Nimeamini sasa ikitokea kwenye uchaguzi ikawa SAMIA vs LISSU, Upinzani utachukua nchi

Nimeamini sasa ikitokea kwenye uchaguzi ikawa SAMIA vs LISSU, Upinzani utachukua nchi

Attachments

  • 1754496621496.jpg
    1754496621496.jpg
    64.9 KB · Views: 27
Marehemu Shehe Yahya alishawahi kutabiri kuwa akitoka Rais Kikwete atakuja Rais atakayetwala kwa muda mfupi(Magufuli)na baada ya hapo atatokea Rais mwanamke na baada ya hapo upinzani watachukua nchi!

Imethibitika Rais Samia hana ushawishi wowote kuanzia ndani ya chama chake hadi kwa wananchi wote kwa ujumla. Rais Samia licha ya kuwa makamu wa rais kwa miaka 5 anaonekana hajui matatizo ya Watanzania na wala hajui Watanzania wanataka nini.

Serikali ya Rais Samia kila kukicha inajitenga na wananchi wanyonge kwa kuwapatia huduma mbovu sana kwenye kila nyanja. Rais Samia hajui kukemea rushwa na ufisadi.

Hajui umuhimu wa viwanda kwa watanzania . Kutokana na ulegelege huu ikitokea kwenye uchaguzi mkuu akawekwa Rais Samia na Tundu Lissu basi utabiri wa shehe Yahya unatimia asubuhi na mapema kwa Rais Samia kushindwa vibaya sana kwenye sanduku la kura na Tundu Lisu wa chama cha upinzani kuibuka mshindi na kushika dola.
Tujitokeze kuupigia kura upinzani.
 
Back
Top Bottom