika sana. Nitakufa punde.
usijitabirie kufa kama Mungu ahajakupangia kufa hutakufa, usiwe mwenye kukata tamaa best
liko tumaini cha kufanya kaa katika imani, mwombe Mungu sana anaye atakuponya huo ugonjwa unakumbuka kwa biblia jinsi nabii ezekiel aliyeugua karibu ya kufa unajua nini kilimtokea, Mungu alimponya ugonjwa wake na akakoma hivyo kaaa katika imani yakuwa UMEPONA KWA JINA LA YESU usiwe na dhana ya kutaka kufa wakati Mungu ajakupangia kufa, wewe kaa ktika imani toba ya kweli tu
 
Nikufafanulie vizuri hapo kwenye kuchemsha mihogo. Hakikisha mihogo inayonunuliwa ni fresh kabisa na isiwe imeshaanza kuwa bluu. Wakati wa kuchemsha hakikisha maji yanafunika mihogo na tafadhali sana usifunike sufuria na mfuniko iache wazi ili mvuke uondoe kisichohitajika ndani ya mihogo. Ikiishaiva toa mihogo kwenye maji haraka sana uiweke kwenye chombo safi. Wakati wa kuchemsha usichanganye na chochote, hata chumvi usiweke.
Kwa kipindi chote utakachokuwa unakula mihogo kama tiba tafadhali usitumie tangawizi (ginger) wala chochote chenye tangawizi i.e. soda, biscuits etc. Kama unataka kujua kwa nini imekatazwa kufunika wakati wa kuchemsha au kutumia tangawizi, tafadhali nenda Google andika "Cassava for Cancer" utapata majibu mazuri kabisa ya kisayansi.
Nafikiri hii itakuwa imesaidia wengi pia wenye tatizo kama la Folk. Mungu awafanyie wepesi.
 
kwanza kabisa nikupe pole kwa magumu uliyoyapitia na unayoendelea kupitia, binafsi imenipa simanzi sana moyoni na nimejifunza kitu kikubwa ndugu folk, POLE SANA.

yote kwa yote inaonesha umepitia kipindi kirefu cha maumivu mpaka nafsi yako imekata tamaa ya kuishi, siwezi kukulaumu kwa kukata tamaa lakini nakusii endelea kupambana japo kwa imani, usiruhusu nafsi yako ikiri umauti at least sio kinyonge namna hiyo. tafadhali kumbuka kuna ndugu na jamaa zako wa karibu akiwemo Mama yako mzazi ambao naamini wanatamani kuendelea kuuona uwepo wako at least pambana uwatie moyo, mrudie muumba wako na utafute amani na watu wote.

kamakuna habari ningependa kuisikia miezi 6 au mwaka baadae, ni kupata ushuuda wako popote natakapo kuwepo kwamba u mzima na waafya na ni Mungu alikupigania kwa mapenzi yake (nakuombea mapenzi ya Mungu yatimwizwe juu ya maisha yako mkuu trust me.)

sijui imaniyako, lakini bible inasema...... Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo;. mimi naamini hilo unaliweza.
 
Siamini kama kuna mtu mwenye uwezo wa kutabiri muda wa kifo cha mtu. Hilo sitoliamini kamwe. Kama Allah amekupa mtihani wa maradhi rudi kwake yeye ndie anaeweza kukuponesha ukaona maajabu.wala usikate tamaa ni dhambi kufanya ivo

Unaweza kuishi hadi ahadi yako itakapofika hayo ni majaribu tu.
kabisa hicho kitu hakipo Mungu ndiye anayepanga siku gani mtu anaondoka duniani sio sisi wanadamu wanamtisha tu huyo ndugu yetu
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it was..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk

ukweli kdg + uongo kdg = [ ? ]
 
Death is painless ndugu.

Kisayansi au ni fikra zako tu tunaruhusiwa kuchangia?

Tuachane na hayo!

Mkuu Marehemu mtarajiwa

Kumbuka kwamba pamoja na kwamba daktari kakuambia baada ya miezi minne, unaweza ukafa hata sasa usingizini au kwa sababu yeyote nyingine.

Aidha, jambo pekeee ambalo litakusaidia katika kuyaendea mauti ambayo sote tupo kwenye foleni, ni kuikubali hali yako na kuhakikisha umetubu kama imani unayo na kama sivyo katika kipindi hiki, fanya yote yale yaliyo kwenye uwezo wako na kwa muda uliobaki, mfano tembelea ndugu, gawa mali zako, tumia muda mwingi kukaa na watu unaowapenda.

Kila la kheri katika ulimwengu wa roho.

Amin
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom