Nimeambiwa nitafariki baada ya miezi 4 kutokana na kansa ya kongosho (pancreatic cancer stage 4)

Status
Not open for further replies.
Blv in doctor but take god with you kwa kuwa doctor is just a normal human being alichokifanya ni probability huwezi jua inaeza pona au la just have faith :
Ila ugua pole mkuuu
 
Pole sana ndugu yetu hii ni njia yetu sote tutapita hapa
 
hakika sote tutarejea KWAKE YEYE PEKEE, usihuzunike ndugu yangu matatizo ni yetu sote.
 
Kwa muafrika ndio huambiwa kwa style hiyo unayotaka.
Ila mzungu huelezwa kwa style ya mleta mada.
Style zote ni sahihi kwa mazingira yake
 
Mshukuru Mungu sana kakupa nafasi ya kujua siku yako ya kuondoka.

Pata muda wa kutengeneza roho yako ili ukapumzike huko maana pia umeteseka hapa duniani.

Pata nafasi ya kutubu dhambi zako, kusamehe majirani na ndugu ambao uliona wamekuroga kumbe ni kansa ilikuwa ikikukula, pata muda pia wa kujisamehe na kuomba msamaha wengine wote wa karibu yako.

Wote tutakufa tu ila hatuijui siku....huenda mie nikakutangulia ingawa hapa nakuonea huruma. Natamani sana nami niijue siku ya kufa kwangu.

Mtume Paulo alisema " kuishi kwetu ni Kristo na kufa ni faida"

Mungu akuwezeshe ufe kifo chema
 
Follk usiache kwenda kwenye makanisa ya kiroho hata kama imani yako haikuruhusu bali mwamini Mungu tu yote yanawezekana kwake aminiye
 
Braza hivi akili yako iko sawa kweli wewe? Wewe si unasema ni engineer wa UDSM first class? Hebu uwe na staha na ubinadamu basi mkuu hapa kuna mtu ana magumu kabisa anahitaji faraja na msaada wa kiroho wewe unaleta masuala ya utapeli Forex hapa.

Kwani huuoni Uzi wa Forex kule? Si ukayasemee haya kule?

Kuna vitu mtu anafanya hadi unahoji juu ya uzima wa akili yake!? Asee?
 
Pole sana kaka Mungu mwingi wa huruma na rehema akutie nguvu......na zaidi damu ya yesu kristo inaenayo mema ikanene mema juu ya afya yako.....waebr 12:24. Maana kwa kupigwa kwake yesu sisi tumepona......cha muhimu ni kumlilia Mungu maana anasema njooni kwangu ninyi wote mlemewao na mizigo nami nitawapumzisha
 
Kwakuwa hakuna kitu chenye nguvu kubwa kuzidi imani basi naweza kukubaliana nawe utakufa kweli baada ya miezi minne( 4)
Inawezekana kweli unaumwa na umeambiwa hivyo lakini imani yako kwenye kufa baada ya miezi minne ndio itakupeleka kaburini zaidi....
Imani ina nguvu sana pengine Mungu angeweza kukubakisha hata zaidi ya miaka 20 lakini kwa imani uliyo onesha juu ya kifo ni ngumu kuruhusu Mungu kukunusuru maana umeani sana kwenye kifo baada ya miezi minne na nina hakika daktari hakukutajia ni tarehe ngapi kwa sababu hata yeye hana uhakika...
Nina hakika kama leo hiyo imani yako juu ya kifo after four months ukiihamishia kwenye uhai zaidi bila shaka utakaa zaidi ya miaka 10...
Mimi naamini hutokufa baada ya muda huo unachotakiwa kufanya ni kuamini wewe utaishi na uendelee kuswali/kusali ukimtumaini Allah/Mungu....
Hakika amini kwenye kuishi kwanza...futa mawazo ya kufa ili mwezi wa 9 uje uandike thread nyingine hapa...

Naamini hutokufa kwani ajue muda wako ni Allah pekee...
Kama Mungu kakuweka tangu 2013 ulipoleta hapa habari yako na sasa ni zaidi ya miaka saba ..kwanini ashindwe kukupa tena miaka hata 30?
Tatizo lako pengine una hangaika kila sehemu pengine una kwenda kwa waganga huku unachanganya na kwa Mungu.....
Chagua moja kuanzia leo tegemea Mungu tuu na ushauri wa madaktari....
 
Daah,pole sana mdau mwenzetu wa jf
Sipingani na wataalamu hatakidogo ila Mungu mwenyeenzi yote anaweza kuzidisha miezi minne hata mara ishirini.

Nakuombea uugue pole na usitawaliwe na hofukuu(phobia) kwani hofu pia itauchochea ugonjwa upatenguvu zaidi ya kukushambulia

Nami ninasematu ugua pole na usijawe na hofu sana WAPO WANAOKUPA POLE LEO NAO WANAWEZA WAKATANGULIA KABLA YAKO
 
uko sahihi mkuu. Hata sasa hivi akitaka kubadili imani yake kwa dhati atapata muujiza. Binadamu tuna nguvu Kubwa ila wengi hatujui Tu.
 
Amekata tamaa,amechoka na maumivu ya mfululizo.Binadamu tunapitia magumu mengi,magumu mengine ni magumu sana kiasi kwamba unafikia hatua ya kukufuru.

Ndugu yetu anahitajika kumshukuru Mungu kwa kila jambo, ajikabidhi mikononi mwake na ajiweke tayari kwa lolote. Maombi ya shukurani ni muhimu sana kwake maana yatampunguzia mzigo wa mawazo ya hofu.
Kwa imani tu,Mungu anaweza kutenda ambayo hayakutarajiwa
"Amuachie Mungu aendelee kumtendea atakavyo ona ina mfaa"

Pole sana ndugu yangu mgonjwa,wewe ni mshindi.Hata ukiondoka leo,tupo tulio jifunza kutoka kwako.Nikiugua siku tatu mfululizo najiongelesha kwa maneno yasiyo faa,lakini mwenzagu ni zaidi ya miaka kumi.
"Mungu akiona inampendeza kukutwaa,basi,ikawe hivyo[emoji120] [emoji120] [emoji120] "

MIMI NI NANI BWANA MUNGU WANGU, HATA NIWE HAPA?...ni kwa neema na rehema.SHUKURANI.
 
Asante ndugu, Jana nimelia sana kwani nimemkosea nini Mungu Mimi.
Usilie bado mtetezi wetu yu hai kila binadamu hupitia mapito sali usikate tamaa hafu nime Ku PM naomba unijibu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…