Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Nimeanza na biashara ya kununua mazao mwaka huu huko mkoani Njombe yaani maharage ,mahindi na alizeti,mfano kwa sasa mahindi debe ni elfu tano, nimeweza kutumia muda finyu nilionao kufanya organization nzima ya ununuzi, nina mpango wakusafirisha na kufungua store yangu mwenyewe dar na kuuza mwenyewe. Pia nimelima kidogo mwaka huu huko mkoani lkn 2014 nitaingia rasmi kwenye kilimo cha mahindi, alizeti na maharage.Siku hizi wadau unaweza ukapulizia dawa za kuua magugu mara baada ya kupanda ili magugu yasiote hivyo kupunguza tatizo la kusumbuana na vibarua. Pi hapo hapo nitaendelea kununua hayo mazao pia

Kuhusu dawa ya magugu inakuwaje? haina madhara shambani?
 
Yuko mzee mmoja hapo Njombe mjini karibu na kituo cha Polisi Stand, yuko vizuri kwa hii kitu, sasa hivi ndio amefanikiwa kupata nembo ya unga wake na kibali cha TFDA, je uko tayari nikuunganishe naye akupe za uvunguni?
 
Kuhusu dawa ya magugu inakuwaje? haina madhara shambani?

Hizi dawa zina madhara kama zilivyo mbolea za chumvichumvi na madawa mengine ya kilimo lakini zinasaidia sana kwa maeneo ambayo vibarua wanasumbua na pia si ghali sana mkuu!
 
Umepata michango ya kukupa moyo mkuu lakini mi nakukumbusha kuwa l hekta =l00m by l00m na sio 70m by 70m. Pili umelenga umwagiliaji au rehema za Mungu kama ni umwagiliji nakupa hongera na kama ni mvua za Mungu basi usijipe matumaini kupitiliza usijeukasema pekee yako barabarani. Kumbuka nguvu ya soko inategemea mahitaji hilo nalo jiandae nalo. Kuna wadudu wanyama na ndege waharibifu nalo pia jiandae.yapo na mengine wanzangu watanisaidia kujazia vinginevyo nakupa HONGERA SANA wasomi wanatakiwa sasa mashambani kuibadili TIIZEEDII YETU

Umemwambia kweli kabisa. Awe tayari Kwa lolote. Mwisho tunakutia moyo Bwana mkubwa kwa mawazo mazuri.
 
jf

hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Naomba
maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni tshs 60,000. Kwa hiyo nitapata average tshs 90m by july this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by july 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

by next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka sa au zimbabwe. By 2015 wakati dr slaa anakuwa rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you jf - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.

naomba contacts zako.email au simu
 
all tha best kiongozi mungu akusaidie na kumbuka maamuzi ya maisha yako mikononi mwako ni suala tu la kuamua kwamba u can face any challenge all da best kiongozi
 
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.

Mkuu! Hebu tuambie, mradi wako huu umefikia wapi? Ninge au tungependa sana kufanya hivyo. Muda umepita sana sasa na nataraji utakuwa billionaire. Hebu mwagika hapa
 
Hivi hii average ya hekari 1 kwa gunia 30 mmmmh naona mahesabu yako yalikwua too optimistic hapa.

Lakini umesaidia sana kutufumbua macho na sisi wengine ndio tunasubiri kuvuna mahindi sasa kutokana na post yako hii ila sasa hayo makadirio ni tofauti kabisa.
in the beginning lazima kuwe na changamoto, wewe unataka mteremkoooo tuuu, usikate tamaa
 
Nategemea kutumia Atrazine na 2-4-D, kwa majaribio vuli, naomba uzoefu wenu kwenye matumizi ya dawa hizo au jamii yake kudhibiti magugu kwenye mahindi. Salaam
Hizi dawa zina madhara kama zilivyo mbolea za chumvichumvi na madawa mengine ya kilimo lakini zinasaidia sana kwa maeneo ambayo vibarua wanasumbua na pia si ghali sana mkuu!
 
Heshima kwako ELNINO,

Wazo lako zuri sana binafsi nimeshalifanyia kazi tangu mwaka 2008, baada ya kugundua mshahara pekee bila kuwa na kipato kingine cha uhakika ni balaa kadri siku zinavyosonga mbele kwasababu majukumu yanazidi kuongezeka eg:watoto na nk.

Nimenunua shamba eka 250 kwa tsh 3.5 mil maeneo ya Kabuku Tanga na kuanza kulima mwaka huo huo(2008).Project yangu nimeigawanya katika sehemu kuu mbili [1] Mazao ya msimu eg;Mahindi,Dengu,Choroko,Mbahazi,Alizeti na Ufuta

[2] Mazao ya kudumu eg Maembe ya kisasa,Machungwa,Mananasi,korosho na Minazi.

Mazao ya msimu yamenisaidia sana kupunguza gharama za uendeshaji ambazo kwa kweli ni kubwa kuliko ulizozitaja hasa ukizingatia kila mwezi naenda shambani mara mbili.

Zipo faida nyingi ambazo tayari nimeshaanza kuziona hata hivyo kitu kilicho wazi kabisa ni kuongezeka kwa kipato mara dufu.

Ushauri wangu kwa wanaJF wote tuchangamkie kilimo kwasababu kinalipa sana,tuache kubweteka mijini au kufanya shughuli ambazo tayari watanzania wengine wameshazianzisha eg saloon,biashara ya taxi au daladala.Ardhi Tanzania bado ni rahisi sana nina uhakika kama unapata mshahara kuanzia 500,000/= na kuendelea unao uwezo wa kumiliki shamba kubwa ambalo litakusaidia wewe na kizazi chako.Tumekataa wana EAC kumiliki ardhi Tanzania wakati sisi wenyewe tunaiangalia bila kuifanyia kazi itafika siku hatutakuwa na sababu za kuwakatalia
.

Hongera sana Elnino umeamua jambo jema Mungu akubariki.

Naomba kuwasilisha.

Vipi hii project yako inaendeleaje mkuu?
 
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Vp mzee project yako na plan yako imeenda vyema?
 
mkuu mi nina miaka 19 tu. nimetishwa na kasi ya mabepari kama nyie. mwezi wa kwanza mwakani mungu akipenda nakamata hekari 100, moro.mkoa wa pwani wamekamata mafisadi wenyewe, nikisubiri miaka yetu sita pata kitu
 
Mkuu sana ELnino, vipi maendeleo ya shughuli za kilimo Turiani?

Ama jamaa kishakua fisadi na hataki kuongea nasi,au deal ili bounce na anaona soo kurudi kutupa feedback.

ELNINO,

Unajua nilivyosoma uzi wkao kwa mara ya kwanza ulinihamasisha sana nikaenda kukurupusha pori kubwa nikaanza kupunguza visiki. Kumbe baadae mzee ulichemsha sasa dah energy yote ikapungua aisee.

updates to follow!!
3rd Jan 2013

They say patience is a virtue
 
mkuu mi nina miaka 19 tu. nimetishwa na kasi ya mabepari kama nyie. mwezi wa kwanza mwakani mungu akipenda nakamata hekari 100, moro.mkoa wa pwani wamekamata mafisadi wenyewe, nikisubiri miaka yetu sita pata kitu

Hata sasa umechelewa dogo, utapata nje ya mabonde kusiko na maji na nyani/nguruwe lundo, wewe utakuwa ndio kinga ya mashamba yetu yasishambuliwe na wanyama waharibifu !!!!!!!!!! Utani dogo.

Wazo zuri.
 
kwa kuanza ni mvua za rehema ya mwenyezi mungu - cha kuzingatia pale ni kupanda at a right time na mbegu ya muda mfupi. Wanyama, ndege na wadudu hapo hamna tatizo kabisa, hayo ndiyo mambo yaliyofanyiwa kazi wakati wa upembuzi yakinifu ( feasibility study) ambao ulifanyika kwa uangalifu mkubwa.

Kwa sababu mtaji ni mdogo, suala la umwagiliaji litakuja baadaye sana - kwa sasa najikita kwenye kilimo cha nvua za mungu.

pia nimejipanga kununua mahindi extra toka kwa wakulima wenzangu wadogo wadogo wakati wa msimu wa uvunaji- let say gunia zingine 1000, hapo naweza pata kwa bei nzuri - na nitauza hapa dar, hii itaniongezea mtaji wangu kukua zaidi.

Kadri mtaji unavyokuwa ndiyo kadri nitakavyobadili mfuno wa ukulima wangu - kwa sasa nimeanza kwa hivi.

I do agree with you kwamba challenges lazima ziwepo katika kila jambo unataka kufanya - i'm ready to face them.

Mkuu hapo kwenye red ndio kila kitu. Whatever happens you are ready to face....
 
Ardhi ni njia sahihi ya kufikia maendeleo kamili.

kutokua na maendeleo ni karibu na umasikini vyote ni kama nguvu za asili mfano wa labda kama gravity, unaitaji kiasi fulani cha mwendo kasi (mtaji na mawazo), kuishinda nguvu hii 'umasikini' kwa mmoja~ujasiri/maono na jamii~sera.
 
Uko sahihi kabisa
 
Kuhusu kutegemea au kutotegemea mvua hili linategemea sana na mkoa unaolima. Mikoa kama Mbeya, Rukwa, Ruvuma, Kigoma kwa kweli huko bado suala la mvua sio issue.Kama mkulima unayeanza unaweza ukaitumia mvua hii hii na ikakutoa had ukapata mtaji wa kunnua pump na hata Tractor. Ila km utataka kulima mkoa wa Pwani, kwa kweli usicheze mbali na mto na ufikirie zaid kilimo cha umwangiliaji.

Mkuu me ninashamba maeneo ya Vigwaza kati ya ruvu na Chalinze, ni kama km 15 toka Morogoro road. Hakuna mto karibu. Ila nataka kulima ufuta only kwa kuzitaimu mvua za za mwanzoni. Kwa ujuzi wako hapo inaweza ikatoboa?
 
Back
Top Bottom