Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

Nimeamini masharti ya marehemu wakiyasema kabla ya kukata roho

Hakuna, dawa ni kuwa Zombi tu, umuoe mke wangu halafu watoto mnawapeleka kwa bibi, acha zenu ninyi
Hapana watoto tunawalea Tena wanakuwa wangu kabisaaaa ili kuwa sahaulisha Kama hata baba yao hayupo tena.wahisi upo
 
Hamnaga hayo mambo
Watoto wa enzi za Mkapa mmejikuta google ndiye mwalimu wenu basi mnajifanya kujua kila kitu shecsnmzi. Ulizeni bibi na Babu zenu mjifunze Mambo yaliyopo kwenye jamii zenu.
Kaulize kitu kinaitwa "nchweke" kwa wahaya, maiti inaongea!
 
Majuzi Tumeenda kuzika sehemu fulani, Kukawa na mjadala kwamba Marehemu alitoa maagizo akifa watu wasile chochote msibani.

Wanakamati ya mazishi wakalazimisha watu kushinda njaa kisa marehemu.

Nikawauliza hivi marehemu angesema akifa asizikwe mwili wake ubaki chumbani tu mngezika komalia kauli ya marehemu kama mnavyokomalia watu wasipewe chakula?
Hii ya kulazimisha kula msibani ndio mwishowe baada ya msiba familiia ya marehemu inakuwa na madeni kibao ya kupikaa msosi.. Maana msibba sio harusi kusema watu wanajipanga, msiba ni ghafla hujui familia imefikwa na msiba ikiwa katika hali gani ya kiuchumi, daftari ya mchango ikipita watu wanaikodolea macho tu.
 
Kuna kisa kilitokea katika msiba wa mfanyakazi mwenzetu Tabora. Maeneo ya mirambo barracks kulikua na mochwari, tulipeleka nguo za marehemu kutoka kwake kwa ajili ya kumsitiri ili asafirishwe kwenda kuzikwa kwao kijijini, tulienda na timu ya staff hakuwepo ndugu yoyote

Tukaingiza jeneza ndani ya chumba cha mochwari, sasa ikafika wakati wa kumvalisha nguo marehemu, yule jamaa wa mochwari akaita staff wawili wanawake waingie na nguo kusaidiana kumvalisha marehemu, sisi tulibaki nje basi baada ya muda wale wenzetu wawili waliambiwa watoke nje sababu marehemu alikataa kuvaa nguo ikabidi sisi tuliokua nje kuingia na kusaidia kumvalisha marehemu na kumuandaa, yule jamaa wa mochwari akatuambia kuwa marehemu aligoma kabisa kuvaa walipoingia wale wadada.

Tulipoingia sisi tukamvalisha na akaandaliwa fasta ila tulikumbuka kuwa kati ya wale wafanyakazi wenzetu kuna mmoja alikuwa haelewani kabisa na marehemu ila ilibidi aingie sababu alikuwa ni kiongozi wetu.

Wakati tupo ndani tulikuwa tuna mdadisi mambo mengi yule jamaa anayefanya kazi mochwari akatuambia maiti zinakuaga na vituko vingi sana na pia kuna watu wanawapokea kama maiti mochwari na wanakuwa hawajafa ila jamaa alisema huwa anawamalizia au anawaacha wafe kiukweli kuepuka taharuki.

Alitupa stori ya bibi mmoja wa miaka zaidi ya themanini ambaye aliletwa mochwari kuhifadhiwa ila hakupoa na kuwa wabaridi na alikuwa akipumua kwa mbali na kila ndugu wakija kuchukua mwili kwa ajili ya kwenda kuzikwa ilibidi wawaambie ndugu wasubiri hadi waliposhirikisha wazee wa Mila ikagundulika kuwa kuna kipenzi cha huyo bibi alihitajika kumvalisha na kumsafisha bibi yake ndio mambo yawe sawa.
Niliishi miaka ya nyuma huko milambo tulikuwa jirani na huyo jamaa aliyekuwa anafanya hizi kazi za kuandaa mwili wa marehem.yani msiba ukitokea alafu akakusimilia yaliyotokea pale eneo la kazi unaweza usiamini tena hata wanajeshi wanaolinda palepamoja na smg zao walikuwa wakati mwingine wanakimbia kwenda kumuita jamaa aje azitulize maiti
 
Asikudanganye Mtu popote pale ulipo kuwa kauli za Watu waliokufa namaanisha Marehemu wakizisema huwa hazitimii. Ni kwamba huwa hawatanii kabisa na wayasemayo hutokea na hutimia.

Mwaka jana nilihudhuria Msiba Mmoja ambapo kumbe Marehemu wakati anakata Roho alisema akifa azikwe Dar es Salaam na Ndugu wakampuuza wakamsafirisha wanafika tu Segera wakapata Ajali na wale wale waliolazimisha asafirishwe Wakafa na Msafara ukageuka na kuja Kuzikwa Dar kama ambavyo Marehemu aliagiza.

Mwaka huu Mwezi February kuna Marehemu alisema akifa tu asizikwe Dar es Salaam na akazikwe Kijiini Kwao na Ndugu walipolazimisha Kumzikia Dar es Salaam kwa Kigezo cha Kuokoa Gharama Jeneza lake liligoma Kubebeka ila baada ya muda tu Ndugu walipokubaliana asafirishwe kama alivyoagiza Jeneza lilikuwa jepesi mno Kubebeka na akasafirishwa Kijiini Kwake kwa Maziko.

Leo hii kwa wale Wakazi wa Chang'ombe Temeke nadhani Ajali mbaya iliyotokea Mataa na kusababisha Vifo na Majeruhi mmeisikia.

Ni kwamba Marehemu ambaye ndiyo alikuwa anasafirishwa kwenda Kuzikwa kabla ya kufa kwa Hasira alisema kuna Watu Wawili katika Familia yake akifa hataki waende Kumzika kwani wakati anaumwa na Kalazwa Hospitali walishindwa kwenda Kumuona huku uwezo huo wakiwa nao isipokuwa Dharau na Kupuuza kuliwatawala.

Na katika Ajali hi ya leo ambayo ilikuwa na Msafara wa Gari kadhaa Gari ambayo imegongwa na Kuharibika vibaya ni ya Watu wale wale Walengwa Wawili ambapo wote Wamefariki huku Mmoja Viganja vyake vikikatika.

Hivyo basi baada ya Msiba huu kutokea Msafara wa kumsafirisha Marehemu umeendelea na wale Watu aliowakataa wasimzike nao Wamefariki hivyo Maiti zao zipo Mochwari kwa sasa ukisubiri Msafara ulio Safarini ukirejea ndiyo waanze Kuhangaika nao na Wawazike.

Hata hivyo kuna Mbinu moja nilipewa na Wabobezi wa Kusafirisha Maiti / Marehemu wenye Masharti magumu hasa ya Kusafirishwa kuwa mkianza tu Safari tafuta Jiwe Kubwa / Jiwe Dogo liweke juu ya Jeneza na Marehemu / Mwili hautowasumbueni hadi mnafika. Bado sijaiamini ila kama hapa JamiiForums kuna wenye kuijua zaidi watufafanulie tafadhali.

Jamani tujitahidi mno na sana Kuziheshimu Kauli za mwisho mwisho za Marehemu kwani nimeamini kuwa kwa 85% huwa zinatimia japo kwa 15% zinaweza zisitimie vile vile kama ilivyo kwa Chanjo ya UVIKO-19 ambapo kwa 15% inaweza isikusaidie na ikakuathiri ila kwa 85% huwa inasaidia Kukukinga.
hii ya kuweka jiwe ni kweli nimewai ona wanatafutwa watani wanakuja kuweka basi mnafika salama
 
Ndugu popote pale ulipo pokea Saluti yangu ya Kipekee kabisa Kwako kwa Elimu hii nzuri na Kubwa ambayo nakuhakikishia nimeipokea vyema na naamini Watu wengi pia wamefaidika nayo.

Ubarikiwe mno na Asante sana sasa Marehemu wetu Wabishi na wenye Masharti ya Kukomoana watatukoma kwani tumeshapata sasa Dawa yao ya Kuwatuliza Udongoni bila Kututesa na Kutusumbua pia.
dah....hii yako nimesoma lkn imenifikirisha kidogo kama hauamini nitachokwambia isome tena then utanielewa nini namaanisha....yani umeandika as if umeshaona kwenye watakaokufa karibuni sisi nyote humu kwenye hii thread hatumo maana umekazia kabisa 'WATATUKOMA' wakati sote humu wala hatujui who's next.
 
Kuna kisa kilitokea katika msiba wa mfanyakazi mwenzetu Tabora. Maeneo ya mirambo barracks kulikua na mochwari, tulipeleka nguo za marehemu kutoka kwake kwa ajili ya kumsitiri ili asafirishwe kwenda kuzikwa kwao kijijini, tulienda na timu ya staff hakuwepo ndugu yoyote

Tukaingiza jeneza ndani ya chumba cha mochwari, sasa ikafika wakati wa kumvalisha nguo marehemu, yule jamaa wa mochwari akaita staff wawili wanawake waingie na nguo kusaidiana kumvalisha marehemu, sisi tulibaki nje basi baada ya muda wale wenzetu wawili waliambiwa watoke nje sababu marehemu alikataa kuvaa nguo ikabidi sisi tuliokua nje kuingia na kusaidia kumvalisha marehemu na kumuandaa, yule jamaa wa mochwari akatuambia kuwa marehemu aligoma kabisa kuvaa walipoingia wale wadada.

Tulipoingia sisi tukamvalisha na akaandaliwa fasta ila tulikumbuka kuwa kati ya wale wafanyakazi wenzetu kuna mmoja alikuwa haelewani kabisa na marehemu ila ilibidi aingie sababu alikuwa ni kiongozi wetu.

Wakati tupo ndani tulikuwa tuna mdadisi mambo mengi yule jamaa anayefanya kazi mochwari akatuambia maiti zinakuaga na vituko vingi sana na pia kuna watu wanawapokea kama maiti mochwari na wanakuwa hawajafa ila jamaa alisema huwa anawamalizia au anawaacha wafe kiukweli kuepuka taharuki.

Alitupa stori ya bibi mmoja wa miaka zaidi ya themanini ambaye aliletwa mochwari kuhifadhiwa ila hakupoa na kuwa wabaridi na alikuwa akipumua kwa mbali na kila ndugu wakija kuchukua mwili kwa ajili ya kwenda kuzikwa ilibidi wawaambie ndugu wasubiri hadi waliposhirikisha wazee wa Mila ikagundulika kuwa kuna kipenzi cha huyo bibi alihitajika kumvalisha na kumsafisha bibi yake ndio mambo yawe sawa.
Dunia ina mengi hii duu
 
Watoto wa enzi za Mkapa mmejikuta google ndiye mwalimu wenu basi mnajifanya kujua kila kitu shecsnmzi. Ulizeni bibi na Babu zenu mjifunze Mambo yaliyopo kwenye jamii zenu.
Kaulize kitu kinaitwa "nchweke" kwa wahaya, maiti inaongea!
Hamnaga hizo mambo za laana ya maiti. Mnaoamini hayo ni ujinga unakuwa unawasumbua kwa kichwa. Eti maiti inaongea! Kama siyo ujinga ni nini?
 
dah....hii yako nimesoma lkn imenifikirisha kidogo kama hauamini nitachokwambia isome tena then utanielewa nini namaanisha....yani umeandika as if umeshaona kwenye watakaokufa karibuni sisi nyote humu kwenye hii thread hatumo maana umekazia kabisa 'WATATUKOMA' wakati sote humu wala hatujui who's next.
Next si Wewe Ndugu au umesahau leo?
 
Hamnaga hizo mambo za laana ya maiti. Mnaoamini hayo ni ujinga unakuwa unawasumbua kwa kichwa. Eti maiti inaongea! Kama siyo ujinga ni nini?
Kidonge chako cha Kuutibu huo Ugonjwa wako mkubwa wa Akili ulionao na unaokusumbua muda mrefu umekumbuka Kukimeza leo?
 
Uje tuu ukiuke maagizo yake maneno mengi ya nini? Ila usisahau kuleta mrejesho
Nakwambia hivi tusidanganyane!!

Kama maiti zingekuwa na uwezo wa kupingana na walio hai basi maiti ya Osama Bin Laden ingekataa katu katu kutupwa baharini.

Lakini Wamarekani waliitupa baharini na wakarudi kwao salama salmini.
 
Kwani osama aliacha maagizo? Hapa wanaongelewa watu ambao wanaacha maagizo kabla ya kufa ebooo
 
Back
Top Bottom