Inategemea upo mkoa. Gani hapa Tanzania , kama upo mkoani jaribu biasharavya Nafaka msimu huu Mahindi yameanza na Bei rafiki sana Gunia la KG 110 ni 38000/ Hadi. 40,000/.
Nunua Mahindi Gunia 500 Kwa Thamani ya Tshs 20milioni ,
Then nunua mpunga Gunia 200 za debe kumi kumi Kwa Thamani ya Tshs 10Millioni ,
Alizeti Gunia 300 KG 70 Kwa Thamani ya Tshs 15Milioni.
Hifadhi Kwa muda wa miezi Sita , hapo ni January 2025 Bei zotakuwa. Juu sana Kwani Mazao yanakuwa hamna mashambani.
Mahindi unaweza uza Hadi Tshs 80,000/ mara 500 Gunia = 40milioni.
Mpunga Gunia 200 Mara 140,000/ = 28milioni.
Alizeti Gunia 90000/ mara Gunia 300 = 27milioni
Jumla ya kipato Kwa kuwekeza 45milioni Kwa miezi Sita ni 95milioni.
Option ya pili kama upo Dar es salaam nenda maeneo ya pembeni yanauokuwa Kwa Kasi Nunua ekari tatu za ardhi katika maeneo matatu tofauti then unapima. Viwanja baada ya mwaka Moja Hadi miaka miwili. Ekari Moja inatoa wastani wa Viwanja 10 vya kuanzia 400sq Kila Kiwanja utauza zaidi ya Tshs 4Milioni, hapo mchawi ni kwenye kupoint maeneo Gani yarayokuwa Kwa Kasi.