Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Binadamu wameshindwa kwann usimgeukie Mungu??
 
Dunia ina tiba nyingi sana... Na moja ya tiba nzuri na yenye nguvu ni wewe!! Yes wewe na nafsi yako Imani yako iliyotukuka.... Ukiamini utaishi hata kwa imani ndogo mithili ya punje ya haradali basi hakika utaishi na kupona....
 
Tatizo la huyu ndugu ashauliki.
Kaka usimuhukumu yawezekana ukufuata ushauri wako kutokana nahali yauchumi uwezi jua ila kiukwel inasikitisha sana japo kuwa hatujui miongoni mwetu kama tutakufa kabla hata yahiyo miezi 4
 
Si malaika,si binadamu na wala si shetani,bali ni Mwenyezi Mungu mwenye ajuaye muda na saa na dakika.Na ndiye mwenye mamlaka ya kifo.
Kuwa chanya(positive)katika kufikiri.
Huyo ni shetani anakujaribu kwa roho ya mauti.
AMINI HUWEZI KUFA KWA AJILI YA HUO UGONJWA WA SARATANI.
Maradhi hayasababishi kifo,bali kifo kipo tu na sote kwake tutarejea.
Kuanzia sasa ondoa hiyo hofu.Tumia muda wako kukamilisha mipango yako ya maisha uliyojiwekea ya muda mrefu.
Usisahau kumrudia Allah kwa maombi.
 
Niliambiwa nikipatiwa good medication naweza kuishi hadi miezi nane. Lakini matibabu ni gharama kubwa na sihitaji msaada niko Kwenye critical stage na napata maumivu makali sana. Nahisi ni vema nife nipumzike.
Pole sana sana....pamoja na maisha yangu kuwa mabaya na yanayonichosha kupindukia...maumivu na fadhaa ..kukata tamaa na upweke usiomithilika...lakini bado nakuhurumia vile najua unateseka kiasi gani.....
Ni kweli hali si nzuri lakini nakuomba kwanza usilipe uzito hilo la mda wa kufa...na yakubali matokeo yoyote hii itakutoa hofu na kuona kama umeonewa..
Sali na fanya ukaribu zaidi na Mungu...huwezi jua..Mungu ana miujiza unaweza usipone ila ukafa bila maumivu..
Endelea na tiba...lakini pigania roho yako isiwe na mawaa!
Na kumbuka huko peke yako...tuko wengi safarini na tunakuombea dua..
Wengine humu tunafika kuomba kifo...maana kujiua nako ni tatizo jengine.
Kila kitu huja kwa sababu...labda pia Mungu kakuwekea mazuri huko baada ya tabu nyingi ulizopitia!
Hutalia na kuumia wala kusikitika tena!
Usione tuna kuja humu jf ukadhani tuna furaha na amani ya nafsi! Ni kujipumbaza na kutafuta faraja!
Sali na umtubie Muumba...usikubali familia yenu iwe na maumivu pia mda wote!
 
Thread Inaumiza sana hii....pole mkuu, Mungu ndie muweza wa yote, mtumainie yeye usikate tamaa
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Pia soma > Atakayenisaidia hili nitampa Tsh milioni moja taslimu

Bye bye Mother earth.
Pole mkuu. Bado lipo tumaini.
Jaribu kutumia vidonge vya Vitamin C.
Watalaam wanasema kuwa kiwango cha juu cha dozi ya vitamini C kina uwezo wa kuponya magonjwa kama kansa na HIV.
Hakikisha kila siku una meza millgram 2000 za vidonge vya vitamin C.
Vinaweza kukusaidia kupata nafuu au hata kupona kabisa. Ya Mungu mengi...
 
Nmeumia sana mchana wa leo. Pole saana mkuu na najua moyo wako maumivu unayoyapitia. Jitakase na andaa makazi mapya kwa ajili ya roho yako. You are still too young to die
 
Pole sana sana....pamoja na maisha yangu kuwa mabaya na yanayonichosha kupindukia...maumivu na fadhaa ..kukata tamaa na upweke usiomithilika...lakini bado nakuhurumia vile najua unateseka kiasi gani.....
Ni kweli hali si nzuri lakini nakuomba kwanza usilipe uzito hilo la mda wa kufa...na yakubali matokeo yoyote hii itakutoa hofu na kuona kama umeonewa..
Sali na fanya ukaribu zaidi na Mungu...huwezi jua..Mungu ana miujiza unaweza usipone ila ukafa bila maumivu..
Endelea na tiba...lakini pigania roho yako isiwe na mawaa!
Na kumbuka huko peke yako...tuko wengi safarini na tunakuombea dua..
Wengine humu tunafika kuomba kifo...maana kujiua nako ni tatizo jengine.
Kila kitu huja kwa sababu...labda pia Mungu kakuwekea mazuri huko baada ya tabu nyingi ulizopitia!
Hutalia na kuumia wala kusikitika tena!
Usione tuna kuja humu jf ukadhani tuna furaha na amani ya nafsi! Ni kujipumbaza na kutafuta faraja!
Sali na umtubie Muumba...usikubali familia yenu iwe na maumivu pia mda wote!
Pole Sana aisee, ni kweli, tumebeba mizigo mizito Sana, wakati mwingine tunalemewaaaa. Kila mmoja ana jambo ndani ya moyo wake kama alivyowahi kusema R. Kelly "Within all of us there is a storm but he who has faith in heaven will weather any storm"
 
Ripoti ya daktari inasema baada ya miezi 4 nitakufa kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4.)

Kwa hiyo miezi minne ijayo nitaweza kuona kile marehemu wanachoona sijui kufa kunaumaje?

Juzi nimepita kando ya makaburi nikaishia kutabasamu tu nilipogundua next 4 month nitafukiwa chini alafu watu watawanyike waniache pale nikiwa shimoni mwenyewe, upweke utakuwa mkubwa mno.

Nikiwa kijana kindakindaki wa miaka 28 tu nafukiwa ardhini. Masikitiko.

Pia soma > Atakayenisaidia hili nitampa Tsh milioni moja taslimu

Bye bye Mother earth.

Hutakufa bali utaishi.. Kwakuwa ufao ni mwili huu wa nyama uharibikao.
 
Ndugu yangu Maombi ni silaha ya mwisho ikishikikizwa na imani basi hakuna kilichokikubwa
 
Mkuu kwani upo wp ww kuna mafaili tunataka kupeleka kwa Mwl Nyerere.
muombe Mungu fanya toba pia
 
Daktari sitegemei kama anaweza kutoa majibu ya aina hiyo kwa mgonjwa! Kuna lugha fulani ya jinsi ya kuhudumia na kutoa majibu kwa mgonjwa si rahisi rahisi namna hiyo. Watu wa kuhudumia wagonjwa wa ishi kwa matumaini wanalijua hili iweje daktari aliyesomea miaka mitano?
Unazungumzia theory

Kama una Ndugu yako wa Cancer iliyo final stage mwambie akuhadhithie
 
Duh! Pole sana mkuu! Nimesikitika ila ngoja nikwambie hivi;

Kwamba unapaswa kujua we are divine energy..sisi sio huu mwili sisi ni roho hivyo iandae roho yako kupata pumziko la milele na watu wengi walio experience near death situation wanaelezea how wonderful it was..maana kifo sio process bali its the state of changing from physical state kwenda spiritual blissful state yenye raha isiyomithilika we unadhani kwanini Mungu haishi mwilini na anaishi rohoni? Huku mwilini kuna uchafu na maumivu nenda tu into the real immortal part...the truest of all.

Kufa sio adhabu its the must process kwa kila kiumbe na hakuna maumivu kwani maumivu yako mwilini pekee sababu ya nerve, brain, neurons e.t.c but unaumiaje rohoni? Unaumiaje ubongo ukicease kufanya kazi? Haumii kabisa,Trust me!

Death is painless ndugu.

Tangulia mkuu, tunakuja!

Candle in the wind.

Love you folk
Umenipeleeeka mbali saaana mkuu, its a Great think! Over
 
MFALME DAUDI alipatwa na maumivu makali ya kihisia na ‘fikira nyingi zinazofadhaisha.’ Hata hivyo, hakuwahi kutilia shaka kwamba Muumba anatuelewa sana. Aliandika hivi: “Ee Yehova, umenichunguza kabisa, nawe unanijua. Wewe mwenyewe umepata kujua kuketi kwangu na kusimama kwangu. Umeichunguza fikira yangu tokea mbali. Kwa maana hamna neno hata moja katika ulimi wangu, lakini, tazama! Ee Yehova, tayari unajua yote.”—Zaburi 139:1, 2, 4, 23.

Sisi pia tunaweza kuwa na hakika kwamba Muumba wetu anatuelewa na anaelewa jinsi kushuka moyo kunavyoathiri akili na mioyo yetu isiyo mikamilifu. Anajua kinachofanya tushuke moyo na jinsi tunavyoweza kukabiliana na hali za sasa. Isitoshe, ametuonyesha jinsi atakavyoondoa kushuka moyo kabisa. Hakuna mtu mwingine yeyote anayeweza kutusaidia hivyo isipokuwa Mungu wetu aliye na huruma “mwenye kufariji wenye huzuni.”—2 Wakorintho 7:6,
Amen!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom