Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Nimeamini jamani hakuna kitu kigumu kama wajasiriamali

Walioniacha hoi ni watu wa mabank.
Mikopo wamesitisha kutoa kwa wateja wenye biashara zilizoathirika kwa asilimia kubwa na hata wanaobahatika kuendelea kuchukua mkopo kiwango wamepunguza.
Lakini kukaa mezani na wateja wao kufanya rescheduling kuona mkopo utalipwaje kwa kipindi hiki hawataki wanadai kwa karaha sana.
Nabaki natoa macho.
Hata wakipiga mnada ni ujinga tu unapoteza wateja na mnada unaweza usifanikiwe.
Mwenzi wa 11 mwanzoni nilimaliza mkopo wa mil 20 EFC BANK Afisa wngu alikuwa amenipa offer ya mkopo mwingine wa mil 40 au 50 lkn biashara zenyewe niliona zipo slow sna nikakataa nikachukua hati ya kibanda ni kaweka ndani kumbe mbele Kuna balaa nzito sijui ingekuwa je na balaa ili mungu mkubwa sna...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eee Mungu tunaomba toba na rehema, wewe ni Mungu unaerehemu, ni Mungu unaeponya, ni Mungu unaesamehe. Samehe Baba, ponya Baba na uturehemu pale tulipokwenda kinyume na mapenzi yako, Baba tunaomba utuvushe kwenye janga hili, tunajua kuna magonjwa mengi yanayochukua uhai wa binadamu lakini katika hili tumeshindwa Baba, dunia imejaa hofu na woga, dunia inaomboleza, hatujui mwisho wetu utakuwaje, Mungu tunaomba maisha yetu yarudi kama tulivyokuwa tukiishi siku zote, tumekutenda dhambi lakini Baba kumbuka rehema na uondoe ghadhabu juu ya nchi, watu wanaangamia kwa njaa, maisha magumu kwa kuwa hakuna kazi, watoto wanatamani kwenda shule lkn hawewezi tena, kumbuka rehema sawa sawa na neno lako kutoka Habakuki 3:1-2..Amen!
Hata tukiambiwa turudishe watoto shule sijui watu tutaanzia wapi, coz imagine July watoto wanarudi shule na ada ya muhula mpya, hela ndio hiyo hakuna. Mwaka mgumu sana huu.
 
Ndiyo shule zinaendeshwa na ada za wanafunzi kwa asilimia mia.
Japokuwa huwa kuna vimradi vidogo vidogo kama duka navyo havisaidii hata kwa asilimia 1
Hivi shule sizinaendeshwa kwa ADA za wanafunzi.
 
Cha muhimu isitishie uhai. Ikiingia kwa mmoja wa wanafamilia mambo yanazidi kuwa magumu zaidi na zaidi. Baada ya kusalimisha uhai tutatafuta tena tu. Kwa sasa sidhani kama kuna anayewazia mali, uhai kwanza tuvuke wazima.

Lawama nyingi lazima ziende kwa serikali kwa kutuacha wananchi wake tukiwa hatuna baba!
 
Nakataa.
Wale wanaouza chakula uwanja wa ndege? Niambie kama sasa hivi wanauza? Wale waliokuwa wanatender za kuwapikia kampuni za watalii au wafanyakazi utalii? Wale wa macatering na wapishi wa masherehe.
Yaani hii ya msosi ni mule mule tu.
Kama mtu alikuwa anakul akwa mama ntilie asubuhi chai chapati mchana na usiku.
Sasa hivi atakuwa anagusa hapo mara moja au mbili kama akiwa hajajiongeza kuchemsha mwenye msosi kupunguza gharama.
ya misosi tu...
 
yaani hapa ndipo unapojua kuwa mabenki ni wezi tuu.....kwa sababu katika hali kama hii ya sasa wanatakiwa kuwa na ufikirio maana kushindwa kurudisha mkopo kwa muda huu sio kutokana na uzembe wa mkopaji bali kutokana na uncorseen circumstances ambazo zipo nje ya uwezo wa mwadamu yoyote yule.
Na ndio maana kihistoria Banks zilizianzishwa na vikundi vya Mafiazi kabla kua banks hizi tunazoziona sasa hivi,so bank by nature sio marafiki.
 
Kwenye magazeti vipi mkuu haijaathirika?
Corona mtu mbaya sana yaani angekuwa mcheza mpira tungemwita Ronaldinho yaani anapiga miguu yote..

Poke sana aisee madhara bado yanaweza vuka hadi mipaka na kuingia kwenye mishahara ya watumishi wa umma kwa jinsi navyoona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii thread imenigusa sana. Wajasiriamali ni watu yatima hasa hawa wanaochipukia . Kwa TZ hatuna Serikali. Rais naye yuko pale kama mwajiriwa tu.. anamtegemea Mungu ..yani he cant think, he cant take advice, he cant impliment any precautions, na alipuuzia hadi tumefika huku.
Shit!
 
Hapa ni kuomba serikali itoe tamko aise.
Hivi BOT na CRB wana kazi gani? Ujue nimeshangaa sana nilitegemea uchumi kusimama walau banks na hizi financial institutions zitakaa chini na wateja wao kujua wanafanyaje.
Cha ajabu wanadai Chao tena full na ukimaliza hukopeshwi tena.

yaani hapa kweli changamoto jamaa hawana huruma kabisa.
 
Na ndio maana kihistoria Banks zilizianzishwa na vikundi vya Mafiazi kabla kua banks hizi tunazoziona sasa hivi,so bank by nature sio marafiki.

kabisa yaani. sasa unajua sometimes haya mambo tunajitakia wenyewe. yaani kukosa uaminifu ndio unatuponza wengi lah sivyo tungekuwa twakopeshana wenyewe kwa wenyewe tuu.
 
Hakika ni kumuomba Mwenyezi Mungu hili balaa lisiendelee kuiathiri Nchi yetu. Maana hapa biashara zangu fulani zilizokua zinanipa pesa ya kula nje ya mshahara wangu muelekeo wake sio mzuri kama hapo mwanzo.

Ni kuendelea kupambana na kumuomba Mwenyezi Mungu,kwa upande wangu sitegemei kuifunga itaendelea hivyohivyo mpaka pale hali itakapotengemaa tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
yaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walioniacha hoi ni watu wa mabank.
Mikopo wamesitisha kutoa kwa wateja wenye biashara zilizoathirika kwa asilimia kubwa na hata wanaobahatika kuendelea kuchukua mkopo kiwango wamepunguza.
Lakini kukaa mezani na wateja wao kufanya rescheduling kuona mkopo utalipwaje kwa kipindi hiki hawataki wanadai kwa karaha sana.
Nabaki natoa macho.
Hata wakipiga mnada ni ujinga tu unapoteza wateja na mnada unaweza usifanikiwe.
Tupambane tu amu, kilio ni cha wengi lakini kila mtu anakufa kwa timing yake hivyo tupambane coz we're fit to do so.
 
kabisa yaani. sasa unajua sometimes haya mambo tunajitakia wenyewe. yaani kukosa uaminifu ndio unatuponza wengi lah sivyo tungekuwa twakopeshana wenyewe kwa wenyewe tuu.
Na ukiwa mwaminifu hata benki huendi. Suppliers wanakupa mzigo hadi unakataa. Hapa inabidi niwalipe suppliers, nafikiria na hali hii niwalipe what if tuki-lockdown kesho itakuwaje. Nisipowalipa naharibu credit score soon nitapoteza credit facility. Nina siku mbili za kuamua.
 
Kufa kufaana Mimi nakusanya saa hizi raw material naweka store after Corona kama nitavuka salama tatengeneza margin profit.Japo project zingine zimesimama sababu ya corona
Ukifa na hiyo Corona hiyo raw materials itakua haina maana tena.bado ni mapema mno kutabiri kuwa hali itarudi Kama zamani.na hata baada ya kurudi haitakua Kama zamani so don't predict bright future atleast for Now.
 
kabisa yaani. sasa unajua sometimes haya mambo tunajitakia wenyewe. yaani kukosa uaminifu ndio unatuponza wengi lah sivyo tungekuwa twakopeshana wenyewe kwa wenyewe tuu.
Kwa bongo hii kukopeshana ni kujivuka kitanzi, mda wowote unaweza kufa. Hata vicoba ambavyo wengine tuliwatumia wake zetu kuwekeza na kukopa nadhani sio sehemu salama kwa sasa.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Na ukiwa mwaminifu hata benki huendi. Suppliers wanakupa mzigo hadi unakataa. Hapa inabidi niwalipe suppliers, nafikiria na hali hii niwalipe what if tuki-lockdown kesho itakuwaje. Nisipowalipa naharibu credit score soon nitapoteza credit facility. Nina siku mbili za kuamua.
Walipe tu mkuu, unajiwekea hazina kubwa sana, credibility yako itaongezeka 100x, Corona sio mwisho wa maisha, tutaishi tu japo tutaumia.
 
Back
Top Bottom