Heshima kwako ELNINO,
Wazo lako zuri sana binafsi nimeshalifanyia kazi tangu mwaka 2008, baada ya kugundua mshahara pekee bila kuwa na kipato kingine cha uhakika ni balaa kadri siku zinavyosonga mbele kwasababu majukumu yanazidi kuongezeka eg:watoto na nk.
Nimenunua shamba eka 250 kwa tsh 3.5 mil maeneo ya Kabuku Tanga na kuanza kulima mwaka huo huo(2008).Project yangu nimeigawanya katika sehemu kuu mbili [1] Mazao ya msimu eg;Mahindi,Dengu,Choroko,Mbahazi,Alizeti na Ufuta
[2] Mazao ya kudumu eg Maembe ya kisasa,Machungwa,Mananasi,korosho na Minazi.
Mazao ya msimu yamenisaidia sana kupunguza gharama za uendeshaji ambazo kwa kweli ni kubwa kuliko ulizozitaja hasa ukizingatia kila mwezi naenda shambani mara mbili.
Zipo faida nyingi ambazo tayari nimeshaanza kuziona hata hivyo kitu kilicho wazi kabisa ni kuongezeka kwa kipato mara dufu.
Ushauri wangu kwa wanaJF wote tuchangamkie kilimo kwasababu kinalipa sana,tuache kubweteka mijini au kufanya shughuli ambazo tayari watanzania wengine wameshazianzisha eg saloon,biashara ya taxi au daladala.Ardhi Tanzania bado ni rahisi sana nina uhakika kama unapata mshahara kuanzia 500,000/= na kuendelea unao uwezo wa kumiliki shamba kubwa ambalo litakusaidia wewe na kizazi chako.Tumekataa wana EAC kumiliki ardhi Tanzania wakati sisi wenyewe tunaiangalia bila kuifanyia kazi itafika siku hatutakuwa na sababu za kuwakatalia.
Hongera sana Elnino umeamua jambo jema Mungu akubariki.
Naomba kuwasilisha.