UPDATE KWA WANA JAMII
Msimu wa kilimo 2010
Kwanza kheri za xmas. Niliamua kulima heka 50 za kuanza ambapo nilinunua heka moja kwa Tshs. 50,000 kufanya jumla yote kuwa Tshs. 2.5m. Kilimo kilianza msimu wa kilimo 2010 ambapo heka zote zililimwa kwa Trekta kwa Tshs 30,000/- Kila hekari. Tulipanda mvua za mwanzo kwa mikoa ya morogoro ambapo ni Mid January.
Mahindi hayakuota kwa uhakika hivyo ilibidi turudie tena kupanda wakati wa kupalilia. Baada ya marudio tathmini ilionyesha Mahindi yameota vizuri sana hivyo ikanipa moyo wa kupata mafanikio.
Uangalizi ulikuwa mzuri kwani tuliweka kambi kule kule shambani, mimi pamoja na majukumu mengine ya kiofisi (muajiriwa) nilipata nafasi mara moja kwa mwezi atleast kutembelea na kuona jinsi kazi inavyokwenda.
Wakati wa mahindi kubeba watoto Mvua huko Tuliani ilipotea kwa muda, hapo tukawa na wasiwasi sana, ilivyorudi mahindi yakawa yamedhoofu, hata hivyo jambo hili halikunifanya niwe na mawazo mengi kwani bado wakulima wenyeji walinipatia moyo kwamba mavuno yatakuwa mazuri.
Kipindi cha mavuno nilikuwa shambani, kazi ilianza vizuri, tulivuna na kupigapiga mahindi yetu na kupaki kwenye magunia, hapa sasa ndiyo ilikuwa kuona matokeo ya kazi yetu yote tuliyoifanya tangu kununua shamba, kulima, kupalilia, kuvuna na parking.
Ndgu zangu kwa ufupi hali ilikuwa mbaya sana, malengo yangu hayakutimia hata nusu yake, tulipata magunia 60 tu kwa hekari zote 50. niliishiwa nguvu na niliamua mahindi hayo yabakie huko huko shambani kwa muda wakati natafakari wapi tumekwama na je option B ni ipi.
Labda niwape tu gharama kwa ufupi:
Ununuzi wa shamba 2.5m; Kulima kwa heka ni Tsh. 30,000; kupalilia kwa heka 15;000 hii ni pamoja na kurudia kurudia kupanda sehemu ambazo hazikuota; kuvuna tuliingiza nguvu kazi wenyewe plus additional ya Tshs. 50,000.
Jumla ya gharama zote bila Man Power yangu ya ndugu yangu ambaye ni Project Manager inakuwa Tshs. 4.8m. mapato tukapata gunia 60 @56,000 = 3,360,000/=
Msimu wa kilimo 2011:
Kumbukeni nilianza na magunia yangu 60 niliyopata hasara toka msimu uliopita (sikuyauza); baada ya kufanya tathmini kwa kina nikaona ni vigumu sana kutoka kwa kutumia hiki kilimo cha kizamani hasa ukizingatia sina mtaji wa kutosha, hivyo nikaamua kubadilisha plan nzima. Kwa sasa tukaamua msimu huu hatutafanya kilimo badala yake tutanunua mazao toka kwa wenzetu na kuuza wakati yatakapopanda bei, ingawa bado kwa wakati huo nilifikiria sana kufanya food processing yaani uchumi wa kilimo. (agro -economics)
Mwezi wa tatu mwaka huu, tulianza kuwapa advance wakulima wenzetu - Mahindi na pesa ili mavuno yakifika basi warudishe mkopo kwa mahindi. hapa ni hesabu zilifanyika sababu ukipata gunia moja basi utarudisha mawili na ukipata Tshs mia basi utarudisha mia mbili.
Hatukuwa na wasiwasi sababu hawa tuliowakopesha ni wakulima wenzetu na majirani - wakuu mwezi wa tano tulianza kupokea mafao, tulikusanya mahindi gunia mia 300. Gunia hizi hatukuziweka tu, nilianza muda huo huo mwezi wa tano kusafirisha dar kwa ajiri ya processing.
Animals food processing:
Moja kwa moja nilijiingiza kwenye processing ya vyakula vya mifugo kazi ambayo naifanya mpaka sasa, na bado tunanunua mahindi kwani hayo gunia 300 hayatoshi ya yaliisha mapema tu. Nimeshafungua kampuni ya inafanya kazi mpaka sasa ingawa mwanzo huwa mgumu ila tunafanya vizuri kwani sasa kampuni ina miezi sita na mapato yanaonekana.
Je nitaendelea na Kilimo au nitanunua mazao na kufanya food processing tu?
Wakuu kilimo si lelemama, lazima mtu ujipange kweli kweli, kwa sasa nasitisha kilimo kwa muda lakini nitaendelea na kufanya processing ya vyakula vya mifugo; ila bado nitakuwa vijijini kwani nahitaji haya mazao kwa kazi yangu hii.
Bado nina muda kama nilivyowaahidi kwamba kufikia 2015 basi niwe nimetokana na huu umaskini - kwa sasa mungu akibariki nitakuwa naachana na ajira mwezi tarehe kama ya leo mwakani kwani kazi za kampuni yangu zimeanza kuzidi na zinahitaji uwepo wangu.
Kwa wale mnaotaka kulima siwakatishi tamaa ila muwe waangalifu sana kwani katika kilimo unaweza kuingiza Tshs 10m then ukapata 2m tu, mimi nimebadilisha upepo kwa muda, nikirudi kwenye kilimo basi nitarudi kivingine si hivi.
Mwisho Xmas njema na Kheri ya mwaka mpya.
Elnin0: